KUNA magonjwa mengi ya hatari kwa wanawake ambayo huwakumba kwenye viungo vya uzazi na dalili za kuyatambua ni nyingi japokuwa wanaume pia huweza kupatwa na matatizo hayo.
DALILI KWA WANAWAKE
Kwa upande wa wanawake, wanaweza kutambua kwamba wana ugonjwa ambao utaathiri viungo vya uzazi kwa kutokwa na majimaji au ute kwenye uke.
Wanawake wanapaswa kutafuta msaada wa kimatibabu kwa daktari wakigundua lolote kati ya haya yafuatayo:-
Majimaji ya ukeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida na yenye rangi tofauti na wingi kuliko ilivyo kawaida au kuhisi maumivu au kusikia kama unaungua au muwasho wakati wa kwenda haja ndogo.
Dalili nyingine ya kupata maradhi haya au kitaalamu Sexually transmitted disease
ni kusikia maumivu na muwasho katika maeneo ya uke au maumivu ukeni wakati wa kufanya ngono.
Wanawake wengine watatambua kuwa wana magonjwa hatari kwa kutokwa na vidonda na malengelenge katika eneo la uke.
Kumbuka, baadhi ya maambukizi huenda yasiwe na dalili hivyo kama una wasiwasi au umetokewa na dalili hizi ni vyema kuchunguzwa na daktari haraka iwezekanavyo, ama nenda katika kliniki.
DALILI KWA WANAUME
Mwanaume anaweza kupata magonjwa yanayoweza kuathiri viungo vyake vya uzazi na dalili zake ni hizi zifuatazo:-
Majimaji kutoka uumeni ambayo yana harufu isiyo ya kawaida, au yakiwa mengi, kuhisi muwasho ndani ya uume, wakati na baada tu ya kwenda haja ndogo au kutokwa na vijidonda au malengelenge juu au katika sehemu za kiume.
Wengine wanatokwa na vipele au uvimbe katika sehemu za siri.
Kila mtu awe mwanaume au mwanamke ambaye ataona dalili zilizotajwa hapo juu ili kugundua ugonjwa ni lazima aende kuonana na daktari na kufanyiwa vipimo.
itaendelea wiki ijayo
0 comments:
Post a Comment