Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paulo Makonda akimhoji fundi bomba wa Hospitali ya TMJ, Mansool Mramba kuhusiana na hospitali hiyo kutiririsha majitaka.
Makonda (katikati) akiangalia moja ya mitaro huku akishuhudiwa na Muhandishi wa Barabara wa Manispaa ya Kinondoni, Ismail Mafita.
Makonda akiangalia majitaka yanayonititirishwa na Hospitali ya TMJ.
…akiangalia uchafu uliotupwa ndani ya makaravati ambayo yamejengwa kwa fedha nyingi za serikali.
Makonda akisalimiana na mmoja wa viongozi wa serikali, Tawi la Bonde la Mpunga.
Makonda akiangalia moja ya chemba ya majitaka iliyojengwa sehemu isiyohusika katika Barabara ya Chwako ambayo ujenzi wake bado haujakamilika.
Mkuu wa Wila ya Kinondoni, Paul Makonda, leo amefanya ziara ya kukagua barabara na Miundombinu eneo la Msasani ambalo limekuwa likikumbwa na mafuriko wakati wa mvua za masika na kusababisha maafa kwa wakazi wake.
Wakati wa ziara hiyo iliyojumuisha Wahandisi wa Barabara wa Manispaa ya Kinondoni, Ismail Mafia na Baraka Mkuya ameupata siku saba uongozi wa Hospitali ya TMJ kuanzia leo ubadili mfumo wa kupitisha majitaka unaotiririsha maji hayo sehemu isiyohusika vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Makonda aliyefanya ziara hiyo ya kukagua barabara na miundo mbinu ili kujiepusha na mafuriko yanayotokea katika eneo hilo, akiwa ameambatana na Theophile Kileo ambaye ni Mwandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) LTD, inayojenga barabara na miundo mbinu alikagua ujenzi huo na kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanaotupa uchafu kwenye mitaro hiyo na kusababisha maji kutwama.
Mkuu huyo wa wilaya amewataka wakazi wa eneo hilo kuacha kufanya hivyo kwa sababu serikali inatumia fedha nyingi kuijenga miundombinu hiyo na kusema mafuriko yatakapokuja watakaokuwa katika wakati mgumu ni wao.
Aidha, aliutaka uongozi wa serikali ya Mtaa, Tawi Bonde la Mpunga Kata ya Msasani kuhakikisha inapambana na watu wote wanaochafua mazingira hususan kutupa takakata kwenye mitaro. (HABARI/ PICHA NA KULWA MWAIBALE/GPL)
0 comments:
Post a Comment