Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, October 29, 2014

UVIMBE KWENYE MJI WA MIMBA (FIBROID)-3

Uvimbe huweza pia kukandamiza viungo jirani na uzazi (pressure effets) ambapo mirija ya mkojo na kibofu cha mkojo na utumbo mkubwa wa haja kubwa na uvimbe unaweza kusababisha usipate choo(consipation) wakati mwingine huweza kusababisha mkojo usitoke (urinal retention), dalili zingine ni kama kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspararemia), uchafu sehemu za siri na kushindwa kubeba mimba (infertity) asilimia kati ya 27- 40 ya wenye uvimbe hupata...

Friday, October 24, 2014

MGONJWA KWANZA KUUMWA EBOLA NCHINI

Serikali ya Mali imethibitisha kuhusiana na taarifa za mtoto wa miaka 2 kukutwa na maambukizi ya Ebola akiwa ni mtu wa kwanza kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Machi 2014. Taarifa kutoka mtandao wa the World Post zimesema, mtoto huyo amegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo aliporejea nchini humo akitokea Guinea, moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola Afrika Magharibi. Mali inakuwa nchi ya...

T.I AULIZWA MAREKANI KUHUSIANA NA EBOLA TANZANIA BAADA YA KUFANYA TAMASHA KUBWA BONGO

Alikua mgeni kwenye stage ya Tamasha la Fiesta lililofanyika Leaders club October 18 2014 akiwa na timu yake ya watu wasiopungua watano na kuisimamia hiyo show kwa zaidi ya dakika 60. Baada ya show Jumamosi, T.I aliondoka Tanzania Jumapili kurudi kwao Marekani kwa ajili ya kuhakikisha promo inakwenda vizuri sababu album yake mpya ilikua inatoka Jumanne ya October 21. Akiwa NewYork T.I alijikuta yuko mbele ya camera akihojiwa na mwandishi...

Thursday, October 23, 2014

TAMBUA SABABU ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (MISCARRIAGE)

Wiki iliyopita tuliongelea sana tatizo la kuharibika kwa mimba na tukagusia baadhi ya dalili ambazo zinaweza kumpata mwanamke anayeweza kukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba. Na dalili hizo ni kama; DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage) Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba. Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito. Dalili nyingine kubwa ni...

Tuesday, October 21, 2014

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO-2

MADHARA YA TUNDU KATIKA MOYO Madhara ambayo yanaweza kusababishwa na tundu katika kuta za chini za moyo ni Eisenmenger syndrome, hali ambayo hutokea pia pale mtu anapokuwa na tundu katika kuta za juu za moyo. Tatizo hili hutokea wakati mtiririko wa damu unapoongezeka kutoka kushoto kwenda kulia kupitia tundu katika kuta za moyo, suala ambalo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya mapafu na kusababisha shinikizo la damu katika mapafu. Hali...

UVIMBE KWENYA MJI WA MIMBA (FIBROID)-2

Naendelea kuelezea dalili za uvimbe kwenye mji wa mimba ili uweze kuzijua na kuchukua hatua mapema. Dalili hutegemea na sehemu uvimbe ulikojishikiza, ukubwa wa uvimbe na kama mama ana ujauzito, uvimbe huambatana na kutokuwa na mpangilio wa hedhi hii hutokea kwa akina mama asilimia 30 ambapo mama huingia kwenye siku zake mara mbili kwa mwezi au kutoingia kabisa akifuatiwa na kumwaga damu nyingi wakati wa hedhi ambapo anaweza kupata upungufu...

Wednesday, October 15, 2014

MARK ZUCKERBERG KUCHANGIA EBOLA

Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg (kulia) akiwa na mkewe, Priscilla Chan. Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema yeye na mkewe Priscilla Chan, watachanga dola milioni 25 za kusiadia vita dhidi ya Ebola....

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO

Kama kawaida safu hii huwa tunajadili masuala mbalimbali yanayohusu afya na tiba ili kupata ufahamu zaidi juu ya kuimarisha afya zetu na ya jamii kwa ujumla. Leo tutazungumzia ugonjwa unaojulikana kama tundu katika kuta za ventrikali za moyo au kwa kitaalamu Ventricular Septal Defect (VSD). Tatizo hili hutokea mara nyingi ambapo watoto 2-6 kati ya 1,000 uzaliwa nalo. Tundu katika kuta za chini za moyo au VSD ni pale panapokuwepo na uwazi katika...

Tuesday, October 14, 2014

EBOLA OUTBREAK: UN HEALTH WORKER DIES IN GERMANY HOSPITAL

The Ebola patient was being treated at St Georg hospital in Leipzig Continue reading the main story Ebola outbreak How not to catch Ebola Living with Ebola Why so dangerous? Mapping the outbreak A UN medical worker infected with Ebola has died at a hospital in Germany. Doctors at the hospital in Leipzig said the man, 56, originally from Sudan, died despite receiving experimental drugs to treat the virus. More than 4,400 people have died from...

Monday, October 13, 2014

WAZIRI SOPHIA SIMBA AZINDUA KAMPENI YA SARATANI DAR ES SALAAM

KAMPENI ya kuchangia matibabu ya saratani ya matiti nchini imezinduliwa leo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wananchi kuchangia shilingi 1,000 kwa kila mtu ili kuunga mkono hatua hiyo. Kampeni hiyo inaendeshwa na Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania (Tanzania Breast Cancer Foundation) na wataalam wake wanasema ugonjwa huo unatibika ukiwahiwa mapemaWaziri wa Maendeleo...

Sunday, October 12, 2014

TAHARUKI YA EBOLA UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA, KENYA

TAHARUKI imezuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi nchini Kenya, leo asubuhi baada ya abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki dunia muda mfupi alipowasili uwanjani hapo. Abiria huyo mwanamke alikuwa akitokea Juba, Sudan Kusini lakini kukawepo tetesi kuwa huenda amefariki kwa ugonjwa wa Ebola. Vipimo vya madaktari vimeonesha kuwa mgonjwa huyo hakufa kwa Homa ya Ebola. Katibu wa Afya wa Baraza la Mawaziri nchini Kenya,...

Thursday, October 9, 2014

IDADI YA WATU WENYE MATATIZO YA AKILI YAKIFIA ZAIDI YA WATU 450,000

Tanzania ina zaidi ya watu 450,000 wenye matatizo ya afya ya akili ambao wengi wao ni vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea tatizo lililotajwa kusababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi. Mganga mkuu wa serikali Dkt. Donald Mbando ametoa takwimu hizo leo wakati akiongea na waandishi wa habari kueleke maadhimisho ya siku ya Afya ya akili duniani ambayo kitaifa yataadhimishwa tarehe 10 mwezi huu katika viwanja...

Monday, October 6, 2014

BAYLOR YAKABIDHI VIFAA VYA MPANGO TIBA YA UTAPIA MLO MKALI KWA WATOTO MKOA WA MBEYA LEO

Shirika lisilo la Kiserikali la BAYLOR Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania na Shirika la UNICEF la Umoja wa Mataifa limekabidhi vitanda 10 vyenye thamani ya zaidi shilngi milioni 10 kwa wilaya 5 za Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya watoto wenye utapia mlo na wanaoishi na maambukizi ya VVU Mkoani hapa. Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mashirika hayo Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki hiyo ya BAYLOR Mkoani Mbeya Dr. Theopista Jacob Masenga ambapo mgeni rasmi...

Wednesday, October 1, 2014

DR. FADHIL EMILY WA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC AHUDHURIA KIKAO CHA KUTETEA TIBA ASILIA AKIWEPO MH. KINGUNGE GOMBALIMWIRU DODOMA

Dr. Fadhil Emily akiongea na bloger wa Fadhaget Sanitarium Clinic alisema, alikwenda Dodoma kwa mualiko wa kuhudhuria kikao cha kutetea Tiba Asilia. Mambo yaliyoongelewa ni kutaka serikali ya Tanzania kutambua kuwa Chuo cha Mheshimiwa Dr. Dadao ni cha uhakika na kutambua kuwa wasomi waliopo hapo chuoni wana mafunzo bora na wanaweza kufanya kazi ya kuwahudumia watu kwa njia ya Tiba Asilia. Kikao hicho kilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa serikali...

BREAKING NEWS: EBORA YATUA MAREKANI

Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas. Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo. Mgonjwa huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo. Zaidi ya watu 3,000 tayari wamefariki dunia...

MATATIZO YA UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA (CONGENITAL HEART DISEASE) -2

Wiki iliyopita tulikuwa tumeanza kuzungumzia juu ya matatizo ya moyo ya kuzaliwa sehemu ya kwanza, leo tunaendelea sehemu ya pili na ya mwisho.Vilevile sababu nyingine inayoweza kufanya mtoto azaliwe na matatizo ya moyo ni ugonjwa wa kisukari kwa mama wakati wa ujauzito. Leo tuangalie tatizo la mtoto kuzaliwa na tundu katika kuta za juu za moyo au Atrial Septal Defect (ASD). Wakati kijusi (fetus) kinapoendelea kukua, kuta kati ya atria mbili za...