Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Saturday, March 29, 2014

UNAFAHAMU UGONJWA WA KISUKARI NA SABABU ZAKE?

Ugonjwa wa Kisukari ni miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwamo Tanzania.

Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi ya kongosho inaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho na kusababisha kuongezeka au kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg2XeKd8RdhS86PIkpkNcmq10YvMMFPSpeVM30ebQABtAKpjEKhq-Y07XyIIYIah8tm4qQeRyoDnp3n36puDMHy_xrmVz7BjuYWKBdfuC_JOW7tvPqKArfQDogyDwkO-NkG-idXTaXlsQJ4/s1600/apples.jpg
Aina za kisukari
Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo:

Kisukari Namba Moja
Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana. Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans.

Iwapo tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa seli hizi katika tezi kongosho ni pamoja na kushambuliwa kwa tezi hiyo.

Mashambulizi katika kongosho huweza kufanywa na magonjwa yanayosababisha upungufu wa kinga ya mwili.

Uharibifu katika tezi kongosho hupelekea kukosekana kabisa kwa wa tezi ya insulin au huifanya tezi hiyo kuzalishwa kwa kiwango kidogo.

Wagonjwa wa aina hii ya kisukari huhitaji kupewa dawa za insulin kwa njia ya sindano katika maisha yao yoteili waweze kuishi. Ndiyo maana aina hii ya kisukari huitwa pia kisukari kinachotegemea Insulin au Insulin Dependent Diabetes Mellitus (IDDM)

0 comments:

Post a Comment