Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, June 29, 2014

KWANINI MWANAMKE ASHIKI MIMBA?

MWANAMKE kutoshika mimba kumegawanyika katika makundi makubwa mawili. Kwanza ni hali iitwayo ‘primary Infertility’ ambapo mwanamke hana historia ya kupata ujauzito. Pili kuna hali iitwayo ‘Sekondari Infertility’, hapa mwanamke anayo historia kama alishawahi kupata ujauzito haijalishi kama alizaa au alitoa au iliharibika.Matatizo ya kutoshika mimba kwa mwanamke kitaalamu tunaita ‘infertility’ au ugumba.Kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na...

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKULETEA UKWELI KUHUSU UGONJWA WA SIKO SELI (SICKLE CELL)

Siko seli ni nini? Siko seli ni ugonjwa wa kurithi unaosababisha mabadiliko yasiyo ya kawaida katika chembechembe nyekundu za damu. • Kwa kawaida chembe nyekundu za damu zina umbo la mviringo ambalo huzirahisishia kupita kwenye mishipa midogo ya damuili kusafirisha hewa safi ya oxygen katika sehemu mbali mbali za mwili. • Kwa mtu mwenye ugonjwa wa siko seli chembe hizi huwa tofauti, zinanata na zina umbo la mwezi mchanga (siko). • Tanzania ni moja...

Friday, June 27, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAKUPA ELIMU YA KUTOKWA NA MAJIMAJI KWENYE MATITI (GALACTORRHEA)

Tatizo hili husimama lenyewe kama ugonjwa ingawa pia inaweza kuwa ni dalili kama mwanamke ni mjamzito, ananyonyesha au ametoa mimba au ameharibikiwa na mimba.Kusimama kwake kama ugonjwa ni pale yanapotoka wakati mwanamke hana historia ya dalili hizo hapo juu. Tatizo hili huwapata wanawake wengi na kwa mujibu wa takwimu huathiri asilimia tano hadi 32 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa.Pamoja na kuwapata zaidi wanawake, hali ya kutokwa na majimaji...

Wednesday, June 18, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAPENDA KUKUFAHAMISHA AINA ZA KIHARUSI (STROKE) SEHEMU YA PILI

WIKI iliyopita tulielezea ugonjwa wa kiharusi na aina zake na tukafafanua kwa nini unawapata watu. Endelea kuelimika. Iwapo mgonjwa ataathirika sehemu ya ubongo kwenye shingo kuelekea kwenye uti wa mgongo (brainstem), mgonjwa anaweza kuwa na dalili za kuhisi mabadiliko ya harufu, ladha, kusikia na kuona, kulegea kwa misuli ya macho (ptosis), kupungua kwa ufahamu na kulegea kwa misuli ya uso, ulegevu wa ulimi (kushindwa kutoa nje au kusogeza upande...

Friday, June 13, 2014

THE FADHAGET INAPENDA KUKUPA DALILI ZA SARATANI YA KIZAZI SIKU YA LEO

Saratani ya kansa huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au ‘Endometrial Carcinoma. Saratani ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi ‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata tumbo kuvimba. Saratani hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila...

Tuesday, June 10, 2014

FAHAMU AINA ZA KIHARUSI (STROKE)

Kiharusi au kwa Kiingereza Stroke ni kitendo cha baadhi ya viungo vya mwili kuwa na ganzi au kutojiweza kufanya kazi zake za kawaida.Kuna aina mbili za kiharusi, lakini kabla ya kuchambua hayo tuangalie, ni nini kinasababisha mtu kukumbwa na ugonjwa huu? Mtu anaweza kupata dalili za ugonjwa huu wa kiharusi na baada ya dakika chake zikaisha. Kiharusi kinampata binadamu baada ya eneo la ubongo kukosa damu kwa saa 24 ama zaidi au kunapotokea kizuizi...

WANAWAKE WANAVYO-SHAMBULIWA NA U.T.I

U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra) Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection. Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu...

Monday, June 2, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAPENDA KUKUPA BAADHI YA SABABU ZA MWANAMKE KUSHINDWA KUPATA UJAUZITO

Moja ya matatizo yaliyoko katika jamii zetu na yamesababisha wanandoa wengi au wanawake wengi kukosa furaha, ni kukosa uwezo wa kupata ujauzito kwa mwanamke. Sote tunafahamu kuwa, swala la mwanamke kupata ujauzito linahusisha pande zote mbili, yaani upande wa mwanamke na pia upande wa mwanamme, wote wawili wanapokuwa katika afya nzuri ndipo ujauzito unaweza kupatikana kwa mwanamke. Miongoni mwa sababu zinazoweza kumfanya mwanamke ashindwe kupata...