Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, May 6, 2014

YASEMEKANA RAY C AMEUGUWA UGONJWA WA DENGE ALAZWA MWANANYAMALA

Ray C akiwa amelazwa katika moja ya wodi za hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana Jumatatu. Picha na Rafael Lubava

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo jana Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

MWANAMUZIKI mwenye sauti ya mvuto, Ray C, amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam akikabiliwa na homa kali.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, mwanamuziki huyo ambaye amekuwa katika tiba ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya hospitalini hapo, alifikishwa hapo jana Jumatatu asubuhi na baadhi ya madaktari walibainisha kuwa Ray C anasumbuliwa na ugonjwa wa dengue ambao umelipuka katika maeneo mengi jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

“Tumemfanyia vipimo, ana homa kali sana lakini hana malaria. Baada ya kuchunguza dalili, tumechukua vipimo na kubaini kwamba amepata maambukizi ya dengue, hivyo tunaendelea kumpa matibabu kwa sasa,” alieleza daktari ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Mwanaspoti iliyofika wodini alimolazwa mwanamuziki huyo, lilijaribu kuzungumza naye, lakini manesi wazuia wa kusema hapaswi kuamshwa kwa kuwa alikuwa amepewa dawa za kutuliza maumivu na kushusha homa.

Ray C amekuwa katika tiba ya kuacha dawa za kulevya na amekuwa akisaidiwa kurejea katika sanaa ya muziki ambayo alikuwa akiifanya vizuri kabla ya kuingia kwenye wimbi hilo.

Ugonjwa huo dengue uliotajwa kumsumbua kwa sasa umewakumba wananchi wengi wa Dar es Salaam na unaenezwa na mbu weusi waitwao Aedes Egypitia.

Mbu hao ambao huonekana zaidi mchana, huzaliana katika maji safi yaliyotuama.

Usiku wa kuamkia juzi Jumapili, Ray C alikuwapo kwenye ukumbi Mlimani City kwenye hafla ya Tuzo za Muziki za Kilimanjaro ambapo hakuonekana kuwa na dalili zozote za kuumwa.

0 comments:

Post a Comment