Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, December 17, 2014

TAMBUA VIMBE MBALIMBALI KWA MWANAMKE NA JINSI YA KUZIONDOA PASIPO UPASUAJI

Leo tutazungumzia vimbe mbalimbali ambazo hutokea katika mwili wa mwanamke kwani wengi hawajui kama kizazi cha mwanamke kinaweza kutokewa na vimbe tofautitofauti katika maeneo tofauti kwa sababu vimbe zina vyanzo mbalimbali. Jambo la msingi la kuzingatia leo ni kwamba aina zote hizi za vimbe tuna uwezo wa kuziondoa pasipo kufanya upasuaji. AINA ZA VIMBE Zipo aina tofautitofauti za vimbe katika mwili wa mwanamke, nazo ni kama; VIMBE KATIKA MJI WA...

JINSI YA KUGUNDUA MAAMBUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)

Baadhi ya wagonjwa watahitajika kulazwa hospitali ambapo watapewa dawa za saa na kuwa chini ya uangalizi wa haraka wa manesi na madaktari.Wagonjwa wanaohitaji kulazwa ni kama wale wanaodhaniwa kuwa wana uvimbe au jipu kwenye mfuko wa mayai yaani tube ovarian abscess au wale wenye kutapika sana na wenye homa kali pia wenye maumivu makali ya tumbo yanayofanana na kidole tumbo. Wagonjwa ambao hawakupata nafuu baada ya matumizi ya dawa ya awali baada...

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-4

Baada ya vipimo hivyo kama vitaashiria saratani ya tezi dume basi daktari anaweza kuamuru vipimo vingine ili kuthibitisha uwepo wa ugonjwa huo kama vile Transrectal Ultrasound au Prostatic Needle Biopsy. Tukumbuke kuwa kuwahi kugundua saratani mapema kabla ya dalili, kuna faida kubwa kwa muathirika kwani saratani ikigundulika mapema ni rahisi kutibika. TIBA YAKE Kuna njia kadhaa za matibabu ya saratani ya tezi dume. Hata hivyo uamuzi wa njia gani...

Thursday, December 11, 2014

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-3

Wiki iliyopita tulizungumzia sana madhara yanayoweza kumkuta mtu mwenye vidonda vya tumbo. Lakini leo sanasana tutaweza kuangalia dalili kubwa za tatizo hili ni zipi na mtu anapoziona katika mazingira yake ya kawaida basi aweze kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuweza kuliondoa tatizo hili kwa urahisi kabisa. DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO Dalili za tatizo hili la vidonda vya tumbo hutegemeana sana na tatizo linakuwa limefikia katika kiwango...

Wednesday, December 10, 2014

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-3

TUMEELEZA kuhusu kansa ya tezi dume, leo tutafafanua vihatarishi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo ni baadhi yake: Kwanza kabisa ni umri. Nafasi ya kupata saratani ya tezi dume huongezeka sana hasa ukifikia umri wa karibu miaka 50 na kuendelea. Nasaba ni kihatarishi kingine ambapo wanaume wenye historia ya tatizo hili kwenye familia zao, yaani wale ambao mmoja wa ndugu zao wamewahi kuugua ugonjwa huu huwa katika...

Tuesday, December 9, 2014

UTAGUNDUAJE MAABUKIZI KWENYE UZAZI (DIAGNOSIS OF PID)

Kama tulivyokwisha kusoma wiki iliyopita katika safu hii dalili za maambukizi kwenye viungo vya uzazi kwa mwanamke kama vile kutokwa uchafu sehemu za siri, homa, maumivu chini ya kitovu, kutokwa na hedhi bila mpangilio, maumivu wakati wa tendo la ndoa na maumivu wakati wa kutoka hedhi na nyinginezo, hivyo basi ili kugundua ugonjwa wa PID ni lazima kuchukua historia vizuri ya mgonjwa. Daktari atampima tumbo mama ili kugundua maumivu ya tumbo kama...

Friday, December 5, 2014

MTOTO ALIYEZALIWA AKIWA NA UZITO WA KILO 13 NA UREFU WA INCHI 22

Tumezoea kusikia watoto wakizaliwa na uzito wa kilo mbili na nusu hadi tano lakini hii inaweza kuwa sehemu ya maajabu kwani si rahisi mama kujifungua mtoto mmoja na si mapacha mwenye uzito mkubwa kama huyu aliyezaliwa huko Marekani. Mwanamke huyo mw enye makazi yake nchini Marekani ameushangaza umma baada ya kujifungua mwanaye wa kike mwenye uzito wa kilo 13 kwa mara ya kwanza ikiwa ni uzao wake wa tano. Mtoto huyo aliyepewa jina la Mia Yasmin amezaliwa...

HUYU NDIYE DAKTARI ANAYETUMIA PAMPU YA BAISKELI KUFANYA UPASUAJI.

Daktari anayetumia pampu ya baiskeli kulifurisha tumbo la mwanamke anayetaka kukatwa kizazi nchini India. Jimbo moja nchini India limesitisha shughuli ya kufungwa kizazi wanawake baada ya daktari mmoja kupatikana akitumia pampu ya kuweka pumzi kwenye baiskeli kuweka hewa kwenye matumbo ya wanawake waliokuwa wanafanyiwa operesheni hizo. Daktari Chandra Rout, aliyetumia pampu hiyo kwa wanawake 56, Ijumaa wiki jana, aliambia BBC kuwa pampu hizo...

FAHAMU UGONJWA WA SARATANI YA TEZI DUME (PROSTATE CANCER)-2

Wiki iliyopita nilianza kuelezea ugonjwa wa saratani ya tezi dume, leo nitafafanua dalili za ugonjwa huu kama ifuatavyo: Daktari mmoja ambaye ni miongoni mwa waathirika wa saratani hiyo na mwanzilishi wa kampeni ya kuangamiza saratani ya tezi dume nchini Tanzania ya ‘50 Plus Campaign’ anasema kuwa, ugonjwa huu ukitambuliwa mapema huweza kutibika kwa urahisi. Kuna vihatarishi vingi vinavyochangia mwanamume kupata saratani ya tezi dume. Vifuatavyo...

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-2

Kama tulivogusia wiki iliyopita kuhusiana na visababishi vinavyoweza sababisha tatizo hili la vidonda vya tumbo, navyo ni kama;•Kutofuata ratiba nzuri ya chakula. •Mawazo (Stress). •Kula chakula kingi kupita kiasi, hii imekuwa kama hali ya kawaida hasa kwa wanaume wengi na hata wengine kudiriki kusema kwamba “Sifa ya mwanaume ni kula sana” wakati hii siyo sahihi na kama mwanadamu anakuwa na tabia hii ya kula sana basi kunauwezakano mkubwa wa kupata...

MAGONJWA YA KIKE NA JINSI YA KUKABILIANA NAYO (GYNO PROBLEMS)-2

Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ‘Pelvic Mass’ Uvimbe katika viungo vya uzazi vya mwanamke ni tatizo sugu linalosumbua wanawake wengi walio katika umri wa kuzaa. \Hakuna chanzo halisi cha uvimbe ingawa baadhi husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni. Uvimbe katika viungo vya uzazi vipo nje na ndani. Uvimbe unaweza kuwa mkubwa kama mimba au mdogomdogo na mwingi. Uvimbe pia unaweza kuwa katika vifuko vya mayai ‘Ovarian Cyst’ ambapo...

Monday, December 1, 2014

SIKU YA UKIMWI DUNIANI; MKOA WA NJOMBE BADO UNAONGOZA KWA MAAMBUKIZI

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dkt. Fatma Mrisho akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani isemayo, Tanzania Bila Maambukizi Mapya ya VVU, Vifo Vitokanavyo na Ukimwi na Ubaguzi na Unyanyapaa inawezekana inayolenga kupunguza maambukizi Mapya ya Ukimwi, kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi na kukomesha vitendo vya unyanyapaa kwa asilimia Sifuri....