Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, October 29, 2014

UVIMBE KWENYE MJI WA MIMBA (FIBROID)-3

Uvimbe huweza pia kukandamiza viungo jirani na uzazi (pressure effets) ambapo mirija ya mkojo na kibofu cha mkojo na utumbo mkubwa wa haja kubwa na uvimbe unaweza kusababisha usipate choo(consipation) wakati mwingine huweza kusababisha mkojo usitoke (urinal retention), dalili zingine ni kama kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa (dyspararemia), uchafu sehemu za siri na kushindwa kubeba mimba (infertity) asilimia kati ya 27- 40 ya wenye uvimbe hupata tatizo la kutokushika mimba.

Dalili zingine ni kutokwa au kuharibika mimba (spontaneous abortion), hii hutoka kwa wagonjwa kati ya asilimia 40 kabla ya kutoa uvimbe na asilimia 20 baada ya upasuaji wa kutoa uvimbe.

Vipimo
Vipimo muhimu kujua au kutambua uvimbe kwenye kizazi ni kama vile mgonjwa anapohudhuria hospitali anavyopimwa tumboni (bimanual pelvic examination).Vipimo vya mahabara ni kama kujua wingi wa damu ili kujua kama mgonjwa amepungua damu (andemia) na aina ya pili ni upimaji kugundua kama mtu husika ana upungufu wa madini ya chuma (iron defficienty).

Vipimo vya damu kujua kama mgonjwa amepata maambukizi kwenye uvimbe, tunapima ESR kuona kama imepanda.Vipimo vingine Ultasound husaidia kugundua aina ya uvimbe na kutofautisha kama mgonjwa ana ujauzito au ni uvimbe pekee.

Vipimo vingine ni kama dawa kupitishwa kwenye mirija na baada ya hapo kupigwa x-ray pia husaidia kugundua kama uvimbe uko ndani.Vipimo vingine ni kama MRI hivyo ni vya uhakika zaidi na ni uhakika kwani hujua ukubwa wa uvimbe na madhara yake, vipimo vingine kama IVP husaidia kuona kama uvimbe umeenea kwenye mfumo wa mkojo hasa kibofu cha mkojo.

Kipimo kingine ni HYSTROSCOPY hiki husaidia kugundua na kuondoa uvimbe kama aina ya subrmucous myoma.Magonjwa yanayofanana na uvimbe kwenye kizazi (differential diagnosi) mara nyingi ni muhimu na husaidia kutofautisha na ujauzito pia kutofautisha uvimbe mwingine kwenye maeneo ya mfumo wa kizazi, pia kutofautisha na saratani ya mfuko wa mayai (avarian cancer).

Itaendelea wiki ijayo.

Friday, October 24, 2014

MGONJWA KWANZA KUUMWA EBOLA NCHINI


Serikali ya Mali imethibitisha kuhusiana na taarifa za mtoto wa miaka 2 kukutwa na maambukizi ya Ebola akiwa ni mtu wa kwanza kupata maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo tangu ugonjwa huo ulipozuka mwezi Machi 2014.

Taarifa kutoka mtandao wa the World Post zimesema, mtoto huyo amegundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo aliporejea nchini humo akitokea Guinea, moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola Afrika Magharibi.

Mali inakuwa nchi ya sita kutangaza kupatikana mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola katika ukanda wa Afrika Magharibi, lakini ndani ya siku 7 nchi za Senegal na Nigeria zimetangaza kutokuwa na mgonjwa mwenye maambukizi ya Ebola.

Ripoti iliyotolewa na WHO imeonesha vifo zaidi ya 4,900 vimetokea katika nchi za Sierra Leone, Guinea na Liberia.

Timu ya wanasayansi wa kimataifa imejipanga kutafiti uwezekano wa kutumia damu ya mtu aliyewahi kupona Ebola kama tiba ya ugonjwa huo.

Mali inapakana na nchi ya Guinea kwa upande wa Kusini Magharibi, lakini mtoto huyo anakuwa mgonjwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na maambukizi ya Ebola nchini humo.

T.I AULIZWA MAREKANI KUHUSIANA NA EBOLA TANZANIA BAADA YA KUFANYA TAMASHA KUBWA BONGO




Alikua mgeni kwenye stage ya Tamasha la Fiesta lililofanyika Leaders club October 18 2014 akiwa na timu yake ya watu wasiopungua watano na kuisimamia hiyo show kwa zaidi ya dakika 60.

Baada ya show Jumamosi, T.I aliondoka Tanzania Jumapili kurudi kwao Marekani kwa ajili ya kuhakikisha promo inakwenda vizuri sababu album yake mpya ilikua inatoka Jumanne ya October 21.

Akiwa NewYork T.I alijikuta yuko mbele ya camera akihojiwa na mwandishi wa habari aliemuuliza kuhusu ishu ya Iggy na Snoop ambayo alisaidia kuimaliza na baada ya hapo akamuuliza T.I vp Tanzania ilikuaje? Ebola je?

T.I alichojibu ni hiki >>> ‘Tanzania ilikua poa sana, sijaona Ebola yoyote wala kuona hata dalili za kuwepo kwa ugonjwa huo, sijaona chochote cha kunifanya niifikirie Ebola au kuhisi uwepo wake‘

Unaweza kumtazama T.I hapa chini

BONYEZA HAPA KUONA VIDEO

Muda mfupi kabla ya T.I kuja Tanzania ziliripotiwa stori kwamba rapper huyu amekua kiburi kwa kuamua kwenda Afrika pamoja na kwamba bara hili limekumbwa na ugonjwa hatari wa Ebola.

Mtandao wa TMZ uliripoti kwamba Management ya T.I imesisitiza ni lazima mkali huyu afanye hiyo show ya Fiesta na kwamba hakuna dalili zozote za Ebola kwenye ardhi ya Tanzania.

TMZ walizidi kuripoti kwamba Utafiti wa Oxford University ulisema Tanzania ni miongoni mwa nchi 15 za Afrika zilizo kwenye hatari ya kukumbwa na Ebola na ndio maana walishauri kama ingekua noma basi T.I afanye show akiwa kwenye puto kama Akon.



Thursday, October 23, 2014

TAMBUA SABABU ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (MISCARRIAGE)


Wiki iliyopita tuliongelea sana tatizo la kuharibika kwa mimba na tukagusia baadhi ya dalili ambazo zinaweza kumpata mwanamke anayeweza kukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba. Na dalili hizo ni kama;

DALILI ZA KUHARIBIKA KWA MIMBA (Miscarriage)

  • Dalili kubwa kabisa ya kwanza ni damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba.
  • Dalili kubwa ya pili ni mwanamke kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito.
  • Dalili nyingine kubwa ni uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo {miscarriage}. Wiki iliyopita tuliishia hapo, na sasa wiki hii;

Maumivu makali ya tumbo, wakati mwanamke anapokuwa ni mjamzito lakini wakati huo huo anapatwa na maumivu makali ya tumbo ya mara kwa mara yakiambatana na maumivu ya kiuno pamoja na kutokwa na damu nyepesi au nzito basi ujue ujauzito wako uko kwenye hatari ya kutoka, ni vizuri ukawasiliana na kituo cha karibu cha afya au ukawasiliana nasi kwa matibabu zaidi.


VYANZO VYA KUHARIBIKA KWA MIMBA {Miscarriage}

Vyanzo vikubwa vya kuharibika kwa mimba ni kama vifuatavyo;
Chromosome abnormalities, mimba nyingi ambazo huharibika hadi wiki ya ishirini husababishwa na tatizo hili la chromosomes, na chromosomes huwa zinabeba genes ambazo huyatambulisha maumbile ya mwanadamu kwa nje, yaani jinsia yake, ngozi yake itakuaje, macho yake na vitu vingine vingi nisingependa tuingie ndani sana lakini matatizo haya ya chromosomes huchangia sana kuharibika kwa mimba.

Maambukizi katika mji wa uzazi wa mwanamke {Infections}, kuna kitu kinaitwa Pelvic Inflammatory Diseases {PID} yaani kuvimba kwa kuta za mji wa mimba au kuvimba kwa mirija ya uzazi nayo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba kwa mwanamke, lakini pia Candida au fangasi nazo pia huchangia sana kuharibika kwa mimba.

Chanzo kingine kikubwa ni utoaji wa mimba za mara kwa mara, wanawakie au wasichana wenye tabia ya kutoa mimba moja au mbili au tatu basi nao pia hukutwa na tatizo hili la kuharibika kwa mimba kwani uingizaji wa vyuma ndani huweza kuharibu shingo ya kizazi ya mwanamke na pia kukumbwa na tatizo hili la miscarriage au kuharibika kwa mimba.

Chanzo kingine kikubwa ni magonjwa ya zinaa {sexually transmitted diseases}, magonjwa kama gonorrhea, kaswende mara nyingi sana huathili mfumo wa uzazi wa mwanamke na hasa hasa kwenye mji wa mimba na kuufanya kuwa legevu na hata ujauzito unapotunga basi huweza kutoka kwa haraka zaidi na hivyo kusababisha tatizo hili la kutoka kwa mimba {Miscarriage}.

Chanzo kingine cha mimba kuharibika ni tatizo la kisukari kwa mwanamke, hii nayo huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuharibika kwa mimba na mtu ambaye hafanyi uangalizi wa karibu wa tatizo la sukari basi husababisha glucose isitumike kama energy na hivyo kuleta madhara katika kizazi hasa ujauzito.

Kitu kingine ni hormones {homoni} kuvurugika, kwa mfano hormone ya progesterone mara nyingi hufanya ile kazi ya kutunza mimba iendelee kukuwa, na kama kunatokea unbalance au kuvurugika kwa homoni hii basi mara nyingi tatizo hili la mimba kuharibika hutokea. Kama unakumbwa na moja ya mambo kama haya na usingependa kupatwa na tatizo hili la kutokwa kwa mimba basi ni vema kama utaawasiliana nasi kwa ushauri na tiba zaidi.Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.Nawatakia afya iliyo njema kabisa.
Itaendelea wiki ijayo.

Tuesday, October 21, 2014

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO-2




MADHARA YA TUNDU KATIKA MOYO
Madhara ambayo yanaweza kusababishwa na tundu katika kuta za chini za moyo ni Eisenmenger syndrome, hali ambayo hutokea pia pale mtu anapokuwa na tundu katika kuta za juu za moyo.
Tatizo hili hutokea wakati mtiririko wa damu unapoongezeka kutoka kushoto kwenda kulia kupitia tundu katika kuta za moyo, suala ambalo huongeza mtiririko wa damu katika mishipa ya mapafu na kusababisha shinikizo la damu katika mapafu.

Hali hii husababisha ongezeko la shinikizo la damu katika upande wa kulia wa moyo na kubadilika kwa shanti kutoka kulia kwenda kushoto.

Matokeo yake ni kuwa damu isiyo na oksijeni iliyotakiwa kwenda kwenye mapafu kwa ajili ya kusafishwa huchanganyika na damu yenye oksijeni iliyoko upande wa kushoto na kusambaa mwilini.
Madhara mengine ya tundu la VSD ni kupata ugonjwa wa kiharusi, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri pia maambukizi katika kuta za ndani za moyo (endocarditis) ugonjwa ambao tutauelezea katika matoleo yajayo.

Akinamama waliozaliwa na tatizo hili, ambao wametibiwa na hawakupata madhara wanaweza kushika mimba na kupitisha kipindi cha ujauzito bila matatizo yoyote.
Isipokuwa wale ambao hawakutibiwa au ambao tayari wameshapata madhara, hushauriwa kutoshika ujauzito kwa sababu ya hatari zinazoweza kutokea katika kipindi cha ujauzito.
Vilevile kwa akinamama waliozaliwa na tatizo hili, uwezekano wa watoto wao kuzaliwa na tatizo hili huwa mkubwa.

TIBA
Inafaa kujua kuwa, karibu nusu ya wagonjwa wenye tatizo hili huwa hawahitaji matibabu ya aina yoyote ile kwa kuwa tatizo hili hujirekebisha katika miaka ya mwanzo ya maisha yao.
Hata hivyo, kwa wale ambao watahitaji matibabu, hutibiwa kwa dawa au upasuaji kwa kutegemea ukubwa wa tatizo lenyewe.

Dawa zinazotumika kutibu ugonjwa huu ni zile ambazo hupunguza kasi ya moyo, huongeza nguvu ya mapigo ya moyo na zile ambazo hupunguza maji mwilini au diuretics.
Utaratibu wa kuziba tundu umegawanyika katika sehemu mbili na hufanyika iwapo tundu ni kubwa sana, au halikujirekebisha lenyewe wakati mtoto alipokuwa anakua na pale ikiwa dawa alizopewa mgonjwa hazikusaidia.

Pale inapohitajika upasuaji, mgonjwa hufanyiwa oparesheni ambapo kifua hufunguliwa ili kuziba tundu la VSD.

Matibabu mengine ni kupitisha mrija katika mshipa wa damu hadi katika sehemu ya tatizo kwenye moyo na kuliziba kwa kutumia kifaa maalumu. Kwa njia hii, huwa hakuna haja ya kufanya upasuaji wa kufungua kifua cha mgonjwa.

MWISHO

UVIMBE KWENYA MJI WA MIMBA (FIBROID)-2





Naendelea kuelezea dalili za uvimbe kwenye mji wa mimba ili uweze kuzijua na kuchukua hatua mapema.

Dalili hutegemea na sehemu uvimbe ulikojishikiza, ukubwa wa uvimbe na kama mama ana ujauzito, uvimbe huambatana na kutokuwa na mpangilio wa hedhi hii hutokea kwa akina mama asilimia 30 ambapo mama huingia kwenye siku zake mara mbili kwa mwezi au kutoingia kabisa akifuatiwa na kumwaga damu nyingi wakati wa hedhi ambapo anaweza kupata upungufu wa damu.
UVIMBE KATIKA KIZAZI

Dalili
Dalili za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi ni kutokwa na damu kusipokuwa na mpangilio (abnormal uterine bleeding).

Hii huwapata akina mama kiasi cha asilimia 30 na huwa damu inatoka sana au kuendelea kutokwa na damu kwa muda mrefu zaidi ya siku 10 ambapo mgonjwa hupata madhara ya kupoteza madini ya chuma na kusababisha upungufu wa damu (iron deficiency anaemia) wale wenye uvimbe kwenye misuli ya uzazi ujulikanao kama sub mucous myoma wenyewe hupitiliza muda wa kuona siku zao na kutokwa vitone vidogo vya damu

. Kutoka kwa damu hutokana na muingiliano wa mishipa ya damu kwenye uzazi ambapo hukandamizwa na kusababisha kuta za ndani ya uzazi kutofanya kazi zake vizuri na wale wenye uvimbe wa ndani ya ukuta wa uzazi (pedunulated submcous) wenyewe hupata tatizo la kutokwa damu mara kwa mara ambapo mgonjwa anaweza kutokwa damu leo halafu ikisimama baada ya siku tatu inatoka tena.

Maumivu ya tumbo husababishwa na kukandamizwa kwa mishipa ya fahamu ya mfuko wa uzazi na wakati mwingine uvimbe hupata vijidudu (infection)na kuleta maumivu makali ambayo husambaa hadi kiunoni na kwenye miguu.

Itaendelea wiki ijayo.

Wednesday, October 15, 2014

MARK ZUCKERBERG KUCHANGIA EBOLA

Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg (kulia) akiwa na mkewe, Priscilla Chan.

Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg amesema yeye na mkewe Priscilla Chan, watachanga dola milioni 25 za kusiadia vita dhidi ya Ebola.

UGONJWA WA TUNDU KATIKA MOYO KWA WATOTO




Kama kawaida safu hii huwa tunajadili masuala mbalimbali yanayohusu afya na tiba ili kupata ufahamu zaidi juu ya kuimarisha afya zetu na ya jamii kwa ujumla.
Leo tutazungumzia ugonjwa unaojulikana kama tundu katika kuta za ventrikali za moyo au kwa kitaalamu Ventricular Septal Defect (VSD).

Tatizo hili hutokea mara nyingi ambapo watoto 2-6 kati ya 1,000 uzaliwa nalo.
Tundu katika kuta za chini za moyo au VSD ni pale panapokuwepo na uwazi katika sehemu ya kuta ya septum inayotenganisha chemba za ventrikali zilizo chini ya moyo.

Moyo unapoanza kuumbika huanza kama bomba lililo wazi na kuendelea kujigawa katika sehemu mbalimbali na kuunda kuta.
Iwapo kitendo hicho hakitatekelezwa ipasavyo, hutokea uwazi katika kuta ya septum kwenye chemba za chini.

Kuwepo tundu hilo huruhusu damu yenye oksijeni kupita kutoka chemba ya kushoto ya chini ya moyo na kuingia katika chemba ya kulia ya chini ya moyo, badala ya kuingia kwenye mshipa wa aorta na kuelekea nje ya moyo kama inavyotakiwa.

Tundu la VSD linaweza kuwa dogo, la kati au kubwa. Tundu dogo katika kuta za chini za moyo huruhusu damu ndogo tu kutoka upande mmoja wa moyo kwenda wa pili hivyo haliathiri utendaji wa kawaida wa moyo na kwa kawaida huwa halihitaji matibabu maalumu.

Matundu ya aina hiyo huziba yenyewe wakati moyo unapoendelea kukua kipindi cha utotoni. Matundu yenye ukubwa wa kati na kubwa katika kuta za chini za moyo huruhusu kiwango kikubwa zaidi cha damu kupenya toka upande mmoja wa moyo kwenda mwingine, na mara nyingi huhitaji matibabu maalumu.

Watoto wenye tundu dogo katika moyo, huweza kukua bila matatizo yoyote, wakati wale wenye tundu kubwa huanza kuonyesha dalili mapema.

Vifuatavyo ni vihatarishi ambavyo vinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa na tundu katika kuta za chini za moyo. Mama kuwa na maambukizi ya Rubella katika kipindi cha ujauzito au kuwa na ugonjwa wa kisukari cha wakati wa ujauzito ambao haujadhibitiwa na kuwa mnywaji wa pombe au mtumiaji wa madawa ya kulevya.

Mjamzito akitumia bila ushauri wa daktari baadhi ya dawa za hospitali katika kipindi cha ujauzito pia huweza kusababisha mtoto azaliwe na tundu katika kuta za chini za moyo.

DALILI
Iwapo tundu ni dogo huwa halina dalili yoyote na pale mtoto anapoendelea kukua tundu hilo hujifunga lenyewe. Lakini tundu likiwa kubwa, japokuwa mtoto anayezaliwa huwa haonyeshi dalili yoyote katika kipindi hicho lakini baadaye huwa na dalili zifuatazo.

Rangi ya ngozi yake, midomo na kucha hubadilika na kuwa ya bluu, kunyonya au kula huwa kwa shida sana, ukuaji na kupumua kwa shida, kuchoka haraka, kujaa miguu na kuvimba tumbo, kuwa na mapigo ya moyo ya haraka.

Mtoto mwenye tatizo hili anapopimwa na daktari kwa kifaa, huweza kusikia ishara ya ongezeko la sauti ya ziada ya mapigo ya moyo wa mtoto hali ambayo kitaalamu huitwa holosystolic murmur.

Itaendelea wiki ijayo.

Tuesday, October 14, 2014

EBOLA OUTBREAK: UN HEALTH WORKER DIES IN GERMANY HOSPITAL

The Ebola patient was being treated at St Georg hospital in Leipzig
Continue reading the main story

Ebola outbreak
How not to catch Ebola
Living with Ebola
Why so dangerous?
Mapping the outbreak

A UN medical worker infected with Ebola has died at a hospital in Germany.

Doctors at the hospital in Leipzig said the man, 56, originally from Sudan, died despite receiving experimental drugs to treat the virus.

More than 4,400 people have died from the outbreak, mainly in West Africa.

The rate of new cases at some of the "epicentre" areas has slowed down, the World Health Organization says, but the number of cases in the capitals of the worst-affected countries is rising.

Senior WHO official Bruce Aylward told reporters on Monday that the outbreak was also continuing to spread geographically to new districts in the capitals of Sierra Leone, Liberia and Guinea.

Elsewhere:
  • The US and UK are among countries to have introduced scanning at airports
  • A Spanish nurse remains in critical condition after becoming the first person to contract the disease outside of Africa last week, although doctors say there are signs of improvement
  • UN Ebola mission leader Tony Banbury has called for massive support from governments worldwide, saying: "We need everything. We need it everywhere, and we need it superfast."

Monday, October 13, 2014

WAZIRI SOPHIA SIMBA AZINDUA KAMPENI YA SARATANI DAR ES SALAAM

KAMPENI ya kuchangia matibabu ya saratani ya matiti nchini imezinduliwa leo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, jijini Dar es Salaam ambapo amewataka wananchi kuchangia shilingi 1,000 kwa kila mtu ili kuunga mkono hatua hiyo.

Kampeni hiyo inaendeshwa na Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania (Tanzania Breast Cancer Foundation) na wataalam wake wanasema ugonjwa huo unatibika ukiwahiwa mapema


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).


Kulia ni Bingwa wa Magonjwa ya Saratani Hospitali ya Ocean Road, Dk. Dominista Kombe (katikati); Mkurugenzi wa Habari hospitali hiyo, Assah Mwambene; Waziri Simba na Mkurugenzi wa Asasi ya Saratani ya Matiti Tanzania, Angela Kuzilwa, wakiwa katika uzinduzi huo.

Wanahabari wakiwa kazini.





.
Sehemu ya hotuba ya waziri Simba.

Sunday, October 12, 2014

TAHARUKI YA EBOLA UWANJA WA NDEGE WA JOMO KENYATTA, KENYA

TAHARUKI imezuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi nchini Kenya, leo asubuhi baada ya abiria aliyekuwa mgonjwa kufariki dunia muda mfupi alipowasili uwanjani hapo.

Abiria huyo mwanamke alikuwa akitokea Juba, Sudan Kusini lakini kukawepo tetesi kuwa huenda amefariki kwa ugonjwa wa Ebola.


Vipimo vya madaktari vimeonesha kuwa mgonjwa huyo hakufa kwa Homa ya Ebola. Katibu wa Afya wa Baraza la Mawaziri nchini Kenya, James Macharia amethibitisha kuwa mgonjwa huyo hakuwa na Homa ya Ebola.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa waliwaona maofisa wa afya wakielekea katika Kliniki ya Port ambapo mgonjwa huyo alikimbizwa kabla ya mauti kumfika.

Viwanja vya ndege ni baadhi ya maeneo yaliyo katika uangalizi kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola ambao mpaka sasa umeua watu zaidi ya 4,000 kwenye ukanda wa magharibi mwa Afrika.
Shirika la Ndege la Kenya Airways lilisitisha safari zake katika ukanda wa magharibi mwa Afrika kwa kuogopa maambukizi ya ugonjwa huo.

Thursday, October 9, 2014

IDADI YA WATU WENYE MATATIZO YA AKILI YAKIFIA ZAIDI YA WATU 450,000

Tanzania ina zaidi ya watu 450,000 wenye matatizo ya afya ya akili ambao wengi wao ni vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea tatizo lililotajwa kusababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi.


Mganga mkuu wa serikali Dkt. Donald Mbando ametoa takwimu hizo leo wakati akiongea na waandishi wa habari kueleke maadhimisho ya siku ya Afya ya akili duniani ambayo kitaifa yataadhimishwa tarehe 10 mwezi huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Dkt. Mbando amesema ugonjwa wa afya ya akili pia umekuwa ukiwakumba wazee ambapo umekuwa ukiathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda na hivyo kuwa na mwenendo au tabia tofauti usioendana na jamii na kushauri kufikishwa mara moja katika vituo vya afya au hospitali kwa mtu mwenye dalili kama hizo.

WAKATI HUO HUO Serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imepata madaktari 5 ambao wamejitolea kwenda kusaidia nchi za Afrika magharibi ambazo zimekumbwa na ugonjwa wa Ebola.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mganga mkuu wa serikali Dakta DONAN MMBANDO amesema kuwa kutokana na ugonjwa huo kuwa tishio Afrika magharibi hasa nchi za sierra leone na Liberia madaktari hao wamejitolea kwenda kusaidiana na madakitari wa nchi hizo.

Kwa upande wa Tanzania Dakta MMBANDO amesema kuwa serikali imeboresha maandalizi ya mwitikio wa ugonjwa huo endapo utaingia hapa nchini kwa kutoa mafunzo kwa wataalam,kuboresha zaidi kituo maalum cha Temeke kwa ajili ya wagonjwa watakaohisiwa.

Aidha MMBANDO ameongeza kuwa kwa upande wa mipakani vipo vipimo maalum kwa ajili ya kutambua viashiria tu ili hatua ziweze kuchukuliwa endapo mtu atagundulika kuwa na ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Ebola hauna tiba maalum wala chanjo bali unatibiwa kulingana na viashiria vinavyoonekana ambapo MMBANDO amesema mpaka sasa watu walioathirika na ugonjwa huo ni 7500 huku waliofariki ni 3500 wakiwemo wauguzi.

Monday, October 6, 2014

BAYLOR YAKABIDHI VIFAA VYA MPANGO TIBA YA UTAPIA MLO MKALI KWA WATOTO MKOA WA MBEYA LEO

Shirika lisilo la Kiserikali la BAYLOR Mkoa wa Mbeya nchini Tanzania na Shirika la UNICEF la Umoja wa Mataifa limekabidhi vitanda 10 vyenye thamani ya zaidi shilngi milioni 10 kwa wilaya 5 za Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya watoto wenye utapia mlo na wanaoishi na maambukizi ya VVU Mkoani hapa.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya mashirika hayo Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki hiyo ya BAYLOR Mkoani Mbeya Dr. Theopista Jacob Masenga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro na kwamba wilaya tano zitanufaika na msaada huo.

Wilaya zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Wilaya ya Mbozi,Mbeya,Mbarali na Rungwe katika mpango wa mwaka 2014/2015 na wilaya zilizosalia zitaingizwa katika mpango wa mwaka 2015/2016 ili kusogeza huduma karibu na wananchi na kuondoa usumbufu wanaoupata wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao wengi wao ni watoto.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na vitanda 10 vya kisasa , magodoro 10 na makabati 10 ya kuhifadhiwa dawa ambapo Kaimu Mkurugenzi amesema vitasaidia kurahisisha utendaji wa kila siku wa huduma za tiba.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa aliyapongeza mashirika hayo kwa moyo wa kujitolea kuokoa maisha ya watoto na kwamba serikali inaunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na mashirika hayo na itaendelea kushirikiana nayo ili kuendelea kupunguza vifo vya watoto na udumavu wa ubongo ambao usipodhibitiwa ndani ya siku 1000 maisha ya mtoto yanakuwa yameharibika.

Kwa upande wake mganga mkuu wa Mkoa Seif Mhina ameyashukuru mashirika hayo ambayo yanatoa msaada mkubwa mkoani Mbeya na kwamba kituo hicho kinasaidia kupunguza msongamano katika Hospitali ya Mkoa ambapo hupokea zaidi ya wagonjwa 300 kwa siku.





Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akikata utepe kupokea vifaa Tiba

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro kushoto akimkabidhi vifaa tiba Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Seif Mhina akiishukuru BAYLOR kwa Msaada huo

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akihutubia wananchi waliohudhuria hafla hiyo

Kaimu Mkurugenzi wa Kliniki ya BEYLOR Mkoa wa Mbeya Dkt. Theopista Masenga akisoma Risala mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro na wageni waalikwa wakati wa Hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo

Hivi ndivyo vifaa tiba ambavyo vimetolewa na BAYLOR

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akipata maelekezo ya Moja ya vitanda hivyo hinavyofanya kazi

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro alioneshwa kabati la kisasa linalotumika kuhifadhia dawa na Chakula.

Baadhi ya watumishi wa BAYLOR

Baadhi ya wananchi waliofika katika Hafla hiyo fupi



Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Mpoki Nulisubisya akiongea na wananchi waliofika katika Makabidhiano ya msaada wa vifaa tiba katika kituo cha BAYLOR

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akimsalimia mmoja wa watoto ambaye ni Mgonjwa anayesoma Darasa la kwanza, alifurahishwa na jibu la Mtoto huyo alipo ulizwa akiwa mkubwa anataka kuwa nani na kujibu kuwa angependa kuwa Dactari.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika kitengo cha upimaji

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akiwa katika Kitengo cha Kifua kikuu

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro akioneshwa eneo la mafunzo ambapo licha ya wagonjwa hao kupata matibabu lakini wanapatiwa mafunzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushonaji

Picha ya pamoja

Wednesday, October 1, 2014

DR. FADHIL EMILY WA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC AHUDHURIA KIKAO CHA KUTETEA TIBA ASILIA AKIWEPO MH. KINGUNGE GOMBALIMWIRU DODOMA

Dr. Fadhil Emily akiongea na bloger wa Fadhaget Sanitarium Clinic alisema, alikwenda Dodoma kwa mualiko wa kuhudhuria kikao cha kutetea Tiba Asilia. Mambo yaliyoongelewa ni kutaka serikali ya Tanzania kutambua kuwa Chuo cha Mheshimiwa Dr. Dadao ni cha uhakika na kutambua kuwa wasomi waliopo hapo chuoni wana mafunzo bora na wanaweza kufanya kazi ya kuwahudumia watu kwa njia ya Tiba Asilia. Kikao hicho kilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania akiwemo Waziri wa Afya na Mh. Kingunge Ngombalimwiru.

Katika kikao hicho Dr. Fadhil Emily aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala Tanzania.


 Wa pili kutoka kulia ni Dr. Fadhil Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic na wa tatu kutoka kulia ni Mh. Kingunge Gombalimwiru


BREAKING NEWS: EBORA YATUA MAREKANI




Mgonjwa wa kwanza wa ugonjwa hatari wa virusi vya Ebola amegundulika nchini Marekani, imethibitishwa katika mji wa Dallas, Texas.
Maafisa katika kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa ametengwa katika hospitali hiyo.
Mgonjwa huyo anasemekana kuwa ni mtu anayeaminika kuambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia kabla ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo.
Zaidi ya watu 3,000 tayari wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi na idadi ndogo ya wafanyakazi wa Marekani wa mashirika ya misaada wamepata nafuu baada ya kupelekwa kutibiwa Marekani.

Jumatatu, maafisa wa kituo cha afya cha Texas katika hospitali ya Presbyterian ya Dallas wamesema mgonjwa ambaye hakutajwa jina alikuwa akichunguzwa virusi vya Ebola na ametengwa katika hospitali hiyo.

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mpaka sasa zaidi ya watu 3,000 wamekufa kutokana na virusi vya Ebola, wengi wa waliokufa ni kutoka Liberia.
Nchini Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika kuna wagonjwa 19 waliothibitika kuugua ugonjwa wa Ebola na watu wanane wamekufa tangu mgonjwa wa kwanza kuthibitishwa nchini humo mwezi Julai..

Kuna mgonjwa mmoja aliyethibitika nchini Senegal, lakini hakuna taarifa za kifo mpaka sasa.
Ebola ni ugonjwa hatari wa virusi kuwahi kuzuka duniani.

CHANZO: BBC

MATATIZO YA UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA (CONGENITAL HEART DISEASE) -2




Wiki iliyopita tulikuwa tumeanza kuzungumzia juu ya matatizo ya moyo ya kuzaliwa sehemu ya kwanza, leo tunaendelea sehemu ya pili na ya mwisho.Vilevile sababu nyingine inayoweza kufanya mtoto azaliwe na matatizo ya moyo ni ugonjwa wa kisukari kwa mama wakati wa ujauzito.

Leo tuangalie tatizo la mtoto kuzaliwa na tundu katika kuta za juu za moyo au Atrial Septal Defect (ASD).
Wakati kijusi (fetus) kinapoendelea kukua, kuta kati ya atria mbili za moyo inayoitwa kitaalamu interatrial septum nayo pia hukua ili kutenganisha chemba ya kulia na kushoto.

Lakini katika kipindi hiki huwa kuna tundu kati ya kuta hizo linaloitwa foramen ovale. Tundu hili ni la kawaida kwa kipindi hiki cha kijusi na husababisha damu yenye oksijeni kutoka kwenye kondo la nyuma (placenta) kutokwenda kwenye mapafu ambayo bado hayajakomaa na kuelekea sehemu nyingine za mwili hasa kichwani.

Kipande cha tishu kinachoitwa kitaalamu septum primum hufanya kazi kama valvu katika tundu hilo. Mara tu mtoto anapozaliwa, shinikizo katika mishipa ya damu ya mapafu (pulmonary circulatory system) hushuka na kusababisha tundu hilo kufunga kabisa.

Iwapo tundu hilo halitafunga wakati huu mtoto huzaliwa akiwa na tundu katika moyo. Tundu hilo huwa halifungi kabisa kwa karibu asilimia 25 ya watu, hivyo pindi shinikizo la damu linapoongezeka katika mishipa ya damu ya mapafu kutokana na sababu mbalimbali, au kutokana na matatizo ya kikohozi cha muda mrefu, husababisha tundu la foramen ovale kutofunga na kubakia wazi.

Tatizo hili hutokea kwa mtoto mmoja katika kila watoto 1,500 wanaozaliwa. Lakini kwa kuwa pindi mtoto anapozaliwa huwa hakuna dalili zozote za tatizo, mara nyingi huwa haligunduliki mapema hadi pale anapokua.

Zipo aina kuu 6 za tundu katika kuta za juu za moyo lakini aina ya Ostium secundum hutokea kwa wingi, na huchangia kwa asilimia 6 hadi 10 ya magonjwa yote ya moyo ya kuzaliwa nayo. Tatizo hilo hutokana na ukubwa wa tundu la foramen ovale na kutokukua vyema ukuta unaoitenganisha. Hata hivyo, karibu asilimia 70 ya watu wenye tatizo hili huweza kufikisha miaka 40 ndipo dalili huanza kujitokeza.

Katika baadhi ya nchi zilizoendelea kama Marekani watoto wote wanaozaliwa hupimwa ili kuona kama wana tundu katika mioyo yao, na wale wanaopatikana na tatizo hilo hufanyiwa matibabu ya upasuaji na kurekebishwa tatizo hilo.

Itaendelea wiki ijayo.