Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, November 11, 2014

MAAMBUKIZI KATIKA MFUMO WA KIZAZI (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)



Mambukizi katika mfuko wa kizazi au kitaalamu pelvic inflammatory disease ni maambukizi ya vijidudu yanayoshambulia sehemu ya ndani ya viungo vya uzazi kama vile mji wa mimba, mirija ya uzazi (follopian tubes), mifuko ya uzazi (ovaries), na viungo vingine vya uzazi vilivyopo kwenye nyonga ya mwanamke ambapo vijidudu hivyo huweza kuleta madhara makubwa kama kutengeneza jipu kati ya mirija ya uzazi na mifuko ya mayai (tubo-ovarian abscess).

SABABU ZA MAAMBUKIZI HAYO (aetiology)
Vijidudu vinavyopanda kwenda kwenye mji wa mimba kutoka katika uke (ascending infection), magonjwa ya zinaa (Sexual transmitted diseases-STDS), vifaa vya hospitali vinavyotumika katika vipimo au kutolea tiba (instrumentation) pia vijidudu huweza kusafiri kupita katika mishipa ya damu (haematogenous and hymphatic spread).

Wadudu wanaoambukiza kwa wingi ambao ni wa magonjwa ya zinaa kama wadudu wa kisonono (neisela gonococca na chylamydia trachomitis). Hawa ni wadudu hatari sana wanaotesa akina mama na kuwasababishia maumivu makali ya tumbo la chini ya kitovu.
Pia kuna vijidudu vingine ambavyo havitegemei oxygen na ambavyo vinategemea oxygen (aerobic organism and anaerobic organism).

Licha ya vijidudu, kuna vihatarishi vinavyoweza kusababisha maambukizi kwenye mji wa mimba, hivyo ni kama kuwa na wapenzi wengi yaani multiple sexual partners, matumizi ya kitanzi kwa ajili ya kuzuia mimba (IUCD), kusafisha kizazi, kuugua magonjwa ya zinaa mara kwa mara, mwanamke kunawa na sabuni zenye kemikali nyingi sehemu za siri.

Pia kuna vitu ambavyo husaidia mwili kujikinga na maambukizi ya vijidudu katika mfumo wa uzazi, kama msichana kuwa hajavunja ungo (intact hymen), pia kuna vinyweleo kwenye njia ya mimba ambavyo vinazuia vijidudu kupanda na ute unaotoka kwenye shingo ya kizazi yaani cervicl mucosa barrier.

0 comments:

Post a Comment