Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, December 17, 2014

TAMBUA VIMBE MBALIMBALI KWA MWANAMKE NA JINSI YA KUZIONDOA PASIPO UPASUAJI

Leo tutazungumzia vimbe mbalimbali ambazo hutokea katika mwili wa mwanamke kwani wengi hawajui kama kizazi cha mwanamke kinaweza kutokewa na vimbe tofautitofauti katika maeneo tofauti kwa sababu vimbe zina vyanzo mbalimbali. Jambo la msingi la kuzingatia leo ni kwamba aina zote hizi za vimbe tuna uwezo wa kuziondoa pasipo kufanya upasuaji. AINA ZA VIMBE Zipo aina tofautitofauti za vimbe katika mwili wa mwanamke, nazo ni kama; VIMBE KATIKA MJI WA...

JINSI YA KUGUNDUA MAAMBUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)

Baadhi ya wagonjwa watahitajika kulazwa hospitali ambapo watapewa dawa za saa na kuwa chini ya uangalizi wa haraka wa manesi na madaktari.Wagonjwa wanaohitaji kulazwa ni kama wale wanaodhaniwa kuwa wana uvimbe au jipu kwenye mfuko wa mayai yaani tube ovarian abscess au wale wenye kutapika sana na wenye homa kali pia wenye maumivu makali ya tumbo yanayofanana na kidole tumbo. Wagonjwa ambao hawakupata nafuu baada ya matumizi ya dawa ya awali baada...

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-4

Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile Transrectal Ultrasound au Prostatic Needle Biopsy. Tukumbuke kuwa kuwahi kugundua saratani mapema kabla ya dalili, kuna faida kubwa kwa muathirika kwani saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika. TIBA YAKE Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani...

Thursday, December 11, 2014

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-3

Wiki iliyopita tulizungumzia sana madhara yanayoweza kumkuta mtu mwenye vidonda vya tumbo. Lakini leo sanasana tutaweza kuangalia dalili kubwa za tatizo hili ni zipi na mtu anapoziona katika mazingira yake ya kawaida basi aweze kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuweza kuliondoa tatizo hili kwa urahisi kabisa. DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO Dalili za tatizo hili la vidonda vya tumbo hutegemeana sana na tatizo linakuwa limefikia katika kiwango...

Wednesday, December 10, 2014

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-3

TUMEELEZA kuhusu kansa ya tezi dume, leo tutafafanua vihatarishi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake: Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea. Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika...

Tuesday, December 9, 2014

UTAGUNDUAJE MAABUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)

Kama tulivyokwisha kusoma wiki iliyopita katika safu hii dalili za maambukizi kwenye viungo vya uzazi kwa mwanamke kama vile kutokwa uchafu sehemu za siri, homa, maumivu chini ya kitovu, kutokwa na hedhi bila mpangilio, maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu wakati wa kutoka hedhi na nyinginezo, hivyo basi ili kugundua ugonjwa wa PID ni lazima kuchukua historia vizuri ya mgonjwa. Daktari atampima tumbo mama ili kugundua maumivu ya tumbo kama...

Friday, December 5, 2014

MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA NA UZITO WA KILO 13 NA UREFU WA INCHI 22

Tumezoea kusikia watoto wakizaliwa na uzito wa kilo mbili na nusu hadi tano lakini hii inaweza kuwa sehemu ya maajabu kwani si rahisi mama kujifungua mtoto mmoja na si mapacha mwenye uzito mkubwa kama huyu aliyezaliwa huko Marekani. Mwanamke huyo mw enye makazi yake nchini Marekani ameushangaza umma baada ya kujifungua mwanaye wa kike mwenye uzito wa kilo 13 kwa mara ya kwanza ikiwa ni uzao wake wa tano. Mtoto huyo aliyepewa jina la Mia Yasmin amezaliwa...

HUYU NDIYE DAKTARI ANAYETUMIA PAMPU YA BAISKELI KUFANYA UPASUAJI.

Daktari anayetumia pampu ya baiskeli kulifurisha tumbo la mwanamke anayetaka kukatwa kizazi nchini India. Jimbo moja nchini India limesitisha shughuli ya kufungwa kizazi wanawake baada ya daktari mmoja kupatikana akitumia pampu ya kuweka pumzi kwenye baiskeli kuweka hewa kwenye matumbo ya wanawake waliokuwa wanafanyiwa operesheni hizo. Daktari Chandra Rout, aliyetumia pampu hiyo kwa wanawake 56, Ijumaa wiki jana, aliambia BBC kuwa pampu hizo...

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-2

Wiki iliyopita nilianza kuelezea ugonjwa wa saratani ya tezi dume, leo nitafafanua dalili za ugonjwa huu kama ifuatavyo: Daktari mmoja ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya ‘50 Plus Campaign’ anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo...

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-2

Kama tulivogusia wiki iliyopita kuhusiana na visababishi vinavyoweza sababisha tatizo hili la vidonda vya tumbo, navyo ni kama;•Kutofuata ratiba nzuri ya chakula. •Mawazo (Stress). •Kula chakula kingi kupita kiasi, hii imekuwa kama hali ya kawaida hasa kwa wanaume wengi na hata wengine kudiriki kusema kwamba “Sifa ya mwanaume ni kula sana” wakati hii siyo sahihi na kama mwanadamu anakuwa na tabia hii ya kula sana basi kunauwezakano mkubwa wa kupata...

MAGONJWA YA KIKE NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO (GYNO PROBLEMS)-2

Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ‘Pelvic Mass’ Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ni tatizo sugu linalosumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa. \Hakuna chanzo halisi cha uvimbe ingawa baadhi husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni. Uvimbe katika viungo vya uzazi vipo nje na ndani. Uvimbe unaweza kuwa mkubwa kama mimba au mdogomdogo na mwingi. Uvimbe pia unaweza kuwa katika vifuko vya mayai ‘Ovarian Cyst’ ambapo...

Monday, December 1, 2014

SIKU YA UKIMWI DUNIANI; MKOA WA NJOMBE BADO UNAONGOZA KWA MAAMBUKIZI

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo Vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri....

Thursday, November 27, 2014

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?

watu wengi wanahangaika sana na tatizo la vidonda vya tumbo, pasipo kuwa na uhakika kama wanaweza kupona. Lakini leo tutaweza kujua maana ya vidonda vya tumbo (Ulcers), dalili zake, visababishi vyake na hata jinsi gani Watanzania waweze kujiepusha na maradhi hayo na tiba yake. MAANA YA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS) VIDONDA VYA TUMBO hotokea pale kuta za tumbo zinapotoa asidi iitwayo Hydrochrolic acid katika tumbo ambayo kazi yake ni kufanya mmeng’enyo...

FATUMA RAMADHANI RASHID AKIMBIWA NA MUNGU KISA TUMBO KUJAA MAJI

Stori: Waandishi Wetu MAMA wa watoto watano, Fatuma Ramadhani Rashid (37) amejikuta akitelekezewa watoto hao na mumewe Matola, kisa akidai ni yeye tumbo lake kujaa maji. Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Juni 12, mwaka huu, Ukonga-Mongolandege, Dar ambapo mama huyo alikuwa akiishi na mume wake huyo lakini mara baada ya kuanza kwa dalili za ugonjwa huo mumewe alianza visa na kutoweka nyumbani. Mama wa watoto watano, Fatuma Ramadhani Rashid aliyetelekezwa...

Wednesday, November 26, 2014

JK APOKEA SALAMU ZA KHERI TOKA KWA RAIS BARACK OBAMA WA MAREKANI

Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh.Liberata Mulamula akiwasilisha kwa Rais Dkt.Jakaya M rishoKikwete salamu za kumtakia kheri na afya njema kutoka kwa Rais wa Marekani Barack Obama jijini Baltimore, Maryland, Marekani. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha na ujumbe kutoka Ubalozi wa Tanzania ulioko jijini Washington DC uliomtembelea kumjulia hali na kwasilisha salamu za Rais Barack Obama. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Balozi...

STEVEN JOHN ANATESEKA NA SARATANI YA TUMBO..TUMSAIDIE

Stori: Makongoro oging’ “Maishi yangu yako hatarini, nachungulia kaburi, nimeteseka kwa muda mrefu bila kupona wala msaada, nimetoka katika ukoo maskini unaotegemea kwa asilimia kubwa kilimo cha jembe la mkono, nitapata wapi shilingi milioni moja na laki tano na arobaini na tano elfu ili nikatibiwe?” Hii ni sehemu ya kilio cha Steven John anayesumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya tumbo. Steven John anayesumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya tumbo....

BABY MADAHA ADAIWA KUAMBUKIZWA GONJWA BAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII wa Bongo Fleva, Baby Madaha anadaiwa kuambukizwa gonjwa hatari la zinaa ambalo halikutajwa jina lakini likielezwa kuwa linampa wakati mgumu kisaikolojia. Chanzo kimoja kimeiambia show bize kuwa, nyota huyo amekuwa akitumia dawa za kusafisha haja ndogo kwa muda mrefu lakini bila mafanikio. Msanii wa Bongo Fleva, Baby Madaha. Show bize ilimsaka Baby Madaha mwenyewe ambapo aling’aka kwa ukali. “Hizo habari nani kakupa wewe?...

MTOTO CAREEN MPONDO (4) ANATESEKA NA UGONJWA WA FIGO ANAHITAJI MSAADA WAKO

Stori: Imelda Mtema Mtoto Careen Mpombo (4) (pichani), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam, yuko katika mateso makali kufuatia kusumbuliwa na figo moja ambayo haifanyi kazi. Mtoto Careen anayesumbuliwa na figo moja ambayo haifanyi kazi. Licha ya kuugua figo, mtoto huyo pia ana ugonjwa wa mafindofindo (Tonsillitis) unaomfanya akose raha kutokana kuwa na maumivu makali yanayosababisha ashindwe kula. Akizungumza na gazeti hili, mama mzazi...

MWIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA DK CHENI ALISHWA SUMU TENA!

Stori: Imelda Mtema Staa wa kiume wa sinema za Kibongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, kwa mara nyingine alilazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar baada ya kudaiwa kula chakula kinachosadikika kuwa na sumu (poisonous food). Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ akiwa hoi hospitalini. Akizungumza na mwandishi wetu wikiendi iliyopita Dk Cheni alisema kuwa alikuwa mshehereshaji (MC) kwenye harusi moja iliyofanyika maeneo ya Sinza jijini Dar ndipo...

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)

Wiki hii wasomaji wengi wamependa nijadili kuhusu kansa ya tezi dume au Prostate Cancer kwa kitaalamu zaidi.Ugonjwa huu huweza kusababisha vifo. Ili kuujua vyema ugonjwa huo tafadhali fuatilia makala haya. Saratani ya tezi dume upo katika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vinavyotokana na kansa kwa wanaume duniani. Pia ni chanzo kikuu cha vifo vinavyosababishwa na saratani kwa wanaume wenye umri wa miaka 50 na kuendelea. Hata hivyo, satarani...

Monday, November 24, 2014

TARATIBU ZA TIBA ZA RAIS WA TANZANIA DKT. J.K KIKWETE ZAKAMILIKA

Taratibu za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete (Pichani), zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014. Taratibu hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa 12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani, walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba. Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea...

JINSI YA KUTUNZA NGOZI YENYE MAFUTA

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang'ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta. Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:• Kuridhi.•...

JINSI YA KUONDOA MADOA YA CHUNUSI

JUISI YA LIMAO NA MAJI YA ROSEChukua maji ya rose kiasi kama ni kijiko kimoja na maji ya limao nayo yawe kijiko kimoja paka eneo liloathiriwa na madoa, kaa kwa muda wa nusu saa mpaka saa moja kisha osha uso wako, fanya hivyo kwa muda wa wiki tatu utapona madoa doa yote usoni. Juisi ya limao na liwa Chukua juisi ya limao kiasi changanya na liwa kisha paka eneo lililoathirika, kaa kwa muda wa dakika tano utaona matokeo. Juisi ya limao na unga wa...

Saturday, November 22, 2014

MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI KUFANYIKA KITAIFA MKOANI NJOMBE

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) , Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri....

RAIS KIKWETE ATOLEWA NYUZI KATIKA MSHONO, AFYA YAKE YAZIDI KUIMARIKA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland baada ya kutolewa nyuzi katika mshono baada ya kufanyiwa upasuaji wiki iliyopita. Rais Kikwete anatarajiwa kurudi tena hospitalini hapo Jumatatu kwa ukaguzi wa maendeleo ya kidonda na ushauri. Kulia kwake ni Daktari wa Rais Profesa Mohamed Janabi.…Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore Maryland...

Thursday, November 20, 2014

HOSPITALI YA AGA KHAN YATOA VIPIMO VYA BURE KWA WABUNGE DODOMA‏

Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi John Komba akipimwa urefu kwenye viwanja vya Bunge na jopo la madaktari kutoka hospitali ya Aga Khan. Zaidi ya wabunge 200 pamoja na wafanyakazi wa bunge walipata semina ya afya pamoja kupima afya zao bure mwishoni mwa wiki kwenye zoezi ambalo liliongozwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Seif Rashid. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mh. Margaret Sitta akichukuliwa damu kwa ajili ya vipimo...

NABO PHILIPO ASUSIWA WATOTO NA MKE WAKE MARIANA SILAYO ETI WANA KIFAFA

MAMA AWAKIMBIA WANAYE WENYE KIFAFA Bw. Nabo Philipo aliyekimbiwa na mkewe. HILI nalo ni tukio! Mwanaume mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Nabo Philipo ameibuka na kudai kuwa, mkewe Mariana Thomas Silayo (pichani) amekimbia nyumbani na kumwachia watoto wawili wenye ugonjwa wa kifafa. Akizungumza kwa uchungu na gazeti hili hivi karibuni, Nabo alisema alifunga ndoa na Mariana mwaka 2002 na kujaliwa kupata watoto wawili, Madelin na Joyce Nabo na...