Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, January 27, 2015

MAGOJWA YANAYOAMBATANA NA UNENE (OBESITY)-2



Magonjwa yanayo ambatana na unene tumekuwa tukiyajadili tangu wiki iliyopita, leo tunahitimisha mada hii. Kupungua uzito, kuudhibiti au kutunza uzito alionao mtu baada ya kupunguza uzito ni jambo la msingi mno na ni suala linalohusisha kufanya mazoezi, kula lishe bora na mabadiliko mengineyo kama ifuatavyo:-

1) Mabadiliko ya tabia, mtu mwenye unene wa kupindukia anapaswa kupunguza kiwango cha chakula anachokula lakini kiwe chenye virutubisho vyote muhimu kwa afya vinavyotakiwa ili kuustawisha mwili.

2) Suala lingine muhimu ni kuushughulisha mwili na kufanya mazoezi. Mazoezi husaidia kupunguza uzito hasa kipindi cha miezi sita ya mwanzo na kuufanya mwili uwe na uzito uliokusudiwa kwa muda mrefu.
Pia hupunguza mafuta ya mwilini, huongeza ufanisi wa moyo, hupunguza tatizo la shinikizo la damu (hypertension) na kuifanya sukari iwe katika kiwango kinachohitajika.

Kama hujazoea kufanya mazoezi, ni vizuri uanze taratibu na ujiwekee lengo kwa kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku, siku tano kwa wiki, (tunashauriwa kufanya mazoezi dakika 30 kila siku kwa siku tano kwa wiki).

Mazoezi mazuri ni kama kuogelea, kuendesha baiskeli, kutembea, kunyanyua vitu vizito lakini visiwe vyenye uzito mkubwa, mazoezi ya viungo na kadhalika.
Kama mtu ni mnene sana, basi ni bora azungumze na daktari wake kabla ya kuanza mazoezi mapya ili kuona ni mazoezi gani yaliyo salama kwa afya yake.

Baada ya kuanza mazoezi kwa mara ya kwanza, mwili hupata maumivu, hii ni hali ya kawaida lakini kama mtu atapata maumivu zaidi ya saa 2 na kuendelea baada ya kufanya mazoezi ni vizuri kumuona daktari.

3) Iwapo mabadiliko ya lishe na ufanyaji mazoezi hayatasaidia, wataalamu pia huwapatia dawa watu walio na unene wa kupita.

PICHA ZA TUKIO:KICHANGA CHA MIEZI MINNE CHAOKOA FAMILIA ISITEKETEE KWA MOTO

KICHANGA kinachokadiriwa kuwa na umri wa miezi nane, wiki iliyopita kiliiokoa familia yake kuteketea kwa moto, baada ya kuamka usiku na kulilia kunyonya, kitendo kilichomshtua mama yake aliyebaini nyumba yao ilikuwa ikiungua, huko Kibamba Lungwe jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya nyumba iliyoungua.

Akisimulia tukio hilo, mama wa kichanga hicho, Asha Mohamed, alisema alishtuka baada ya mtoto kuanza kulia akitaka kunyonya, alipoamka ndipo akaona mwanga mkali juu ya paa, hali iliyomlazimu kuamka na kwenda kumgongea Abuu ili kutafuta njia ya kutoka,” alisema mama huyo akiongeza kuwa sebuleni, moto ulikuwa umetapakaa.

Kijana Abuu Masoud (15), baada ya kuamshwa, alionyesha ujasiri na upendo mkubwa kwa kujitoa mhanga kuwasaidia wadogo zake watatu waliokuwa wamelala katika moja ya vyumba vya nyumba hiyo.
Baada ya kuingia katika chumba hicho, alifanikiwa kumtoa mtoto mmoja.






Watoto walionusulika kuteketea kwa moto.

“Nilipofungua mlango wa sebuleni nikaona moto na moshi mwingi sana, roho iliniuma sana kwani chumba cha pili kulikuwa na wadogo zangu watatu wamelala, nikaamua kuvaa ujasiri na kujitosa katika chumba kile na kufanikiwa kutoka na mtoto mmoja, wakabaki wawili,
baada ya kurudi ndani nikapata wazo la kuzima Mean switch, nilipoenda kuishika ikaniangukia kichwani kwani ilikuwa imeshaungua, ndiyo nikaungua na kushindwa kuwatoa waliobakia, ingawa baadaye kuna msamaria mwema mmoja alijitokeza na kuja kubomoa mlango na kuwatoa wengine,” alisema kijana huyo.




Kitanda walichokuwa wamelala.

Mama wa mtoto mchanga alifanikiwa kutoka pasipo kudhurika.
Aidha baba mwenye nyumba hiyo, Khalfani Maketemo, ambaye wakati nyumba yake inaungua yeye na mkewe walikuwa hospitali alikokuwa amelazwa, anadai chanzo cha moto huo ni shoti iliyoanzia kwenye bati na anaamini ni kutokana na kuunganishwa vibaya kwa waya unaopitisha umeme kutoka kwenye nguzo kwenda kwenye nyumba.

Wakizungumza na mwandishi wetu baadhi ya majirani walisema; “Uunganishwaji wa umeme ni wa kubabaisha, waya unagusana na bati jambo ambalo ni hatari kama waya utachubuka na mvua kunyesha’’.Familia hiyo kwa sasa haina sehemu ya kujisitiri nyumba nzima imeteketea.

OXFAM YATANGAZA MRADI KUPAMBANA NA EBOLA





Misaada ya kila hali bado inahitajika katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola Shirika la misaada Oxfam limetoa wito wa kutolewa kwa msaada wa thamani ya mamilioni ya dola kusaidia nchi za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na Ebola, mradi huu wa msaada unaitwa Marshall Plan Zaidi ya Watu 8,500 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola, wengi wao nchini Sierra Leone,Guinea na Liberia. Mradi wa Marshall ulitumika baada ya vita ya pili ya Dunia kwa ajili ya kuwanusuru waathirika barani Ulaya. Oxfam imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuridhia mpango wa utoaji misaada kutoka kwa nchi tajiri. Shirika hilo limesema msaada wa fedha unahitajika katika maeneo matatu-kuchangia pesa kwa Familia za waaathirika wa Ebola, kuwekeza katika kazi pia kusaidia kutoa elimu kuhusu maswala ya kiafya, elimu na usafi. Utafiti umebaini kuwa asilimia 60 ya Watu waishio kwenye meaeneo yaliyoathirika wanadai kuwa hawajapata chakula cha kutosha kwa kipindi cha juma moja lililopita sababu kubwa ikilezwa kuwa kushuka kwa kipato na kuoanda kwa gharama za chakula. Nayo Bank ya dunia imekisia kuwa takriban 180,000 wamepoteza kazi zao nchini Sierra Leone tangu kuanza kwa ugonjwa huo, huku wengine wanaotunza familia zao nchini Liberia nao wakipoteza ajira.

Monday, January 26, 2015

MWANAMKE AWAUA WATOTO WAKE WAWILI NA KUWAZIKA NDANI YA NYUMBA YAKE



Mwanamke mmoja mkazi wa mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini kata ya Chemchem amewaua watoto wake wawili na kuwazika ndani ya nyumba yake.
Mwanamke huyo amedai kuwa kilichomfanya awalishe sumu watoto wake ni ugumu wa maisha uliokuwa ukimkabili baada ya kukimbiwa na mumewe.


Kwa mujibu wa jirani yake, siku ya tukio mwanamke huyo alisikika akichimba shimbo ndani ya nyumba yake kabla ya kutangaza kupotelewa na watoto wake siku ya pili yake.

Taarifa ya kupotea kwa watoto hao ilimpa mashaka jirani huyo na kumlazimu akatoe taarifa polisi.

“UMASKINI WETU UMENIFANYA NIISHI KWA DAWA ZA KUPUNGUZA MAUMIVU”

Makongoro Oging’ na Issa Mnally, Kibaha/Uwazi
Janeth Mlahagwa (18) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi “Albino”, mkazi wa Kijiji cha Mtumbatu, Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro ambaye anadai kwamba kifo kilimsonga kutokana na hali yake kuwa mbaya kila kukicha kwa kukosa matibabu na badala yake alikua akipewa vidonge vya kupunguza  maumivu.

Janeth Mlahagwa akiwa na mama yake.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni katika hospitali binafsi ya upasuaji wa mifupa na viungo cha Burere, wilayani Kibaha kwa Mathias, Mkoa wa Pwani, Janeth alisema kwamba kutokana na umaskini wa wazazi wake ambao ni wakulima wa jembe la mkono alinazimika kupewa vidonge vya kutuliza maumivu ambavyo havijamsaidia.
Janeth ambaye amefuatana na mzazi wake katika hospitali hiyi ni mtoto wa kwanza kati ya watoto sita katika familia yao na watatu kati ya hao ni Albino.
ALIVYOKUTWA KIJIJINI
Akieleza zaidi alikuwa na haya ya kusema:
“ Namshukuru Mungu aliyempeleka Mkurugenzi wa Hospitali ya Berere, Dk. Joseph Theodore Bake ambaye alitembelea kijijini kwetu na kunikuta nikiwa katika hali mbaya naakanichukua kuja kunitibu hapa na ugonjwa umeshajulikana baada ya vipimo.

...Janeth akiwa amejipumzisha.
UVIMBE UNAOMTESA
 “Mateso ninayoyapata leo hii ni kwa sababu ya uvimbe katika shavu, ulianza kama kipele Julai, mwaka jana, baadaye kipele hicho kikaanza kuvimba.
“Mama akawa ananipeleka katika zahanati mbalimbali lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwani nilikuwa napewa dawa za kutuliza maumivu tu ambavyo havikunisaidia kunitibu.
UKATA ULIFANYA NISIPATE TIBA
“Bahati mbaya, ukata katika familia ulichangia mimi kuwa na hali mbaya kwani wazazi wangu hawakuwa na la kufanya kwa sababu hawakua na fedha za kunipeleka hospitali kubwa.“Baadaye wakawa wanajitokeza waganga wa kienyeji kuja kunitibia lakini familia ilikataa kwani wengi wao wanakua na nia mbaya, nilibakia kulia na kumuomba Mungu.
MUNGU ASIKIA MAOMBI
“Mungu alinisikia maombi yangu akawa amejitokeza Dk. Bake aliyekuja kijijini kwetu akaniona nimelala nje ya nyumba yetu huku nikilia kutokana na maumivu makali, alisimamisha gari lake na kuja kwangu kuniangalia.
“Baada ya kuniona aliwaita wazazi wangu na kuwaambia waniandae na kuja huku Kibaha. Alituchukua katika gari lake na kuja nasi hadi hapa Kibaha katika hospitali ya Bake.
“Alitugharamia kitu kitu, nilifarijika sana kuona kuwa nathaminika na mtu msomi kama huyu kwani pale kijijini baadhi ya watu waliniona kama siyo binadamu, kuumwa kwangu kulikuwa hakuwasikitishi.


MATOKEO YA UCHUNGUZI

 “Baada ya kufika hapa Kibaha siku iliyofuata nilifanyiwa uchunguzi na Dk. Bake na kuona ugonjwa unaonisumbua ni dalili ya kansa, ili kuhakikisha alichukua kipande cha nyama katika shavu akapeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili na kudhihirika wazi kwamba ni kansa.“Niliambiwa matibabu yake ni katika Hospitali ya Ocean Road ambapo ameniahidi kunipeleka huko kutibiwa.
“Nasikitika kwa sababu shule sijasoma, nimekua nkiiishi kwa hofu hasa ninaposikia kwamba maalibino wenzangu wamekua wakiuawa hovyo, sitembei mbali na nyumbani kwa hofu ya kukamatwa.
“Namshukuru sana Dk. Bake ambaye amenionea huruma kuliko hata serikali na tunaishi na mzazi wangu hapa kwa gharama yake, Mungu ambariki”alisema Janeth huku akitokwa na machozi
DAKTARI ANENA
Dk. Bake naye amesema kwamba ameamua kumsaidia mtoto huyo kutokana na hali aliyonayo na alikua akiishi na ugonjwa kwa kusubiri kifo.
“Huyu ni binadamu kama wengine kiasi kwamba anapolia na kukata tamaa juu ya maisha yake inasikitisha wakati sisi tupo, nilijisikia vibaya alipokua akilia bila msaada, niliamua nimchukue,  ili kumtoa hofu niliwachukua na wazazi wake. Nitajitahidi kumtibu huko Ocean Road na gharama zote nitazisimamia”alisema Dk Bake ambaye ni bingwa wa upasuaji wa mifupa na viungo.

ASKARI WAWILI WAUAWA PWANI

Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa, Pwani/Uwazi
MAZITO yameibuka kufuatia tukio la majambazi kuvamia Kituo cha Polisi Ikwiriri, Rufiji, Pwani na kuwaua askari wawili kisha kuchukua bunduki 7, risasi 60 na mabomu kadhaa, Uwazi limeichimba.Tukio hilo lililozua hofu ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania, lilijiri Januari 21, mwaka huu na hadi wakati tunaenda mitamboni, hakuna mtuhumiwa anayeshikiliwa.
Ndugu wa karibu wa marehemu, Judith Timothy (32) wakilia kwa uchungu.
Askari waliouawa katika kituo hicho ni Edger Jerald Mlinga (43) na Judith Timothy (32). Afande wa tatu alifanikiwa kukimbia na hivyo kuokoa maisha yake.
UWAZI LAANZA KUCHIMBA
Muda mfupi baada ya kutokea kwa tukio hilo, timu ya waandishi wa gazeti hili ilitua katika eneo la tukio na kushuhudia damu ya askari hao waliouawa kwa kukatwa mapanga, Judith licha ya kukatwa alipigwa risasi tumboni.
MAJIRANI WAONGEA NA UWAZI
Baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na kituo hicho walizungumza na Uwazi na kusema kile walichokiona.“Mimi muda wa tukio nilisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwenye kituo hicho. Nilijua kuna watuhumiwa wanabanwa na askari maana kelele hazikuwa za mtu mmoja kulikuwa na ya kike pia.
Majirani wakimfariji mmoja wa ndugu wa marehemu msibani.

“Lakini nilipozidi kusikiliza kwa umakini nilibaini kuwa, kelele hizo zilikuwa za kuomba msaada kwani walikuwa wakishambuliwa na wakawa wanapiga mayowe, ‘tunauawa’,” alisema mkazi mmoja wa Ikwiriri huku akiomba hifadhi ya jina lake.
WANANCHI WATOKA, MLIO WA RISASI WASIKIKA
Wakiendelea kuzungumza, majirani hao walisema walijikuta wakijikusanya kwa ajili ya kwenda kituoni hapo kujua kulikoni lakini ghafla walisikia mlio wa risasi hivyo wakarudi ndani mbio na kujifungia.“Baadaye sana sikusikia tena mlio wa risasi wala mayowe ya kuomba msaada. Mimi nilitoka kwenda kituoni, nikashangaa kukuta watu wengi wamesimama nje.
“Nilipofika nikaambiwa kituo kilivamiwa na majambazi, wamewaua askari wawili. Kweli, maana miili yao ilikuwa chini kwenye dimbwi kubwa la damu. Nilishtuka sana kwani kama askari wenye silaha wanavamiwa na majambazi je sisi raia tusio na silaha?” alihoji jirani huyo.
Mwili wa marehemu, Edger Jerald Mlinga (43) ukichuliwa kwenye jeneza.

ASKARI WA KIKE ALIPONZWA NA SIMU

Habari zaidi zinasema kuwa, marehemu Judith yeye aliponzwa na simu yake ya mkononi.
“Yule afande mwanamke alishamaliza kazi akaondoka, lakini alipofika mbele akienda  nyumbani akagundua amesahau simu, ikabidi arudi.“Kule kurudi ndiyo na majambazi nao wakatokea,” alisema afande mmoja kwa ombi la kutotaja jina lake gazetini.
UTENDAJI WA KAZI ULIKIUKWA?
Taarifa kutoka chanzo chetu ndani ya jeshi la polisi zinadai kuwa siku ya tukio kituoni hapo kulikuwa na polisi watatu, wawili walipaswa kuwepo kaunta ndani, mmoja awepo nje.Hata hivyo, wote walikuwa nje na ndipo ghafla wakavamiwa na kundi hilo la watu wasiopungua kumi nao wakashindwa kujitetea na kujikuta wawili wakiuawa.
UGAIDI WATAJWA
“Huu ni ugaidi kabisa! Haiwezekani kituo kikatekwa kirahisi na askari kuuawa. Hawa watu wanaovamia vituo vya polisi na kuchukua silaha wanazipeleka wapi? Niliwahi kusikia kuwa kuna kundi la watu ndiyo wanaoteka vituo na kupora silaha kwa lengo la kukusanya silaha.“Nasikia hao watu iko siku huko mbele watakuja kufanya uasi mkubwa sana hapa Tanzania,” alisema jirani mwingine.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrich Matei (kulia) akifafanua jambo.

AL SHABAAB WATAJWA

Habari zaidi kutoka kwa vyanzo vya kiserikali zinasema kuwa, upo wasiwasi wa kundi la Al Shabaab kutumia nafasi hiyo kukusanya silaha ili baadaye wawape vijana ambao wamekuwa wakipewa mafunzo na kundi hilo.
Habari zikakumbushia kuwa, Julai mwaka 2013, mkoani Mtwara kuna vijana 11 walikamatwa wakiwa na CD 25 zenye mafunzo ya wapiganaji wa Al Shabaab na Al Qaeda.“Serikali lazima iliangalie hili. Silaha zinatekwa, hadi mabomu yanachukuliwa na majambazi, wanapeleka wapi? Mbona hatusikii matumizi makubwa ya mabomu sehemu mbalimba za nchi? Ni majambazi kweli au makundi ya Al Shabaab?” alihoji mtoa hoja hii akiomba kufichwa kwa jina lake.
MKE WA MAREHEMU MLINGA
Baada ya kuzungumza na majirani, Uwazi ilikwenda Hospitali ya Mkuranga, Pwani ambako miili ya marehemu ilihifadhiwa na kuzungumza na ndugu. Kwa upande wake, mke wa marehemu Afande Mlinga, Walivyo Ahamed Wapiwapi alisema kifo cha mumewe kimempa mshtuko mkubwa kiasi kwamba hajajua ataishije na watoto wanne aliowaacha.
Marehemu Edger Jerald Mlinga enzi za uhai wake.
“Nakumbuka saa moja na nusu siku moja kabla ya tukio mume wangu alirudi kutoka kazini, alikaa kidogo, ilipofika saa tatu akaaga kwamba anakwenda kazini.“Siku hiyo hakurudi tena mpaka kesho yake saa nne asubuhi napigiwa simu na mashemeji zangu kwamba mume wangu ameuawa kituoni,” alisema mwanamke huyo huku akimwaga machozi.Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu, mwili wake ulisafirishwa juzi na ulitarajiwa kuzikwa jana Jumatatu kwenye Kijiji cha Mbokomu, Kilimanjaro.
MDOGO WA MAREHEMU JUDITH
Naye mdogo wa marehemu Judith, Oscar Mwambije alisema:
“Mimi taarifa za kuuawa kwa dada nilizipata usiku uleule kutoka kwa kaka anayeishi Mwanza ambaye ndiyo wa kwanza kupata habari hizo.“Aliniambia Judith amepigwa risasi kazini na kufariki dunia palepale na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi.
“Tulikuja hadi hapa chumba cha kuhifadhia maiti Mkuranga tukakuta akishushwa katika gari la polisi na tulithibitisha kuwa ndiyo yeye dada Judith,” alisema mdogo wa marehemu huku akilengwalengwa na machozi.Kwa mujibu wa familia, marehemu Judith amezikwa Ijumaa iliyopita kwenye Kijiji cha Itete wilayani Rungwe, Mbeya. Ameacha mtoto mmoja.

MAELEZO YA KAMANDA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrich Matei akiwa Mkuranga na waandishi wetu alisema: “Msako mkali sana unaendelea, lazima wahusika wapatikane.”
MKURUGENZI MAKOSA YA JINAI
Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Tanzania (DCI), Kamishna Diwani Athuman alipohojiwa na Uwazi kuhusiana na tukio hilo kutokana na madai ya wananchi kwamba kuna kundi la watu linakusanya silaha na baadaye kuanzisha vurugu au vita nchini, alisema:
“Wanaofanya uhalifu wana sababu zao, hao pia wana sababu zao, kwa namna gani watatumia hizo silaha, hatujui ila msako mkali wa kuwatafuta unaendelea na ninawaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuwatia nguvuni watu hao,” alisema Kamanda Athuman.
KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Kuvamiwa kwa Kituo cha Polisi Ikwiriri kumekuja mara baada ya vituo vingine navyo kuvamiwa, kuibwa silaha na polisi kuuawa.Kituo cha Polisi Bukombe, Geita Septemba, mwaka jana, saa tisa usiku kilivamiwa ambapo askari wawili waliuawa na bunduki 10 na mabomu kuporwa.Mwaka huohuo, Kituo cha Polisi Kimanzichana, Mkuranga, Pwani nacho kilivamiwa na majambazi. Polisi mmoja aliuawa na mwingine kujeruhiwa, bunduki tatu ziliibwa.

MIMBA KUYEYUKA (BLIGHTED OVUM) INATOKEAJE?


TATIZO hili pia huitwa ‘anembryonic gestation’. Hutokea pale mfuko wa mimba unapoendelea kukua bila ya kuwa na mtoto ndani. Kifuko cha mimba huitwa ‘gestational sac’ na mtoto ni ‘embryo’.

HALI HALISI
Mwanamke anakuwa mjamzito ambapo ana dalili zote za ujauzito na katika wiki sita za mwanzo akifanya Ultrasound mtoto anaweza kuonekana lakini baada ya hapo dalili za mimba zinaanza kupungua taratibu na mama akifanya Ultrasound mimba itaonekana mfuko wake tu lakini ndani hakuna kitu!

MWENDELEZO
Hapa ndipo tunasema mama amepata blighted ovum. Mimba ilikuwepo lakini imeyeyuka! Hali hii ikiendelea mama ataanza kutokwa na damu taratibu.Wakati mwingine anaweza kupatwa na tatizo hili hata bila yeye mwenyewe kujijua kama ni mjamzito.

HUKATISHA TAMAA
Blighted ovum ni tatizo linalokatisha tamaa kwa mwanamke anayetafuta ujauzito na wakati mwingine haamini kilichotokea.

NINI SABABU?
Tatizo hili hutokana na hitilafu katika yai lenyewe kutokana na kasoro za kromozom zinazorutubisha yai. Kromozom zinazorutubisha yai ni za kiume zikiungana na za kike, hivyo mimba ikitungwa na kasoro haiendelei, inatoka mapema. Mwanamke anaweza kutokewa na tatizo hili hata zaidi ya mara mbili.
Kasoro za kromozon zinaweza kusababishwa na mambo mengi kama maambukizi, kemikali na mionzi au hali isiyoeleweka.Kromozom za kiume na za kike pia huchangia hali hii. Kromozom za kike ni aina ya X na zile za kiume ni za aina ya Y.

HALI YA MWANAMKE
Mwanamke ana aina moja tu ya kromozom ambazo ni za kike na mwanaume ana kromozom za aina mbili, za kiume na kike. Kromozom pia zikichoka husababisha mimba iwe na kasoro hivyo huharibika na kutoka.
Kama tulivyoona, mimba inaweza kuyeyuka ghafla na mwanamke anaweza kupoteza hata mimba tatu au zaidi.

Itaendelea wiki ijayo.

Saturday, January 24, 2015

MWANAFUNZI KIDATO CHA PILI AJIFUNGUA KWENYE DALA DALA, NI BAADA YA KUMEZA DAWA ZA KUTOA MIMBA



Mwanafunzi wa Shule moja ya sekondari Jijini Dar es Salaam kajifungua kwenye daladala Maeneo ya azizi ally baada ya kumeza dawa za kutoa mimba,
Kwa lugha nyingine Tunaweza kusema mwanafunzi huyo amefanya Abortion kwani Kichanga hicho kinakadiriwa kuwa na Miezi mitatu au Minne hivi, mwanafunzi huyo inasemekana anasoma kidato cha pili katika Moja ya shule Jijini Dar....
HABARI ZAIDI TUTAWAJUZA

VIDONGE HATARI VYAUZWA KA NJUGU PHARMACY DAR!


Na Waandishi wetu/Risasi Jumamosi
Hali inatisha! Vidonge vinavyodaiwa ni vya
kutoa mimba vimezagaa kwenye maduka ya madawa baridi ‘famasi’ jijini Dar
na kuuzwa kinyume cha sheria iliyowekwa na wahusika kwa kuwa
hairuhusiwi kuuziwa dawa hizo pasipokuwa na kibali cha daktari.
Wauzaji wa moja ya duka la dawa linalouza dawa za kutolea mimba.
Kikosi chetu cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers
Ltd kiliingia kazini kuzisaka famasi zinazodaiwa kujihusisha na biashara
ya dawa hizo zilizotajwa kwa jina la Misoprostol 200.
ENEO LA KWANZA
Zoezi lilianzia kwenye famasi za
Mwenge, Dar (majina yanahifadhiwa kwanza) ambapo OFM walikwenda kwa
lengo la kutaka kununua dawa hizo ambapo muuzaji wa kwanza ambaye ni
mwanaume alikiri kuziuza kwa bei ya sh 10,000.
Kamanda wa OFM (kulia) akimbana kwa maswali mmoja wa wauzaji hao.
Katika famasi nyingine maeneo hayo, muuzaji wa pili aliiuza kwa  sh
25, 000 huku akikiri kuwa anauza dawa hizo kinyume cha sheria.“Naziuza
kimakosa tu maana haziruhusiwi kuuzwa pasipokuwa na kibali cha daktari.
Ili umuuzie mtu lazima aje na cheti cha dokta kinachoonesha anahitaji
kuzitumia na matumizi yake rasmi ni kwa ajili uchungu endapo mjamzito
anataka kujifungua baada ya kazidisha miezi bila kuzaa,” alisema
mfamasia huyo bila kujua anazungumza na makachero wa OFM.
Moja ya dawa zinazutumika kutolea mimba ikiwa mkononi mwa kamanda wa OFM.
ENEO LA PILI
Baada ya hapo, OFM ilitua maeneo ya
Tandale ambapo ilihitaji huduma hiyo kwenye famasi mbalimbali huku
tukio zima likirekodiwa hatua kwa hatua.OFM waliingia kwenye famasi hiyo
kwa awamu na kuulizia vidonge hivyo kama vinapatikana na kutajiwa bei
ya sh 20,000.
OFM waliomba kupata maelekezo ya matumizi yake ambapo mhudumu mwanamke, alitoa maelekezo:

“Hizi dawa huwa naziuza sana kwa watu mbalimbali kama wanafunzi na wake
za watu kwa lengo la kutolea mimba. Vidonge vingine huingizwa sehemu za
siri na nyingine unameza. Isipokuwa ukikosea tu kidogo kuziweka
zinaweza kuharibu mfumo mzima wa uzazi hivyo unahitajika umakini mkubwa
mno.”
Makamanda wa OFM wakichukua maelezo zaidi kutoka kwenye duka hilo la dawa.
ENEO LA TATU
Maeneo ya Magomeni OFM ilibaini dawa hizo zinauzwa
sh 15,000 hadi sh 30,000. Hata hivyo, OFM walinunua vidonge hivyo
(vielelezo vipo ofisini) kwa bei ya sh 25,000 kwenye duka moja lililopo
Magomeni-Kagera.
ZINA MADHARA?
Kwa mujibu wa mtaalam wetu wa afya na uzazi, athari
za utoaji mimba kwa kutumia dawa hizo ni pamoja na kuharibu taratibu za
kimaumbile kwenye kizazi na kusababisha ugumba.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
MAGONJWA SUGU
Pia mtoaji mimba huwa na hatari ya
kupata magonjwa sugu ya via vya uzazi yanayoathiri shingo ya kizazi na
mirija ya mayai. Wanaotumia vidonge hivyo wana uwezekano wa kupata kansa
ya uzazi hasa kwa wale wanaoingiza sehemu za siri.
WAZIRI UPO?
Ili kupata mzani wa uchunguzi huo,
OFM ilimsaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid ili
kumjulisha habari hiyo lakini simu yake ya kiganjani haikuwa hewani
hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.Imeandaliwa na: Mayasa Mariwata,
Hamida Hassan, Shani Ramadhani na Gladness Mallya.


Thursday, January 22, 2015

TATIZO LA NYAMA KUJITOKEZA NJIA YA HAJA KUBWA {HEMORRHOID}

Wiki iliyopita tuliweza kuona nini maana kubwa ya tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika sehemu au maeneo ya haja kubwa na leo tutaweza kuona basi vyanzo au visababishi hasa vya tatizo hili kwa mwanadamu.

VISABABISHI
Sasa wataalamu bado hawajawa na majibu kamili kuhusiana na tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika maeneo ya haja kubwa husababishwa na kitu gani hasa lakini wameweza kutoa baadhi ya vitu ambavyo vinaaminika kwa kiwango kikubwa sana husababisha hali hii kujitokeza kwa mwanadamu, na vitu hivyo basi ni kama vifuatayo;

Kupata choo kigumu kupita kiasi kwa mwanadamu wataalamu wanaita constipation mara nyingi imekuwa ni chanzo kikubwa sana cha tatizo hili la mtu kutokwa na kinyama katika maeneo ya haja kubwa na kuna uwezekano ikawa ni bawasili ya ndani au ya nje yenye kuonekana, kwa hiyo kama mtu anakumbwa na hali ya kupata choo kigumu basi kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akasumbuliwa na tatizo hili la bawasili.

Hali ya kuharisha sana {heavy diarrhea}, kwa mtu ambaye anapatwa na hali ya kuharisha kwa muda mrefu basi naye pia anauwezekano mkubwa sana wa kukumbwa na tatizo hili la kutokwa na kijinyama katika maeneo ya haja kubwa au bawasili {hemorrhoid}.

Kukosekana kwa baadhi ya vyakula, kuna baadhi ya vyakula vinapokosekana katika mwili wa mwanadamu au visipotumika sana kwa mtu huweza kusababisha mtu kupata choo
kigumu kupita kiasi na kama anapatwa na hali hii basi kunauwezekano mkubwa sana mtu huyo akakumbwa na tatizo la bawasili na vyakula hivyo ni mboga za majani na matunda kwa wingi ndani ya mwili.

Hali ya ujauzito kwa akina mama, hii pia imekuwa ni sababu kubwa sana inayosababisha suala zima la kutokwa na kijinyama maeneo ya haja kubwa na hii ni kwa sababu hali ya ujauzito kwa mama husababisha kukua au kuongezeka kwa mji wa mimba ambao hutumika hasa kumuhifadhi mtoto na kwa sababu hii basi inaweza kusababisha vascular structure au vijinyama katika maeneo ya haja kubwa kwa mama kuongezeka ukubwa na hivyo basi kuwa ni tatizo,

lakini mara nyingi mwanamke akishajifungua kunauwezekano kikapotea lakini kama kinabaki basi ni vema kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu zaidi.Kukaa kwa muda mrefu, hali ya kukaa kwa muda mrefu kwa mwanadamu nayo pia imekuwa ni kisababishi kikubwa sana cha tatizo kubwa la tumbo kujaa gesi na kupata choo kigumu kupita kiasi {constipation}.

Mara nyingi watu wanaokumbwa na shida hii kunauwezekano mkubwa sana wa kutokwa na kinyama au bawasili, hasa kwa wanaotumia sana vyoo vya kukaa na kufanya hivyo kwa muda mrefu.
Hali ya wanadamu kunyanyua vitu vizito kupita kiasi kwa mwanadamu na ikawa ni zoezi endelevu kwa muda basi hali hii inaweza sababisha mtu kupatwa na tatizo la kutokwa na kijinyama au bawasili.
Itaendelea wiki ijayo.

, na hata kwa mtu anaefanya kazi mgumu sana pia kunauwezekano akakutwa na tatizo hili.
Na pia kunasababu ya kurithi, hali hii ya ya kutokwa na kijinyama kwa upande mwingine wataalamu wametoa sababu ya kwamba inakua ni hali ya kurithi kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine {genetic}, na ni vema kulitibia pale tu linapojitokeza.

Na kama unapatwa na hali kama hiyo basi na wewe pia unaweza wasiliana nasi kupitia namba zetu kwa ajili ya ushauri na tiba zaidi. Kwa ushauri, vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.Nawatakia afya iliyo njema kabisa.
Itaendelea wiki ijayo. Asante.

Tuesday, January 20, 2015

MIAKA MITATU MUHIMBILI BILA MATIBABU



Kijana Amosi Ng’arare Marale Sasi,(22) anayesumbuliwa na uvimbe usoni.

Na Haruni Sanchawa/Uwazi

Alikuja Muhimbili ili akafanyiwe upasuaji India, alipelekwa akarudishwa bila kutibiwa, awaita ndugu zake hospitalini.

Kijana Amosi Ng’arare Marale Sasi,(22) mkazi wa Kijiji cha Kizaru, Kata ya Mryaza, wilayani Musoma Vijijni amepoteza mwelekeo wa maisha baada ya ndoto yake ya kusoma hadi chuo kikuu kuishia njiani kutokana na matatizo ya ugonjwa wa ajabu ambao unamtesa kwa kipindi cha miaka 18.

MUHIMBILI MIAKA MITATU
Kijana huyo ambaye yupo Muhimbili kwa zaidi ya miaka mitatu sasa alikuja katika hospitali hiyo kwa lengo la kupatiwa matibabu tangu mwaka 2011, hata hivyo, baada ya uchunguzi iligundulika kwamba matibabu yake ni mpaka apelekwe nchini India.

INDIA AFIKA HAKUTIBIWA
Katika mahojiano na mwandishi wa habari hii wiki iliyopita katika Jengo la Sewahaji, wodi namba 23, Amosi akionekana mwenye uso wenye huzuni alisema Oktoba 14, 2014 alipelekwa India kwa matibabu lakini baada ya kufika huko hakuna kilichofanyika.

“Nilipelekwa India katika Hospitali ya Apolo, tulikaa kule mwezi mzima na ofisa moja wa ustawi wa jamii kutoka hapa Muhimbili ambaye alinipeleka lakini cha ajabu ni kwamba ilipofika Novemba 19 mwaka jana, niliambiwa nijiandae kwa kurudi nyumbani (Tanzania) kesho yake.

“Niliuliza kwa nini nirudishwe nyumbani wakati sijatibiwa? Nikaambiwa kwamba ni uamuzi uliofikiwa na taarifa zaidi nitajulishwa hapa nyumbani.


Kijana Amosi Ng’arare Marale Sasi akiuguza uvimbe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

ARUDISHWA MUHIMBILI
“Tulipanda ndege Novemba 20 mwaka jana na kutua hapa Tanzania, nilirudishwa wodini Muhimbili. Niliambiwa nisubiri siku nyingine nitapelekwa tena huko India, nilishangaa nikaona ningoje.
“Sasa ni muda mrefu sijajulishwa chochote nimekua nikiishi hapa bila kujua hatima ya maisha yangu, na bado najiuliza kwa nini nipelekwe India halafu nirudishwe bila matibabu?”alihoji Amosi huku akitokwa machozi.

HISTORIA YA UGONJWA
“Nilizaliwa nikiwa sina tatizo la aina yoyote nikiwa na miaka minne baba akawa amefariki dunia nikabaki na mama ambaye alikua akitulea na ndugu zangu na kipato chake kinategemea kilimo cha jembe la mkono.
“Nilipofikisha umri wa miaka mine ndipo nilipoanza kupata tatizo hili kwa kutokwa na kipele kilichokuwa kinawasha. Mama alinipeleka hospitali mbalimbali kabla ya kupelekwa Bugando na hapa Muhimbili,” alisema Amosi.

Msemaji wa Hospitali ya Muhimbili hakupatika ambapo maofisa wake walisema yupo kwenye vikao vya uongozi.

Yeyote aliyeguswa na habari hii na angependa kumsaidia Amosi anaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0765 765747 au 0715 756384.

Sunday, January 18, 2015

WANANCHI MKURANGA WAASWA KUCHANGIA DAMU.


Wananchi wilayani Mkuranga wametakiwa kujenga utamaduni wa kuchangia damu kwenye benki ya damu iliyoko katika hospitali ya wilaya hiyo ili kupunguza tatizo la uhaba wa damu linaloikabiri hospitali hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa jana wilayani Mkuranga na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya hiyo, Dkt. Anwar Milulu wakati akipokea msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) kwa lengo la kuwasaidia wagojwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa hospitali hiyo kwa sasa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa damu kutokana na mwamko mdogo wa wakazi wa wilaya hiyo wanaojitokeza kuchangia damu jambo linalosababisha upungufu wa damu na usumbufu kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa damu .

“Kama mnavyoona hospitali yetu iko barabarani kwa sasa tunakabiliwa na tatizo la upungufu wa damu, baadhi ya wagonjwa hutufikia wakiwa katika hali mbaya ya kuhitaji kuongezewa damu kiasi cha kutufanya tuwapeleke katika hospitali ya Taifa Muhimbili kuokoa maisha yao” Alisema Dkt. Milulu.

Alieleza kuwa lishe duni na kutozingatia ulaji wa mboga za majani kama inavyoshauriwa na wataalam wa afya ni miongoni mwa sababu zinazochangia kuendelea kwa tatizo la upungufu wa damu kwa akina mama wajawazito na watoto.

Dkt. Milulu alifafanua kuwa hospitali hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa wagonjwa hususan akina mama wajazito na watoto pindi wanapohudhuria Kliniki kwa lengo la kuwaeleza umuhimu wa uzingatiaji wa lishe bora na namna ya kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu miongoni mwa jamii.

Aidha, alisema Serikali inaendelea kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya ukosefu wa maji,uhaba wa miundombinu na dawa yanayoikabili hospitali hiyo kutokana na idadi kubwa ya wagonjwa wa kawaida na wale walio katika makundi maalum wanaohudumiwa na hospitali hiyo ikilinganishwa na uwezo wake.

“Serikali inaendelea kushughulikia tatizo la maji,miundombinu na upungufu wa dawa unaoikabili hospitali yetu maana idadi ya wananchi tunaowahudumia ni wengi ikilinganishwa na uwezo wa miundombinu ya hospitali”

Kuhusu changamoto ya rasilimali watu na wataalam wa kada mbalimbali alisema kwa sasa hospitali hiyo ina idadi inayoridhisha ya Madaktari, Wauguzi, wahudumu, wataalam wa maabara na madereva ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Alitoa wito kwa uongozi wa chuo hicho kuendelea kuisaidia hospitali hiyo katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wanafunzi wa chuo cha CBE kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wagonjwa.

Nao baadhi ya wananchi waliokuwa wakipatiwa huduma katika hospitali hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti licha ya kuushukuru uongozi wa chuo cha CBE kwa kuwakumbuka kwa kuwapatia msaada wa mashuka hayo walikiri kuwepo kwa mwamko mdogo wa wananchi kuchangia damu katika benki ya damu ya hosptali hiyo.

Aidha, waliiomba Serikali kulishughulikia tatizo la maji , miundombinu na uhaba wa dawa uliopo katika hospitali hiyo na kuwaomba wadau wengine wajitokeze kuisaidia hospitali hiyo ili iweze kutoa huduma bora kwa wananchi.

Awali akizungumza msaada huo Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emanuel Mjema alisema kuwa chuo chake ifikapo Januri 21, 2015 Chuo cha Elimu ya Biashara kinatimiza miaka 50 hivyo msaada walioutoa ni sehemu ya huduma kwa jamii.

Alisema katika kuelekea kutimiza miaka 50 ya chuo cha CBE mbali na kujikita katika masuala ya kuelimisha jamii katika taaluma mbalimbali ikiwemo Biashara, Ugavi na manunuzi, Vipimo, TEHAMA na Utawala katika biashara kimekua kikitoa huduma mbalimbali kwa jamii.

Alisema katika kuelekea maadhimisho ya miaka 50 chuo hicho kimekuwa kikitoa misaada ya vitu mbalimbali na elimu ya ujasiriamali kwa wananchi katika mikoa yote ambayo kina matawi yake ikiwemo Dar es salaam, Mbeya, Zanzibar, Mwanza na Dodoma.
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (katikati) akitoa ufafanuzi kuhusu msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na chuo hicho katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga ikiwa ni sehemu ya mpango wa chuo hicho kutoa huduma kwa jamii.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) akimkabidhi Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) msaada wa mashuka yenye 90 yaliyotolewa na chuo hicho kusaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika jana wilayani Mkuranga kama sehemu ya Chuo hicho kuadhimisha miaka 50 toka kianzishwe mwaka 1965.
Baadhi ya Wauguzi na wahudumu wa afya wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga wakiangalia moja ya shuka kati ya mashuka 90 yaliyotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga Dkt. Anwar Milulu (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Emanuel Mjema (kulia) kabla ya kukabidhiwa msaada wa mashuka 90 yaliyotolewa na CBE kusaidia wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakaPicha na Aron Msigwa – MAELEZO.zi wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga jana.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Saturday, January 17, 2015

MTI WA AJABU WAGUNDULIKA MBEYA, UNADAIWA KUGAWA UTAJIRI



Wananchi wa kijiji cha Ijoka, Mkoani Mbeya wameingia kwenye imani za kishirikina baada ya kuandamana na kwenda kupasua mti ulianguka ambao wanadai una utajiri ndani yake.Wakazi hao walisema walielezwa na mganga wa jadi kutoka Malawi Peter Lungola, kuwa mti huo ukitumiwa vyema utaleta utajiri.Mganga huyo alifika kijijini humo miaka 20 iliyopita na kuwaeleza kuwa amti huo una asili kubwa ya utajiri na kuwa chini ya mti huo kuna nyumba za kifahari zilizojaa hazina kubwa ya fedha.Inasemekana mti huo ulianguka wiki iliyopita na kuanza kupumua kitendo kilichowashangaza wengi. Wazee wa kijiji hicho walishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kula majani ya mti huo huku wengine wakichukua magome yake na kuyahifadhi majumbani mwao.

SITTI MTEMVU ATEMBELEA KITUO CHA WENYE ULEMAVU WA NGOZI HOSPITALI YA MKOA ILALA


Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe Mussa Azzan Zungu akiongea na Waandishi wa Habari ( pichani hawapo) mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya kuhifadhia taka na Sabuni.


Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Faundation, Sitti Mtemvu (wa tatu kulia) akimkabidhi vifaa vya kuhifadhia taka Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto), kwa ajili ya Hospitali ya Mkoa wa Ilala Dar es Salam. kuanzia kushoto nyuma ya mbunge ni Diwani wa kata ya Kinyerezi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Leah Mgitu katikati ni mama mzazi wa Sitti Mariam Mtemvu, wa kwanza kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi Edson Fungo na anaefuatia ni Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Mkoa Ilala
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Sun Tanzania Bi. Vicky Ntetema (kulia) , akifafanua jambo wakati Mwenyekiti huyo alipotembelea kituo hicho

Afisa utetezi Bw. Kondo Seif (wa kwanza kushoto) akitolea maelezo ya ukosefu wa rangi asili mwilini ambayo huathiri ngozi, macho na nywele na kukosekana kwa melani mwilini, akisema miongoni mwa athari zake ni wepesi wa kuungua na jua unapotembea juani na ufanyapo kazi juani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Under The Sun Tanzania Vicky Ntetema (kulia) akimuonyesha Mwenyekiti wa Sitti Tanzania Foundation, Sitti Mtemvu (kushoto) Picha ya mtoto alie tekwa akiwa mgongoni mwa mama yake. Wa pili kushoto ni Mama mzazi wa Sitti.

Friday, January 16, 2015

TUHUMA NZITO: MAMA AMCHARANGA VIWEMBE MWANAYE

Stori: Gabriel Ng’osha na Denis Mtima/Ijumaa
Unyama wa kutisha! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina la Feromena, mkazi wa Meko-Mtongani, Kunduchi jijini Dar, anatuhumiwa kumcharanga viwembe mwanaye wa kumzaa aliyetajwa kwa jina moja la Zena mwenye umri wa miaka kumi.

Mtoto anayefahamika kwa jina la Zena anayedai kunyanyaswa na mama yake.

Tukio hilo la kulaaniwa lilijiri Jumanne wiki hii nyumbani kwa mwanamke huyo maeneo hayo ambapo mama huyo inadaiwa alimsulubu mwanaye huyo anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Mtakuja.


Sehemu ya majeraha ya viwembe kichwani kwa mtoto Zena.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mama huyo alidaiwa kumfungia ndani mwanaye huyo na kuanza kumpa kipigo cha mbwa mwizi.Walidai kwamba ukiachana na siku hiyo, mama huyo amekuwa akimsulubu mwanaye huyo mara kwa mara kwa kumcharanga viwembe na vitu vyenye ncha kali hivyo kumwachia majeraha sehemu mbalimbali za mwili.
Sehemu ya majeraha yaliyo mgongoni mwa zena.

Mjumbe wa mtaa huo aliyejitambulisha kwa jina la Elizabeth Mziga alikiri kupokea malalamiko kutoka kwa majirani juu ya unyanyasaji na uteswaji wa mtoto Zena.Mjumbe huyo alisema kuwa tuhuma hizo alishazifikisha polisi ambapo mama huyo alikamatwa lakini baada ya muda alionekana akidunda mtaani kama kawa.

Mama mzazi wa mtoto Zena,Bi.Feromena akibanwa kwa maswali.

Baada kujazwa habari na majirani na mjumbe huyo, kile kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu cha Global Publishers kiliingia mzigoni ambapo kilianza kwa kumsaka mtoto huyo na kuzungumza naye.
Alipopatikana, mtoto Zena alieleza namna mama yake alivyokuwa akimfanyia matendo ya kinyama huku akimnyima haki ya msingi ya kwenda shule.
Mama Zena, Bi. Feromena akiwa chini ya ulinzi.

Alisema mama yake amekuwa akimtuhumu kumwibia fedha zake na kwenda kutumia shuleni hivyo hakupaswa kurudi tena shuleni na kuongeza kuwa siku ambazo alikuwa akilala kwa amani ni zile ambazo alikuwa ametoroka nyumbani na kwenda kulala kwa majirani.


Wananchi wakishuhudia mkasa huo wa kusikitisha.

OFM ilishuhudia mwili wa Zena ukiwa na makovu na kuvimba huku akidai kuwa aliunguzwa na ‘frampeni’ (kikaangio) hasa sehemu za kiunoni na mgongoni.Alisema mama yake alimtishia kuwa endapo atamwambia baba yake atakiona cha mtema kuni.

“Jamani mama amekuwa akinipiga na kunikata viwembe bila kuniambia kosa langu. Naombeni msaada nateseka,” alisema Zena kwa masikitiko makubwa.OFM, kwa kwa kushirikiana na mjumbe wa eneo hilo walikwenda kuripoti tukio hilo kwenye Kituo Kidogo cha Polisi cha Mtongani lakini hakukuwa na dawati la jinsia hivyo polisi walikwenda kumkamata mama huyo kwa ajili ya kumpeleka kituo kikubwa.
Moja ya wazee akionesha jalada la kesi aliyofunguliwa mama zena.

Kwa upande wake mama huyo alipoulizwa sababu hasa ya kumsulubu mwanaye alisema si kweli bali anachojua ni siku moja aliyompiga baada ya kuchukua fedha zake na kwenda kununulia maandazi.
“Sijui aliyemkatakata viwembe,” alisema mama Zena kwa kifupi.

Baada ya kufikishwa kwenye kituo kikubwa cha Polisi cha Kawe, mama huyo alifunguliwa jalada la kesi namba KW/RB/439/015-SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI hivyo anasubiri kufikishwa kwenye mkono wa sheria.

WATOTO WAWILI WATEKETEA KWA MOTO KIJIJI CHA MBELA, MWANZA

WATOTO wawili wa familia moja, mmoja wa kike mwenye umri wa miaka minne na mwingine wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja wameteketea kwa moto na mmoja kujeruhiwa leo baada ya kibatari kulipuka na kuteketeza nyumba kijiji cha Mbela wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza.


Muonekano wa nyumba baada ya kibatari kulipuka na kupelekea watoto wawili wa familia moja kufaliki dunia wakiwa ndani ya nyumba hiyo leo kijiji cha Mbela Wilayani, Misungwi mkoa wa Mwanza.

Mmoja ya watoto hao baada ya kuteketea kwa moto.


Wananchi wakiwa eneo la tukio.


Mtoto akifunikwa na kanga baada ya kupoteza maisha.

Wananchi wakiwa katika hali ya huzuni mmoja wao wa pili kutoka kulia mbele akiwa amembeba mtoto aliyejeruhiwa na moto huo.

...Wakiendelea kushangaa katika eneo la tukio.