Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Thursday, April 2, 2015

DR. FADHIL EMILY WA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC MBEZI BEACH ALIVYOWEZA KUTOA VIFAA MBALIMBALI KWA WANAFUNZI WA TSJ KATIKA TSJ BASH JIJINI DAR

Picha zimepigwa na RUMAFRICA +255 715 851 523

MKURUGENZI wa Kliniki ya The Fadhaget Sanitarium iliyoko Mbezi–Afrikana jijini Dar, Dk. Fadhili Emily ametoa msaada wa vifaa vya kujifunzia wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times School Of Jounalism ‘TSJ’ kama zawadi kwa kutambua umuhimu wa habari nchini. Dk. Fadhili alifanya makabidhiano hayo jana wakati wanafunzi wa chuo hicho walipokuwa wamekwenda kufanya sherehe fupi kwa ajili ya mapumziko katika Viwanja vya Fun City, Kigamboni jijini Dar wakiwa na walimu wao pamoja na mkuu wa chuo hicho, Blandina Semaganga.

Miongoni mwa zawadi ambazo Dk. Fadhili aliwazawadia wanachuo hao ni pamoja na ‘tape recoder’, kamera na jezi za mpira wa miguu. Mbali na kuwasaidia wanachuo hao, Dk. Fadhili alisema atakuwa bega kwa bega kusaidia wanafunzi wa vyuo vingine vya habari kwani kufanya hivyo ni moja ya kuwatia nguvu wanafunzi wawapo vyuoni. Alisema kuwa kwa kutambua na kuthamini mchango kwa Watanzania katika kuunga jitihada za kuendeleza huduma zake za afya katika kliniki yake ya The Fadhaget Sanitarium ataweza kuwapatia elimu juu ya matumizi mazuri ya teknolojia ya simu za mikononi na jinsi ya kujilinda na matumizi mabaya ya simu.

Naye mkuu wa chuo hicho, Blandina alimpongeza Dk. Fadhili kwa kuweza kuwapatia msaada huo kwani ametambua vikwazo vinavyosababisha wanafunzi wengi wa vyuo vya habari kukosa vifaa vya kujifunzia na kuomba juhudi hizo ziendelee kwa wadau wengine.

MKUU WA CHUO CHA TSJ NA MAGENI RASMI WAKIWASILI NDANI YA ENEO LA TUKIO
 Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha TSJ, Blandina Semaganga(wa nne kutoka kushoto)
Rais wa wanafunzi TSJ John Kisaka (kushoto) Dr. Emily Fadhili wa The Fathaget Sanitarium Clinic (wa tatu kuliko kushoto), Mkuu wa Chuo cha TSJ
Blandina Semaganga
Mkurugenzi wa Rumafrica wa pili kutoka kulia Rulea Sanga akiwa amshikilia kipaza sauti cha Clouds TV

Dr. Fadhili Emily akihojiwa na waandishi wa Habari eneo la Fun City Kigamboni Dar


Baadhi ya wanaandish wa habari kutoka TSJ na vyombo mbalimbali vya habari kama Star TV
Uncle Jimmy wa Clouds TV kipindi cha CHOMOZA

 
 John Kissaka (kushoto)-Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TSJ akiwa na "Cordinator" wa Chuo Suzan Ndosi
 Mgeni Rasmi Dr. Fadhili Emily wa klinik ya The Fadhaget (kulia) na akiwa na Sweetbeth Bruno
 
MC

KIPINDI CHA KUTAMBULISHANA
  John Kissaka (kulia)-Rais wa Wanafunzi wa Chuo cha TSJ
 Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha TSJ, Blandina Semaganga (aliyesimama)

Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic Mbezi Beach


Mwanafunzi Florida Moses akijaribu kujibu swali linalolohusu kutoa maana ya FM
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha TSJ, Blandina Semaganga

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
 
 Crew ya The Fadhaget Sanitarium Clinic

KIPINDI CHA BURUDANI KUTOKA KWA WASANII WA TSJ

Mwanafunzi wa TSJ akipga picha

Mwanachuo Florida Moses akitumbuiza
 
Mwanachuo Florida Moses akitumbuiza
 
 Mwanachuo Florida Moses akitumbuiza
 
 
Mwanachuo Florida Moses akitumbuiza
 


Kutoka kulia ni Mc. Bony Magupa (mtangazaji wa Praise Power Radio) wanaofuata ni Crew ya Smart Visual Production.

ANGALIA MATUKIO MENGINE KWA KUBONYEZA "Read More" HAPO CHINI

MAMIA WAMZIKA ABDUL BONGE KIJIJINI KWAO MKUYUNI, MATOMBO MKOANI MORO


Maziko ya Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge yakifanyika leo kijijini kwao Mkuyuni, Matombo mkoani Morogoro.


Mwili wa Abdul Bonge ukiombewa kabla ya maziko leo.

Wanamuziki mbalimbali wakiwemo Shetta, Diamond Platnumz, Profesa J, Quick Racka wakishiriki maziko ya Abdul Bonge.


Mwanamuziki Diamond Platnumz akishiriki swala ya kumuombea marehemu.
Mwili wa Abdul Bonge ukitolewa ndani kupelekwa eneo la kuombewa.


Mdogo wa marehemu Abdul Bonge ambaye ni Meneja wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’ akilia wa simanzi juu ya jeneza lenye mwili wa mdogo wake.


Bab Tale akiwa na majonzi baada ya mwili wa mdogo wake kutolewa nje.


Waombolezaji wakijaribu kumtuliza Bab Tale.


Wanamuziki Shilole (kushoto), Madee (katikati) wakiwa na Meneja wa TMK Wanaume Family, Yamoto Band na Diamond, Said Fella wakati wa mazishi ya Abdul Bonge leo mkoani Morogoro.


Wanamuziki Dully Sykes, Diamond Platnumz na Shetta wakiwa katika mazishi ya Abdul Bonge leo.

HATIMAYE mdau wa muziki nchini ambaye ni Mwanzilishi na aliyewahi kuwa Meneja wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale 'Abdul Bonge' amezikwa leo Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro.

Mamia ya waombolezaji wakiwemo wanamuziki Diamond Platnumz, Dully Sykes, Shetta, Shilole, Dogo Janja, Profesa J, Quick Racka na wengineo wameshiriki mazishi ya Abdul Bonge.

Abdul Bonge alifariki dunia jioni ya Machi 28 mwaka huu baada ya kuanguka alipokwenda kusuluhisha ugomvi wa rafiki yake maeneo ya Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam.

Mtandao huu unatoa pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Abdul Bonge kwa msiba huu uliotokea.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU ABDUL BONGE MAHALI PEMA PEPONI. AMEN.

(Picha zote na Dustan Shekidele, GPL, Morogoro)

MAMA AWAFUNGIA NDANI WANAYE 3 KWA MIAKA 10

Na Haruni Sanchawa, Mafia
NI mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.

Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Kanga Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani wakimsindikiza mwandishi wa gazeti la Uwazi, Haruna Sanchawa (hayupo pichani) kuelekea nyumbani kwa Bi. Mwasiti Ally.

Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa wasomaji wake waishio Mafia na kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake.

UWAZI LACHANJA MBUGA KUFUATILIA
Baada ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.

UWAZI LAANZA NA JIRANI

Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.


Bi. Mwasiti Ally akiwafungulia wanaye aliowafungia ndani kwa miaka 10.

MAMA MZAZI SASA
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri. Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini? “Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”


Ally Juma ni mmoja kati ya watoto wa wanodaiwa kufungiwa ndani kwa miaka 10 na mama yao mzazi Mwasiti Ally (pichani).

HISTORIA YAO FUPI
Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.

AWATAFUTA WATU KUMSAIDIA
Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.


Bi. Mwasiti Ally akimnyanyua mwanaye Ally Jum.

“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.

Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la baharini.

WAJENGEWA KIJUMBA, WAFUNGIWA HUMO
Mwasiti alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.

HALI ZAO NDANI YA KIJUMBA
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.”


Ally Juma mwenye ugonjwa wa akili.

NINI KILITOKEA BAADA YA KUWAFUNGIA?
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu.”Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).


Muhadia Juma mwenye ugonjwa wa akili, naye anadaiwa akufungiwa ndani mama yao mzazi kwa miaka 10.

SIKU YA KUJIFUNGUA
Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.


Mzee Juma anayedaiwa kumpa mimba dada yake Muhadiya Juma, akiwakimbia wanakijiji walioongozana na mwandishi wa gazeti la Uwazi.

MJUMBE NAYE
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.


Mjumbe wa nyumba 10 pamoja na Bi. Mwasiti Ally wakimuonesha mwandishi wa gazeti la Uwazi kaburi la mtoto wa Muhadiya.

“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.

“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo kujisaidia. “Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.


Bibi wa watoto hao.

WITO
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.

Ushahidi wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano, mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata mmoja kati ya watoto wote saba!

SKENDO WODINI: MAMA ADAI KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME, APEWA WA KIKE TENA MAITI

Na Mwandishi Wetu, Moro
SKENDO mpya imeikumba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kufuatia mwanamke mmoja, Rukia Fikiri (pichani) kudai kujifungua mtoto wa kiume kisha baadaye kukabidhiwa mtoto wa kike akiwa amefariki dunia, Uwazi linatiririka.Tukio hilo la kushangaza lilijiri Machi 25, mwaka huu katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.


Rukia Fikiri(kulia) akiwa na ndugu zake wakiwa wamebeba maiti ya mtoto wanaodai kubadilishiwa na manesi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

MSIKIE MWENYEWE
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita hospitalini hapo, Rukia alisema alijifungua mtoto wa kiume mwenye afya njema saa 6 usiku wa Machi 24, mwaka huu na kwamba baada ya kujifungua alionyeshwa kisha aliondolewa leba na kupelekwa Wodi ya Wazazi 7 B.

“Lakini kutokana na uchungu wa uzazi kule wodini nilipitiwa na usingizi. Nilipokuja kuamka, manesi waliokuwa wakinihudumia na mtoto wangu waliniambia mtoto amefariki dunia.“Niliumia sana, nilitoa taarifa kwa ndugu zangu akiwemo mume wangu ambapo walifika hapa tukakabidhiwa maiti huku manesi wakisema wameifunga kwa nguo, wakasema tukaifungulie nyumbani,” alisema Rukia, akaongeza:

“Tulienda nyumbani kwa wakwe zangu eneo la Chamwino. Tulipofungua maiti kwa lengo la kuiosha ili tukaisitiri, tulishangaa kuona ni ya mtoto wa kike badala ya wa kiume.”“Haraka sana tukagundua manesi walitubadilishia. Tulikaa kikao cha dharura cha familia, tukakubaliana tuirudishe maiti hapa. Mimi ninamtaka mtoto wangu wa kiume awe hai au amekufa,” alisema mwanamke huyo huku akiangua kilio kwa uchungu.


Rukia Fikiri anayedai kubadilishiwa mtoto huyo.

MUME NAYE AZUNGUMZA
Mume wa Rukia, Hamidu Fikiri naye alipata fursa, akazungumza na Uwazi na kusema:
“Kitendo walichofanya wale manesi ni cha kushangaza sana, kama nisipopewa mwanangu tutaelewana vibaya, mimi nimeshakwenda polisi.”

Mama mzazi wa Hamidu, Mariam Seif ambaye ni bibi wa mtoto alisema kitendo cha mjukuu wake ‘kuibwa’ wodini kimemsikitisha na hawezi kuzika mtoto wa mtu mwingine.“Tulipomrudisha mtoto hapa hospitalini, manesi walikuwa wakitupiana mpira, wale wa wodi 7 B wanasema tatizo liko leba, wa leba wanasema kinyume chake,” alisema bibi huyo.Taarifa zinasema, polisi waliamuru mwili wa mtoto huyo uhifadhiwe hospitalini hapo huku uchunguzi ukiendelea.

Uwazi lilipompigia simu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Rita Lyamuya hakupatikana ofisini kwake na hata alipotafutwa kwa njia ya simu yake ya mkononi, iliita bila kupokelewa.



MASWALI MAGUMU
Ndani ya cheti cha mzazi kulazwa na kuruhusiwa kuna maandishi ya msingi wa uzazi yanayosomeka: Complete Abortion ‘CA’ (mimba kuharibika) ikimaanisha ndicho kiini cha mzazi huyo kufikishwa hospitalini hapo.

Uwazi lilijiuliza kwa nini cheti hicho kiandikwe hivyo wakati mzazi anadai alijifungua salama tena leba?
Daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo), alipoulizwa na gazeti hili kuhusu hali hiyo, alisema: “Complete Abortion ni mimba imetoka kabla ya muda wa kujifungua. Lakini kama huyo mama aliingizwa leba ina maana alijifungua, wasingeandika Complete Abortion, wangeandika SB, kwamba amejifungua salama.

“Mwanamke wa CA hawezi kupelekwa leba. Kutakuwa na tatizo katika uandishi wa hicho cheti. Kwani mtoto mwenyewe alikuaje hata kama alifariki dunia?”Uwazi: “Mwili wa mtoto upo kamili, ila ni marehemu tu.”
Dokta: “Sasa CA mtoto hawezi kuwa kamili. Nadhani hapo katika uandishi wa cheti pana tatizo.”
Gazeti ili linaendelea na uchunguzi.

MUME AMCHOMA KISU MKEWE, NAYE ANYWA SUMU

Mayasa Mariwata na Makongoro Oging’
MWANAMKE mmoja mwenye asili ya Kiarabu, Salma Amuri (39) (pichani) mkazi wa Mji Mpya, Kawe jijini Dar, amenusurika kifo baada ya kuchomwa visu sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo tumboni na mumewe aliyetambulika kwa jina moja la Selemani.Mwanaume huyo naye baada ya tukio hilo alijaribu kujiua kwa kunywa sumu, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.


Salma Amuri anayedaiwa kuchomwa visu na mumewe akiwa hoi hospitalini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa chanzo chetu, tukio hilo lilitokea saa saba usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita ambapo mwanamke huyo alijeruhiwa vibaya kiasi cha kufanya utumbo wake kutoka nje, kabla ya ndugu na wasamaria wema kuwachukua wawili hao na kuwakimbiza Hospitali ya Mwananyamala, wote wakiwa mahututi.
Gazeti hili lilizungumza na mwanamke huyo hospitali ambapo alieleza kisa cha tukio hilo.

“Migogoro ndani ya ndoa yetu tuliyofunga miaka ishirini iliyopita na kufanikiwa kupata watoto na wajukuu, ilianza tangu Novemba, mwaka jana baada ya kutembelewa na ndugu yangu aliyekuja Tanzania akitokea Saudi Arabia anakoishi.

“Mume wangu alikuwa ananishutumu kwamba ameambiwa na majirani mimi natembea na huyo mtoto wa mama yangu mdogo, jambo ambalo siyo la kweli kwani hata kiumri, ni mdogo, hajafikisha hata miaka thelathini,” alisema mwanamke huyo.


Moja ya jeraha alolipata mwilini mwake.

“Usiku siku ya tukio saa saba usiku alirudi nyumbani akawa amekaa sebuleni lakini baada ya kumtaka twende tukalale aligoma, mimi nikarudi ndani, mara akaja na kuniambia ameamua kujiua huku akinionesha sumu aliyokuwa ameiandaa kwenye chupa ili anywe.”Aliongeza kuwa alivamiwa ghafla na kushambuliwa kwa kisu kisha alipoteza fahamu akajishitukia akiwa pale hospitali.

Jitihada za kumsikia mumewe ambaye awali naye alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo, ziligonga mwamba kwa kuwa alikuwa amelazwa chini ya ulinzi wa polisi.Kamanda wa Polisi Kanda ya Kinondoni, jijini Dar, ACP Camillius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo. “Mumewe alihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na hali yake kuwa mbaya na mwanamke yupo Mwananyamala, uchunguzi bado unaendelea,” alisema Wambura.

MWIMBA INJILI ALIPUKIWA NA BOMU AKIWA DUKANI

Na Makongoro Oging’
Mwimba Injili, Victor Mwailenge (29) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Migombani,Tunduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya, Machi 17, mwaka huu anadai kukumbwa na majeraha makubwa mkononi yaliyotokana na mlipuko wa bomu lililotupwa na polisi katika vurugu baina ya askari na wananchi.
Mwimba Injili, Victor Mwailenge akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na bomu.

Kijana huyo aliliambia Uwazi juzi katika mahojiano kwa njia ya simu ya kiganjani kuwa, wakati vurugu hizo zikitokea kutokana na mgogoro wa ardhi wiki iliyopita alivuka mpaka na kuingia nchini Zambia na kujihifadhi katika duka la rafiki yake ndipo bomu lililorushwa na askari lilimfuata huko.

Majeruhi huyo ambaye anaimba nyimbo za Injili katika Kanisa la Moravian alikuwa na haya ya kusema juu ya mkasa uliompata:“Saa 10.30 alfajiri nikiwa maeneo ya Black Market, mpakani mwa Tanzania na Zambia kutokana na vurugu nililazimika kuvuka mpaka kwani mimi nilikuwa sihusiki katika vurugu hizo, nilitarajia kwamba zikiisha nivuke mpaka nirudi nyumbani Tunduma,” alisema kijana huyo.


Muonekano wa jeraha alolipata baada ya kulipukiwa na bomu hilo.

Alipoulizwa sababu za vurugu hizo alisema: “Kisa ni mgogoro wa ardhi, wananchi wanataka eneo hilo la Sogea liwe la shughuli za kijamii kama soko, kupaki magari na kujengwa hospitali lakini CCM nao wanasema ni lao.
“Lakini pia yupo mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la mama Komba naye alidai kuwa ni eneo lake na kwamba ana hati, alienda mahakamani akaambiwa aende baraza la usuluhishi la ardhi kata ili haki ipatikane.

“Kabla ya ufumbuzi kupatikana viongozi waliwaambia wananchi kuchimba msingi ili wajenge zahanati, polisi walifika katika eneo hilo na kusitisha zoezi hilo, waligoma kutawanyika ndipo walitawanywa kwa nguvu kwa kutumia mabomu, hasira ziliwapata hali iliyowafanya wajibu mapigo.

“Polisi hao walidaiwa kumpiga Diwani wa Kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka hali iliyoamsha hasira kwa wananchi, ghasia ziliongezeka. “Siku ya pili kila moja alifungua duka, ghafla tulishangaa kuona polisi, vurugu zikaanza upya na polisi kurusha mabomu ndipo moja lilinipata nikalidaka na kunilipukia mkononi.


“Kwa sasa siwezi kufanya kazi yoyote na anahitaji msaada kwani nina mke na watoto wanne wanaomtegemea.” Aliyeguswa na habari ya Victor anaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0752 339 274.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya SACP, Ahmed Msangi alipoulizwa alisema ni kweli vurugu hizo zilitokea, “Hivi sasa watu 26 walikamatwa kutokana na hilo,” alisema.

PAUL MAKONDA, DK SLAA WAMJULIA HALI ASKOFU GWAJIMA


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilibroad Silaa (kushoto), akimjulia hali Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akimjulia hali Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima aliyelazwa Hospitali ya TMJ kwa ajili ya matibabu baada ya kupata mshituko katika mahojiano na polisi akituhumiwa kutoa lugha isiyofaa kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilibroad Silaa (kushoto), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda walipokutana Hospitali ya TMJ walipofika kumjulia hali Askofu Gwajima.

MUSOMA VIJIJINI HUDUMA ZA AFYA, MAJI SAFI, ELIMU NI TATIZO KUBWA

Musoma Vijijini ni moja kati ya wilaya sita zinazounda Mkoa wa Mara. Upande wa Kaskazini, inapakana na Tarime na Musoma Mjini, Upande wa Mashariki, kuna Wilaya ya Sengerema, Kusini kuna Wilaya ya Bunda na Magharibi inapakana na Ziwa Victoria.


Mheshimiwa Nimrod Mkono.

Pia Musoma Vijijini ni jimbo la uchaguzi linaloongozwa na Mheshimiwa Nimrod Mkono kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM). Wiki iliyopita, Uwazi lilifunga safari hadi kwenye jimbo hilo ambalo kwa sasa makao makuu yake yapo Butiama na kuzungumza na wananchi mbalimbali walioeleza matatizo yanayowakabili.

MATATIZO YA WANANCHI
Matatizo yaliyoelezwa na wananchi kadhaa waliozungumza na gazeti hili, ni uduni wa elimu, ukosefu wa huduma bora za afya, kukosekana kwa maji safi na salama na ukosefu wa umeme jimboni humo kwa muda mrefu.

“Angalau Profesa Muhongo alipokuwa Wizara ya Nishati na Madini alikumbuka kwao kwa kutandaza nguzo za umeme sehemu mbalimbali, hata hivyo bado umeme haujawaka kwani kabla hajakamilisha kazi yake ndiyo sakata la Escrow likamuondoa madarakani, tunamuomba mbunge wetu atusaidie,” alisema Mwita Magafu, mkazi wa jimbo hilo.

Tatizo lingine kubwa linalowasumbua wananchi wa jimbo hilo, ni uduni wa elimu unaochangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa vyumba vya madarasa, uhaba wa walimu, madawati na vifaa vya kujifunzia.
Elias Kajana Majinge ni Chifu wa Kabila la Wajita ambapo katika mahojiano na gazeti hili, alisema maendeleo ya elimu katika jimbo hilo yapo chini sana na yanazidi kuzorota kila kukicha huku kukiwa hakuna jitihada zozote za kuinua kiwango cha elimu jimboni humo.

“Zaidi ya wanafunzi 80 husoma katika darasa moja katika shule za msingi. Matokeo ya shule za sekondari ni mabaya mno, kwa mfano mwaka 2013, kati ya wanafunzi 1587 waliofanya mtihani wa taifa wa kuhitimu kidato cha nne kutoka shule 17 za sekondari za kata, waliopata daraja la kwanza walikuwa saba tu,” alisema Majinge na kuongeza kuwa waliopata daraja la pili walikuwa 55, wakati daraja la tatu walikuwa 195, daraja la nne walikuwa 497, daraja sifuri walikuwa 628, hali inayotoa tafsiri halisi ya jinsi elimu ilivyo duni jimboni humo.
Majinge aliongeza kueleza kwamba wanafunzi wengi wa shule za msingi, huhitimu darasa la saba wakiwa hawajui kusoma wala kuandika.

“Shule nyingi hazina madawati, hakuna madarasa hakuna walimu, hata kama wapo hawaingii madarasani,” alisema Majinge.Wananchi wa Musoma Vijijini walieleza pia kuwa kero nyingine inayowasumbua ni ukosefu wa huduma za afya, ambapo kuna kituo kimoja tu cha afya jimbo zima kiitwacho Murangi pamoja na zahanati kadhaa ambazo hata hivyo hazikidhi mahitaji ya wananchi wote wa jimbo hilo, huku kukiwa hakuna hospitali kubwa hata moja.

“Kama una mgonjwa wako amezidiwa, inabidi mumbebe kwenye machela kwenda Musoma Mjini au Bunda, huko ndiyo kuna hospitali, vinginevyo atakufa huku mkishuhudia, Kituo cha Afya cha Murangi hakina dawa wala wauguzi wa kutosha, hizo zahanati ndiyo usiseme. Tunaomba serikali itusaidie jamani,” alisema Marwa Mturo mkazi wa jimbo hilo.

“Pia hili jimbo lina migogoro mingi ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima na kuna wakati kuliwahi kutokea mapigano yaliyosababisha vifo. Tunamuomba Mkono atimize ahadi zake alizotuahidi wakati akiomba kura,” alisema Issa Rajab, mkazi wa Saragana.

Kero nyingine ambayo Uwazi iliibaini, ni ukosefu wa maji safi na salama licha ya kwamba jimbo hilo linapakana na Ziwa Victoria pamoja na Mto Mara. Wananchi wengi hunywa maji ya ziwani pamoja na ya kwenye mito, ambayo pia hutumika kunyweshea mifugo na kilimo jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya zao.

Baada ya kusikiliza kero za wananchi, Uwazi lilimtafuta Mheshimiwa Mkono ambaye mpaka gazeti hili linakwenda mitamboni, namba yake ya simu haikuwa ikipatikana hewani. Hata hivyo, jitihada za kumtafuta bado zinaendelea ili atoe ufafanuzi wa kero zilizoainishwa na wananchi wa jimbo lake.

SOKO LA BUGURUNI: SHILINGI MIL.27 HUKUSANYWA KWA MWEZI, LAKINI HALI YA UCHAFU SOKONI HAPO NI HATARI

Na Makongoro Oging’
Soko la Buguruni ni moja kati ya masoko makubwa yanayotegemewa katika Jiji la Dar es Salaam kwa serikali kujipatia kipato pia wateja kujipatia mahitaji ya kila siku lakini cha kushangaza ni kwamba uchafu umekithiri.

Muonekano wa soko la Buguruni.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko hilo, Said Habibu Kondo amesema soko hilo lina wafanyabiashara 3,000 na kila mmoja hutozwa ushuru na manispaa kati ya shilingi 300 hadi 400 kwa siku ambapo kwa mwezi zinakusanywa zaidi ya shilingi milioni 27,000,000.

Hata hivyo, fedha hizo hazisaidii katika ukarabati au uzoaji wa taka sokoni hapo.
Uchunguzi uliofanywa na Fukunyuafukunyua sokoni hapo umegundua kwamba wafanyabiashara na wateja wao wako hatarini kiafya ikiwa ni pamoja na hatari ya kulipuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu kutokana na uchafu uliokithiri kila kona huku manispaa ikilegalega katika uzoaji wa taka.

BIDHAA JUU YA YA MATOPE
Wafanyabiashara hao walionekana wakipanga bidhaa juu ya matope na uchafu ukiwa umefunikwa na inzi wa kila aina hali inayowafanya baadhi ya wateja kususa kununua na kuamua kurudi nyumbani bila kitu.

“Manispaa ya Ilala imekuwa mstari wa mbele katika ukusanyaji wa ushuru kila siku bila kukosa lakini kwa uzoaji wa taka wamekuwa wakitokea mara moja moja jambo ambalo ni hatari kwa afya zetu na walaji pia,” alisema mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina la Chuku Hamisi.

“Angalia tunavyonyeshewa mvua, matunda mengi yameoza, manispaa haitaki tuweke maturubai wala mabati mapya,wameshindwa kutulinda kiafya, fedha zinazokusanywa hatujui zinafanya kazi gani nina wasiwasi huenda zinaliwa,” alisema Chuku.

Uchafu uliokithili kwenye soko hilo.

Wafanyabiashara hao waliendelea kusema kwamba manispaa hawana haya, wanakusanya ushuru katika uchafu,walidai kwamba kati ya fedha zinazokusanywa hapo walitakiwa kutoa asilimia kumi kwa ajili ya soko hilo lakini inasemekana hata siku moja hawajafanya hivyo.

“Zamani kulikuwa na mkandarasi aliyekuwa akifanya kazi ya usafi na ukusanyaji wa taka ambapo hali ya soko ilikuwa nzuri lakini tangu waingie mgogoro na manispaa hali ni mbaya sana kwani kumekuwa na rundo la takataka kwa muda mrefu bila kuzolewa.

“Ni aibu manispaa kuongeza viwango vipya vya tozo bila uboreshaji wa soko, baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wanashindwa kuingiza bidhaa zao kutokana na uchafu hivyo hurudia nje,” alisema mfanyabiashara mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Karua.

MWENYEKITI SOKONI ANENA
Alipoulizwa Mwenyekiti wa Wafanyabiashara, Said Habib Kondo alikiri kuwepo kwa hali ya uchafu sokoni hapo.
“Ni kipindi kirefu nimekuwa nikiwaambia manispaa kuboresha soko, wanasema wanataka kulijenga upya, sisi kama viongozi wa wafanyabiashara wa soko hatuna fungu, mikakati yetu ni ‘kuwaimbia’ manispaa suala hili,” alisema Kondo.

Fukunyuafukunyua ilipiga hodi kwa Msemaji wa Manispaa ya Ilala, David Sanga na kumuuliza kuhusiana na kero hiyo alikiri kuwepo.“Ni kweli mkandarasi aliyekuwa akikusanya ushuru, kufanya usafi na kusomba taka tuna mgogoro naye hivyo manispaa ndiyo imechukuwa nafasi yake kwa kufanya shughuli zote alizokuwa akizifanya,” alisema.

Kuhusu madai ya marejesho ya asilimia kumi sokoni hapo ili lijihudimie alisema analifuatilia suala hilo.Yeyote mwenye kero au malalamiko awasiliane nasi kwa namba hizo hapo juu.

WATANO WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI JIJINI MWANZA

Picha / Habari: Johnson James, GPL / Mwanza

Watu watano katika Wilaya ya Nyamagana jijini hapa wamenusurika kifo baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wakiwa kwenye maandalizi ya kujenga jengo lililotegemewa kuwa na ghorofa saba, eneo la Nyerere Road, leo majira ya saa sita mchana.

Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Kunisaga amesema kuwa amesikitishwa na tukio hilo ambapo watu hao wameangukiwa na ukuta wakati wakijenga msingi wa jengo hilo na hii ni kutokana na kuwa na wakandarasi ambao hawajengi majengo kwa kiwango kinachotakiwa.

Katika hatua nyingine, Kunisaga amesema kuwa hali ya Watanzania kuwa wanapoteza uhai wao kila kukicha kutokana na kuangukiwa na vifusi, serikali haiwezi kukubaliana nayo hivyo amesitisha ujenzi wa jengo hilo.

Majeruhi waliokumbwa na tukio hilo wameongea na waandishi wa habari japo kwa taabu na kusema kuwa ukuta uliowaangukia ulikuwa umeunganishwa kama uzio hivyo wakati wakiendelea kuchimba msingi, uzio huo ulikuwa ukiendelea kutitia hivyo kusababisha kuporomoka na kuwaangukia.

Daktari wa zamu wodi ya dharura, Ernest Elisenguo amethibitisha kupokea majeruhi watano ambao wametokana na tukio la kuporomokewa na kifusi na kuwataja kuwa ni Ramadhan Hussein Nyarandu, Rashid Mkumba Hamis, Elias Bahati, Benson Agustino na Mtani ambapo watatu kati ya hao hali yao imeendelea vizuri na wameruhusiwa kwenda nyumbani ila wawili kati yao bado hali zao siyo nzuri na wataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Majeruhi Rashid Mkumba Hamis, ameeleza kama ifuatavyo: "Mimi ni fundi na nilikuwa natengeneza 'bezi' kwa ajili ya kushikilia nguzo za ghorofa wakati ninaendelea na kazi yangu nikaanza kusikia udongo ukiniangukia mgongoni, ghafla nikasikia matofali yananiangukia.

Katika kujiokoa matofali yakawa yameniangukia kwenye miguu na bahati mbaya kwa mujibu wa madaktari ni mwamba nimevunjika mguu ila namshukuru mungu kuona niko salama."
Rashid Mkumba Hamis ambaye ni mmoja wa majeruhi aliyevunjika mguu.

Majeruhi katika tukio hilo wakihojiwa na wanahabari (hawapo pichani).





Vikosi vya uokoaji vikitoa msaada eneo la tukio.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Kunisaga akiongea na wanahabari baada ya ajali hiyo.

Eneo la msingi uliokuwa unajengwa na kuangukiwa na ukuta.


Wananchi wakishuhudia tukio hilo.

Vijana wakijaribu kuokoa baadhi ya mali zilizofukiwa na kifusi hicho.