Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, March 3, 2015

MAGONJWA YA ZINAA YANAYOSABABISHA KUZIBA KWA MRIJA WA MKOJO-2




Dalili, mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo, kwa mwanaume hutokwa na manii zilizochanganyika na damu, kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu, kutoa mkojo kidogo sana tena kwa shida, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote.
Wengine huona dalili za mkojo kujitokea wenyewe, hivyo mhusika kujikojolea, kusikia maumivu wakati wa kukojoa au chini ya tumbo au kwenye kinena, mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa na uume kuvimba.
Daktari akiona moja ya dalili hizo mgonjwa anaweza kuchunguzwa kwa vipimo tofauti kama vile kile cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy), kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya mkojo kutoka, X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram) atapimwa kama ana magonjwa ya zinaa kwa kumfanyia uchunguzi wa mkojo (Urinalysis) pamoja na kuotesha mkojo (Urine culture).
TIBA
Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo mojawapo ya tiba au dawa pekee ya uhakika ni mgonjwa kufanyiwa upasuaji ambao unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo.
Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena hufanyika.
Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye bomba lililowekwa chini ya tumbo.

USHAURI

Mgonjwa mwenye tatizo hili atibiwe haraka maana tatizo likiachwa linaweza kusababisha kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo kushindwa kufanya kazi.
Watu wajikinge na magonjwa ya zinaa ambayo yanasababisha tatizo hili, wawe makini na kazi zinazoweza kusababisha kuumia sehemu nyeti na kuzalisha tatizo hili.

0 comments:

Post a Comment