Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, August 4, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUJUZA JUU YA MAGONJWA YA UVIMBE KWENYE KIZAZI CHA WANAWAKE




Kwa wanawake tatizo lao kubwa ni ‘Fibroid’ ambao ni uvimbe katika sehemu za uzazi (uterus) ambapo hutengenezwa na kambakamba zilizofungamana yaani muscle fibre. Fibroid huanza kwa ukubwa kama punje ya njugu mawe lakini huweza kukua na kuwa kama boga.

Fibroid hupatikana zaidi kwa wanawake wa umri kati ya miaka 30 na 40 na hupungua ukubwa mara tu wanapoingia katika umri wa utu uzima, ingawa sababu au chanzo hasa cha fibroid hakijulikani, utafiti unaonyesha kuwa huchochewa na ‘oestrogen’ mwilini.

Mara nyingi fibroid hukua kwa mwanamke pale kiwango cha ‘oestrogen’ kinapoongezeka mwilini na pia fibroid hupungua wakati kiwango cha ‘oestrogen’ nacho kikipungua.
Oestrogen ni mkusanyiko wa homoni ambazo ndizo zinazoukuza mwili wa mwanamke kijinsia. Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi.

Pia wanawake wenye uzito wa zaidi ya kilo 70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata tatizo hili kutokana na kiwango kikubwa cha oestrogen katika umri huo.Zamani fibroid ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa sababu vidonge hivyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha oestrogen. Hivi sasa vidonge hivi havina kiwango kikubwa cha oestrogen kama ilivyokuwa zamani.

Fibroid zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Zipo zinazotokea ndani ya mji wa mimba na nyingine zinatokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba. Karibu asilimia 75 ya wanawake wenye fibroid hawajui kama wana tatizo hilo. Utambuzi wa dalili za fibroid hutegemea ukubwa wake na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mtu.Fibroid ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na fibroid kubwa inayoota nje ya kizazi.

DALILI
Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na maumivu ya tumbo.
Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa, na mgonjwa kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo, kutopata mimba na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Fibroid zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na fibroid, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus).

Mwanamke anapokuwa mjamzito pia akawa na fibroid, mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye fibroid na kuifanya isinyae hivyo kusababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati wa kujifungua, kama fibroid itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

USHAURI
Dalili zikiwepo na kuhisi unalo tatizo la fibroid, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo kujua kama unao ugonjwa au la. Daktari atafanya vipimo vya ‘Ultrasound’ (mionzi) au kitatumika kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke kitaalamu huitwa hysteroscopy au kufanyiwa upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke kitaalamu huitwa Laparosopy.

TIBA
Kuna njia kuu mbili za kutibu fibroid. Moja ni kwa kutumia dawa. Mkusanyiko wa dawa zijulikanazo kama ‘GnRH analogues’ hupunguza kiwango cha oestrogen mwilini na hivyo kusababisha fibroid kusinyaa.
Dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa fibroid pia hupunguza mzunguko wa hedhi.

Matumizi ya dawa za ‘GnRH analogues’ yasizidi miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa baadaye. Mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi,wanawake wengine baada ya wiki chache hujikuta wakirudiwa na tatizo hili ambalo huanza kukua tena na mwanamke huanza kupata hedhi kama awali lakini ikiambatana na maumivu makali.

Baadhi ya wanawake huwa hawapati hedhi tena kwa maisha yao yote.

Upasuaji ni njia nyingine ya kutibu ugobnjwa huu na huhusisha mambo yafuatayo: Kuiondoa fibroid yenyewe na kuacha kizazi jambo ambalo kitaalamu huitwa myomectomy; kukiondoa kizazi kabisa kitaalamu huitwa hysterectomy na kuzuia damu kwenda kwenye fibroids yaani uterine artery embolisation.
Pia iko njia ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni kwa ajili ya kuziua kwa kemikali maalumu.

0 comments:

Post a Comment