Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, December 5, 2014

MAGONJWA YA KIKE NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO (GYNO PROBLEMS)-2


Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ‘Pelvic Mass’
Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ni tatizo sugu linalosumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa.

\Hakuna chanzo halisi cha uvimbe ingawa baadhi husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni.
Uvimbe katika viungo vya uzazi vipo nje na ndani. Uvimbe unaweza kuwa mkubwa kama mimba au mdogomdogo na mwingi.

Uvimbe pia unaweza kuwa katika vifuko vya mayai ‘Ovarian Cyst’ ambapo hizi zipo aina mbili. Kuna Lutel Cyst ambayo hupona yenyewe na nyingine huwa ndogo tu katika vifuko vya mayai na hupona kwa dawa.

Kuna Cyst nyingine huwa kubwa kiasi kwamba humsababishia mwanamke apate maumivu makali upande mmoja wa tumbo kwa chini. Uvimbe ukifikia hali hii tiba yake ni upasuaji.Kuna aina nyingine ya uvimbe unakuwa nje ya kizazi, nje ya mrija na nje ya kifuko cha mayai ‘Tubal Ovarian Mass’ au kwa kifupi huitwa ‘TOM’. Aina hii ya uvimbe husababisha maumivu.

Uvimbe huu wa Cyst na TOM daima huwa na maji tu na wakati mwingine damu. Ukiwa na damu ndipo huwa na maumivu makali chini ya tumbo aidha kulia au kushoto. Uvimbe wa damu tiba yake ni upasuaji.

Kuna tatizo lingine ambalo ni vivimbe katika vifuko vya mayai. Tatizo hili hutokea katika vifuko vyote viwili vya mayai na husambaa na mwanamke hufunga kupata hedhi bila ya kuwa na mimba. Tatizo hili pia husababisha mabadiliko kwa mwanamke mikononi, miguuni na wengine huota ndevu na hata sauti hubadilika na kuwa nzito.

Athari za kuwepo na uvimbe katika viungo vya uzazi ni kutoshika mimba, mimba kuharibika, maumivu yasiyoisha chini ya kitovu, maumivu wakati wa tendo la ndoa, damu kutoka ukeni bila ya mpangilio.
Uchunguzi na tiba ya tatizo hili hufanyika katika hospitali za mikoa kwenye kliniki za magonjwa ya kike na matatizo ya uzazi. Endapo uvimbe utakuwa mkubwa sana kwa kuchelewa kutibiwa, athari zake ni kuondolewa kizazi.

Maumivu wakati wa hedhi
Maumivu wakati wa hedhi ni tatizo li nalowasumbua wanawake.
Zipo aina mbili za maumivu, kwanza ni ‘Primary Amenorrhoea’ ambapo ni maumivu yanayowasumbua sana wasichana hasa baada ya kuvunja ungo.

Maumivu haya husababishwa na matatizo katika mfuko wa homoni kutokana na kizazi cha usichana kuwa hakijatanuka vizuri na bado kinaendelea kukua.Tatizo hili huisha kwa tiba baada ya uchunguzi wa kina katika mfumo wa homoni, vilevile likiendelea kwa muda mrefu huwa linaisha baada ya kujifungua.

Msichana pia anaweza kupatwa na tatizo la kutokwa na damu kidogokidogo au nyingi kwa muda mrefu hata zaidi ya mwezi. Hii inatokana na tatizo katika mfumo wa homoni.

Aina nyingine ya maumivu haya ni Secondary Dysmenorrhoea. Hii huwapata wanawake ambao awali hawakuwa na maumivu wakati wa usichana na wanafikia utu uzima wanaanza kupata maumivu. Maumivu haya ya hedhi katika umri wa zaidi ya miaka ishirini huweza kusababishwa na maambukizi sugu katika mfumo wa uzazi.

Matatizo ya maumivu wakati wa hedhi huchunguzwa na kutibiwa kwenye hospitali ya mkoa katika kliniki za magonjwa ya kike na uzazi. Tiba inaweza kuwa ni dawa au upasuaji kutegemea na ukubwa wa tatizo.

Matatizo katika mfumo wa uzazi wa watoto
Matatizo haya yapo mengi ambayo huwasumbua watoto wadogo wa kike na wa kiume kabla ya balehe na kuvunja ungo.Watoto kama ilivyo watu wazima hupatwa na matatizo katika mfumo wa uzazi na athari kubwa hutokea baadaye ukubwani. Tunazungumzia mfumo wa uzazi wa watoto na jinsi ya kuyagundua katika makala zijazo.

0 comments:

Post a Comment