
Wiki iliyopita tulizitazama aina za vimbe, tuliishia katika kipengele cha pili kilichosema: Fibroids au Mayoma:Hizi ni vimbe zinazotokea katika mji wa mimba na hizi ndizo vimbe zinazowasumbua watu wengi sana katika jamii yetu ya sasa, na dalili zake ni kama; Hapa mwanamke hupatwa na maumivu chini ya kitovu lakini ni katikati siyo upande wa kulia wala upande wa kushoto na mara nyingi maumivu haya huambatana na maumivu ya kiuno, maumivu ya mgongo...