Musa Mateja MREMBO kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’, amepiga mwereka wa aina yake baada ya kuteleza ukumbini, Risasi Jumamosi limeshuhudia. Tukio hilo lilijiri juzikati katika Hoteli ya Regence, Mikocheni jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa (bethidei). Mrembo kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho’. Wakati sherehe ikipamba moto, wageni waalikwa walimmwagia...