Tatizo la baadhi ya wanandoa kutokushika mimba limekuwa likiongezeka
mwaka hadi mwaka na wengine hukata tamaa mapema kwani huweka fikra za
kupata mimba kuanzia mwezi wa kwanza wa ndoa yao.
Mtu ambaye ana tatizo la kutoshika mimba kitaalamu tunasema
Infertility na kushindwa kupata mimba kwao huitwa Conceive. Kwa kawaida
kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, wanandoa asilimia 50 wanapata mimba
ikiwa watajamiiana bila kutumia kinga wakifanya tendo hilo ndani ya
miezi mitatu na asilimia 75 baada ya miezi sita na asilimia 95 baada ya
mwaka mmoja.
Sababu za tatizo la kutopata mimba ni nyingi sana na baadhi yake ni
hizi zifuatazo.
Matatizo ya mbegu za kiume (Sperm disorders). Asilimia
35 ya wanaume wana tatizo hili na lingine ni kutopevuka kwa mayai kwa
wanawake yaani kitaalamu huitwa Ovalatory dysfunction, asilimia 20.
Matatizo mengine ni yale yasiyo ya kawaida ya ute wa shingo ya uzazi
ambapo ni asilimia 5 tu, wengine huwa na matatizo ya homoni na wapo
ambao hawapati mimba na sababu zao hazijulikani ni asilimia 10, wengine
ni kutokana na kuwa na msongo wa mawazo na wasiwasi.
Tatizo lingine la kutoshika mimba husababishwa na hitilafu katika
mirija ya uzazi (tubal dysfunction), hawa huwa asilimia 30. Sababu zote
hizi nitaeleza moja moja kwa kirefu katika matoleo yetu yajayo lakini
wote wenye tatizo hili wanashauriwa kuhudhuria kliniki za akina mama ili
waonane na madaktari.
Lakini pia wanashauriwa kufuatilia siku zao za mzunguko wa hedhi na
tendo la ndoa mara kwa mara hasa baada ya siku 10 kutoka siku anamaliza
hedhi na aanzie siku ya kwanza ya kupata hedhi. Ushauri Wanawake
wanashauriwa wawe wanapima joto la mwili asubuhi na jioni kipindi cha
kushika mimba na kama litaongezeka kwa nyuzi joto 0.5 wanashauriwa
kipindi hicho kufanya tendo la ndoa.
Kwa nchi za Ulaya na Marekani wana kipimo cha kuonesha siku ambayo
yai litapevuka, hivyo mtu kuwa na uhakika na siku ya kupata mimba
akiamua.
Kipimo hicho kinaitwa Luteinizing hormone prediction test kits.
Wanawake wanaotaka kupata mimba wanashauriwa kuepuka ulevi na uvutaji wa
sigara wa kupindukia. Lakini hata wale wenye mimba wanashauriwa kuepuka
vitu hivyo.
Itaendelea siku nyingine.
0 comments:
Post a Comment