Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kusisaidia Hospitali hiyo. Kutoka kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT, Erwin Telemans na Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (wa pili kushoto), akibadilishana hati na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Hospitali ya CCBRT baada ya kutiliana saini mkataba wa kusaidi matibabu ya ulemavu wa miguu Dar es Salaam jana. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Mifupa wa Hospitali hiyo, Prosper Alute na Meneja Uwajibikaji kwa Jamii, Woinde Shisael.
Joyce Moshi akiwa amembeba mtoto wake Gedion ambaye anatibiwa katika Hospitali hiyo kutokana na miguu yake kupinda ambapo sasa anaendelea vizuri.
Na Dotto Mwaibale
HOSPITALI ya CCBRT, imepokea dola 150,000
(zaidi ya sh. mil. 320) kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kwa
ajili ya kugharamia matibabu ya watototo wanaozaliwa na ulemavu wa nyayo
zilizopinda kwa miaka mitatu ijayo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Meneja
Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez alisema hiyo si mara ya kwanza kwa kampuni
hiyo kugharamia matibabu ya walewavu kwani miaka mitatu iliyopita pia
waligharamia matibabu ya watoto wenye ulemavu wa midomo.
"Tuna amini watoto wenye ulemavu wa
unyayo uliopinda watapatiwa matibabu mapema, hivyo tunaomba wazazi wenye
watoto wao wanaozaliwa na ulemavu huo kujitokeza CCBRT kupatiwa
matibabu kwani ni bure na kwa mwaka tunatoa dola 500," alisema
Gutierrez.
Kwa upande wa Daktari wa Mifupa wa
hospitali hiyo, Prosper Alute akizungumzia ugonjwa huo, alisema
unasababishwa na kurithi kutoka kwa wazazi au ndugu na kunywa pombe
kupindukia au kutumia dawa zenye viambata kali.
Alisema asilimia 50 ya watoto wanaozaliwa
hupata ugonjwa huo kwa miguu yote ambapo tangu kuingia kwa mwaka huu
hadi Aprili, watoto 117 wamegundulika kuwa na ugonjwa huo ambao ni sawa
na wastani wa watoto 10 kwa wiki.
Alisema ugonjwa huo usipotibiwa kwa haraka unaweza kumsababishia mtoto kutembea kwa shida na wakati mwingine kutotembea kabisa.
Kwa upande wa Joyce Mosha, Mkazi wa
Mwenge, ni mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake, Gidion ana miezi miwili
alikutwa na tatizo hilo na kufanyiwa upasuaji, alisema mara baada ya
kujifungua madaktari waligundua mtoto wake kuwa na tatizo hilo, hivyo
waliamua aanze kupatiwa matibabu.
"Namshukuru Mungu alifanyiwa upasuaji
mdogo na hivi sasa anaendelea vizuri, alipogunduliwa ana tatizo hilo
kwanza walimfunga plasta ngumu (POP) kwa wiki tano na kisha kumfanyia
upasuaji mdogo wa mfupa na kumpa viatu maalumu vya kuvaa na vingine huwa
anavaa usiku tu wakati wa kulala," alitoa ushuhuda Joyce.
0 comments:
Post a Comment