Na Haruni Sanchawa, Mafia
NI mambo ya kushangaza sana ambayo yamenaswa na Gazeti la Uwazi katika Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani ambapo mwanamke mmoja aitwaye Mwasiti Ally wa Kijiji cha Kanga, amewafungia wanaye watatu kwa miaka kumi ndani ya chumba kimoja kwa madai kuwa ni wagonjwa wa akili.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Kanga Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani wakimsindikiza mwandishi wa gazeti la Uwazi, Haruna Sanchawa (hayupo pichani) kuelekea nyumbani kwa Bi. Mwasiti Ally.
Uwazi lilipata habari hizi kupitia kwa wasomaji wake waishio Mafia na kuamua kufunga safari hadi kisiwani humo kufuatilia tukio hilo la aina yake.
UWAZI LACHANJA MBUGA KUFUATILIA
Baada ya kufika Mafia mjini, Uwazi liliendelea na safari ya umbali wa kilomita 40 kutoka mjini hadi kwenye kijiji hicho kwa ajili ya kuthibitisha madai hayo ya kushangaza.
UWAZI LAANZA NA JIRANI
Kabla ya kuzungumza na mama huyo, Uwazi lilibahatika kuwapata majirani ambapo mmoja wao alisema watoto hao ambao ni baba mmoja, mama mmoja, walianza kuwa katika hali ya kushangaza kiakili mwaka 2001.
“Alianza mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza kuzaliwa. Cha ajabu, kila mwaka mwingine akafuatia hadi wa tatu. Jambo hilo liliishangaza familia na hata sisi majirani,” alisema jirani mmoja.
Bi. Mwasiti Ally akiwafungulia wanaye aliowafungia ndani kwa miaka 10.
MAMA MZAZI SASA
Naye mama mzazi wa watoto hao akizungumza na Uwazi alisema: “Ni kweli watoto wangu hawa wana matatizo ya akili, hawako sawa. Nateseka nao sana.“Ilikuwa mwaka 2001, binti yangu mkubwa, Muhadia Juma (pichani) ndiye alianza, tukajaribu kumfikisha hospitali lakini hakuwa vizuri. Mwaka 2002 akafuatia mdogo wake aitwaye Ally Juma. Nikashangaa ni nini? “Nikiwa nahangaika nao hawa, mwaka 2003 akafuatia mdogo wao, anaitwa Mzee Juma. Nilizidi kuchanganyikiwa kabisa.”
Ally Juma ni mmoja kati ya watoto wa wanodaiwa kufungiwa ndani kwa miaka 10 na mama yao mzazi Mwasiti Ally (pichani).
HISTORIA YAO FUPI
Mwanamke huyo alisema amejaliwa kuzaa watoto saba, watatu ambao wote ni wakubwa ndiyo wamepatwa na matatizo ya akili na wanne ambao ni wadogo wapo sawa na wameolewa wakiendelea na maisha yao ya ndoa.
AWATAFUTA WATU KUMSAIDIA
Akiendelea kuzungumza na Uwazi, mwanamke huyo ambaye ni mjane alisema baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya alianza kutafuta watu wa kumsaidia ambapo alizunguka kwa waganga mbalimbali wa kienyeji akiamini wanaye hao wamerogwa.
Bi. Mwasiti Ally akimnyanyua mwanaye Ally Jum.
“Nimehangaika sana ndugu mwandishi lakini kikubwa kwa watoto wangu wana matatizo ya akili hadi hivi sasa nimekwishafika sehemu mbalimbali, ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Mafia lakini hakuna mafanikio,’’ alisema mama huyo.
Hata hivyo, aliongeza kusema kuwa tangu mwaka 2003 aliona imeshindikana na watoto hao wanazidi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuwaogopa watu, kuchekacheka, kula kwa fujo na kutojijali pia kukimbilia eneo la baharini.
WAJENGEWA KIJUMBA, WAFUNGIWA HUMO
Mwasiti alisema muda wote huo alikuwa akiishi nao nyumba moja lakini ilipofika mwaka 2005 aliamua kuomba msaada kwa watu ili wajengewe kijumba chao waweze kuishi humo wenyewe ambapo ilimlazimu awafungie ndani hadi hivi leo.
HALI ZAO NDANI YA KIJUMBA
Wote wamebadilika na kuwa na afya mbaya huku kucha za mikononi na miguuni kurefuka sana, nywele zimekua ndefu kiasi cha kutisha na sura zao kuonekana kama za misukule na kuwa kama walemavu wa miguu. Lakini mama mtu anatoa sababu ya kuwafungia:“Sababu kubwa ya kuwafungia ndani tangu mwaka 2005 ni usalama wao. Niliamini kwa kuwaachia tu wangeweza hata kupotea.”
Ally Juma mwenye ugonjwa wa akili.
NINI KILITOKEA BAADA YA KUWAFUNGIA?
“Miezi ya hivi karibuni nilishanga sana kumwona Muhadia ana ujauzito, aliyempa ni Mzee ambaye kidogo bado anajiweza kinguvu.”Mama huyo alisema baada ya kubaini Muhadia kupata ujauzito, familia ilijitahidi kuwa naye karibu hadi siku ya kujifungua ambapo alijifungua mtoto wa kiume na kupewa jina la Hassan Abdallah (Abadallah si baba).
Muhadia Juma mwenye ugonjwa wa akili, naye anadaiwa akufungiwa ndani mama yao mzazi kwa miaka 10.
SIKU YA KUJIFUNGUA
Inadaiwa kuwa, siku ya uchungu wa Muhadia, familia ilishirikiana na uongozi wa kijiji wakafanikiwa kumpeleka katika hospitali ya wilaya ambapo alijifungua salama.Baada ya kujifungua, Muhadia alirudishwa kijijini lakini baada ya siku 21, mtoto Hassan alifariki dunia na kuzikwa kijijini hapo.
Mzee Juma anayedaiwa kumpa mimba dada yake Muhadiya Juma, akiwakimbia wanakijiji walioongozana na mwandishi wa gazeti la Uwazi.
MJUMBE NAYE
Naye mjumbe wa mtaa aliyejitambulisha kwa jina la Mzee Seleman alipoulizwa kuhusu hali ya familia hiyo alisema ni kweli mjane huyo amekuwa akiishi na watoto hao kwa shida sana zaidi ya miaka kumi sasa tangu walipoanza kupata matatizo.
Mjumbe wa nyumba 10 pamoja na Bi. Mwasiti Ally wakimuonesha mwandishi wa gazeti la Uwazi kaburi la mtoto wa Muhadiya.
“Watoto wale wanamsumbua sana mama yao, wamekwisha changiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya matatizo waliyonayo lakini hadi leo hakuna mafanikio kama unavyowaona,’’ alisema mjumbe huyo.
“Inawezekana wakipata msaada hata kama akili hazitakuwa sawa lakini afya zao zitaimarika kwani kwa sasa kila kitu wanafanyia mlemle ndani, ikiwemo kujisaidia. “Hakuna mtu mwingine anayeweze kuingia katika chumba walichofungiwa zaidi ya mama yao mzazi tu,” alisema mjumbe huyo.
Bibi wa watoto hao.
WITO
Kwa hali ya familia hiyo, kunatakiwa nia ya makusudi kwa serikali, taasisi na watu binafsi kwenda kutoa elimu za kijamii ikiwemo kuishi na watu wenye ulemavu na kadhalika, kwani inaonekana elimu bado ni tatizo kwa eneo hilo kiasi kwamba, kuwafungia wagonjwa hao ndani haionekani kama ni suala linaloweza kumfikisha mtu kwenye nyombo vya sheria.
Ushahidi wa uduni wa elimu unaonekana hata kwenye kujua mambo muhimu. Mfano, mwanamke huyo hajui tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa mtoto wake hata mmoja kati ya watoto wote saba!

0 comments:
Post a Comment