Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Thursday, April 2, 2015

MWIMBA INJILI ALIPUKIWA NA BOMU AKIWA DUKANI

Na Makongoro Oging’
Mwimba Injili, Victor Mwailenge (29) ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Migombani,Tunduma, Wilaya ya Momba mkoani Mbeya, Machi 17, mwaka huu anadai kukumbwa na majeraha makubwa mkononi yaliyotokana na mlipuko wa bomu lililotupwa na polisi katika vurugu baina ya askari na wananchi.
Mwimba Injili, Victor Mwailenge akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na bomu.

Kijana huyo aliliambia Uwazi juzi katika mahojiano kwa njia ya simu ya kiganjani kuwa, wakati vurugu hizo zikitokea kutokana na mgogoro wa ardhi wiki iliyopita alivuka mpaka na kuingia nchini Zambia na kujihifadhi katika duka la rafiki yake ndipo bomu lililorushwa na askari lilimfuata huko.

Majeruhi huyo ambaye anaimba nyimbo za Injili katika Kanisa la Moravian alikuwa na haya ya kusema juu ya mkasa uliompata:“Saa 10.30 alfajiri nikiwa maeneo ya Black Market, mpakani mwa Tanzania na Zambia kutokana na vurugu nililazimika kuvuka mpaka kwani mimi nilikuwa sihusiki katika vurugu hizo, nilitarajia kwamba zikiisha nivuke mpaka nirudi nyumbani Tunduma,” alisema kijana huyo.


Muonekano wa jeraha alolipata baada ya kulipukiwa na bomu hilo.

Alipoulizwa sababu za vurugu hizo alisema: “Kisa ni mgogoro wa ardhi, wananchi wanataka eneo hilo la Sogea liwe la shughuli za kijamii kama soko, kupaki magari na kujengwa hospitali lakini CCM nao wanasema ni lao.
“Lakini pia yupo mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina moja la mama Komba naye alidai kuwa ni eneo lake na kwamba ana hati, alienda mahakamani akaambiwa aende baraza la usuluhishi la ardhi kata ili haki ipatikane.

“Kabla ya ufumbuzi kupatikana viongozi waliwaambia wananchi kuchimba msingi ili wajenge zahanati, polisi walifika katika eneo hilo na kusitisha zoezi hilo, waligoma kutawanyika ndipo walitawanywa kwa nguvu kwa kutumia mabomu, hasira ziliwapata hali iliyowafanya wajibu mapigo.

“Polisi hao walidaiwa kumpiga Diwani wa Kata ya Tunduma, Frank Mwakajoka hali iliyoamsha hasira kwa wananchi, ghasia ziliongezeka. “Siku ya pili kila moja alifungua duka, ghafla tulishangaa kuona polisi, vurugu zikaanza upya na polisi kurusha mabomu ndipo moja lilinipata nikalidaka na kunilipukia mkononi.


“Kwa sasa siwezi kufanya kazi yoyote na anahitaji msaada kwani nina mke na watoto wanne wanaomtegemea.” Aliyeguswa na habari ya Victor anaweza kuwasiliana naye kwa simu namba 0752 339 274.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya SACP, Ahmed Msangi alipoulizwa alisema ni kweli vurugu hizo zilitokea, “Hivi sasa watu 26 walikamatwa kutokana na hilo,” alisema.

0 comments:

Post a Comment