Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Thursday, October 9, 2014

IDADI YA WATU WENYE MATATIZO YA AKILI YAKIFIA ZAIDI YA WATU 450,000

Tanzania ina zaidi ya watu 450,000 wenye matatizo ya afya ya akili ambao wengi wao ni vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea tatizo lililotajwa kusababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi.


Mganga mkuu wa serikali Dkt. Donald Mbando ametoa takwimu hizo leo wakati akiongea na waandishi wa habari kueleke maadhimisho ya siku ya Afya ya akili duniani ambayo kitaifa yataadhimishwa tarehe 10 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Dkt. Mbando amesema ugonjwa wa afya ya akili pia umekuwa ukiwakumba wazee ambapo umekuwa ukiathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda na hivyo kuwa na mwenendo au tabia tofauti usioendana na jamii na kushauri kufikishwa mara moja katika vituo vya afya au hospitali kwa mtu mwenye dalili kama hizo.

WAKATI HUO HUO Serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imepata madaktari 5 ambao wamejitolea kwenda kusaidia nchi za Afrika magharibi ambazo zimekumbwa na ugonjwa wa Ebola.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mganga mkuu wa serikali Dakta DONAN MMBANDO amesema kuwa kutokana na ugonjwa huo kuwa tishio Afrika magharibi hasa nchi za sierra leone na Liberia madaktari hao wamejitolea kwenda kusaidiana na madakitari wa nchi hizo.

Kwa upande wa Tanzania Dakta MMBANDO amesema kuwa serikali imeboresha maandalizi ya mwitikio wa ugonjwa huo endapo utaingia hapa nchini kwa kutoa mafunzo kwa wataalam,kuboresha zaidi kituo maalum cha Temeke kwa ajili ya wagonjwa watakaohisiwa.

Aidha MMBANDO ameongeza kuwa kwa upande wa mipakani vipo vipimo maalum kwa ajili ya kutambua viashiria tu ili hatua ziweze kuchukuliwa endapo mtu atagundulika kuwa na ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola hauna tiba maalum wala chanjo bali unatibiwa kulingana na viashiria vinavyoonekana ambapo MMBANDO amesema mpaka sasa watu walioathirika na ugonjwa huo ni 7500 huku waliofariki ni 3500 wakiwemo wauguzi.

0 comments:

Post a Comment