Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, January 14, 2015

JINSI YA KUPUNGUZA UNENE WA KUPINDUKIA-2


Tulieleza jinsi watu wenye vitambi au wanene wanavyopata shida na maradhi mbalimbali na wiki iliyopita tulieleza jinsi ya kupunguza unene, leo tunaendelea kuelekeza.

Anza kukimbia kwa kasi ndogo halafu ongeza kasi. Au unaweza kukimbia kwa kasi ya juu dakika 5 na kisha kupunguza hadi 3. Hii inaitwa interval training, yenye lengo la kukupa uwezo wa kufikisha dakika 30, kuchoma mafuta mwilini na kupunguza mapigo ya moyo ili yarudi kwenye kiwango cha kawaida.
Hii ni kwa sababu wakati unapofanya mazoezi mapigo ya moyo huongezeka sana na pia kuupa moyo wako uwezo wa kufanya kazi vizuri.

Fanya mazoezi ya tumbo (sit-ups) mara 15-20. Ikiona ni vigumu kwako unaweza kuanza hata kwa mara 10 na utakuwa unaongeza kadiri siku zinavyoenda na kadiri utavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu na tumbo.

Unaweza kutumia benchi au kulala sakafuni. Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups, kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4. Siyo lazima unywe yote kwa wakati mmoja. Unaweza ukawa unakunywa huku ukiendelea na mambo mengine mpaka bilauri 4 ziishe.

Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu. Limao na ndimu siyo tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini.
Mlo wa asubuhi (Breakfast): Kunywa kikombe kimoja cha kahawa au chai kwa kuweka kijiko kimoja kidogo cha sukari. Yai moja la kuchemsha na kipande kimoja cha mkate wa kahawia au ngano isiyokobolewa (brown bread).

Usithubutu kuweka siagi wala kitu kingine chenye mafuta na sukari nyingi. Kula matunda kadiri unavyoweza lakini epuka ndizi tamu.

Chakula cha mchana (Lunch): Kula robo kuku wa kuchoma au wa kuchemsha na si vinginevyo. Saladi au kachumbari ya mbogamboga tofauti lakini isiwe na sosi ya mayonnaise.
Kunywa maji ya uvuguvugu glasi 4 tena. Jitahidi kuepuka snacks au asusa, ice cream, chokoleti, biskuti na kadhalika. Jizoeshe kula matunda kwa wingi kila unapohisi njaa.
Jioni tembea au kimbia tena kwa muda wa nusu saa pamoja na kufanya mazoezi ya sit-ups wakati unasubiri chakula cha usiku.

Chakula cha usiku (Dinner): Kula supu ya samaki yoyote yule bakuli kubwa la kutosha. Unaweza kutumia karoti, nyanya au tungule, brokoli, cauliflower, pilipili mboga na za kuwasha, ndimu au limao, kitunguu maji na thomu na kadhalika, epuka viazi vyovyote vile kwenye supu.

Wiki ijayo tutaangazia namna ya kujua kiwango cha kalori za chakula zinazohitajika kuliwa kwa siku ili kudhibiti unene.

0 comments:

Post a Comment