Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, September 26, 2014

JINSI YA KUZIONDOA VIMBE MBALIMBALI KATIKA MWILI WA MWANAMKE PASIPO KUFANYA UPASUAJI




Wiki iliyopita tulizitazama aina za vimbe, tuliishia katika kipengele cha pili kilichosema:
Fibroids au Mayoma:Hizi ni vimbe zinazotokea katika mji wa mimba na hizi ndizo vimbe zinazowasumbua watu wengi sana katika jamii yetu ya sasa, na dalili zake ni kama;

Hapa mwanamke hupatwa na maumivu chini ya kitovu lakini ni katikati siyo upande wa kulia wala upande wa kushoto na mara nyingi maumivu haya huambatana na maumivu ya kiuno, maumivu ya mgongo na maumivu hayo huenda hadi sehemu za mapaja na kushuka hadi miguuni na maumivu haya huwa makali sana hasa wakati wa hedhi. Sasa ukiona unaandamwa na dalili hizi basi ujue kuna uwezekano ukawa na Fibroids au Mayoma.

Kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo, mwanamke ukiona tumbo linaongezeka ukubwa na unasikia kama kuna kitu kinatembea ndani ya tumbo, wakati huohuo unaandamwa na maumivu makali chini ya kitovu kwa katikati na maumivu makali sana wakati wa hedhi basi ni dalili kubwa sana nawe ukawa na Fibroids au Mayoma.
SASA ENDELEA…

Polycystic ovarian syndromes {PCOS} au Multiple cysts: Hizi ni zile vimbe ndogondogo nyingi zinazoweza kutokea kwenye kifuko cha mayai cha mwanamke, lakini nazo pia huweza kutokea katika pande zote mbili za vifuko vya mayai kwa mwanamke. Nazo zina dalili zake mbalimbali, nazo ni kama;

Hapa napo tunapata dalili tofauti, ya kwanza ni mwanamke kuwa na vinyweleo vingi sana katika mwili wake hasa kwenye mikono au kwenye miguu au anakuwa na ndevu au kifuani (garden love) na hii ni kwa sababu mwanamke huyu anakuwa na hormone nyingi sana za androgen yaani anakuwa na hormone nyingi za kiume, basi ukiona dalili kama hizo ni vema kuwahi hospitali.

Pia kuna hali ya kuvurugika hedhi ya mwanamke na kuwa haieleweki na kuwa na maumivu ya kiuno upande wa kulia au wa kushoto nayo pia inakuwa ni dalili kubwa sana ya PCOS au Multiple cysts hivyo ni vema kuchukua hatua za haraka.

Pia hali ya kutokwa na uchafu sehemu za siri kwa mwanamke ni moja ya dalili, na hasa uchafu huo unapokuwa hauna harufu wala hauwashi basi ujue kuwa kuna uwezekano mkubwa nawe ukawa na PCOS au Multiple cysts.

Hydrosulpinx:Hii ni ile hali ya mwanamke kujaa maji katika mirija yake ya kizazi na mirija hiyo inakuwa haipitishi mayai ya uzazi.

Dalili yake kubwa ni kuwa na maumivu makali sana kwenye kiuno ambayo huweza kutokea upande mmoja au yakatokea pande zote mbili na huenda hata maumivu yanayotokea upande, yote haya yanaisha bila kufanya upasuaji.

Dalili zipo nyingi sana na tukianza kuziongelea zote basi zinaweza kuchukua hata mwezi. Lakini tutaishia hapo kwa sasa na wiki ijayo tutaendelea na kuona Vyanzo vya Vimbe Katika Mwili wa Mwanamke.
Kama umeshawahi kupima na ukaambiwa kwamba una uvimbe katika mji wako wa mimba na hupendi kufanya upasuaji basi ni bora ukawasiliana nasi kupitia namba zetu.

Kwa ushauri, vipimo na tiba dokta wetu anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.

Itaendelea wiki ijayo.

Wednesday, September 24, 2014

UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA (CONGENITAL HEART DISEASE) UNAVYOLETA SHIDA KWA BINADAMU



Leo tutajadili baadhi ya matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo, yaani Congenital Heart Disease.

Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo ni mengi, kuanzia yale yanayosababishwa na matatizo madogomadogo ambayo kwa kawaida huwa hayaonyeshi dalili au kuathiri maisha ya kawaida ya mtu, hadi yale makubwa yanayohitaji kutibiwa kwa haraka.

Mara nyingi matatizo ya moyo ya kuzaliwa ni yale yanayozuia mtiririko wa damu katika moyo au kwenye mishipa ya damu, au kusababisha damu ipite njia nyingine isiyokuwa ya kawaida kwenye moyo.

Matatizo mengine ya moyo ya kuzaliwa lakini yasiyotokea sana ni pale baadhi ya chemba za moyo zinapokosekana au badala ya kuwepo chemba mbili mtoto huzaliwa na chemba moja ya ventricle au wakati mwingine upande wa kulia au wa kushoto wa moyo huwa haujaumbika kwa ukamilifu hali ambayo kitaalamu huitwa hypoplastic heart.

Miongoni mwa sababu zinazosababisha watoto kuzaliwa na matatizo ya moyo ni pamoja na mmoja kati ya wazazi kuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa. Iwapo mama alikuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa kuna uwezekano wa asilimia 2.5 hadi 18 wa kuzaa mtoto mwenye tatizo la moyo pia. Iwapo baba alikuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa uwezekano wa kuzaliwa mtoto mwenye tatizo la moyo ni kuanzia asilimia 1.5 hadi 3.

Si kawaida mtoto zaidi ya mmoja kuzaliwa na tatizo la moyo katika familia moja. Kuna uwezekano mtoto aliyeko tumboni wakati moyo unapoumbwa akapatwa na maambukizi ya maradhi kama vile rubella, au kuathiriwa na dawa anazotumia mama wakati wa ujauzito au sumu kama vile lithium na hata pombe.

Yote hayo yanaweza kusababisha mtoto azaliwe na matatizo ya moyo. Lakini pia baadhi ya matatizo ya jenetiki huambatana na matatizo kadhaa ya moyo ya kuzaliwa. Matatizo hayo ya jenetiki kitaalamu huitwa Down’s Syndrome, Digeorge syndrome na Turners Syndrome.

Jambo lingine linaloweza kusababisha mtoto azaliwe na matatizo ya moyo ni pale mama anapokuwa na tatizo la kijenetiki linalojulikana kama Phenylketonuria (PKU). Hali hiyo hutokea wakati mwili unaposhindwa kuyeyusha sehemu ya protini inayoitwa phenylalanine (Phe).

Phenylalanine kwa kawaida hupatikana katika kila chakula lakini kiwango chake kinapokuwa juu mwilini huweza kuharibu ubongo na kusababisha mtindio wa ubongo. Baadhi ya wajawazito hupata tatizo hilo ambalo huzidisha uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya moyo na ya ubongo pia.

Itaendelea wiki ijayo.

Friday, September 19, 2014

VIDONDA VYA TUMBO VINAVYOWATESA WENGI BILA KUJUA!

Vidonda vya tumbo ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi, wanaume na wanawake na hata watoto wadogo. Tatizo hili husumbua sana na kumfanya mgonjwa asiweze kumudu shughuli zake za kila siku.
Ugonjwa huu huathiri kwa ujumla katika suala zima la afya.
Tatizo hili huanza taratibu na dalili za awali huwa hazionyeshi kama mtu ana ugonjwa huu.

Chanzo cha ugonjwa
Ugonjwa huu hutokana zaidi na maambukizi ya bakteria waitwao ‘Herictobacter Pylori’ au maarufu kama H. Pylori hushambulia tabaka la ndani la tumbo.

Aina hii ya bakteria ni wagumu kufa kwa kuwa wana uwezo wa kuishi kwenye mazingira ya tindikali tumboni. Tumboni kuna tindikali ya Hydrochloric Acid ambayo husaidia katika mmeng’enyo wa chakula.
Bakteria hawa wanaposhambulia tabaka la ndani la kizazi, hutegemea vishimo vishimo ambavyo ni vidonda hivyo tindikali inapotoka huchoma kwenye hivyo vidonda na kumfanya mgonjwa ahisi maumivu makali.

Aina za vidonda vya tumbo
Vidonda vya tumbo vipo vya aina mbili, kwanza ni vile vilivyopo mwanzoni mwa tumbo la chakula, Gastric Ulcers na ya pili ni Duodenal Ulcers katika sehemu ya pili ya tumbo. Maumivu na dalili za aina hizi mbili hufanana sana.

Ili kutofautisha aina hizi za vidonda, vipimo maalum hufanyika kama vile ‘OGD” na “Barium Meal’, vipimo ambavyo hufanyika katika hospitali za rufaa.

Dalili za ugonjwa
Hapa tutazungumzia dalili kuu za vidonda vya tumbo kwa ujumla. Mgonjwa wa vidonda vya tumbo katika hatua za awali huwa hajigundui kama ana tatizo.

Mgonjwa hulalamika kuhisi homa za mara kwa mara na kujihisi kama ana malaria au homa ya tumbo ‘Taifoidi’, wengine hulalamika kutumia sana dawa za taifoidi lakini hakuna nafuu.
Mwili unanyong’onyea, maumivu ya viungo, kuhisi baridi kuumwa kichwa na tumbo kujaa gesi.
Mgonjwa pia hulalamika maumivu ya tumbo eneo la chembe ya moyo ambapo ni chini ya kifua na juu ya kitovu.

Maumivu ya muda mrefu husambaa tumbo lote na tumbo huunguruma mara kwa mara .
Maumivu ya chembe ya moyo yaani chini ya kifua na juu ya kitovu husambaa hadi kifuani na kuzunguka mpaka mgongoni.

Mgonjwa hulalamika kuhisi moto kifuani na maumivu yaani kiungulia. Akilala usiku hali ya moto huongezeka na mgonjwa akicheua hutoa majimaji ya moto na machungu.

Mgonjwa hupata choo kigumu na vipande vipande kama cha mbuzi na wakati mwingine huwa cheusi.
Mgonjwa hupoteza hamu ya kula na wakati mwingine hutapika damu. Macho hupoteza nguvu ya kuona kwa kuwa muda wote anakuwa na maumivu, mwili unachoka na anakosa raha kutokana na kuwaza sana juu ya maumivu anayopata kiasi cha kumfanya mgonjwa akonde.

Mkojo unakuwa wa njano sana, hufunga kupata choo kikubwa na kusababisha maumivu ya kiuno kwa ndani ambayo husambaa hadi miguuni. Hamu ya tendo la ndoa pia hupotea.

Uchunguzi wa ugonjwa
Uchunguzi wa awali hufanyika katika vituo vya afya na hospitali za wilaya, mikoa na rufaa. Ni ugonjwa unaotibika hospitali na vipimo ni kama Ultrasound, OGD, Barium Meal na vipimo vya damu ili kuangalia maambukizi ya H. Pylori na wingi wa damu.

Choo kikubwa pia kitapimwa. Ni muhimu pia kuangalia matatizo mengine kwa undani. Kipimo cha OGD ambacho kitapitishwa katika mfumo wa chakula kitasaidia kutoa majimaji yatakayopimwa maabara.

Ushauri
Ni vema mgonjwa azingatie kuhudhuria hospitali kwani ugonjwa wa vidonda vya tumbo huchunguzwa na kutibiwa hospitali ingawa tiba huchukua muda mrefu. Ugonjwa huu dalili zake zinafanana sana na saratani au kansa ya tumbo hivyo ni vizuri uwahi hospitali ili ugundulike mapema.Unaweza ukawa unatumia dawa nyingine pasipo uchunguzi wa kidaktari mwishowe ukajikuta tayari hali inakuwa mbaya na kusababisha utumbo kutoboka au kansa.

Thursday, September 18, 2014

TAMBUA VYAKULA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA SARATANI

UTAFITI mbalimbali uliokwishafanywa unaonyesha kuwa magonjwa mengi ya saratani (cancer) yanatokana na vyakula tunavyokula kila siku katika maisha yetu. Katika siku za hivi karibuni, ongezeko la magonjwa haya limekuwa kubwa kwa sababau vyakula vinavyosababisha magonjwa hayo, ndivyo vinavyoliwa sana kuliko vile vinavyozuia.

Wiki iliyopita tuliwaorodheshea baadhi ya vyakula vinavyoaminika kusaidia kuzuia magonjwa ya kansa ambapo wiki hii tunawaletea orodha ya vyakula vinavyoaminika kuongoza kwa kuwa chanzo cha magonjwa hayo hatari:

VYAKULA VYA KUKAANGA

Vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni ma madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.

VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI

Vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini Japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage, n.k

SUKARI

Matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.

Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.

NYAMA ILIYOIVA SANA
Upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo Kikuu cha Utah (University of Utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (Rectal Cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.

POMBE
Unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini Marekani.

NYAMA NA MAFUTA

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Havard nchini Marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.

VYAKULA VYA UNGA MWEUPE

Vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k
Mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.

UNADHANI WANANCHI WAMEPATA ELIMU YA KUTOSHA JUU YA UGONJWA WA EBOLA?

Bado jitihada zaidi zinahitajika, wengi wao wanajua juujuu tu. Serikali inabidi itoe elimu zaidi. Wakati huohuo, serikali inapaswa kuwa makini na watu wanaotoka nchi zilizoathiriwa na ugonjwa huo ili kuzuia kuuingiza nchini.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Herry Samir 'Blue'

Herry Samir
’Mr. Blue’:Bado kabisa hakuna kitu kilichoeleweka, kuna wananchi ambao bado ujumbe haujawafikia vya kutosha na ndiyo maana kuna baadhi ya watu hawajui Ebola ni nini.
Kikubwa waelimishwe juu ya maradhi hayo ambayo ni hatari kwa sababu uua kwa muda mfupi.


Mkali wa bongo flava kutoka (THT) Amini Mwinyimkuu

Amini Mwinyimkuu
Kila mtu anauzungumzia ugonjwa wa Ebola, hivyo inamaanisha kuwa elimu imeeleweka na Watanzania wengi wanaomba usifike katika mataifa mengine, kwa taifa na mataifa yaliyokumbwa na ugonjwa huo Mungu awafanyie wepesi kuepukana nao.


Malkia wa zouk tanzania Hafsa Kazinja Hafsa Kazinja:

Tuesday, September 16, 2014

KUPITIA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC ZIFAHAMU FAIDA ZA KULA LIMAO

Limau lina manufaa chungu nzima kama vile kutuliza, kutibu, kupunguza sumu mwilini n.k.

Shinizo la Mawazo:
Huondoa uchovu wa akili, kisunzi, na pia wasiwasi. Limau lina uwezo wa kutuliza akili kwa kuondoa mawazo. Aidha unapumua harufu ya limau unaweza kujiongezea umakinifu.

Usingizi:
Utumiaji wa limau husaidia kumpa mtu usingizi na kuepusha tatizo la kupata usingizi.

Mfumo wa Kinga:
Limau lina kiwango kikubwa cha Vitamini kwa hivyo ni zuri kwa kuimarisha kinga mwilini, kwa kuzipa nguvu chembechembe nyeupe za damu, na kuimarisha mzunguko wa damu mwilini.

Homa:
Linaweza kutumika kuponya maradhi ya kuambukiza kama homa, malaria na homa ya matumbo.

Matatizo ya Tumbo:
Hutibu maradhi tofauti ya tumbo kama shida za usagaji chakula, , maumivu ya tumbo, na mshipa.

Kupunguza Uzani:
Hutumika na wengi kupunguza Uzani.

Pumu:
Inaaminika kwamba limau linasaidia kutibu pumu.

Nywele:
Aidha limau hutumiwa kwa utunzaji nywele. Limau huzifanya nywele kuwa na afya na za kuvutia, na huondoa uyabisi.

Ngozi:
Limau hutumiwa kutunza ngozi, kwa kuipa afya. Hutibu vidodosi na mba.

MTI WA MWAROBAINI HUTIBU MAGONJWA YA NGOZI

The Fadhaget Sanitarium Clinic siku ya leo imeona itoe elimu ya faida za mti wa mwarobaini hasa katika suala zima la magonjwa ya ngozi yanayosumbua sana wanadamu.

Mwarobaini (Azadirachta indica) ni mti unaofahamika kwa uwezo wake wa kutibu magonjwa ya aina mbalimbali. Inaaminika kuwa mti huu umetoka huko India na Burma . Mwarobaini hushamiri zaidi katika nchi za tropiki na una uwezo mkubwa wa kuhimili ukame. Nchini Tanzania, mti wa mwarobaini huweza kupatikana kwa urahisi kabisa katika maeneo mengi ya mijini na vijijini.

Jina “mwarobaini” linatokana na imani kuwa mti huu una uwezo wa kutibu magonjwa yapatayo arobaini. Majani na mbegu za mwarobaini vimekuwa vikitumiwa kama tiba kwa miaka maelfu katika nchi mbalimbali duniani.

Kati ya magonjwa ambayo mti huu umetumika kutibu au kupoza ni pamoja na matatizo ya kusaga chakula tumboni, kisukari, kansa, magonjwa ya ngozi, malaria, ukungu (fungus), n.k. Matawi yake hutumiwa kama mswaki na magome yake hutumiwa kama dawa ya kusafisha meno.

Mafuta ya mibegu ya mwarobaini hutumika kutengenezea vipodozi na sabuni. Kiziduo cha mibegu au mafuta yake hutumiwa kama dawa ya kuulia wadudu wanaoharibu mimea shambani.


Tumekwisha ziona faida mbalimbali za mti wa mwarobaini, leo nitakufundisha namna ya kutumia mti wa mwarobaini kujitibu magonjwa ya ngozi.

MAHITAJI :
  • Majani ya mti wa mwarobaini.
  • Sufuria
  • Mwiko
  • Jiko la gesi, mkaa au jiko la mafuta.
HATUA ZA KUFUATA:
  1. Chukua majani mabichi ya mti wa mwarobaini na uyaweke kwenye sufuria.
  2. Chukua sufuria yako yenye majani ya mti wa mwarobaini na ui injike kwenye jiko lenye moto wa wastani.
  3. Chukua mwiko wako na uanze kuyakoroga majani yako taratibu hadi yakauke bila kuungua.
  4. Majani yako yakiisha kauka, ipua sufuria yako, chukua majani yako yaliyo kauka, yasage kisha hifadhi unga unga wako kwenye chombo cha plastiki.
MATUMIZI :
Tumia vijiko viwili vya chai kwenye kikombe cha robo lita chenye maji ya moto, mara mbili kwa siku kwa muda wa siku ishirini na moja.

Friday, September 12, 2014

HATIMAYE JOHN SHABANI ATEMBELEA OFISI ZA BBC AKABIDHI WIMBO WA EBOLA

Baada ya mchakato wa takribani miezi miwili ya kuandaa wimbo unaoelezea janga la Ebola, hatimaye mwalimu maaarufu wa muziki wa injili Afrika mashariki akishirikiana na waimbaji mbalimbali amekalisha wimbo huo na kuanza kuhusambaza katika vyombo mbalimbali vya habari.

Wimbo huo unaelezea chanzo cha gonjwa la Ebola, namna unavyoenea, na jinsi ya kujikinga. Imechukua muda kidogo kuandaa wimbo huo, kwani ilihitajika ushirikishwaji wa baadhi ya madaktari na watafiti wa gonjwa hilo. Hata hivyo baada ya kupokelewa ofisi hizo za kituo cha kimataifa cha BBC, John Amepongezwa kwa kuwa msanii wa kwanza duniani kujitolea kurekodi wimbo wa Janga hilo lililogusa dunia.

Pamoja na wimbo wa janga la Ebola, pia John amekabidhi wimbo unaotetea haki za watoto na wanawake. Mmoja kati ya maripota wa bbc bwana John Solombi, ameweza kufanya mahojiano ya kina na John Shabani na kuahidi kupanga muda mzuri zaidi wa mahojiano.

Kwa pamoja tuseme hapana kwa Ebola.

John Shabani akifanya mahojiano na mtangazaji wa bbc, bwana John Solombi



John shabani akikabidhi CD

TATIZO LA KUHARIBIKA MIMBA MARA KWA MARA!

Tatizo la kuharibika mimba mara kwa mara kitaalamu huitwa ‘Recurrent pregnancy loss’. Mwanamke hujitahidi kutafuta ujauzito lakini inakuwa ngumu ujauzito kukua hadi kufikia kujifungua.
Hali hii huleta athari kubwa kwa mwanamke pamoja na kuathirika kiafya kutokana na mimba kuharibika mara kwa mara lakini pia huathirika kisaikolojia kwa kutopata watoto. Ni mojawapo ya tatizo linalochangia ugumba katika jamii.

Kipindi cha ujauzito huchukua majuma arobaini kuanzia mimba inapotungwa hadi mama anakuja kujifungua mtoto kamili. Mtoto kamili na mwenye afya njema huzaliwa katika uzito wa kilo kuanzia mbili na nusu.

Chini ya uzito huu ni watoto wenye matatizo na wanakuwa katika uangalizi maalumu hospitali chini ya usimamizi wa madaktari wa watoto.Kipindi cha ujauzito pia kimegawanyika katika vipindi vitatu ambavyo kitaalamu huitwa ‘Trimesters’, vipindi hivi ni vya miezi mitatu mitatu. Miezi mitatu ya kwanza tunaita kipindi cha uumbaji.

Katika kipindi hiki ndipo viungo vya mtoto vinapoumbwa na kukamilika.Mimba inayoumbwa ikiwa na kasoro mwili wa mama unaofanya kazi vizuri huitoa wenyewe, hapa ndipo tunapopata historia ya mama kwamba amepoteza mimba kadhaa zikiwa na umri wa chini ya miezi mitatu. Ni mara chache vyanzo vyake kutibika.

Vipo vyanzo vingi vinavyosababisha mimba changa ziwe zinatoka, vyanzo hivi ni rahisi kugundulika baada ya kuhudhuria hospitali kwa daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi.
Ujauzito kuharibika katika miezi mitatu ya kwanza chanzo ni mimba yenyewe.

Ujauzito kuharibika katika miezi mitatu ya pili hutokana na tatizo katika mlango wa kizazi wa mama kushindwa kushikilia mimba. Tatizo hili kitaalamu huitwa ‘cervical incompetence’.
Mama anakuwa na historia ya mimba kumtoka kuanzia umri wa zaidi ya miezi mitatu hadi sita. Mimba inaendelea vizuri kwa zaidi ya miezi mitatu ya kwanza na inapofikia miezi mitatu ya pili inatishia kutoka hadi inatoka.

Vyanzo vya mlango wa kizazi kulegea vipo vingi navyo pia vinahitaji uchunguzi wa kina kwa daktari wa kinamama na ikithibitika hivyo, basi mlango wa kizazi utashonwa na mama atapata mapumziko ya muda mrefu na akija kujifungua atafunguliwa kwanza nyuzi kisha atajifungua.
Katika kipindi hiki hata mtoto anaweza kufia tumboni na chanzo kikuu kinaweza kuwa upungufu mkubwa wa damu kwa mama mjamzito, shinikizo la damu kuwa juu na sababu nyingine ambazo daktari atazigundua.

Kwa kawaida presha ya mama mjamzito inatakiwa isizidi 120 kwa 80. Ikizidi hapo ni vema ufuatilie kwa daktari wako.

Shinikizo la damu kuwa juu kwa mama mjamzito dalili zake ni kuvimba miguu, kukosa pumzi wakati wa kutembea, maumivu ya kifua na wakati mwingine macho hayaoni vizuri, akipimwa mkojo ataambiwa kuna protini nyingi kwenye mkojo.

Presha ikizidi kupanda, basi mama mjamzito atapata kifafa cha mimba. Pamoja na dalili hizo, ataanza kurusharusha mikono na miguu na kuwa kama mtoto mwenye degedege au mgonjwa wa kifafa.
Ni dalili ya hatari kwa uhai wa mama na mtoto.

NINI CHA KUFANYA?
Matatizo ya kuharibika kwa mimba mara kwa mara au watoto kufia tumboni ni tatizo linaloathiri afya ya mama na jamii yake kwa ujumla kwa kila kitu.Kama nilivyoelezea hapo awali, tatizo hili lina ufumbuzi endapo mama atahudhuria hospitali mapema. Uchunguzi na tiba hupatikana katika hospitali za wilaya na mikoa popote nchini.

Muone daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na matatizo ya uzazi katika hospitali hizo. Epuka imani potofu katika masuala haya, fuatilia uchauri wa kidaktari.

Wednesday, September 10, 2014

RAIS KIKWETE AKAGUA UTAYARI WA TANZANIA KUKABILIANA NA EBOLA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi vifaa maalumu vinavyofanya kazi ya kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jana Septemba 9, 2014 mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa maelekezo ya namna ya kuhudumia abiria wakati wa ukaguzi wa wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya jinsi madaktari na wauguzi walivyo jiandaa kufanya ukaguzi wa abiria na kutambua wagonjwa wa ebola mara watapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wauguzi waliovalia mavazi maalumu tayari kutoa huduma kwa abiria atayekutwa na ugonjwa wa ebola mara atapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wauguzi waliovalia mavazi maalumu wa wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam jana mara alipowasili kutokea Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid jinsi Tanzania ilivyojipanga kupambana na ugonjwa hatari wa ebola baada ya kukagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.
Wauguzi waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakiwa katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaangalia wahudumu waliopata mafunzo maalumu ya kumhudumia mgonjwa wa ebola wakati alipokagua wodi maalumu iliyotengwa kwa ajili ya wagonjwa wa ebola iliyoko katika eneo la hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam.

GONJWA LINALOSABABISHWA NA KUNYONYA UKE WA MWANAMKE

Saratani imeendelea kuwa tishio hapa nchini huku hofu ikiendelea kuikumba jamii kutokana na wataalamu wa afya kushindwa kufahamu tiba halisi ya maradhi hayo hatari. Takwimu kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road zinaonyesha ongezeko la saratani ya mdomo na koo kwa kiasi kikubwa kutoka kesi 167 mwaka 2006 hadi 277 mwaka 2012. Mkurugenzi wa Idara ya Kinga


Ocean road, Julius Mwaiselage anaeleza kuwa watanzania wasipende kuiga mambo ambayo si sahihi bila kujua madhara yake kama kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo. “Saratani ya mdomo ipo, na nyingine zinasababishwa na zinaa “ anasema Dk Mwaiselage

Tafiti za saratani
Tafiti mbalimbali zimewahi kufanyika nchini na kubaini kuwepo kwa ongezeko la saratani ya mdomo.Utafiti uliofanywa na Dk Innocent Mosha wa Kitengo cha Patholojia cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), umebaini aina za saratani 1,594, kati ya hizo 509 zikiwa ni za midomo kwa mwaka 2003 pekee. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa kati ya saratani 509 za mdomo, saratani 242 zilisababishwa na Virusi vya Human Papiloma ambavyo hutokana na zinaa. “Ninachojua mimi ni kuwa Virusi vya HPV husababishwa na magonjwa ya zinaa, hivyo mtu anayeugua saratani ya aina hiyo, imetokana na zinaa,” anasema Dk Mosha.

Wanaume waathirika zaidi wa Saratani
Takwimu hizo ni zile zilizopatikana kwa watu waliokwenda kufanyiwa uchunguzi katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee. Dk Mosha anasema kuwa wanaume ndiyo huathiriwa zaidi na saratani ya mdomo ambapo kwa hapa nchini, asilimia 53 ya wanaume waliofika MNH kwa ajili ya vipimo, walibainika kuugua saratani hiyo, huku wanawake wakiwa ni asilimia 47. Utafiti kama huo ulifanywa pia na Dk Amos Mwakigonja, mkuu wa Idara ya Patholojia katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili (MUHAS).

Dk Mwakigonja alifanya utafiti wa saratani ya mdomo aina ya Kaposi’s Sarcoma ambapo wagonjwa 78 walibainika na saratani hiyo kuanzia mwaka 1990 hadi 2003. “Saratani za mdomo zipo za aina nyingi na zimetofautiana kulingana na visababishi vyake,” anasema Dk Mwakigonja. Katika utafiti wake Dk Mwakigonja alibaini kuwa wanawake wengi walikuwa na saratani ya mdomo aina ya Kaposi’s Sarcoma kuliko wanaume.

Hata hivyo, utafiti huo ulionyesha kuwa asilimia 50 ya wanaume walikuwa na saratani ya mdomo hatari zaidi (systemic) kuliko wanawake ambao ni asilimia 37.

Mapenzi kwa mdomo husababisha maradhi

Dk Mwakigonja anasema kuwa mapenzi yoyote kwa njia ya mdomo lazima yasababishe maradhi ya zinaa iwapo mmoja ameambukizwa. Pia anasema kwamba sampuli nyingi za wanaume wanaojihusisha na mapenzi na wanaume wenzao (mashoga) zilibainika na saratani ya mdomo. Utafiti huo ni sehemu ya utafiti wa Shahada ya Uzamivu ambao ulionyesha kuwa wagonjwa wengi wa saratani ya mdomo walikuwa ni wanaume wenye umri wa miaka kati ya 38 na kuendelea na wanawake ni 31.

Ufatiti wa WHO Tanzania

Shirika la Afya Duniani (WHO) pia lilifanya utafiti mwaka 2010 nchini kwa kushirikiana na Kituo cha Taarifa za HPV, ambapo ilibainika kuwa asilimia 20 ya saratani za koo na mdomo nchini zinasababishwa na ufanyaji wa mapenzi kwa njia ya mdomo.

Taarifa hizo za WHO zinaeleza kuwa wanaume 747 hugundulika na saratani ya mdomo kila mwaka wakati wanawake 472 hubainika na saratani hiyo pia. Wakati huohuo, wanaume wanaopoteza maisha kutokana na saratani hiyo ni 444, kwa mwaka na wanawake ni 270, kwa mwaka. Utafiti wa WHO umebaini kuwa saratani ya mdomo inashika nafasi ya sita katika aina 24 za saratani 24 zinazoisumbua zaidi Tanzania.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa wanaume wanaoathirika zaidi ni wenye umri wa kati ya miaka 15 na 55, ambao tayari wameshaanza kujihusisha na ngono. Kama maradhi mengine ya kuambukiza, Virusi vya HPV huambukizwa kwa urahisi zaidi kutoka kwa wanawake kwenda kwa wanaume kuliko kutoka kwa wanaume kwenda kwa wanawake. Utafiti huo uliodhaminiwa na mfuko wa Bill na Melinda Gates na Kituo cha Saratani na Mpango wa Utafiti wa Taasisi ya ICO unaeleza kuwa mitandao ya kijamii na picha za ngono ndiyo chanzo cha watu wengi kuiga ufanyaji wa mapenzi ya aina hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la The New York Times, tafiti zimefanyika na kubaini kuwa asilimia 70 ya wagonjwa wanaobainika na saratani ya koo na mdomo duniani, husababishwa na Virusi vya Human Pappiloma vinavyotokana na magonjwa ya zinaa.Tafiti hizo zinaonyesha kuwa wagonjwa wengi wanaogundulika na saratani hiyo ni wanaume wenye umri wa kati, wenye uwezo wa kifedha, wasiovuta sigara wala siyo walevi waliokubuhu.

Utafiti huo ulibaini kuwa wanaume wapo hatarini zaidi kupata saratani ya koo inayosababishwa na Virusi vya HPV. Miaka ya 80, idadi ndogo ya watu waliougua saratani ya koo walihusishwa na maambukizi ya Virusi vya HPV. Kihistoria, watu waliobainika na ugonjwa huo, ni wenye umri wa miaka 70 kwenda juu ambao walikuwa ni wale walevi waliokubuhu na wavuta sigara.

Ilielezwa kuwa Virusi vya HPV vipo kwa wingi kiasi ambacho watu wazima wanaojihusisha na ngono ya aina yeyote ile, huweza kupata maambukizi ya zinaa hata kama siyo saratani. Hata hivyo ilibainishwa kuwa saratani isababishwayo na virusi vya HPV ni rahisi kuitibu kuliko saratani ya koo isababishwayo na tumbaku au pombe kali.

Virusi vya HPV ni nini?
Kwa jina la jumla, saratani ya koo au mdomo huitwa saratani ya kichwa na shingo. (Neck and Head Cancer) HPV ni miongoni mwa virusi hatari zaidi duniani visababishwavyo na magonjwa ya zinaa na vinaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili. Zipo aina zaidi ya 120 za HPV, baadhi huweza kuzalisha usugu (warts) ambazo si saratani katika sehemu za siri, mikononi na miguuni. Maambukizi ya HPV hufanyika kwa urahisi, hata kwa kugusana ngozi au majimaji, huku maambukizi mengine yakisababishwa na ngono.

Virusi hatari na vinavyosababisha saratani ni HPV-16, HPV-18, HPV-31 na HPV 45. Aina hii ya Virusi vya HPV husababisha saratani ambapo uvimbe waweza kujitokeza kwa ndani na unaweza usionekane ukilinganisha na vivimbe vingine vya saratani. Wataalamu wanasema HPV-16 na HPV-18 inahusishwa zaidi na saratani ya shingo ya kizazi na endapo mapenzi kwa njia ya mdomo yatafanywa na mtu mwenye uambukizo huu ni rahisi kuambukizwa

Sunday, September 7, 2014

THE FADHAGET INAKULETEA MAAJABU KUMI YA TANGO KIAFYA


Ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.

Hawakukosea wale waliosema kuwa mboga za majani na matunda ni kinga kwa afya yako. Matunda mengi yana manufaa lakini tango tunasema limetia fora.
http://api.ning.com/files/iDV9E-FRGg78mjrgRcL9Mk3e74WpdotTUb45LjgFG*6A3-UERWlRydv9S4eCBPM5eO6kZbPwh8lHDZexTpzK6myNn7xi9dQe/cucumber_slices5605.jpg?width=550
Kwanza linasifika kwa kuwa na vitamin zote unazohitaji kwa siku. Tango moja lina vitamin B1, B2, B3, B4 na B6, madini ya chuma, potasium na zinc.

Pili, unapojisikia kuchoka mchana, kula tango moja ambalo linaweza kukupa nguvu kwa saa kadhaa.

Tatu, ngozi yako inahitaji tango kutoa seli zilizokufa na makunyanzi. Weka au sugulia vipande vya tango usoni au sehemu iliyoathirika na utaona maajabu baada ya siku chache.

Nne, unataka kuondoa ‘hangover’ au maumivu makali ya kichwa, kula tango ambalo lina sukari ya kutosha na vitamin zitakazoweka mambo sawa mwilini.

Tano, umechelewa kwenda kwenye usaili, viatu ni vichafu, chukua vipande vya tango na sugulia katika viatu. Vitang’aa.

Sita, umemaliza kula, unahisi una harufu mbaya mdomoni nyakati za mchana. Tafuna vipande vya tango na utapata harufu nzuri ya mdomo.

Saba, midomo imekauka na inauma? Chukua kipande cha tango na sugulia mdomoni, utaona mabadiliko katika midomo.

Nane, umekosa muda wa kula mchana, kula tango moja bila kumenya maganda na litaweza kukaa tumboni kwa saa zaidi ya nane.

Tisa, umekosea kuandika katika ubao au ukuta, chukua maganda ya tango na usugulie taratibu, wino au rangi hiyo itafutika kabisa.

Kumi, pia, tango lina uwezo mzuri wa kusafisha vioo ambavyo vimefubaa kwa uchafu au maji ya chumvi.

Friday, September 5, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INAPENDA KUKUPA SOMO LA DALILI NA ISHARA ZA UJAUZITO

Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana

Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.

Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za Ujauzito:

Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii

  • Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
  • Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
  • Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
  • Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
  • Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu ya kichwa
  • Kizunguzungu
  • Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
  • Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
  • Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
  • Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
  • Tumbo kujaa au kuvimbiwa
  • Kununa na kukasirika haraka
  • Kiungulila au kupata choo kigumu
  • Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
  • Kuongezeka uzito
  • Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
  • Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
  • Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign
Dalili nyingine ni pamoja na
Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
  • Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
  • Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
  • Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
  • Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto
  • Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound

DR. FADHILI EMILY ATOA POLE KWA WALIOFIWA NA KUUMIA KATIKA AJALI MBAYA BASI LA J4 COACH ILIYOKEA LEO

Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana baada ya kusikia watu wamepoteza maisha yao katika ajali hii mbaya iliyokea leo na wengine kupata maumivu makubwa katika viungo vyao, inasemekana watu zaidi ya 28 wanahofiwa kupoteza maisha katika ajali ya mabasi ya Mwanza Coach na j4 Express lenye namba za usajili T677 CYC lililokuwa likitokea Sirari kwenda Mwanza kugongana na basi la Mwanza Coach lenye namba za usajili T736 AWJ leo asubuhi.

Miili na majeruhi wakipokelewa katika Hospitali ya mkoa wa Mara.
...
Baadhi ya maiti zikiwa zimefunikwa.


Baadhi ya wakazi wa Mara pamoja na wauguzi wakiangalia maiti wa ajali hiyo


Baadhi ya wakazi wa Mara wakiwa wamekusanyika katika hospitali hiyo.

Wednesday, September 3, 2014

UNAZIFAHAMU DALILI ZA SHAMBULIZI LA MOYO (HEART ATTACK)?

Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.

Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.



Je tatizo hili husababishwa na nini?
Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).

Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?
Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na
• Wavutaji wa sigara
• Wenye umri mkubwa miaka 45 kwa wanaume na 55 kwa wanawake
• Watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao
• Wenye kisukari
• Wenye matatizo ya shinikizo la damu
• Walio na unene kupita kiasi (obesity)
• Wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure)
• Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
• Wanywaji wa pombe kupindukia
• Watumiaji wa madawa ya kulevya hasa cocaine na methamphetamine
• Watu wenye msongo wa mawazo (Chronic high stress levels)
• Upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid

Dalili za shambulizi la moyo
• Maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto
• Kupumua kwa shida
• Kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis)
• Kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations)
• Kichefuchefu
• Kutapika
• Kuchoka haraka sana
• Kupoteza fahamu
Shambulizi la moyo limehusishwa na nini?
Tafiti mbalimbali zimeusisha mambo yafuatayo na shambulizi la moyo
• Msongo wa mawazo
• Maambukizi hasa vichomi vinavyosababishwa na vimelea vya chlamydophila pneumonia.
• Hutokea zaidi asubuhi hasa saa tatu (saa 3 asubuhi)

Vipimo na uchunguzi
• ECG - Kipimo hiki huonyesha ni sehemu gani ya moyo iliyoathirika
• Coronary angiography - Kinasaidia kwa kuangalia wapi ambapo mishipa ya damu imekuwa membamba sana kupita kiasi (narrowing of vessels) au imeziba.
• Cardiac markers levels
• X-ray ya kifua (chest X-ray)
• MPI (Myocardial Perfusion Imaging) - Kipimo hiki hufanywa kwa kutumia mashine maalum ya PET Scan ambapo kinauwezo wa kugundua tatizo la shambulizi la moyo, huchunguza kikamilifu maumivu ya kifua, huangalia mwelekeo wa tiba ya kuzuia damu kuganda, hutoa mwelekeo wa ugonjwa wa shambulizi la moyo kama ni mzuri au mbaya, hutathmini ubora wa tiba ya shambulizi la moyo kabla na baada ya mgonjwa kupata tiba, huweza kutambua hata shambulizi la moyo ambalo si rahisi kugundulika kwa kutumia vipimo vyengine na pia hutathmini ukubwa wa tatizo la shambulizi la moyo. Hata hivyo kwa sasa kipimo hiki hakipatikani nchini kwetu.

Ili kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, mwaka 1979, shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vya kutambua shambulizi la moyo. Vigezo hivyo ni
• Historia ya kuwa na maumivu ya kifua zaidi ya dakika 20
• Mabadiliko katika kipimo cha ECG, na
• Kupanda na kushuka kwa kipimo kiitwacho kitaalamu cardiac biomarkers hasa creatine kinase - MB na troponin

Matibabu

Shambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharua. Lisipotibiwa kwa haraka husababisha kifo katika muda mfupi sana tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha
• Kumpa mgonjwa hewa ya oksijeni
• Mgonjwa hupewa vidonge vya Aspirini ndogo kuzuia damu kuganda (thrombolytic) kwa ajili ya kuyeyusha damu iliyaganda na hivyo kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyozibwa na kuganda huku kwa damu.
• Vile vile mgonjwa hupewa dawa za kuweka chini ya ulimi kiitwacho nitrogylycerin (glyceryl trinitrate) ambazo husaidia kutanua mishipa ya damu (vasodilation)
• Dawa ya kutuliza maumivu kwa mfano morphine
• Dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile clopidogrel
• Kuzibua mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo kwa kutumia - Percutaneous coronary intervention (PCI)
• Upasuaji (CABG)

Njia za kuzuia shambulizi la moyo
• Kuacha kuvuta sigara
• Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
• Kupunguza unywaji wa pombe
• Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
• Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)
• Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.

Madhara ya shambulizi la moyo
• Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
• Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo (Atrial fibrillation) ambayo hatimaye hupelekea kifo
• Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
• Kifo cha ghafla (sudden death)