NiLiaNza wiki iliyopita kueleza kinachosababisha kutoshika mimba. Leo naendelea kufafanua. Kuna njia au aina mbili za wanawake kushindwa kushika mimba au kwa maneno rahisi, ugumba kitaalamu Infertility, ambao unatambuliwa kitabibu.
Aina moja huitwa kitaalamu Secondary infertility na aina nyingine huitwa Primary infertility.
Ugumba unaotokea baadaye maishani hujulikana kitaalamu kama Secondary infertility
Ugumba huu hugundulika pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupeana mimba mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Utafiti umegundua kuwa asilimia kati ya 30 na 40 ya tatizo la ugumba huu huwakumba wanaume ambapo wanawake ni kati ya asilimia 40 na 50.

Asilimia kati ya 10 na 30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa
pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, japokuwa sababu halisi
hazijulikani.
Kwa upande wa wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak
fertility) wakiwa kwenye umri wa miaka 20 na 25 ambapo aliye na umri wa
kati ya miaka 35 na 40 ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia
10 tu.
Ugumba wa asili Primary infertility.
Ugumba wa asili Primary infertility.
Ugumba huu hujulikana pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi
kutungisha mimba kabisa maishani mwao licha ya kujamiiana kwa muda wa
mwaka mmoja tena bila kutumia kinga yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.
Jinsi mimba inavyotungwa
Jinsi mimba inavyotungwa
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka sehemu maalum ya
kutengenezea mayai ya kike iitwayo kitaalamu Ovaries, kitendo hiki
hujulikana kama Ovulation.
Baada ya hapo husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama
Uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi iitwayo kitaalamu
Fallopian.
Mbegu moja (sperm) ya kiume ni lazima itungishe au iungane
(fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea
kwenye Uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana,
muunganiko uliotengenezwa yaani Embryo hushuka mpaka kwenye mfuko wa
uzazi na kujiwekeza hapo.
0 comments:
Post a Comment