SEHEMU YA KWANZA
Mtu ambaye ana tatizo la kutoshika mimba kitaalamu tunasema Infertility na kushindwa kupata mimba kwao huitwa Conceive. Kwa kawaida kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanandoa asilimia 50 wanapata mimba ikiwa watajamiiana bila kutumia kinga wakifanya tendo hilo ndani ya miezi mitatu na asilimia 75 baada ya miezi sita na asilimia 95 baada ya mwaka mmoja.

Sababu za tatizo la kutopata mimba ni nyingi sana na baadhi yake ni
hizi zifuatazo. Matatizo ya mbegu za kiume (Sperm disorders). Asilimia
35 ya wanaume wana tatizo hili na lingine ni kutopevuka kwa mayai kwa
wanawake yaani kitaalamu huitwa Ovalatory dysfunction, asilimia 20.
Matatizo mengine ni yale yasiyo ya kawaida ya ute wa shingo ya uzazi
ambapo ni asilimia 5 tu, wengine huwa na matatizo ya homoni na wapo
ambao hawapati mimba na sababu zao hazijulikani ni asilimia 10, wengine
ni kutokana na kuwa na msongo wa mawazo na wasiwasi.
Tatizo lingine la kutoshika mimba husababishwa na hitilafu katika
mirija ya uzazi (tubal dysfunction), hawa huwa asilimia 30. Sababu zote
hizi nitaeleza moja moja kwa kirefu katika matoleo yetu yajayo lakini
wote wenye tatizo hili wanashauriwa kuhudhuria kliniki za akina mama ili
waonane na madaktari.
Lakini pia wanashauriwa kufuatilia siku zao za mzunguko wa hedhi na
tendo la ndoa mara kwa mara hasa baada ya siku 10 kutoka siku anamaliza
hedhi na aanzie siku ya kwanza ya kupata hedhi. Ushauri Wanawake
wanashauriwa wawe wanapima joto la mwili asubuhi na jioni kipindi cha
kushika mimba na kama litaongezeka kwa nyuzi joto 0.5 wanashauriwa
kipindi hicho kufanya tendo la ndoa.
Kwa nchi za Ulaya na Marekani wana kipimo cha kuonesha siku ambayo
yai litapevuka, hivyo mtu kuwa na uhakika na siku ya kupata mimba
akiamua.
Kipimo hicho kinaitwa Luteinizing hormone prediction test kits.
Wanawake wanaotaka kupata mimba wanashauriwa kuepuka ulevi na uvutaji wa
sigara wa kupindukia. Lakini hata wale wenye mimba wanashauriwa kuepuka
vitu hivyo.
SEHEMU YA PILI
Tatizo la mwanamke kutoshika mimba limegawanyika katika makundi mawili, la kwanza huitwa kitaalamu ‘primary Infertility’.
SEHEMU YA PILI
Tatizo la mwanamke kutoshika mimba limegawanyika katika makundi mawili, la kwanza huitwa kitaalamu ‘primary Infertility’.
Kundi hili ni lile ambao mwanamke huwa hajawahi kushika mimba hata
siku moja na kundi la pili huitwa ‘Secondary Infertility’, hili ni lile
la wanawake ambao wamewahi kushika mimba wakajifungua au mimba
zikaharibika.
Zipo sababu nyingi sana zinazofanya mwanamke asiweze kushika mimba
kama vile kupata maambukizi katika viungo vya uzazi, hali duni ya lishe
na kukumbwa na magonjwa sugu.
Wanawake wengine wanakuwa na matatizo yanayohusu upevushaji wa mayai
ambayo kitaalamu huitwa ‘Ovulatory’. Tatizo hili huathiri wanawake kwa
kiasi kikubwa ambapo mwanamke anapata siku zake kama kawaida lakini
hapevushi mayai.
Hali hiyo husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini.
Hali hiyo husababishwa na matatizo katika mfumo wa homoni mwilini, tatizo linaweza kutokea lenyewe kutokana na mabadiliko ya mwilini.
Lakini pia tatizo hilo linaweza kujitokeza kutokana na matumizi
yanayohusiana na dawa za homoni kutumika kiholela bila kupata ushauri wa
daktari na ndiyo maana tunasisitiza kuwa si vema kunywa dawa bila
kushauriwa na daktari.
Wanawake wengine wanaweza kushindwa kupata mimba kutokana na matumizi ya baadhi ya vyakula au vipodozi vyenye kemikali.
Ieleweke kwamba wanawake wanaotaka kupata mimba wanakuwa na dalili za upevushaji wa mayai na kubwa ni kupata ute wa uzazi.
Daktari anaweza kuona upevushaji huo kwa kutumia vifaa maalumu ambavyo siku hizi hata mwanamke akiwa nyumbani anaweza kupima mkojo siku unazohisi unaweza kupata mimba.

Matatizo mengine yanayosababisha mwanake asipate mimba ni kuwa na
matatizo kwenye mirija kwani inaweza kuziba, kutanuka au kuweka usaha au
maji. Maambukizi katika mirija au upasuaji wa mimba nje ya kizazi au
kufunga kizazi kunaweza kumfanya mwanamke asipate mimba.
Itaendelea wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment