Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, May 9, 2012



"GET TOGETHER PARTY" YAFANA NDANI YA THE ATRIUMS HOTEL USIKU WA JANA
Dokta wenu nilibahatika kufika mahali pale kushirikiana na wenzangu katoika kuhakikisha shughuli ya mtangazaji wetu Erick Brighton inakamilika

Nilifurahi sana kukutana na watu amba sijawahi kukutana nao, na niliweza kubadilishana mawazo na kutiana moyo katika kazi ya BWANA.

Uimbaji na vichekesho vilinifanya nifurahi sana, na nikajifunza kuwa palipo wengi hukosi jambo la kukuburudisha na kukukasilisha, ila kwangu usiku huyo ulikkuwa wa furaha ndani ya kiroho changu

Mungu na akubariki

Blogger Rulea Sanga na mwanakamati ya party hiyo alikuwa na haya ya kusema kuhusu party

"Usiku ulikuwa ni usiku wa furaha na kumtukuza Mungu, Erick Brighton ndiye mlengwa mkubwa katika party ya jana ambaye aliwakusanya watu kwaajili ya kuwakutanisha maproducer, waimbaji, watangazaji wa radio na TV, mabloggers na wachekeshaji, na kubwa zaidi ilikuwa ni siku ya kumchangia Erick katika harusi yake itayofanyika karibuni.

Burudani mabalimbali kutoka kwa waimbaji zilitawala zikiambatanishwa na vichekesho kutoka kwa wachekeshaji kama Masanja Mkandamizaji na Nyerere.

Kamati inawashukuru watu wote waliohudhuria mahali pale na Mungu awabariki, na msingi zaidi ni kuwasisitiza kwa wale walioahidi michango yao waiwakilishe kwa wahusika kabla ya jambo lenyewe la harusi"

 Mchekeshaji, Msanja Mkandamizaji (kushoto kwa hao waliosimama) akikandamiza na mdau wa blogu hii.
 Fadhili wa Fadhaget Santarium Clinic (kushoto) akiwa katika pozi na Mkandamizaji Masanja
 Mzee wa Blogu, Rulea Sanga (kulia) nikijipendekeza kwa mtalaamu wa magonjwa sugu Fadhili wa Fadhaget Santarium Clinic

Kike inapukutika
Mtangazaji wa Praise Power Erick Brighton katikati akijiandaa kuwalisha kike wapenzi wake


0 comments:

Post a Comment