Na Makongoro Oging’
Baadhi ya waathirika wa madawa ya kulevya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam ambao kwa sasa wameachana na matumizi ya madawa hayo walimtaja mchungaji wa kanisa moja (jina linahifadhiwa) ambaye alikamatwa na serikali na kwa sasa kesi yake inanguruma Mahakama Kuu jijini hapa.
Baadhi ya waathirika wa madawa ya kulevya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam ambao kwa sasa wameachana na matumizi ya madawa hayo walimtaja mchungaji wa kanisa moja (jina linahifadhiwa) ambaye alikamatwa na serikali na kwa sasa kesi yake inanguruma Mahakama Kuu jijini hapa.
Waathirika hao ambao wako katika kikundi chao kijulikanacho kwa jina
la Wanamati, walimueleza mwandishi wetu wiki iliyopita kuwa mchungaji
huyo lazima abebe lawama zao kwa kuwa alikuwa akiwasambazia madawa hayo
yaliyowafanya waathirike.
Waathirika ambao wapo zaidi ya 500 waliyasema hayo mara baada ya
kumaliza kikao chao ambacho kilikuwa kikijadili jinsi ya kujikwamua
baada ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.Waathirika hao ambao
hawakupenda majina yao yatajwe gazetini kwa sababu za kiusalama,
walisema mchungaji huyo alikuwa akiwauzia madawa hayo mitaani kwa
kuwatumia mawakala wake ndipo polisi waliamua kumfuatilia na kumkamata
na kwa sasa ana kesi Mahakama Kuu.
Hata hivyo, waathirika hao wameiomba serikali na taasisi mbalimbali
kuwasaidia kimaendeleo kupitia kikundi chao hicho kwa kuwa wameachana na
utumiaji wa ‘unga’ na wangependa wajitegemee kwa kufanya shughuli za
kuzalishaji mali.
Waathirika hao ambao wengi wao wamesema kwa nyakati tofauti kuwa
wamekuwa wakitumia unga kati ya miaka mitano hadi ishirini na kwamba
jamii isiwachukie kwa maana na wao walirubuniwa bila kujua madhara
ambayo wangeweza kuyapata lakini kwa sasa wako vizuri kwani wamekuwa
wakihudhuria kliniki katika Hospitali ya Temeke, Dar.
Wameiomba serikali iendelee kuwapatia dawa za kutibu utumiaji wa
madawa kwa kipindi chote cha miaka miwili wanayotakiwa kutumia ili
waweze kurejea katika hali yao ya zamani.Mwenyekiti wa kikundi hicho,
Said Ismail Ngindo alisema kwamba wameamua kuungana kwa pamoja ili
waweze kufanya shughuli za maendeleo baada ya kuachana na madawa na
wameiomba serikali iwasaide ili wajikwamue kiuchumi.
“Asilimia kubwa ya wanachama wa kikundi hiki hawana ajira…ni kazi
ngumu sana kukaa bila kuwa na kipato, hapa kuna akina mama ambao
wamezalishwa kipindi hicho wakiwa watumiaji wa madawa mitaani, sasa
wanapata shida kubwa ya kuwalea watoto wao, hivyo kunahitajika msaada
mkubwa, “ alisema mwenyekiti huyo.
Taarifa iliyopatikana ndani ya kikundi hicho inasema kwamba imefikia
hatua ya viongozi wa kikundi walioteuliwa na uongozi wa Hospitali ya
Wilaya ya Temeke kuwasimamia wenzao lakini wao wamewachagua viongozi
wao ili wawe wakiheshimika zaidi na wana kikundi.
0 comments:
Post a Comment