Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, January 27, 2015

MAGOJWA YANAYOAMBATANA NA UNENE (OBESITY)-2

Magonjwa yanayo ambatana na unene tumekuwa tukiyajadili tangu wiki iliyopita, leo tunahitimisha mada hii. Kupungua uzito, kuudhibiti au kutunza uzito alionao mtu baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi mno na ni suala linalohusisha kufanya mazoezi, kula lishe bora na mabadiliko mengineyo kama ifuatavyo:- 1) Mabadiliko ya tabia, mtu mwenye unene wa kupindukia anapaswa kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho...

PICHA ZA TUKIO:KICHANGA CHA MIEZI MINNE CHAOKOA FAMILIA ISITEKETEE KWA MOTO

KICHANGA kinachokadiriwa kuwa na umri wa miezi nane, wiki iliyopita kiliiokoa familia yake kuteketea kwa moto, baada ya kuamka usiku na kulilia kunyonya, kitendo kilichomshtua mama yake aliyebaini nyumba yao ilikuwa ikiungua, huko Kibamba Lungwe jijini Dar es Salaam. Sehemu ya nyumba iliyoungua. Akisimulia tukio hilo, mama wa kichanga hicho, Asha Mohamed, alisema alishtuka baada ya mtoto kuanza kulia akitaka kunyonya, alipoamka ndipo akaona mwanga...

OXFAM YATANGAZA MRADI KUPAMBANA NA EBOLA

Misaada ya kila hali bado inahitajika katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola Shirika la misaada Oxfam limetoa wito wa kutolewa kwa msaada wa thamani ya mamilioni ya dola kusaidia nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na Ebola, mradi huu wa msaada unaitwa Marshall Plan Zaidi ya Watu 8,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola, wengi wao nchini Sierra Leone,Guinea na Liberia. Mradi wa Marshall ulitumika baada ya vita ya pili ya Dunia kwa...

Monday, January 26, 2015

MWANAMKE AWAUA WATOTO WAKE WAWILI NA KUWAZIKA NDANI YA NYUMBA YAKE

Mwanamke mmoja mkazi wa mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini kata ya Chemchem amewaua watoto wake wawili na kuwazika ndani ya nyumba yake. Mwanamke huyo amedai kuwa kilichomfanya awalishe sumu watoto wake ni ugumu wa maisha uliokuwa ukimkabili baada ya kukimbiwa na mumewe. Kwa mujibu wa jirani yake, siku ya tukio mwanamke huyo alisikika akichimba shimbo ndani ya nyumba yake kabla ya kutangaza kupotelewa...

“UMASKINI WETU UMENIFANYA NIISHI KWA DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU”

Makongoro Oging’ na Issa Mnally, Kibaha/Uwazi Janeth Mlahagwa (18) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi “Albino”, mkazi wa Kijiji cha Mtumbatu, Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro ambaye anadai kwamba kifo kilimsonga kutokana na hali yake kuwa mbaya kila kukicha kwa kukosa matibabu na badala yake alikua akipewa vidonge vya kupunguza  maumivu. Janeth Mlahagwa akiwa na mama yake. Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni katika hospitali binafsi...

ASKARI WAWILI WAUAWA PWANI

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa, Pwani/Uwazi MAZITO yameibuka kufuatia tukio la majambazi kuvamia Kituo cha Polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani na kuwaua askari wawili kisha kuchukua bunduki 7, risasi 60 na mabomu kadhaa, Uwazi limeichimba.Tukio hilo lililozua hofu ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, lilijiri Januari 21, mwaka huu na hadi wakati tunaenda mitamboni, hakuna mtuhumiwa anayeshikiliwa. Ndugu wa karibu wa marehemu, Judith Timothy...

MIMBA KUYEYUKA (BLIGHTED OVUM) INATOKEAJE?

TATIZO hili pia huitwa ‘anembryonic gestation’. Hutokea pale mfuko wa mimba unapoendelea kukua bila ya kuwa na mtoto ndani. Kifuko cha mimba huitwa ‘gestational sac’ na mtoto ni ‘embryo’. HALI HALISI Mwanamke anakuwa mjamzito ambapo ana dalili zote za ujauzito na katika wiki sita za mwanzo akifanya Ultrasound mtoto anaweza kuonekana lakini baada ya hapo dalili za mimba zinaanza kupungua taratibu na mama akifanya Ultrasound mimba itaonekana...

Saturday, January 24, 2015

MWANAFUNZI KIDATO CHA PILI AJIFUNGUA KWENYE DALA DALA, NI BAADA YA KUMEZA DAWA ZA KUTOA MIMBA

Mwanafunzi wa Shule moja ya sekondari Jijini Dar es Salaam kajifungua kwenye daladala Maeneo ya azizi ally baada ya kumeza dawa za kutoa mimba, Kwa lugha nyingine Tunaweza kusema mwanafunzi huyo amefanya Abortion kwani Kichanga hicho kinakadiriwa kuwa na Miezi mitatu au Minne hivi, mwanafunzi huyo inasemekana anasoma kidato cha pili katika Moja ya shule Jijini Dar.... HABARI ZAIDI TUTAWAJUZA...

VIDONGE HATARI VYAUZWA KA NJUGU PHARMACY DAR!

Na Waandishi wetu/Risasi JumamosiHali inatisha! Vidonge vinavyodaiwa ni vya kutoa mimba vimezagaa kwenye maduka ya madawa baridi ‘famasi’ jijini Dar na kuuzwa kinyume cha sheria iliyowekwa na wahusika kwa kuwa hairuhusiwi kuuziwa dawa hizo pasipokuwa na kibali cha daktari.Wauzaji wa moja ya duka la dawa linalouza dawa za kutolea mimba.Kikosi chetu cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers Ltd kiliingia kazini kuzisaka famasi zinazodaiwa...

Thursday, January 22, 2015

TATIZO LA NYAMA KUJITOKEZA NJIA YA HAJA KUBWA {HEMORRHOID}

Wiki iliyopita tuliweza kuona nini maana kubwa ya tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika sehemu au maeneo ya haja kubwa na leo tutaweza kuona basi vyanzo au visababishi hasa vya tatizo hili kwa mwanadamu. VISABABISHI Sasa wataalamu bado hawajawa na majibu kamili kuhusiana na tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika maeneo ya haja kubwa husababishwa na kitu gani hasa lakini wameweza kutoa baadhi ya vitu ambavyo vinaaminika kwa kiwango kikubwa...

Tuesday, January 20, 2015

MIAKA MITATU MUHIMBILI BILA MATIBABU

Kijana Amosi Ng’arare Marale Sasi,(22) anayesumbuliwa na uvimbe usoni. Na Haruni Sanchawa/Uwazi Alikuja Muhimbili ili akafanyiwe upasuaji India, alipelekwa akarudishwa bila kutibiwa, awaita ndugu zake hospitalini. Kijana Amosi Ng’arare Marale Sasi,(22) mkazi wa Kijiji cha Kizaru, Kata ya Mryaza, wilayani Musoma Vijijni amepoteza mwelekeo wa maisha baada ya ndoto yake ya kusoma hadi chuo kikuu kuishia njiani kutokana na matatizo ya ugonjwa wa ajabu...

Sunday, January 18, 2015

WANANCHI MKURANGA WAASWA KUCHANGIA DAMU.

Wananchi wilayani Mkuranga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwenye benki ya damu iliyoko katika hospitali ya wilaya hiyo ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu linaloikabiri hospitali hiyo. Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Mkuranga na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo, Dkt. Anwar Milulu wakati akipokea msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwa lengo la kuwasaidia wagojwa...

Saturday, January 17, 2015

MTI WA AJABU WAGUNDULIKA MBEYA, UNADAIWA KUGAWA UTAJIRI

Wananchi wa kijiji cha Ijoka, Mkoani Mbeya wameingia kwenye imani za kishirikina baada ya kuandamana na kwenda kupasua mti ulianguka ambao wanadai una utajiri ndani yake.Wakazi hao walisema walielezwa na mganga wa jadi kutoka Malawi Peter Lungola, kuwa mti huo ukitumiwa vyema utaleta utajiri.Mganga huyo alifika kijijini humo miaka 20 iliyopita na kuwaeleza kuwa amti huo una asili kubwa ya utajiri na kuwa chini ya mti huo kuna nyumba za kifahari...

SITTI MTEMVU ATEMBELEA KITUO CHA WENYE ULEMAVU WA NGOZI HOSPITALI YA MKOA ILALA

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe Mussa Azzan Zungu akiongea na Waandishi wa Habari ( pichani hawapo) mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya kuhifadhia taka na Sabuni. Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Faundation, Sitti Mtemvu (wa tatu kulia) akimkabidhi vifaa vya kuhifadhia taka Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto), kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Ilala Dar es Salam. kuanzia kushoto nyuma ya mbunge ni Diwani wa kata ya...

Friday, January 16, 2015

TUHUMA NZITO: MAMA AMCHARANGA VIWEMBE MWANAYE

Stori: Gabriel Ng’osha na Denis Mtima/Ijumaa Unyama wa kutisha! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina la Feromena, mkazi wa Meko-Mtongani, Kunduchi jijini Dar, anatuhumiwa kumcharanga viwembe mwanaye wa kumzaa aliyetajwa kwa jina moja la Zena mwenye umri wa miaka kumi.Mtoto anayefahamika kwa jina la Zena anayedai kunyanyaswa na mama yake. Tukio hilo la kulaaniwa lilijiri Jumanne wiki hii nyumbani kwa mwanamke huyo maeneo hayo ambapo mama huyo inadaiwa...

WATOTO WAWILI WATEKETEA KWA MOTO KIJIJI CHA MBELA, MWANZA

WATOTO wawili wa familia moja, mmoja wa kike mwenye umri wa miaka minne na mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja wameteketea kwa moto na mmoja kujeruhiwa leo baada ya kibatari kulipuka na kuteketeza nyumba kijiji cha Mbela wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza.Muonekano wa nyumba baada ya kibatari kulipuka na kupelekea watoto wawili wa familia moja kufaliki dunia wakiwa ndani ya nyumba hiyo leo kijiji cha Mbela Wilayani, Misungwi mkoa wa Mwanza....