Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, June 16, 2015

SEHEMU YA KWANZA: MATUKIO YA TAMASHA LA FLORA MBASHA LILILODHAMINIWA NA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC ILIYOPO MBEZI BEACH

Jina la Flora Mbasha sio geni masikio mwa watu wengi duniani. Flora Mbasha amejulikana kutokana na uimbaji wake wa nyimbo za Injili nchini na nje ya Tanzania. Huduma yake hii imewagusa watu wengi sana na na kusabaisha watu kuweza kuokoka.

Rumafrica ilibahatika kuhudhuria tamasha la Flora Mbasha siku ya Jumapili 14/06/2015 katika ukumbi wa Ubungo Plaza na kuweza kujifunza mengi sana kutoka kwa mkongwe wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha.
Kwanza, kitu nilichojifunza ni KUJIAMINI, Flora Mbasha ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya tamasha katika jiji la Dar es Salaam, aliweza kuthubutu kufanya tamasha lake la LIVE akiwa na bendi yake ambayo ilitambulishwa siku hiyo kwa mara ya kwanza kabisa.

Pili, ni UWEZO wa kutawala jukwaa, Flora alionekana kulimudu jukwaa kama vile ameshawahi kufanya tamasha la LIVE,

Tatu, HISIA, Flora Mbasha aliweza kuimba nyimbo zake za kuabudu kwa hisia sana mpaka ikasababisha watu wote kukaa kimia huku wengine wakitoa machozi, ilifika kipindi hata mgeni Rasmi Mh. Freeman Mbowe kubaki akishangaa jinsi Flora Mbashaalivyokuwa  akiimba kwa hisia, Flora Mbasha aliweza kutoa machozi baada ya kumaliza kuimba wimbo wake wa kuabudu, na hii inaonyesha ni jinsi gani hata yeye  mwenyewe anavyoweza kuguswa na kile anachokiimba.

Nne, KUPENDWA, nasema hivi ni kutokana na jinsi nilivyoshudia watu kutoka Mwanza, Kigoma na Morogoro waliokuja kumuona Flora Mbasha akiimba baada ya kukaa kimia sana kwa muda mrefu. Mwimbaji mmoja anayeitwa Ency Mwalukasa alishudia kuwa yeye binafsi anampenda sana Flora Mbasha, na nyimbo zake huwa zinamgusa sana na kuinua imani yake na Mungu wake.

Sasa tuone matukio haya, na tutazidi kuwaletea matukio mengine, zidi kutembelea blogu yetu hii. Picha zimepigwa na Rumafrica +255 715 851 523
KIPINDI CHA RED CARPET
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Glory Mainah
 Dancers wa mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper
 MC na mwimbaji wa nyimbo za Injili Sarah Mvungi
  MC na mwimbaji wa nyimbo za Injili Sarah Mvungi
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper na MC Sarah Mvungi
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper na MC Saraha Mvungi
  Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper, mtoto wa MC Saraha Mvungi na MC Saraha Mvungi
 Neema Gasper na dancers wake
 Mdau wa Flora Mbasha

KIPINDI CHA WAIMBAJI WAALIKWA KUMTUKUZA MUNGU KWA UIMBAJI
 Furaha Isaya
  Furaha Isaya akifuatia MC Joyce Omben, Christina Mbilinyi
 Kustoho ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Christina Matai

 Glory Mainah




Meneja wa The Fadhaget Sanitarium Clinic, Lonely

 Waimbaji wa nyimbo za Injili Jesca Sanga (kulia) na Judy Sanga watoto  Mch. Burton Sanga
 Neema Gasper
  Neema Gasper
 MC Bony Magupa



 MC na mwimbaji wa nyimbo za Injili Saraha Mvungi

 Mkurugenzi wa Grace Products LTD (kushoto) ambaye ni mfadhili wa tamasha hili
 Mtoto wa MC Saraha Mvungi akiimba
 MC Joyce Ombeni
 Christina Matai
 Lilian Kimola (kushoto) na Furaha Isaya
 Christina Mbilinyi mwimabji wa nyimbo za Injili Tanzania
 Kutoka kulia ni Glory Mainah, Neema Gasper, Saraha Mvungi na mwanae Sarah Mvungi

 Kulia ni Elizabeth Ngaiza
 Mwimbaji wa Nyimbo Za Injili Elizabeth Ngaiza


 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Celline Theophil (kulia) akiwa na rafiki yake

 Mtangazaji wa Praise Power Redio, Mwimbaji wa nyimbo za Injili, MC na mtangazji wa Channel Ten Bony Magupa akiimba


 Ambwene Masongwe akiimba huku wadau wake wakimpongeza kwa fedha
 Dada alitesoma Risala akimtunza Ambwene Mwasongwe


 Elizabeth Ngaiza
  Elizabeth Ngaiza
  Elizabeth Ngaiza
Kutoka kulia ni Christina Mbilinyi, Christopher Mwahangilam (hajajulikana), Furaha Isanya, MC Joyce Ombeni, MC Bony Magupa
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Glory Mainah
 Christina Mbilinyi na Christopher Mwahangila
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper


 Enct Mwalukasa (kulia)
 Rafiki yake Flora Mbasha kutoka USA
 Kutoka kulia ni Glory Mainah, Elizabeth Ngaiza na Sarah Mvungi

 Dancers wa Mch, Maximillian Majeshi Majeshi

 Jesca Sanga (kushoto) na Judith Sanga

 Christopher Mwahangila
 Mama mzazi wa Flora Mbasha
  Christopher Mwahangila
 Mwimbaji wa nyimbo za Injili Neema Gasper akimpongeza Christopher Mwahangila
 Glory Mainah na Elizabeth Ngaiza (kulia)
MC Bony Magupa akimhoji Christopher Mwahangiala

ENDELEA KUTEMBELEA BLOGU HII KWA MATUKIO MENGINE YA FLORA MBASHA


ZIARA YA DR. FADHILI EMILY WA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC NCHINI SWEDEN


MATUKIO KATIKA PICHA





























Monday, June 15, 2015

Dr. Fadhili Emily Aweka Historia Katika Sayansi Ya Tiba Ulimwenguni



Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic aandika historia Katika tasnia ya Huduma Ya Tiba ulimwenguni, ni baada ya kuandika jina katika kitabu cha wageni katika hospitali kuu ya Kisasa Ulimwenguni KAROLINSKA  iliyopo Bara la Ulaya katika nchi ya Sweden.

Ni pale alipokuwa Mheshimiwa Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mlisho Kikwete wiki iliyopita. Mpaka sasa Dr. Fadhili yuko huko nchini Sweden kwa Ziara yake Binafsi ya Huduma ya Tiba Ulimwenguni.

Yote ni kwa udhamini wa
Fadhaget Sanitarium Clinic , TV51 , OpenAfrica Magazine.

Friday, June 12, 2015

THE FADHAGET SANINTARIUM CLINIC KUDHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA


WAZIRI BERNARD MEMBE ANUSURIKA AJALI YA NDEGE, ZANZIBAR‏



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amenusurika kifo baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutoka Iringa kwenda Zanzibar kutaka kugongana uso kwa uso na ndege nyingine dakika moja kabla ya kutua.

Waziri Membe akiwa na ujumbe wake wa watu wanane, walikuwa wakisafiria ndege ya kukodi kampuni ya 5H NEG Precition Aviation ikirushwa na rubani Mathew Mhahiki, ambaye ameonyesha kushangazwa na tukio hilo alilodai “ni kwa rehema za Mungu tumepona ajali hii.”
Akizungumza na mwandishi wetu aliyeko katika ziara yake, rubani Mhahiki alisema: “Lazima kuna tatizo katika control center hata hivyo tayari nimeongea nao na wameniomba samahani na kudai walipitiwa, maana kwa hali ilivyokuwa ni kwamba tungegongana wakati wa kutua maana nimeshangaa tu kuona ndege hii hapa ndiyo maana nikaamua kumkwepa mwenzangu nikapanda juu.”

Waziri Membe alisema: “Nina uzoefu mkubwa wa kusafiri na ndege mahali pengi duniani, hali hii ilikuwa ni ajali na labda sasa tungekuwa dead bodies, lakini ninajua Mungu yuko upande wetu katika safari hii ya uhakika, lakini pia izingatiwe nimekuja kufanya kazi ya Mungu.”

“Katika safari hii tutashuhudia mambo mengi sana, lakini kwa kuwa kila ninapotaka kuondoka nyumbani ama hotelini mara nyingi nimekuwa nikimtanguliza Mungu maana bila Mungu hii ilikuwa ni mwisho wa maisha yetu tuliokuwa kwenye ndege hii.”

Waziri Membe alikuwa amealikwa mjini hapa na Umoja wa Akimama wa Kikristu (Umaki) wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar waliokuwa wakifanya mkutano wao mkuu unaofanyika kila baada ya miaka mitano akitokea Iringa ambako alikwenda kutafuta udhamini wa chama ili kumwezesha kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM.

Akiwa uwanjani hapo, Waziri Membe alikutana na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba aliyekuja hapa Zanzibar kutafuta wadhamini ambapo makada hao walipata nafasi ya kuzungumza.
Akiwa katika mkutano huo, Waziri Membe alisema: "Miongoni mwa mambo yanayonikera ndani nafsi yangu ni kuona mwanamke bado anaachwa nyuma, hili halipendezi, ni lazima tuhakikishe wanawake wanapata elimu ya ufundi stadi maana mwanamke akiwezeshwa hasa katika eneo hili la elimu wanaweza hata kushinda wanaume wengi.”

“Ni lazima kina mama wawezeshwe kujiajiri ili msiwategemee kina baba kwa kila jambo lakini pia ili kufikia malengo hayo ni lazima tuwape elimu kina mama.”
NA KAJUNA BLOG

TSHIRT ZA FLORA MBASHA ZITAPATIKANA UBUNGO PLAZA


VIDEO: MREMBO: DUDE AMENIZALISHA, AKANITELEKEZA



Mrembo aliyejitambulisha kwa jina la Ester
Eliakim, mkazi wa Kinyerezi, Dar ameibuka na kueleza kwamba alizaa na
staa wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ambaye baadaye alimtelekeza
yeye na mwanaye Cleopatra (mwenye miezi 11).

RED CARPET LITAKUWEPO KWENYE TAMASHA LA FLORA MBASHA-UBUNGO PLAZA