Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Thursday, December 11, 2014

JE, VIDONDA VYA TUMBO VINATIBIKA?-3


Wiki iliyopita tulizungumzia sana madhara yanayoweza kumkuta mtu mwenye vidonda vya tumbo. Lakini leo sanasana tutaweza kuangalia dalili kubwa za tatizo hili ni zipi na mtu anapoziona katika mazingira yake ya kawaida basi aweze kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kuweza kuliondoa tatizo hili kwa urahisi kabisa.

DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
Dalili za tatizo hili la vidonda vya tumbo hutegemeana sana na tatizo linakuwa limefikia katika kiwango gani hasa, lakini tutazizungumzia kwa jumla lakini pia kwa kuzingatia tatizo kwa kila mtu. Dalili hizo ni kama zifuatazo;

Dalili kubwa ni maumivu kama ya kuungua maeneo ya kifua, mara nyingi mtu mwenye vidonda vya tumbo anaweza akawa anasikia maumivu makali sana maeneo ya kifuani kwa mwanaume au mwanamke na wakati mwingine mtu huyu akawa anakisikia au anakihisi chakula kikiwa kinashuka hasa wakati wa kula na wakati mwingine inakuwa ni kama moto unatembea kifuani kuja tumboni na hiyo ndiyo inakuwa dalili kubwa kabisa ya tatizo hili la vidonda vya tumbo.

Lakini kuna dalili nyingine pia mfano kusikia maumivu katika tumbo, mara nyingi maumivu haya katika tumbo huwa ni kama hali ya kuungua tumboni na hii ni kwa sababu kubwa ya kwamba mtu huyu kuta zake za tumbo zinakuwa zimeathirika sana na hasa maumivu haya huwa makali zaidi wakati tumbo likiwa halina kitu au pale mtu huyu akiwa anapata chakula.

Kupungua kwa uzito wa mtu na kukonda zaidi, na hii ni kwa sababu mtu huyu mwenye vidonda vya tumbo anakuwa anapata maumivu wakati anapopata chakula na pia anakuwa akila kidogo anahisi tumbo kujaa lakini kihalisia anakuwa na chakula kichache sana ndani ya tumbo basi matokeo yake ni kudhoofu mwili wa mwanadamu huyu na hivyo kukonda sana. Kama kuna mtu unamjua anakuwa anakumbwa na dalili kama hiyo basi ni vema kufika kwenye vituo vya afya bado mapema kwa ajili ya matibabu zaidi au tupigie simu kwa msaada zaidi.

0 comments:

Post a Comment