Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, November 5, 2014

UVIMBE KWENYE MJI WA MIMBA (FIBROID)-4




MATIBABU YA UVIMBE KWENYE KIZAZI
Wiki iliyopita tulieleza matatizo ya uvimbe kwenye kizazi. Leo tunafafanua matibabu ya uvimbe kwenye kizazi kwamba hutegemea na vitu mbalimbali kama umri au kama mama ameishawahi kupata ujauzito au kama ni mjamzito.

Mgonjwa akiwa na uvimbe wa kizazi daktari anaweza kuangalia dalili alizonazo, ukubwa wa uvimbe na sehemu ya uvimbe ulikojitokeza.
Kama mgonjwa yupo katika hali mbaya au kapungukiwa damu basi ataona kama anahitaji kuongezwa damu bila kuchelewa au mgonjwa mwenye uvimbe kama anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura.

Daktari atamfanyia uchunguzi kujua ikiwa mgonjwa ana maambukizi ya vijidudu kwenye uvimbe au kama uvimbe umejivilinga (torsion) au kama utumbo umejikunja (intestinal obstraction).
Wagojwa ambao wana uvimbe kwenye uzazi wakati huo huo ni wajawazito kwa kweli upasuaji wa kuondoa uvimbe hautakiwi kufanyika.

Wagonjwa walio wengi wenye uvimbe kwenye kizazi hawana dalili yoyote hivyo basi, hawapati tiba, pia wale ambao wana uvimbe mdogo huku wakiwa wameishafunga siku za hedhi, hawahitaji matibabu pia ni lazima daktari achunguze kama hana uvimbe sehemu nyingine ya mfumo wa uzazi.
Mama mwenye ujauzito halafu uvimbe ukajikunja anaweza akafanyiwa upasuaji ili kunusuru maisha yake pia uvimbe hautakiwi kutolewa wakati wa upasuaji wa kumzalisha mama.

Matokeo ya matibabu kama yamefanyika vizuri na kwa wakati unaotakiwa huweza kupunguza ukubwa wa uvimbe kwa zaidi ya asilimia 50 na kuweza kupotea kabisa bila upasuaji kwa asilimia 30 na uvimbe hupotea baada ya miezi mitatu.

Matokeo yake mgonjwa hurudi katika hali yake ya zamani na kama alikuwa na tatizo la kupata mimba basi huweza kupata kirahisi.

Mama anaweza kufanyiwa upasuaji kama anatokwa na damu nyingi au kama uvimbe ni mkubwa sana hivyo hupasuliwa ili kuondoa uvimbe na hupasuliwa tumboni.Ikiwa mgonjwa ana mtoto hupewa dawa za kuondoa uvimbe ikishindikana ndipo upasuaji hufanyika.

MADHARA YA UVIMBE KWA WAJAWAZITO
Madhara ya uvimbe kwenye kizazi ni mtoto kutokaa vizuri kwenye mfuko wa uzazi, kuziba njia za uzazi, kutokwa damu kwa wingi wakati wa kujifungua na kutokwa damu wakati ana mimba pia kupoteza damu nyingi.

Ushauri:
Ni vizuri kuhudhuria kliniki mara kwa mara kwani uvimbe ni ugomjwa unaotibika hospitali.

0 comments:

Post a Comment