Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, January 27, 2015

MAGOJWA YANAYOAMBATANA NA UNENE (OBESITY)-2



Magonjwa yanayo ambatana na unene tumekuwa tukiyajadili tangu wiki iliyopita, leo tunahitimisha mada hii. Kupungua uzito, kuudhibiti au kutunza uzito alionao mtu baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi mno na ni suala linalohusisha kufanya mazoezi, kula lishe bora na mabadiliko mengineyo kama ifuatavyo:-

1) Mabadiliko ya tabia, mtu mwenye unene wa kupindukia anapaswa kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu kwa afya vinavyotakiwa ili kuustawisha mwili.

2) Suala lingine muhimu ni kuushughulisha mwili na kufanya mazoezi. Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na kuufanya mwili uwe na uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu.
Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension) na kuifanya sukari iwe katika kiwango kinachohitajika.

Kama hujazoea kufanya mazoezi, ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki, (tunashauriwa kufanya mazoezi dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki).

Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito lakini visiwe vyenye uzito mkubwa, mazoezi ya viungo na kadhalika.
Kama mtu ni mnene sana, basi ni bora azungumze na daktari wake kabla ya kuanza mazoezi mapya ili kuona ni mazoezi gani yaliyo salama kwa afya yake.

Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili hupata maumivu, hii ni hali ya kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya saa 2 na kuendelea baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.

3) Iwapo mabadiliko ya lishe na ufanyaji mazoezi hayatasaidia, wataalamu pia huwapatia dawa watu walio na unene wa kupita.

0 comments:

Post a Comment