
Wanawake wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara hupata athari nyingi baadaye endapo kama hawatagundua chanzo cha maumivu hayo.
Katika tumbo la mwanamke kuna mfumo wa kawaida wa tumbo ambao ni tumbo la chakula na mfuko wa haja kubwa, kuna kibofu cha mkojo na mfumo wa mkojo.
Pia kuna mfumo wa uzazi ambao ndiyo tunaozungumzia leo kwa undani.
Mfumo wa chakula una matatizo yake mengi ambayo huambatana na kichefuchefu...