Khalid Kangezi akitoa ufafanuzi mbele ya wanahabri (hawapo pichani).
…Akiwa na mwanaye Adam Kangezi (kushoto).
.
…Akiendelea kutoa ufafanuzi.
Wanahabari wakifuatilia tukio hilo
ALIYEKUWA mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Khalid Ahmada Kangezi amekanusha taarifa iliyotolewa na viongozi wa chama chicho kwamba alitaka kumuua bosi wake, Dk. Wilbroad Slaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, alisema siku ya kifo cha marehemu Kapteni John Komba alikuwa akitokea nyumbani kwake Mwenge akielekea kazini nyumbani kwa Dk. Slaa ambapo baada ya kufika getini aliambiwa na mlinzi wa geti hilo kuwa haruhusiwi kuingia ndani na alipouliza sababu alijibiwa kuwa taarifa imetoka kwa mke wa Dk. Slaa.
Alipoendelea kuhoji alipewa majibu kwamba hapaswi kuendelea kumuuliza maswali ndipo aliamua kurudi tena nyumbani kujipanga kwa siku ambayo ingefuatia huku akiendelea kufanya juhudi za kumpata Dr. Slaa ili aweze kumuuliza sababu kuu ya kuzuiwa kuingia ndani.
Siku iliyofuatia ambayo ilikuwa Jumatatu ambapo Komba alikuwa anatakiwa kuagwa rasmi, alidamka asubuhi na mapema kuelekea nyumbani kwa Dk. Slaa kwani alijua kuwa naye angetakiwa kuungana na viongozi wengine kuuaga mwili wa marehemu. Kwa bahati nzuri alifanikiwa kumkuta nyumbani japokuwa alizuiwa tena kuingia ndani ila majibu aliyopewa na Slaa ni kuwa aongee na mkewe wamalizane mgogoro wao na yeye akasema hakutaka kuingilia mgogoro huo.
Kangezi aliongeza kuwa hakutarajia kama mke wa Slaa angekuwa na mgogoro naye kwani walikuwa wakiitana mtu na kaka yake kwa vile wanatoka Mkoa wa Kagera.
Kangezi aliendelea kuelezea kuwa hakuamini kama kweli angeweza kufungiwa nje ya geti la nyumba kutokana na jinsi alivyokuwa akihangaika katika kuhakikisha ulinzi wa Dk. Slaa kwa nguvu ya hali ya juu kutokana na masuala ya vyama na ameishi naye kwa muda wa zaidi ya miaka 14 bila shida wala tuhuma yoyote.
Baada ya kukosa maelewano nyumbani kwa Dk. Slaa, aliamua kwenda katika ofisi za chama hicho zilizoko Kinondoni kwa ajili ya kuonana na kiongozi wake ambapo baada ya kufika alidai alizuiwa na viongozi wa chama hicho tena wakimtaka kuingia katika chumba maalumu kwa ajili ya kuchukua mahojiano naye ambapo alifanya kama alivyotakiwa.
Aliwataja viongozi wa chama hicho aliowakuta humo ambao tayari walimwamuru kuvua nguo zake zote na kubakia kama alivyozaliwa huku akitishiwa kuuawa. Humo alitakiwa kueleza mahusianao yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Philip Mangula, na watu wa usalama wa taifa ambapo alisema alisulubiwa kwa muda wa saa sita na akitakiwa kuandika katika karatasi kukiri kuwa kweli anawasiliana nao na kutokana na kipigo alichokuwa akikipata, akihofia kuuawa, aliamua kutii matakwa yao.
Siku hiyohiyo majira ya usiku alipelekwa katika hoteli iliyoko maeneo ya Sinza–Madukani ambapo alipakizwa katika gari lililokuwemo mwanasheria wa chama chicho, Mabere Malando, hadi kwenye hoteli waliyokuwa wamechukua vyumba na kumwingiza ndani ambako walianza tena kumsulubu hadi akaishiwa nguvu na akitakiwa tena aandike kuwa alikuwa na mpango wa kumdhuru Dk. Slaa kwa kumpa sumu,
Kutokana na uchovu aliokuwa nao aliamua kukiri kufanya hivyo huku akirekodiwa.
Alimalizia kwa kusema kuwa hajawahi kufanya jambo lolote la kutaka kumdhuru Slaa, na hata kiasi cha fedha kilichotajwa kuingiziwa na watu wa usalama wa taifa si kweli na hawezi kutunza fedha katika simu. Alieleza pia kwamba amefanya mambo mengi kwa Dk. Slaa na hivyo hawezi kumdhuru licha ya kufahamu siri zake nyingi.
(PICHA /STORI NA DENIS MTIMA/GPL)
0 comments:
Post a Comment