Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, July 1, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA BAADHI YA SABABU ZA MENO KUOZA KWA WATOTO

Meno mbali na kuwa ni msaada katika kukatakata chakula mdomoni pia ni urembo kwa mwanadamu. Mtu anapokosa meno anaonekana wa ajabu kidogo. Kuna umuhimu wa kutunza sana meno yetu kwa njia mbalimbali tunazofundishwa madarasani na hata kwa marafiki zetu mitaani. Mzazi unapokosa kumtunza mwanao na kuhakikisha meno yake ni imara na bora, siku hayo meno yatakapooza na kung'ooka, mtoto huyo akikua na kupata ufahamu atakulaamu.
http://static.guim.co.uk/sys-images/Observer/Columnist/Columnists/2011/1/29/1296296490076/Young-boy-brushing-his-te-007.jpg
Meno na uzuri au ubora wake huanzia kwa watoto. Tangu mtoto anapoota meno, anapofikisha miaka mitano na kuanza kung’oa, ni kipindi mujarabu kwa mwonekano wake wa kinywa siku za usoni.

Meno na uzuri au ubora wake huanzia kwa watoto. Tangu mtoto anapoota meno, anapofikisha miaka mitano na kuanza kung’oa, ni kipindi mujarabu kwa mwonekano wake wa kinywa siku za usoni.

Lakini watu wengi huoza meno na watoto pia hukumbwa na hali hii.

Kuoza kwa meno ambayo hushambulia zaidi meno ya utotoni (milk teeth or primary dentition), japo wakati mwingine hata huweza kushambulia hata ukubwani. Ugonjwa huu unajidhihirisha kwa kuanza kushambulia meno na vyanzo vyake.

Meno hushambuliwa kwa mpigo hasa kuanzia meno ya juu mbele, ingawa meno ya chini mbele ni mara chache kushambuliwa kwa vile yanakingwa na visababisha vya kuoza na ulimi.

Ugonjwa huu hushambulia hata maeneo ya meno ambayo kwa hali ya kawaida si rahisi kuoza, kama sehemu ya kukatia kwa meno ya mbele (incisal edges) na sehemu ya mbele kati na nyuma kati (facial and lingual surfaces).
http://cdn.inquisitr.com/wp-content/uploads/2013/05/cavities.jpg

Sababu ya kuoza kwa meno utotoni
Nadharia nyingi zinaonyesha kuna uhusiano mkubwa kati ya ugonjwa huu na tabia ya ulaji ya mtoto (feeding habits).

Vinywaji vyenye sukari: Mfano kisababishi kikubwa ni watoto kunywa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na mara nyingi kwa kutumia chupa za kunyonyea (nursing bottles) ndiyo maana ugonjwa huu wakati mwingine huitwa nursing bottle caries.

Hii hujitokeza hasa kwa watoto wanaochwa na yaya zao, ambao huwapa vinywaji hivyo kila wanapohitaji au wakilia.

Pamoja na kwamba ugonjwa huu hutokana zaidi na chupa za kunyonyea lakini pia yawezekana kutokana na mama kumnyonyesha mtoto mara kwa mara au tuseme kila anapo hitaji.

0 comments:

Post a Comment