Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, July 8, 2015

Mtanzania mwenzangu, Tambua Matunda na Faida Zake.

The Fadhaget Sanitarium Clinic ikiongizwa na Dk. Fadhili Emily inapenda kukujuza kidogo faida za matunda mwili mwako. Karibu


Dk. Fadhili Emily

AFRIKA imejaaliwa mimea, madini, rutuba na hali ya hewa safi, ikiwa ni urithi tangu enzi na enzi. Pamoja na bara hili kujaa vyakula vyote vinavyohitajika na wanadamu, bado uhai wa watu wake wengi ni mfupi.

Katika orodha ya wastani wa maisha iliyowahi kutolewa na Shirika la Ujasusi Marekani (CIA) na Umoja wa Mataifa (UN) mwaka 2011, nchi zinazoongoza kwa maisha marefu ni Japan. Wajapani wanaishi hadi miaka 90 na kuendelea, Ulaya, Marekani na China kati ya 75 hadi 90, nchi za bara Asia mathalan India wanaishi miaka 65 na Tanzania ikiwekwa katika wastani wa miaka 50 hadi 53.
Wajapani wanasifika kwa kula vyema, hawali vyakula vyenye mapishi ya mambo mengi, ulaji wao ni mdogo mdogo, wa mara kwa mara, hawajazi sana matumbo na siri yao kubwa ni ulaji wa vyakula ambavyo husaidia kukarabati na kuhifadhi mwili, ikiwemo mimea ya baharini. Mmea mkubwa ambao Wajapani uhutumia unaitwa Kombu ambao unachemshwa na kutumia maji yake kwa kupikia mchuzi, chai na uji.

Moja ya faida ya Kombu ni kukinga na kuuponyesha mwili kutokana na maradhi, kuongeza nguvu za nywele, ngozi na maisha na ndiyo sababu hasa wataalamu wanaeleza kuwa ni nadra kumwona Mjapani asiyekuwa na nywele nyingi.

Vitu vinavyosaidia mwili
Mbegu mbichi za maboga zina faida sana mwilini; kwa kutoa mafuta asilia yasiyodhuru moyo, kutoa kinga ya maradhi, ujenzi na kukarabati ngozi, mifupa, kucha, nywele, kuupa mwili nguvu za rijali. Kiafya kila mtu anatakiwa ale matunda ya aina tano kwa siku ili kupata faida zote mwilini. Matunda humeng’enywa kwa vimeng’enyo tofauti na vyakula mama kama wanga na protini. Faida kuu za matunda ni kuzuia maradhi, kurutubisha, kinga ya mwili, sukari, nguvu na mafuta asilia. Faida nyingine ni madini na vitamini mbalimbali yanayosaidia kujenga, kukarabati na hata kuzuia bakteria na maadui wakubwa wakubwa wa miili.

Cherry
Tunda la ‘Cherry’ hupendwa sana na ndege na lina faida nyingi ambazo husaidia kupambana na maradhi yanayosakama damu au mzungunguko wa maji mwilini kama Jongo. Jongo ni ugonjwa unatokana na kurithi, kunywa sana pombe, ulaji wa nyama nyekundu, mayai, kutofanya mazoezi. Ni muhimu kuzingatia kwamba matunda yanatakiwa kuliwa yakiwa katika kitengo kimoja yaani chachu, asidi au alkali.

Matunda yenye chachu ni embe, nanasi, chungwa, zabibu na kiwi na kwa upande wa matunda yenye alkali ni tikiti maji, ndizi mbivu, tufaha, pera na strawberry. Faida za matunda haya ni kinga ya magonjwa. Husaidia kukinga na kupambana na takataka zinazotolewa na mwili au zinazotoka katika mazingira machafu. Vitamin C ni muhimu sana mwilini kwani ukosefu wake husababisha uchovu, kukosa usingizi, uvivu, kutokuwa na hamu ya kula.

Ukila matunda yenye vitamin C unapata kinga ya majeraha mwilini, vidonda hupona haraka, huboresha wajihi, haiba na nafsi ya ngozi, mifupa, meno na mzunguko mzima wa damu mwilini, hivyo kusaidia usingizi na kwa watoto kusaidia kukua vizuri. Lakini kwa tunda kama papai linasaidia kuukinga mwili na kulainisha tumbo ndiyo maana kama mtu amevimbiwa au haendi haja kubwa sawasawa, akila papai humsaidia.

0 comments:

Post a Comment