Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura, Simon Sayore, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Mhandisi, Mutaekulwa Mutegeki.
Wadau mbalimbli wakiwa katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mmoja wa wadau wa mkutano huo akichangia hoja.
Wadau wakisiliza hoja za mjumbe aliyekuwa akichangia hayupo pichani pamoja na viongozi wengine waalikwa.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Maji Safi na Maji Taka (EWURA), leo imekutana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) pamoja na Dawasco juu ya kujadili ombi lililotolewa na Dawasa la pendekezo la kupandisha bei ya maji.
Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick huku ukihusisha wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti.
Akizungumza katika mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mhandisi, Mutoekulwa Mutegeki, alisema kuwa, Ewura ilianzishwa chini ya Sheria ya EWURA sura namba 414 ya sheria ya Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2006 kwa madhumuni ya kuhakikisha huduma za maji, umeme, gesi na mafuta zinaimarika kwa kusimamia ubora na bei ya huduma kwa wadau wote na taifa kwa ujumla.
Mutegeki alisema kuwa mkutano huo ni sehemu ya uchunguzi unaofanywa na Ewura kupata maoni ya wadau wa huduma ya maji safi na maji taka kabla ya kutoa maamuzi kuhusu maombi yaliyowasilishwa na DAWASA ya kurekebisha bei za huduma za maji.
Mutegeki aliweza kutoa fursa kwa wadau wote walioweza kufika ukumbini hapo kutoa michango yao ya mawazo juu ya kupandisha ama kupunguza bei kutokana na huduma zinazotolewa na mashirika hayo hivyo mapendekezo hayo yatachukukuliwa kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Aidha kwa upande wa DAWASA, wameiomba EWURA kurekebisha bei za huduma zao kwa makundi yote ya wateja wao na kutaka marekebisho hayo kufanyika kwa kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka wa fedha 2014/15 hadi mwaka wa fedha wa 2015/16.
Na Denis Mtima/ GPL
0 comments:
Post a Comment