Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, October 21, 2014

UVIMBE KWENYA MJI WA MIMBA (FIBROID)-2





Naendelea kuelezea dalili za uvimbe kwenye mji wa mimba ili uweze kuzijua na kuchukua hatua mapema.

Dalili hutegemea na sehemu uvimbe ulikojishikiza, ukubwa wa uvimbe na kama mama ana ujauzito, uvimbe huambatana na kutokuwa na mpangilio wa hedhi hii hutokea kwa akina mama asilimia 30 ambapo mama huingia kwenye siku zake mara mbili kwa mwezi au kutoingia kabisa akifuatiwa na kumwaga damu nyingi wakati wa hedhi ambapo anaweza kupata upungufu wa damu.
UVIMBE KATIKA KIZAZI

Dalili
Dalili za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi ni kutokwa na damu kusipokuwa na mpangilio (abnormal uterine bleeding).

Hii huwapata akina mama kiasi cha asilimia 30 na huwa damu inatoka sana au kuendelea kutokwa na damu kwa muda mrefu zaidi ya siku 10 ambapo mgonjwa hupata madhara ya kupoteza madini ya chuma na kusababisha upungufu wa damu (iron deficiency anaemia) wale wenye uvimbe kwenye misuli ya uzazi ujulikanao kama sub mucous myoma wenyewe hupitiliza muda wa kuona siku zao na kutokwa vitone vidogo vya damu

. Kutoka kwa damu hutokana na muingiliano wa mishipa ya damu kwenye uzazi ambapo hukandamizwa na kusababisha kuta za ndani ya uzazi kutofanya kazi zake vizuri na wale wenye uvimbe wa ndani ya ukuta wa uzazi (pedunulated submcous) wenyewe hupata tatizo la kutokwa damu mara kwa mara ambapo mgonjwa anaweza kutokwa damu leo halafu ikisimama baada ya siku tatu inatoka tena.

Maumivu ya tumbo husababishwa na kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu ya mfuko wa uzazi na wakati mwingine uvimbe hupata vijidudu (infection)na kuleta maumivu makali ambayo husambaa hadi kiunoni na kwenye miguu.

Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment