Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Sunday, April 26, 2015

MJAMZITO ATIBUA ONESHO LA YAMOTO BAND


Richard Bukos na Issa Mnally
Dada mmoja aliyedaiwa kuwa mjamzito usiku wa Ijumaa iliyopita alizua tafrani na kusababisha onesho la Yamoto Band kusimamishwa baada ya kuvamia jukwaa na kufanya ndivyo sivyo huku kitumbo chake kikiwa kimejichomoza kiuchokozi kufuatia kuachwa wazi.

Kisa hicho cha kushangaza kilitokea ndani ya Ukumbi wa White House uliopo Kimara jijini Dar ambapo Yamoto Band kwa kushirikiana na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ walikuwa wakifanya makamuzi ya pamoja.

Katika tukio hilo, dada huyo na mwenzake walikuwa wakilivamia jukwaa na kuwasonga wanamuziki ambapo mabaunsa waliposhindwa kuwadhibiti waliamua kuzima muziki na kuwasihi wateremke chini wakatii.

WEMA: MAMA’NGU AMEPOTEZA UWEZO WA KUONA KWA 75%!

Mwandishi Wetu
Pole sana mama! Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa mama yake mzazi, Miriam Sepetu anasumbuliwa na macho ambapo madaktari wamegundua kwamba amepoteza uwezo wa kuona kwa asilimia sabini na tano (75%).

Kwa mujibu wa Wema, aliamua kumpeleka mzazi wake huyo hospitalini (hakuitaja) ndipo alipohakikishiwa tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu.

“Kumnusuru mama yangu asipate upofu wa moja kwa moja inabidi afanyiwe operesheni ya macho,” alisema Wema kwa huzuni kwa kuwa hakuna kama mama.

GOOD NEWS !! H BABA APATA MTOTO..HONGERA FLORA MVUNGI



Posted by: Adella TZA April 25, 2015 Entertainment



Mara ya mwisho mwanafamilia wa Bongofleva H Baba na mke wake ambae ni mwigizaji, Flora Mvungi walifika katika studio za #TZA na kufanya exclusive interview ambayo ilisikika kwenye AMPLIFAYA, na nilikuwekea pia kwenye AyoTV na millardayo.com.. Flora ambae ni mke wa H Baba alikuwa mjamzito wakati huo.

Good Good NEWS.. YES, nimepita kwenye ukurasa wa H Baba Instagram, amepost picha ikiwaonesha wakiwa na mtoto wao mchanga halafu kaandika hivi>>>”Uyu mimtoto wapili mke wangu anajifungua nashuhudia MWANZO wauchungu mpaka kijifungua kwake #Kiukweli heshima kubwa kwa mama Tanzaniteone ulijitahidi sana nakupa #HongeraKwakweli wewe nishujaa nanimfano wakuigwa Kwakweli kunamuda Nilikuwa nashindwa kavumilia natamani nitoke nje ila NASEMA hapana mpaka nishuhudie #mwisho wake!!!! ASANTE SANA “@h_baba123



H Baba ana mapenzi na Afrika yake.. mtoto huyu aliezalliwa tayari kapewa jina la Africa.. wa kwanza anaitwa Tanzanite.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> TwitterInstaFB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribeYouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Saturday, April 25, 2015

WEMA AKUBALI WAGANGA 26 KUMTIBU

Musa mateja
KUFUATIA tatizo la kushindwa kupata ujauzito alilonalo msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu, hivi karibuni waganga wapatao 26 kutoka sehemu mbalimbali nchini walijitokeza na kuomba kuunganishwa na staa huyo ili wamtibu.

Msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu.
Waganga hao wa tiba asilia pamoja na madaktari kutoka hospitali mbalimbali kwa nyakati tofauti walililipigia simu gazeti hili na kueleza kuwa, wanashangaa kuona Wema anakosa amani wakati wao wanaweza kumtibu na kuweza kuitwa mama kama wenzake.

“Unajua wapo wanawake ambao wanakosa amani kwa mambo ambayo hawastahili, hili la Wema kutopata mtoto linatibika, mpeni namba yangu kisha anitafute,” alisema mmoja wa wataalam hao aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.
Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.

“Kuna watu wengi sana ukiacha ambao wamejitokeza kwenu, mimi nina meseji zaidi ya 400 ambazo nimetumiwa kwenye namba yangu ya WhatsApp na simu kibao nimepigiwa watu wakijitolea kuja kushughulikia tatizo langu, kiukweli kabisa nipo tayari.

“Lakini ni vizuri wakati naanza kutibiwa tayari nikawa na mwenza wangu ambaye tutakuwa tumekubaliana na pale tatizo litakapoisha, iwe rahisi kuzaa mara moja,” alisema Wema.

MTANGAZAJI WA CLOUDS TV SAMWELI SASALI NDANI YA RUMAFRICA Online MAGAZINE


ZARI AONYWA VIATU VIREFU NA UJAUZITO

MWANDISHI WETU

UBAVU wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ameonywa kuacha viatu virefu kutokana na ujauzito alionao.
Kwa mujibu wa daktari mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alisema kama anataka kujifungua salama basi ahakikishe anaachana na suala la kuvaa viatu virefu kwa wakati huu ambao ni mjamzito.


Ubavu wa Nasibu Abdul ‘Diamond’, Zarinah Hassan ‘Zari’.

“Kama anajipenda na anampenda mwanaye ajaye, anapaswa kuachana na mambo ya viatu virefu kwa sasa hadi pale atakapojifungua,” alisema daktari huyo.Katika picha za hivi karibuni ambazo Zari amepigwa, tumbo lake linaonesha kwamba tayari mimba yake ni kubwa na yuko mbioni kuelekea kujifungua.

AFYA RADIO YAENDELEA KUFANYA VIZURI TUZO ZA EJAT

Ni vituo vyingi vya media nchini vimeweza kuwakilishwa na wanahabari wao lakini afya radio naweza kuwaita nguri wa tuzo hizo baada ya kuchukua mfurulizo ndani ya miaka minne na mwaka jana tukikumbuka mshindi aliyejizolea tuzo nyingi kuliko wote"overwinners" pia alitoka Afya radio hizi ni picha za matukio yalioendelea hapo jana katika ukumbi wa mlimani city jijini dar es salaam



Harith Jaha "Mr Credit" akipokea tuzo



Mwl: dotto Bulendu kushoto na Faraja john kulia ni mmoja ya walio pata Tuzo

Dotto Bulendu akipokea Tuzo



Faraja John akipokea tuzo



Tuesday, April 21, 2015

GAZETI JIPYA LA FADHAGET UPDATE MAGAZINI NDANI YA RUMAFRICA GOSPO Online MAGAZINE


WASTARA APATA AJALI TENA TABATA JIJINI DAR


Wastara baada ya kupata ajali.

MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma jana amepata tena ajali wakati akielekea nyumbani kwake maeneo ya Tabata-Bima jijini Dar es Salaam.

Wastara alijigonga katika kioo cha mbele cha gari lake baada ya kutaka kuvaana na gari kubwa na kulazimika kufunga breki za ghafla akiwa hajafunga mkanda. Msanii huyo ameumia sehemu za usoni.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wastara aliandika hivi:
"DUA ZENU MUHIMU SANA KWA MBAO MNAONIPENDA NA MSIONIPENDA......hali hii imenichosha sana ya matukio ya ajali kila mara natamani kuwa na amani na maisha yangu couz mungu ana sababu kuniacha niendelee kupumua mpka leo ila kwa wanaochukia kuona napumua wanatamani nizikwe hta mzima ila mtambue nina watot 3 wananitegemea kwa kila kitu smtime mnasema nasikitika sana ni kweli sababu mi sio nabii nikihesabu hii ni ajali ya ya 9 sasa tena ni mbaya sana za kufa kabsa ila labda nimo kwa wale wanaopta ajali kipindi hiki japo kwangu ni too much,, ni jana na leo napumua alhamdulilah duwa zenu niombeni jamani huyu jinamizi akae mbali nami daah too much"

Wastara ameshapata ajali mara kadhaa ikiwemo ile ya mwaka jana wakati akitoka nyumbani kwake Tabata-Bima, Dar na gari lake aina ya Toyota Vitz kwa ajili ya kwenda kununua umeme pamoja na ile ya pikipiki aliyopata mwaka 2008 akiwa na aliyekuwa mumewe, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ambapo ilibidi akatwe mguu wa kulia. Pia aliwahi kupata nyingine ya gari akiwa na Sajuki.

A-Z UGAIDI WA MORO

Na Waandishi Wetu
HII ndiyo A-Z ya wale watu tisa wanaoshikiliwa na polisi jijini Dar baada ya kukamatwa msikitini wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi na bendera nyeusi inayodaiwa kutumiwa na kundi la wapiganaji wa Al Shabaab. Mmoja kati ya watu hao (wa kumi), Hamad Makweka aliuawa.

Polisi wakimjulia hali mwenzao aliyekatwa na sime shingoni.

Watu hao walikamatwa Aprili 14, mwaka huu saa 3:30 usiku katika Kitongoji cha Nyandero Tarafa ya Kidatu wilayani Kilombero, Morogoro wakiwa na silaha hizo ambapo ilidaiwa kuwa, walikuwa wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu wa ‘kigaidi’ mahali.

Ilidaiwa watu hao walilala kwenye Msikiti wa Answar Sunna uliopo Kidatu ambao unamilikiwa na Islamic Foundation.
Baada ya kukamatwa, awali walishikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Morogoro na baadaye kupelekwa jijini Dar kwa siri ambako mahojiano makali yanaendelea.

Habari kutoka ndani ya jeshi hilo zinasema kuwa, watu hao wanahojiwa ili kujua ukubwa wa mtandao wao, walikuwa wakafanye tukio wapi na nani mdhafili wao mkubwa.“Unajua kwa sasa tatizo ni kwamba, inaonekana wahalifu wakubwa tunaishi nao, zamani tuliamini wanaweza kuingia kutoka nje ya nchi.


Vitu walivyokutwa navyo.

“Wale jamaa walikuwa wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu mahali, hilo ni moja lazima waseme. Pia lazima mtandao wao ujulikane. Jeshi la polisi lilifanya kazi yake kwa usahihi ndiyo maana walinaswa kabla ya muda wa kwenda kufanya tukio,” alisema askari mmoja kwa kuomba jina lake lisitumike kwa kuwa si msemaji wa jeshi hilo. Gazeti la Uwazi lilifika kwenye Msikiti wa Suni na kuzungumza na baadhi ya watu. Mtu wa kwanza kuongea naye alikuwa muumini wa msikiti huo, Shani Kinyimbi ambaye alisema:

“Kwa hili lililotokea, mimi nawaomba viongozi wetu wa msikiti huu kuanzia leo mtu asilale ndani na baada ya swala msikiti ufungwe. Hii ni hatari sana, magaidi kugeuza msikiti sehemu ya maficho imeniuma sana msikiti wetu kuchafuliwa.”

Naye kiongozi mmoja wa msikiti huo, Mohamed Menze ambaye ni mweka hazina mkuu alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema:“Tukio hili la kigaidi limeuchafua sana msikiti wetu na dini yetu kwa ujumla. Kiukweli hawa jamaa sisi kama viongozi wa msikiti hatuwajui na wamefika usiku na kukamatwa usiku huohuo.


Gari la polisi likiwa eneo la tukio.

“Hapa msikitini kuna vijana watatu wanalala ambao ni Hafidh Kondo, Rajabu Shomari, Singo na Mustapha Kivale. Kwa mujibu wa vijana hao, juzi (Aprili 14) usiku walifika watu hao wakiwa na mabegi ya kitalii na kuswali ambapo baada ya kuswali waliomba kulala msikitini

“Wakati wakiendelea kuongea na vijana wetu polisi walifika na kuwakamata na baadaye kwenda kwa imamu wetu ambao walimuuliza kama ana taarifa za ugeni huo imamu alikana kuwa na taarifa, polisi waliwakamata watuhumiwa hao na walipopekuliwa kwenye mabegi yao walikutwa na sare za jeshi, bendera, baruti na vitu vingine mbalimbali. Wakati huo mwenzao mmoja alishauawa.”

Diwani wa Kata ya Kidatu, Bryson Mwanzenye alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema:
“Hili ni tukio la kigaidi na kwa sasa kwenye kata yangu hali ni tete, mtu mwenye ndevu nyingi na kipara (Hamad Makweka) ambaye hafahamiki alivamiwa na kupigwa na wananchi wenye hasira hadi kufa.”


Diwani.

Alipotakiwa kueleza alivyomfahamu marehemu Hamad Makweka alisema: “Huyo mtu si mkazi wa kata yangu, anatoka Ruaha lakini mtu anapokufa ndipo mengi yanapoibuka. Inadaiwa huyo marehemu alikuwa ni mwalimu wa kareti ambaye majirani zake wanasema hawakujua kazi yake lakini alikuwa ni mtu wa kusafirisafiri sana.”

Maulidi Aliphonce ambaye ni dereva wa Bajaj ya pili iliyowachukua baadhi ya watu hao kwenda nao msikitini, alisema:
“Mimi niliwachukua watano kati ya wale watu kutoka kituo cha Ruaha. Mwenzangu (Bajaj ya kwanza) aliwachukua watano. Tukiwa tunaenda msikitini, kwa nyuma tulifuatwa na pikipiki mpaka tunafika msikitini.

“Nilipowashusha, ile pikipiki iligeuza na sisi wa Bajaj tukageuza kurudi kituoni kwetu. Lakini mtu mmoja Hamad Makweka aligeuza na mimi licha ya kwamba wakati wa kuwabeba wenzake na yeye alikuwemo lakini alisema anarudi Kidato kwa sababu wenzake watalala msikitini.


Kiongozi wa msikiti.

“Njiani tukakutana na polisi, wakatusimamisha. Wakaanza kumuuliza maswali Hamad, ghafla naye akatoka mbio, polisi mmoja akamkimbiza, Hamad akatoa sime na kumkata shingoni yule askari na kutaka kuendelea kukimbia, lakini polisi mwingine alimpiga risasi ya mguu, akaanguka na kukamtwa.

“Ndipo wananchi wenye hasira kali walipotokea na kumpiga mpaka wakamuua kwa kumchoma moto. Walimpiga kwa sababu alimkata shingo askari kwa kuulizwa maswali kadhaa.” Naye Koplo Nassoro Dabi ambaye ni mchezaji wa zamani wa Timu ya Polisi, Morogoro aliyekatwa shingo kwa sime na marehemu Hamad ambaye kwa sasa amelazwa Zahanati ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia, Morogoro alikuwa na haya ya kusema:

“Namshukuru Mungu hadi leo hii napumua. Kwa kweli nilinusa kifo, sikujua kama jamaa alikuwa na sime kiunoni. Wakati namfukuza aliingia kwenye shimo na kuangua, nilipojiandaa kumkamata alitoa sime na kunikata shingoni nikapoteza fahamu baada ya kutoka damu nyingi.

Msikiti uliohusika na tukio hilo.

“Kama ningejua ana sime ningejua namna ya kumwingia. Lakini kwa kweli ilikuwa hali tete pale. Ila wananchi wa kule wana umoja sana.”Siku za hivi karibuni kumeibuka uhalifu wenye kutia shaka hasa kutokana na silaha wanazokuwa nazo wahalifu hao kiasi kwamba, wapo waliobainika kuwa na ushirika na Kundi la Kigaidi la Al Shabaab la nchini Somalia. Mfano ni kijana Rashid Charles Mberesero (21) ambaye alihusishwa na mauaji ya wanafunzi 148 kwenye Chuo Kikuu cha Garissa nchini Kenya mapema mwezi huu.

UCHAWI! UCHAWI! HAKIMU AFIA MAHAKAMANI

Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
HAYA ndiyo majanga! Hali ya hewa ilibadilika ghafla katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga, Dar kufuatia Mheshimiwa Hakimu Rogart Venance Alphonce (54) kuugua ghafla, kudondoka na kutokwa povu mdomoni na puani, hatimaye kufariki dunia! Inauma sana!


Marehemu Hakimu Rogart Venance Alphonce enzi za uhai wake.

Tukio hilo la kusikitisha na lililoibua vilio kwa watumishi wa mahakama hiyo na wale waliokuwa na kesi, lilijiri Aprili 13, mwaka huu mahakamani hapo wakati makarani wakiandaa mafaili ya kesi mbalimbali.

KUMBE ALIKUWA ANARIPOTI KITUO KIPYA CHA KAZI
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari mahakamani hapo, Mheshimiwa Alphonce siku hiyo ndiyo alikuwa akiripoti mahakamani hapo kikazi akitokea Mahakama ya Mwanzo Lugoba, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ndipo akapatwa na matatizo hayo ambapo wengi walidai kifo chake kilitokana na ushirikina.

“Huyu hakimu si mgeni kwangu, namjua kwa utendaji wake wa kazi na ni mtenda haki katika hukumu anazozitoa, amekuwa akifuata sheria bila kumuonea mtu, watu wasiompenda ni wale wahalifu ambao alikuwa akiwahukumu kwa mujibu wa sheria kulingana na makosa yao.

Mtoto wa marehemu akilia kwa huzuni kubwa.

“Siamini kama huu ni ugonjwa wa kawaida, lazima kuna mkono wa mtu! Inawezekana amepigwa ‘manati’ (kurushiwa uchawi) huko alikotoka ili aje kufia hapa.“Nasema hivi kwa sababu hapa ofisini alifika salama akiwa na mkoba wake. Alipofika alituonesha barua iliyotoka Wilaya ya Ilala kwamba anatakiwa kuanza kazi hapa.”

TUKIO LATOKEA WAKATI WA USAFI WA OFISI
“Tulimchukua hadi kwa mkubwa wetu, hakimu mfawidhi mama Komba ambaye aliisoma ile barua na akatuambia tumwandalie ofisi yake kwa kuifanyia usafi kwani ilikuwa haitumiki kwa muda mrefu, hakimu aliyekuwa akiitumia alistaafu.

“Sasa wakati ofisi yake ikiandaliwa huku yeye bado akiwa katika ofisi ya bosi wetu tulipata taarifa kwamba, alishikwa na kukohoa mfululizo kisha akadondoka chini akitokwa na povu kinywani na mdomoni na kufariki dunia. Jamani si maajabu haya?”

Waombolezaji wakiuaga mwili wa marehemu kwa simanzi kubwa.

WATUMISHI WA MAHAKAMA WACHANGANYIKIWA
“Kila mmoja alichanganyikiwa, tulichukua usafiri na kumkimbiza Hospitali ya Amana ambapo iligundulika kuwa alishafariki dunia.“Hali hii imetutia hofu na majonzi makubwa, ikizingatiwa kwamba katika mahakama hii kuna mahakimu wachache sana,” alisema mtumishi mmoja wa mahakama hiyo ambaye hakupenda kutaja jina lake.

Mfanyakazi mwingine wa mahakama hiyo alisema kuwa, mahakimu wanakumbana sana na mambo ya ushirikina hasa kutoka kwa baadhi ya watu wenye kesi mbaya ambao wanaamini kesi zao zitafutwa kwa imani hiyo.“Utakuta mtu anaona kesi yake ni ngumu na kosa analo kweli, ndipo uchawi huanzia hapo. Atakwenda kwa waganga ili hakimu apate matatizo.

“Sasa huyu unajua siku ileile angeingia ofisini kwake na angepewa mafaili ya kesi, hasa zile za kuahirisha. Au pengine alikotoka nako ndiyo kwenye tatizo,” alisema mfanyakazi huyo akiomba hifadhi ya jina lake.


...Wakiendelea kuuaga mwili wa marehemu.

NYUMBANI KWA MAREHEMU
Uwazi lilifanikiwa kufika nyumbani kwa marehemu maeneo ya Ulongoni A, Ukonga jijini Dar na kuongea na Emmanuel Shabani Kiria (kaka wa marehemu) kuhusiana na kifo hicho cha ghafla ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Marehemu mdogo wangu alikuwa mzima wa afya, nakumbuka zamani ndiyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo lakini alitibiwa hospitalini na kupata nafuu, ndiyo maana alikuwa akiendelea na kazi.

“Juni 13, 2005 ndiyo alimaliza Chuo cha Sheria Lushoto, Tanga akapangiwa kazi mkoani Lindi. Baadaye alihamishiwa Lugoba na mauti yamemkuta siku akiripoti katika Mahakama ya Ukonga. Taarifa niliyopata ni kwamba alizidiwa kazini akakimbizwa Amana lakini kumbe alishafariki dunia.


Mwili ukipelekwa kaburini kwa ajili ya mazishi.

“Uchawi unatajwa lakini mimi siwezi kuzungumzia kwa sababu nilikuwa siishi naye.”
Hata hivyo, kaka huyo wa marehemu aliongeza kusema kwamba mdogo wake ameacha mke na watoto wanne na amezikwa Kibosho mkoani Kilimanjaro.

UONGOZI WA MAHAKAMA WANENA
Uongozi wa mahakama uliyokuwa msibani hapo ulisema kwamba, marehemu alikuwa mtu wa watu ambaye alipenda kushirikiana na wenzake na alikuwa akifanya kazi kwa kuzingatia sheria, hakumuonea mtu.

WATOTO WACHOMWA MOTO, KISA HAWARA WA BABA

Stori: Shani Ramadhani
INASIKITISHA sana! Vijana wawili, Jumanne Omar (17) na Mgeni Rashidi Rajabu (16) (aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Keko), Dar, wakazi wa Mtoni Madafu, Temeke wameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira kali baada ya kudhaniwa kuwa ni wezi.


Marehemu Jumanne Omar enzi za uhai wake.

Tukio hilo la kinyama lilitokea wiki iliyopita Gongo la Mboto, Dar ambapo kijana aliyefahamika kwa jina la Hassan ambaye ndiye mkazi wa huko alidaiwa kuwafuata marehemu hao Mtoni Madafu na kuwaambia ametumwa na mama yake mzazi aende akafanye vurugu kwa hawara ‘mchepuko’ wa baba yake.

Inadaiwa kuwa, Hassan akiwa na vijana wengine wawili, aliongozana na vijana hao kwenda Gongo la Mboto kwa mwanamke huyo ambaye ni mama lishe.Ndugu mmoja wa Jumanne anasimulia: “Walipofika kwa mama lishe huyo ambaye Hassan alidai ndiye mchepuko wa baba yake, waliagiza chakula. Walipomaliza kula yule mama aliwadai pesa, Hassan akasema hawana na hawatoi.

“Tunasikia yule mama akaamua kukusanya vyombo walivyolia chakula ili akaoshe, lakini ghafla Hassan alimpora simu na pesa za mauzo na kukimbia na wale wenzake wawili ambao ni wakazi wa hukohuko Gongo la Mboto na kuwaacha Jumanne na Mgeni.

“Ilibidi mama lishe apige kelele za mwizi, watu wakatokea na kumkamata Mgeni na kuanza kumpiga, baadaye wakamkata kisogoni kwa panga huku Jumanne akikimbia kuomba msaada na kujitetea kuwa wao si wezi naye akakamatwa na kuanza kupigwa.


Marehemu Mgeni Rashidi Rajabu enzi za uhai wake.

“Wakati wananchi hao wakiendelea kuwapiga vijana hao, alitokea dereva wa bodaboda ambaye alishauri kuwa vijana hao wachomwe moto mpaka wateketee.“Alikwenda kuchukua petroli na kuja kuwamwagia kisha akawasha kiberiti na vijana wakaanza kuungua moto huku wakipiga kelele kuomba msaada.”

Ilidaiwa kuwa, baada ya kupata taarifa hizo ndugu walizunguka kutafuta miili ya vijana hao na kuikuta katika Kituo cha Polisi cha Stakishari, Ukonga, Dar na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi kabla ya mazishi.

Dada wa Jumanne anasimulia: “Sisi tulipigiwa simu na mpangaji mwenzetu saa mbili usiku, yeye anafanya shughuli zake hukohuko Gongo la Mboto, akatuambia mdogo wetu anauawa kwa kuchomwa moto, tukashangaa sana na kujiuliza imekuwaje na nini kimempata.

“Tuliondoka hapa na kuanza kupita kwenye hospitali kubwa tukianzia Temeke, Mwananyamala mpaka Muhimbili hatukukuta mwili, tukaamua kwenda Polisi Stakishari ndiyo tukakuta miili ya wawili. Inauma sana jamani mimi mpaka leo hii siamini.”

Naye baba mzazi wa Mgeni, Rashid Rajabu ambaye anaishi Zanzibar alisema:
“Kifo cha mwanangu kimeniumiza sana. Nakumbuka siku si nyingi nimetoka kumlipia ada ya mwaka mzima shuleni kwa sababu ilikuwa amalize kidato cha nne mwaka huu.

“Naamini yote ni mipango ya Mungu japo mwanangu alikuwa kichwa darasani hata wanafunzi wenzake wameumia lakini hawanifikii mimi mzazi. Ngoja tuwaachie wahusika maana nimesikia suala hili limeshafika polisi,” alisema baba huyo.Miili ya vijana hao ambao iliharibika kwa moto, ilizikwa katika Makaburi ya Mtoni kwa Kombo, Jumatatu ya Aprili 13, mwaka huu.

Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.
Uwazi linaendelea kufuatilia sakata hili kwa kina ili kujua nini kilitokea kwa Hassan, yupo wapi na mama lishe alichukuliwa hatua gani.

MC KIPANYA WA KIPANYA NDANI YA RUMAFRICA GOSPO Online MAGAZINE


MWINGINE AFARIKI DUNIA! WALIOFUNGIWA NDANI MIAKA 10

Na Haruni Sanchawa
BINTI Muhadia Juma ambaye alikuwa mmoja wa watoto watatu waliofungiwa ndani ya nyumba kwa miaka kumi na mama yao mzazi, Mwasiti Ally katika Kijiji cha Kanga, wilayani Mafia amefariki dunia Aprili 15, mwaka huu.Huyu ni kijana wa pili kufariki dunia baada ya Ally Juma kuaga dunia hivi karibuni na kufanya aliyebaki hai kuwa mmoja, Mzee Juma.


Mwili wa Muhadia Juma ukizikwa.

Muhadia alichukuliwa kijijini kwao na kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mafia kwa matibabu na mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Nassoro Hamid aliyepata taarifa za kufungiwa ndani kwa miaka kumi na mama yao kupitia gazeti hili toleo la Machi 31, mwaka huu lililokuwa na kichwa cha habari ‘MAMA AWAFUNGIA NDANI WANAYE 3 KWA MIAKA 10.’

Habari kutoka Mafia zinasema Muhadia baada ya kufikishwa hospitalini, alianza kupatiwa matibabu na lishe bora lakini siku hiyo ya kifo chake (Aprili 15) hali yake ilibadilika ghafla na kuaga dunia saa 1.30 usiku.Marehemu huyo alizikwa Aprili 16, mwaka huu katika Kijiji cha Kanga kilichopo kilomita 40 kutoka Mafia mjini ambapo gharama zote za mazishi ziligharamiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya.


Muhadia Juma enzi za uhai wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu juzi, Mkuu wa Wilaya, Dk.Hamid alisema amesikitishwa na vifo vya ndugu hao wawili waliokufa kwa mateso makubwa na ya muda mrefu.“Ni bahati mbaya sana ofisi yangu ilipata taarifa juu ya wagonjwa hao wakiwa katika hali mbaya. Nitoe wito kwa wananchi kwamba wanapokuwa na matatizo kama hayo wasifiche, watoe taarifa serikalini ili washughulikiwe mapema,” alisema.

Monday, April 20, 2015

FUNDI MIAVULI AFIA NDANI KWAKE, AHARIBIKA!



Na Waandishi Wetu
Wakazi wa Mtoni Kwa Aziz Ally, jijini Dar, wiki iliyopita walipatwa na mshangao baada ya mzee mmoja, Hamisi Mzee Hamisi kukutwa chumbani kwake akiwa amefariki dunia.Mzee huyo ambaye alikuwa ni fundi miavuli maeneo ya Kariakoo, inadaiwa hakuonekana nyumbani kwake kwa siku sita mfululizo huku mlango wake ukiwa wazi.

“Kilichotushitua majirani ni harufu kali iliyokuwa ikitokea eneo la usawa wa nyumba ya mzee huyo,” kilisema chanzo.
“Harufu ile ilianza kusikika muda mrefu na ilikuwa kali sana, baada ya kuifuatilia ndipo ikabainika ilitokea chumbani kwa mzee Hamisi, baada ya kuingia ndipo alikutwa akiwa amekufa huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya, wadudu wakiwa wameuzunguka na kutambaa chini,’’ kilisema.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, inasemekana marehemu alikuwa anaishi na kijana wake ambaye hakufahamika jina mara moja baada ya mkewe kuondoka miaka kadhaa iliyopita. Hata hivyo, kijana huyo inasemekana hajaonekana nyumbani hapo kwa siku sita.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mzee Hamisi hakuwa na ndugu yeyote anayefahamika eneo hilo.
Polisi wa Kituo cha Chang’ombe walifika nyumbani kwa mzee huyo baada ya kupewa taarifa na mmoja wa wananchi wa eneo hilo ambapo waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi zaidi.

UGONJWA KWENYE KIBOFU KWA WANAWAKE-2


Mfano ni ukuaji wa viungo kama matiti na kupata hedhi. Pia wanawake wenye uzito wa zaidi ya kilo 70 wana hatari kubwa zaidi ya kupata ‘fibroids’ kutokana na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ katika umri huo.

Zamani ‘fibroids’ ingeweza kusababishwa na matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa sababu vidonge hivyo vilikuwa na kiwango kikubwa cha ‘oestrogen.’ Hivi sasa vidonge hivi vya uzazi wa mpango havina kiwango kikubwa cha ‘oestrogen’ kama ilivyokuwa zamani.

‘Fibroids’ zinatofautishwa kutokana na sehemu ilipotokea. Zipo zinazotokea ndani ya mji wa mimba na zingine zinazotokea kwenye kuta za nje ya mji wa mimba.Karibu asilimia 75 ya wanawake wenye ‘fibroids’ hawajui kama wana ‘fibroids.’ Utambuzi wa dalili za ‘fibroids’ hutegemea ukubwa wake na wapi zilipo kwenye kizazi. Hii pia huchangiwa na dalili anazopata mtu. Fibroids’ ndogo iliyo kwenye kuta za kizazi haitakuwa na dalili sawa na ‘fibroids’ kubwa inayoota nje ya kizazi.

DALILI ZA FIBROIDS
Dalili kubwa inayofahamika zaidi ni ile ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na maumivu ya tumbo na damu hiyo huambatana na mabonge mabonge isivyo kawaida.Dalili nyingine ni kupata maumivu ya kiuno, ugonjwa hubana viungo vingine vya mwili (pressure symptoms) hivyo kupumua kwa shida au kukojoa mara kwa mara au kushindwa kupata choo kikubwa kama kawaida. Nyingine ni pamoja na kutokutunga mimba, au mimba kuharibika na kutoka.

Ni rahisi kwa mtaalamu kugundua ugonjwa huu au uvimbe katika mfuko wa uzazi kwa kumkagua, au kumpima mgonjwa (bimanual examination). Pia huathiri mfumo wa haja ndogo na kubwa na mgonjwa kuhisi mkojo mara kwa mara, mkojo kutoka kidogokidogo, kushindwa kutoka kirahisi, kukosa choo, kutopata mimba na kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

‘Fibroids’ zaweza kusababisha matatizo kama kuharibu mimba au mwanamke kutoshika mimba kutokana na mirija ya uzazi kubanwa au msukumo unaosababishwa na ‘fibroids’, mirija ya uzazi hubanwa na hivyo kushindwa kupitisha mayai kuelekea kwenye kizazi (uterus).

Mwanamke anapokuwa mjamzito na pia akawa na ‘fibroids’, mwili huweza kusitisha kupeleka damu kwenye ‘fibroids’ na kuifanya isinyae hivyo kusababisha maumivu makali ya tumbo na kufanya kizazi kutanuka na kusinyaa na baadaye mimba huweza kutoka kabla ya wakati wake.

Wakati wa kujifungua, kama ‘fibroid’ itakuwa kwenye njia ya kutolea mtoto inaweza kusababisha damu nyingi kutoka au ikishindikana, mama hufanyiwa upasuaji ili kumtoa mtoto aliye tumboni.

USHAURI
Dalili zikiwapo na kuhisi unalo tatizo la ‘fibroids’, mwone daktari kwa ajili ya kupata vipimo kujua kama una ‘fibroids’ au la. Daktari atafanya vipimo vya ‘Ultrasound’ (mionzi), ‘Hysteroscopy’ (kifaa kidogo ambacho huingizwa kwenye kizazi kupitia sehemu ya uke) na ‘Laparosopy’ (upasuaji wa sehemu ndogo ya tumbo pamoja na kuwekewa kifaa kidogo sehemu ya uke).

TIBA
Kuna njia kuu mbili za kutibu ‘fibroids’. Kutumia dawa (drug treatment). Mkusanyiko wa dawa zijulikanzo kama ‘GnRH analogues’ hupunguza kiwango cha ‘oestrogen’ mwilini na hivyo kusababisha ‘fibroid’ kusinyaa. Dawa hizi zikitumika kwa miezi sita hupunguza ukubwa wa ‘fibroid’ kwa aslimia 50 pia hupunguza mzunguko wa hedhi.

Matumizi ya dawa za ‘GnRH analogues’ yasizidi miezi sita kwani dawa hizi huweza kuleta madhara makubwa baadaye. Mara baada ya kuacha kutumia dawa hizi,wanawake wengine baada ya wiki chache hujikuta wakirudiwa na ‘fibroids’ ambazo huanza kukua tena na mwanamke huanza kupata hedhi kama awali lakini ikiambatana na maumivu makali. Baadhi ya wanawake huwa hawapati hedhi tena kwa maisha yao yote.

Upasuaji ni njia nyingine ya kutibu ugobnjwa huu na huhusisha mambo yafuatayo: Kuiondoa ‘fibroid’ yenyewe na kuacha kizazi jambo ambalo kitaalamu huitwa myomectomy; kukiondoa kizazi kabisa kitaalamu huitwa hysterectomy na kuzuia damu kwenda kwenye ‘fibroids’ yaani uterine artery embolisation. Pia iko njia ambayo mtu huchomwa sindano nne tumboni zikielekea zilipo ‘fibroids’ kwa ajili ya kuziua kwa kemikali maalumu.

Ugonjwa unapoingia kwenye kibofu cha mkojo huwa ni tatizo kubwa kwa wanaume pia.
Wanaume, hasa wenye umri mkubwa wanaweza wakawa na ugonjwa wa saratani ya ‘prostate’. Ni tezi iliyo kwenye viungo vya uzazi vya wanaume chini ya kibofu panapopitia mrija wa mkojo.

Kazi ya ‘prostate’ ni kudhibiti kibofu na mtiririko wa mkojo lakini pia ni muhimu katika tendo la ndoa kwani humwezesha mwanamume kuwa na nguvu ya kufikia kilele. ‘Prostate’ ya kawaida kwa mwanamume mtu mzima ina ukubwa kama punje ya karanga na ukubwa huu huongezeka kadiri mtu anavyokua. Katika umri wa miaka 40 tezi huanza kutanuka na kadiri inavyotanuka, hubana mrija wa kupitisha mkojo na kufanya mkojo utoke kwa shida na kusababisha tatizo katika tendo la ndoa.

DALILI
Dalili za kwanza za mgonjwa kuwa na tatizo katika kibofu cha mkojo ni kwenda haja ndogo mara kwa mara, hasa usiku na mara nyingine mtu huweza kujikojolea. Pia mkojo hutoka kidogokidogo ama kwa kukatika katika na wakati mwingine mwanamume hupata maumivu wakati wa kukojoa na hata kutoka damu. Maumivu huenea kwenye sehemu za mgongo, kiuno na sehemu za juu ya mapaja na kupunguza uwezo wa tendo la ndoa au kupata maumivu wakati wa kufikia kilele.

Matatizo mengine ni kupata maambukizi ya magonjwa kwenye kibofu, njia ya mkojo na figo na mkojo hubaki kwenye damu na kuwa sumu. Utafiti waonesha kuwa asilimia 25 ya wanaume wenye umri wa miaka 30 na kuendelea wana chembechembe za ‘prostate cancer’.

‘Prostate cancer’ ndio aina kuu ya ‘cancer’ (saratani) inayowashambulia sana wanaume japokuwa inaweza kutibika mgonjwa akiwahi hospitali.

Friday, April 17, 2015

CELLINE THEOPHIL NDANI YA RUMAFRICA Online MAGAZINE


WEMA, WOLPER WALEWA CHAKARI!

Sifael Paul
Hatari! Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe, wamejikuta wakipiga ulabu hadi kulewa chakari, kisa kikielezwa kwamba wana msongo wa mawazo, Risasi Jumamosi linafunguka.


Masistaduu wawili kunako gemu la Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper Massawe wakipiga mtungi usiku mnene.

ENEO LA TUKIO KINONDONI-MANYANYA
Tukio hilo lililoshuhudiwa na gazeti hili lilijiri hivi karibuni, usiku mnene kwenye pati ya kuzaliwa (birthday) ya meneja wa kampuni ya Wema ya Endless Fame almaarufu Petit Man iliyofanyika kwenye nyumba ya jamaa mmoja maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao.
Katika pati hiyo ambayo mbali na mastaa ilihudhuriwa na watoto wa mjini, watu waligonga msosi wa kufa mtu kisha vikafuata vinywaji.

Tofauti na ‘maraia’ wengine, Wema na Wolper walikuwa wakigonga vinywaji vikali hadi wakawa tilalila na kuanza kufanya vituko, jambo ambalo liliwashangaza wengi.Kadiri muda ulivyokuwa unasonga ndivyo mastaa hao walivyozidi kucharuka tofauti na walipofika kwani walionekana wapole na wastaarabu kupita maelezo.

Baada ya ulabu kuwakolea walianza kupigana picha kwa simu kisha kukata mauno kabla ya Wolper kuzimika kufuatia kuzidiwa na ‘kinywaji’.Kwa upande wake Wema alimpiga vibao mwanaume shoga aliyetajwa kwa jina moja la Danny baada ya kutibuana kabla ya watu kuwaamulia.Ulipofika muda wa kuondoka mahali hapo, ilidaiwa kwamba Wolper ilibidi abebwe ili kupelekwa kwenye gari kwani alikuwa hajiwezi.


Wema Isaac Sepetu na Jacqueline Wolper wakifurahia jambo.

KISA MSONGO WA MAWAZO
Uchunguzi wa Risasi Jumamosi umebaini kwamba, mastaa hao wana msongo wa mawazo hivyo wanaona njia pekee ya kuwaondolea ‘stresi’ ni kunywa pombe.

WEMA
Habari za ndani zilieleza kwamba, tangu Wema ameachana na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amekuwa mtu mwenye mawazo na njia pekee ambayo huitumia ni kujipooza kwa pombe kali.
“Ndiyo maana ana mpaka kaunta ya pombe kali nyumbani kwake,” alisema mmoja wa watu wake wa karibu (Team Wema).

ZARI ATAJWA
Ilisemekana kwamba mbali na mawazo ya Diamond ambaye amehamia kwenye nyumba ambayo Wema alikuwa na mchango mkubwa wakati wa ujenzi, pia suala la jamaa huyo kutanua na mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’ limekuwa likimpa wakati mgumu mwanadada huyo.


Staa katika tasnia ya filamu, Bongo Wema Isaac Sepetu.

SUALA LA UGUMBA
Habari zilieleza kuwa, jambo lingine linalompa Wema msongo wa mawazo ni suala la kukosa mtoto kila anapomtafuta akiamini kuwa watu wanajua yeye ni mgumba.Pia ilielezwa kwamba kuna suala la kuishiwa na kuogopa kufilisika kwani kwa sasa filamu hazilipi na bado anataka kuendelea kuwa na heshima ya kuitwa Madam hivyo njia pekee anayoona inafaa kutuliza mawazo ni kunywa pombe.

WOLPER
Kwa upande wake Wolper uchunguzi ulionesha kwamba, kwanza anapenda fedha hivyo kukosa tenda za kuigiza na kuanguka kwa soko la filamu za Kibongo kumemsababishia msongo wa mawazo kama ilivyo kwa Wema kwani naye anataka kuishi maisha ya kistaa ambayo hayawezekani bila kuwa na mshiko.

WOLPER KALOGWA?
Akizungumzia hali hiyo, Wolper alikiri kuwa na mawazo mengi huku akihisi kuwa huenda amelogwa.
USHAURI WA KISAIKOLOJIA


Staa katika tasnia ya filamu, Bongo Jackline Wolper.

Kwa mujibu wa mtaalam wa saikolojia aliyezungumza na gazeti hili juu ya mastaa aliwashauri kama ifuatavyo;
Mtaalam huyo alishauri mastaa hao kuachana na pombe na kama wana mawazo ya kuumiza, wanatakiwa kujilazimisha kutabasamu mara kwa mara na kusahau jambo linalowaletea mawazo mabaya.

Alisema kuwa, kutabasamu kutawasaidia kuchangamsha akili, ingawa inaweza kuchukua muda kurudi katika hali ya kawaida lakini inasaidia kuamsha hisia za furaha zilizokuwa zimeshambuliwa na mawazo mabaya na kuamini katika ushindi.

WASISAHAU NYUMBA ZA IBADA
Pia aliwashauri kusahau mambo yaliyopita na kujikita katika kufanya kazi kwa bidii hata kama matunda hawayaoni sasa, yatakuja baadaye.Mbali na hivyo wajitahidi kujichanganya katika makundi ya watu sahihi na kujumuika kwenye nyumba za ibada, msikitini (kwa muislam) na kanisani (kwa mkristo).

RAY C NAYE ATESWA NA UGUMBA

Musa mateja
WAKATI staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu akiweka wazi kuwa hawezi kupata ujauzito huku Judith Wambura ‘Jide’ naye akisumbuliwa na tatizo hilo, nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C amefunguka na kusema kuwa hali ya kukosa mtoto ambayo ni sawa na ugumba, inamtesa, kwani katika umri wake wa miaka 33, hajabahatika kuwa naye,Risasi Jumamosi linakujuza.


Nyota wa muziki Rehema Chalamila, Ray C.

Akizungumza na gazeti hili juzikati, Ray C alisema kuwa pamoja na hamu yake ya muda mrefu ya kupata mtoto, lakini ameshindwa ingawa anaamini siku yoyote Mungu atamuwezesha jambo hilo.“Hao kina Jide, Wema mi naona kama ni cha mtoto. Katika uhusiano wangu wa kimapenzi tangu nivunje ungo, nimewahi kushika mimba mara moja tu, wakati huo nikiwa na Mwisho Mwampamba, lakini bahati mbaya ilitoka, tokea hapo sijapata tena,” alisema staa huyo ambaye yupo katika mapambano ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.

Alisema katika umri wake huo anatamani sana kuwa na mtoto, kwani wasichana aliozaliwa nao wakati mmoja hivi sasa wanao watoto wawili hadi watatu, kitu ambacho kinamuumiza.Alipoulizwa kama matumizi ya dozi ya kuacha madawa ya kulevya inachangia tatizo lake hilo, alisema siyo kweli, kwani miongoni mwa ‘mateja’ wenzake anaokunywa nao dawa, wapo wajawazito na wengine wenye watoto.

Hata hivyo, alisema umri wake siyo mkubwa sana kukata tamaa ya kutozaa kwani wapo baadhi ya watu hupata ujauzito na kuzaa katika umri wa miaka 45 na kuendelea.“Sidhani kama umri ni sababu, nafikiri bado nina muda wa kuzaa na kumlea mwanangu nikijaaliwa kuwa naye, lakini pia huwa siishi kumshukuru Mungu kwa hivi nilivyo maana yawezekana kuna jambo ananiepusha nalo,” alisema.

“Kitu kingine kinachonifanya nisipate mtoto mapema ni pamoja na kutopata mwanaume aliyetulia ambaye ninaweza kuzaa naye, nadhani nikimpata mambo yanaweza kwenda vizuri.”Ray C anaingia katika orodha ya masupastaa ambao licha ya umri wao kuwa mkubwa, lakini bado hawajabahatika kupata watoto, baadhi yao wakiwa ni pamoja na Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Baby Madaha na Jacqueline Wolper.

BISHOP JOHN KOMANYA NDANI YA RUMAFRICA Online MAGAZINE


WATU 19 WAFARIKI KATIKA MACHIMBO YA DHAHABU KAHAMA


Wachimbaji wadogo wadogo 19 wa dhahabu wamefariki dunia baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo ya kijiji cha Karore, Kata ya Runguya, Tarafa ya Msalala mkoani Kahama.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justus Kamugisha, amesema usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji ambao walivavamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.

LULU AFUTA AKAUNTI YAKE INSTAGRAM

Muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ .

MUIGIZAJI wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyekuwa na wafuasi wengi kwenye Instagram, ameamua kujiondoa baada ya kushambuliwa kwa matusi na baadhi ya watu kufuatia kifo cha mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.


Kufuatia kifo cha kutatanisha cha Lusekelo Samson Mwandenga ‘Secky’, watu wengi walianza kumtukana Lulu wakimhusisha pia na kifo hicho huku pia wakiweka picha zinazomuonesha alipokuwa na marehemu.
Msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki nacho.

Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga 'Secky' enzi za uhai wake.

AMANDA AAMBIWA ANATUMIA ARV, AWA MBOGO!

Hamida Hassan
Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni aligeuka mbogo kwa shabiki wake aliyefahamika kwa jina la Joel baada ya kuambiwa eti ni mmoja wa wasanii wanaotumia vidonge vya ARV vya kuongeza siku za kuishi kwa waathirika wa Ukimwi.


Staa mwenye ‘figa’ matata, Tamrina Posh ‘Amanda’.

Ishu ilianzia kwenye mtandao wa Facebook ambapo Joel aliona picha ya Amanda akipima ugonjwa ambao haukujulikana ndipo kijana huyo alipokomenti kwamba eti msanii huyo ana ngoma.Akizungumza na Ijumaa, Amanda alisema amechoshwa na watu wanaomkashifu mtandaoni wakidhani kila msanii ni mhuni.

“Nimeona nimtolee uvivu kwani asifikirie Bongo Muvi wote tunatumia ARV, mimi nimepima mara ya mwisho juzi na najiamini najua ninachokifanya, alinikera sana yule kijana ndiyo maana nikampa makavu,” alisema Amanda.