Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, December 9, 2014

UTAGUNDUAJE MAABUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)


Kama tulivyokwisha kusoma wiki iliyopita katika safu hii dalili za maambukizi kwenye viungo vya uzazi kwa mwanamke kama vile kutokwa uchafu sehemu za siri, homa, maumivu chini ya kitovu, kutokwa na hedhi bila mpangilio, maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu wakati wa kutoka hedhi na nyinginezo, hivyo basi ili kugundua ugonjwa wa PID ni lazima kuchukua historia vizuri ya mgonjwa.

Daktari atampima tumbo mama ili kugundua maumivu ya tumbo kama yapo sehemu gani na pia kufanyia vipimo kama vile kupima uchafu kutoka ukeni na vipimo vingine kama Ultrasound.

Magonjwa mengine yanayofanana na PID: Hayo ni kama kidole tumbo (appenditis), mimba kutunga nje ya mji wa mimba hasa ikitungwa kwenye mirija na kupasuka (ruptured actopic pregnance), kupasuka uvimbe kwenye mfuko wa mayai (reptured ovarian mass) au maambukizi ya vidudu kwenye mkojo (urinary tract infection).

MADHARA YA PID
Madhara ya haraka (immediate complication) ni magonjwa yanayoweza kusababishwa na maambukizi kwenye mji wa mimba, vijidudu huweza kusambaa na kuingia kwenye utumbo (peritonitis) au wadudu kuingia kwenye mfuko wa damu (septichemia) ambapo huweza kuathiri viungo kama magoti na mgonjwa kupata ugonjwa wa arthritis na moyo (myocarditis).

Madhara ya muda mrefu ni kama maumivu wakati wa tendo la ndoa (Dyspareunia), kukosa kupata mimba (infertity), maambukizi kuwa sugu (chronic imflammatory diseases) na uwezekano wa mimba kutunga nje ya mji wa mimba yaani ectopic pregnance.

MATIBABU
Mgonjwa atapatiwa tiba kwa muda usiopungua siku 14 dawa zinazotumika ni kama levoflaxacin ikichanganywa na metronidozole.

Pia dawa zingine kama cefriaxone, dnycyline hutumika kwa kipindi cha siku 14. Matibabu haya hutumika kwa wagonjwa wa nje (out patient), wagonjwa watahitaji kuonwa na daktari baada ya siku 2 baada ya kumaliza dawa. Itaendelea wiki ijayo.

0 comments:

Post a Comment