Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Monday, October 6, 2014

BAYLOR YAKABIDHI VIFAA VYA MPANGO TIBA YA UTAPIA MLO MKALI KWA WATOTO MKOA WA MBEYA LEO

Shirika lisilo la Kiserikali la BAYLOR Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania na Shirika la UNICEF la Umoja wa Mataifa limekabidhi vitanda 10 vyenye thamani ya zaidi shilngi milioni 10 kwa wilaya 5 za Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya watoto wenye utapia mlo na wanaoishi na maambukizi ya VVU Mkoani hapa.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mashirika hayo Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki hiyo ya BAYLOR Mkoani Mbeya Dr. Theopista Jacob Masenga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na kwamba wilaya tano zitanufaika na msaada huo.

Wilaya zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Wilaya ya Mbozi,Mbeya,Mbarali na Rungwe katika mpango wa mwaka 2014/2015 na wilaya zilizosalia zitaingizwa katika mpango wa mwaka 2015/2016 ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuondoa usumbufu wanaoupata wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao wengi wao ni watoto.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vitanda 10 vya kisasa , magodoro 10 na makabati 10 ya kuhifadhiwa dawa ambapo Kaimu Mkurugenzi amesema vitasaidia kurahisisha utendaji wa kila siku wa huduma za tiba.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa aliyapongeza mashirika hayo kwa moyo wa kujitolea kuokoa maisha ya watoto na kwamba serikali inaunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na mashirika hayo na itaendelea kushirikiana nayo ili kuendelea kupunguza vifo vya watoto na udumavu wa ubongo ambao usipodhibitiwa ndani ya siku 1000 maisha ya mtoto yanakuwa yameharibika.

Kwa upande wake mganga mkuu wa Mkoa Seif Mhina ameyashukuru mashirika hayo ambayo yanatoa msaada mkubwa mkoani Mbeya na kwamba kituo hicho kinasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali ya Mkoa ambapo hupokea zaidi ya wagonjwa 300 kwa siku.





Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikata utepe kupokea vifaa Tiba

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro kushoto akimkabidhi vifaa tiba Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina akiishukuru BAYLOR kwa Msaada huo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akihutubia wananchi waliohudhuria hafla hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki ya BEYLOR Mkoa wa Mbeya Dkt. Theopista Masenga akisoma Risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na wageni waalikwa wakati wa Hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo

Hivi ndivyo vifaa tiba ambavyo vimetolewa na BAYLOR

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akipata maelekezo ya Moja ya vitanda hivyo hinavyofanya kazi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro alioneshwa kabati la kisasa linalotumika kuhifadhia dawa na Chakula.

Baadhi ya watumishi wa BAYLOR

Baadhi ya wananchi waliofika katika Hafla hiyo fupi



Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Mpoki Nulisubisya akiongea na wananchi waliofika katika Makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba katika kituo cha BAYLOR

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akimsalimia mmoja wa watoto ambaye ni Mgonjwa anayesoma Darasa la kwanza, alifurahishwa na jibu la Mtoto huyo alipo ulizwa akiwa mkubwa anataka kuwa nani na kujibu kuwa angependa kuwa Dactari.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika kitengo cha upimaji

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika Kitengo cha Kifua kikuu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akioneshwa eneo la mafunzo ambapo licha ya wagonjwa hao kupata matibabu lakini wanapatiwa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushonaji

Picha ya pamoja

0 comments:

Post a Comment