Vyanzo vingi vya vimbe bado havijafahamika kitafiti lakini kuna baadhi ya vimbe vyanzo vyake vinajulikana na ni vema na wewe ukavitambua. Navyo ni;Polycystic ovarian syndromes Hizi ni zile vimbe ndogondogo nyingi zinazoweza kutokea kwenye kifuko cha mayai cha mwanamke, lakini nazo pia huweza kutokea katika pande zote mbili za vifuko vya mayai kwa mwanamke. Tafiti nyingi zinasema kwamba vyanzo bado havijapatikana lakini kuna baadhi ya tafiti zinasema kuwa;
Tatizo hili linakuwa ni la kurithi (genetic), yaani kwa maana kwamba ni tatizo lililopo kwenye familia labda bibi au mabibi walikuwa nalo na hivyo linamtokea na mtoto ambaye yuko kwenye familia hiyo, mtoto anakuwa na homoni nyingi za kiume ambazo husababisha kutokea kwa vimbe nyingi kwenye vifuko vya mayai na pia anakuwa na vinyweleo vingi, ndevu, pamoja na nywele za kifuani pia kutofautiana kwa hedhi yake na maumivu chini ya kitovu.
Fibroids au Mayoma
Ni vimbe zinazotokea katika mji wa mimba na hizi ndizo vimbe zinazowasumbua watu wengi sana katika jamii yetu ya sasa, nalo vyanzo vyake ni kama;
Tatizo hili nalo ni la kurithi (genetic), yaani hukaa katika familia na kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto au kutoka kwa bibi kwenda kwa mjukuu, na kuna uwezekano bibi alikuwa na tatizo hili lakini hakupatwa na tatizo la uzazi kwa sababu hakuwa na homoni ambazo huchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa vimbe (over growth) lakini mtoto akalipata kwa sababu anakuwa na homoni nyingi zichocheazo ukuaji wa vimbe.
MADHARA YA VIMBE
Madhara ya vimbe ni makubwa sana nayo ni kama;
Mwanamke kupoteza uwezo wake wa kushika ujauzito, na panapokuwa na hali hii basi kunakuwa na matatizo mengine mengi katika familia kama kusemwa hovyo, unakumbwa na msongo wa mawazo na kukosa raha.
Madhara mengine ni kuandamwa na maumivu makali chini ya kitovu ambayo yanakuwa ni endelevu na yanakufanya usiwe na amani katika kufanya kazi nyingine.
Madhara mengine yanakuwa ni kutokwa na uchafu ambao unakuwa ni endelevu na huu huwakosesha raha wanawake wengi kwani inakuwa ni hali tofauti kidogo na kawaida.
Itaendelea wiki ijayo.
0 comments:
Post a Comment