Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, June 29, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKULETEA UKWELI KUHUSU UGONJWA WA SIKO SELI (SICKLE CELL)

Siko seli ni nini?
Siko seli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika chembechembe nyekundu za damu.
• Kwa kawaida chembe nyekundu za damu zina umbo la mviringo ambalo huzirahisishia kupita kwenye mishipa midogo ya damuili kusafirisha hewa safi ya oxygen katika sehemu mbali mbali za mwili.

• Kwa mtu mwenye ugonjwa wa siko seli chembe hizi huwa tofauti, zinanata na zina umbo la mwezi mchanga (siko).

• Tanzania ni moja wapo kati ya nchi zenye wagonjwa wengi wa siko seli duniani ambapo inakadiriwa kuwa kati ya watoto 8,000 -10,000 huzaliwa na ugonjwa wa siko seli kila mwaka pia inakadiriwa kuwa 13% ya watu wote nchini wana vinasaba vya ugonjwa wa siko seli. (sickle cell traits).

Nini husababisha ugonjwa huu?
• siko seli ni ugonjwa wa kurithi, ugonjwa huu hurithiwa katika njia sawa sawa ambavyo mtu hurithi rangi yake ya mwili, au macho, urefu nk, hivyo basi mtu huzaliwa na ugonjwa huu.

• Vinasaba vya sikoseli hurithiwa sawa sawa kutoka kwa wazazi wote wawili yani baba na mama.

• Mtu hawezi kupata ugonjwa wa siko seli kwa kuambukizwa kwa njia yeyote ile.

HUWEZI KUPATA SIKO SELI KWA KULA, KUCHEZA AU KULALA NA MTU MWENYE SIKO SELI.

Dr. Fadhili Emily

Matibabu
Lengo la matibabu ni kupunguza madhara ama dalili zitokanazo na ugonjwa huu kama vile kutibu na kuzuia maumivu , kuzuiamaambukizi ya vimelea vya ugonjwa ,upungufu wa damu ,kiharusi nk.
• Hakuna tiba moja mahususi kwa wagonjwa wa siko seli hivyo matibabu hutofautiana kutokana na dalili za mgonjwa mfano; kuongezwa damu au maji mwilini na dawa za maumivu.

Je kuna tiba ya siko seli?
Hadi leo tiba pekee ya ugonjwa huu ni kupandikizwa kiini kwenye shina la mfupa kitaalam BONE MARROW TRANSPLANT.

• Tiba hii hufanywa kwa kuchukua urojo wa mifupa kutoka kwa mtu asiye na siko seli (donor) na kupandikiza kwenye mifupa ya mgonjwa hivyo husaidia mifupa yake kuzalisha chembe za damu zilizo nzima.

• Kwa upande mwengine tiba hii,pamoja na kutokupatikana katika nchi nyingi ikiwemo Tanzania, ni hatarishi na husababisha madhara makubwa kwa wagonjwa na mara nyingine hata kifo.

Dalili
Dalili za kuwa na maradhi haya ni homa, maumivu ya kifua, kupumua harakaharaka, uchovu, kuvimba kwa tumbo au sehemu za chini yake, kupoteza nguvu na macho kukosa nuru ya kuona vizuri.

Tiba na ushauri
Ukiona dalili kama hizi zinakutokea mara kwa mara muone daktari mara moja ambaye atakupima damu yako kubainisha iwapo una huo ugonjwa na atakupa matibabu.
Daktari wako atakupa ushauri, atakupatia dawa pia atakupa ushauri wa vyakula ambavo utakuwa ukitumia hasa mboga za majani kwa wingi,samaki,dagaa maziwa na matunda ambayo yatakusaidia kwa kiasi ili tatizo hilo lisikudhuru kwa kiasi kikubwa.
Wapo watu wanaishi muda mrefu bila kusumbuliwa na tatizo la kupungukiwa na damu kwa sababu wanazingatia masharti.
Ugonjwa wa upungufu wa damu mwilini ni hatari sana hivyo inapaswa wanaosumbuliwa na maradhi hayo kuzingatia masharti ikiwa ni pamoja na kula vyakula vinavyoongeza damu hasa mboga za majani.
Aidha, watumie dawa za kuongeza damu watakazoshauriwa na madaktari wao.

0 comments:

Post a Comment