Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Saturday, June 6, 2015

MAZISHI YA KAMISHNA MKUU MSTAAFU WA JESHI LA MAGEREZA YAFANYIKA MOSHI


Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele. Mazishi hayo yamefanyika jana Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old Moshi Mkoani Kilimanjaro.


Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.


Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Dayosisi ya Kasikazini akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.


Kabuli la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa limepambwa na mashada ya maua baada ya mazishi.

Friday, June 5, 2015

TUMBO LA LULU LAYEYUKA GHAFLA

Brighton Masalu
Miezi miwili iliyopita kuliibuka madai mazito kwamba staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameongezeka tumbo hivyo mashabiki wake wakapiga vigelegele kwamba huenda ana mimba lakini sasa tumbo hilo limeyeyuka na yupo ‘flati skriini’.


Staa bei mbaya wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika, Lulu kwa sasa anakatiza viunga vya chuo anachosoma cha Magogoni jijini Dar akichukua masomo ya Uhusiano wa Umma, akiwa hana lile tumbo la Aprili.Gazeti hili lilizungumza na baadhi ya wanafunzi wenzake ambao walidai msanii huyo alikuwa hafiki chuoni hapo kwa muda mrefu lakini sasa amejaa tele ‘mwepesii’.

“Hakuwa akija chuoni kwa muda, baadaye akawa anahudhuria kwa ‘kupibu’ kisha kuacha tena ila ameanza juzi tu kutokana na kuwepo kwa mitihani,” alisema mmoja wa wanachuo hao.Kama taaluma inavyoelekeza, mwandishi wetu alimtafuta Lulu kupitia simu yake ya mkononi huku ikiita bila majibu.

Baadaye alitumiwa ujumbe wa kwanza uliosomeka: “Tafadhali naomba upokee simu, nahitaji kuzungumza na wewe jambo muhimu.” Hata hivyo, hakujibu.Baada ya kuona kimya, mwandishi wetu alimtumia ujumbe ulioonesha madai hayo: “Kuna tetesi kuwa ulinasa mimba na kuficha na sasa inadaiwa kutoka na kwamba hata chuoni haukuwa ukihudhuria, hili likoje?”
Baada ya kimya cha saa kadhaa, Lulu alijibu:

“Hao wanaodai nina mimba walinipa wao? Sina nafasi ya kufafanua.”
Hivi karibuni Lulu aliripotiwa na mitandao ya kijamii kuwa huenda ana mimba.

MWANAMITINDO JOKATE (KIDOTI) ADHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA


UKATILI WA MAMA

Dustan Shekidele, Morogoro
UCHUNGU wa mwana si aujuae mzazi? Sasa mama mzazi huyu vipi?! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke Pendo Mabuko amejikuta akipokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira waliokerwa na kitendo chake cha kumtupa barabarani mwanaye wa kumzaa baada ya kunyimwa matumizi ya mtoto huyo na mwanaume aliyezaa naye, Daniel ambaye ni mume wa mtu.
Mtoto anayedaiwa kutupwa na mama yake, Pendo Mabuko.

Tukio hilo lililojaza umati lilitokea Ijumaa iliyopita, saa 10 jioni katika Mtaa wa Simu ‘A’ Kata ya Mji Mpya mkoani hapa.
Wakihojiwa na gazeti hili, mashuhuda wa tukio hilo, Asha Hussein, Mussa Juma na Paskal Msimbe kwa nyakati tofauti, walisema:

”Tukiwa hapa barabarani tulimshuhudia huyu mwanamke na mwanaume mmoja wakizozana kwa muda mrefu, tulipowasogelea ili kuwasuluhisha, mwanaume alipanda bodaboda na kutimka.
“Ndipo huyu mwanamke akamtupa mtoto kisha naye akaanza kuondoka huku akisema amechoka kumlea mtoto wa mtu, sisi tukamzuia.
Mwanamke huyo akilia baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananchi waliokelwa ha kitendo hicho.

“Tulimlazimisha kumchukua mwanaye lakini aligoma, tukaamua tukuite wewe mwandishi kwa msaada zaidi.”
Wakati mwandishi wetu anawasili eneo la tukio, aliwashuhudia baadhi ya wananchi wenye hasira wakimshushia kichapo mwanamke huyo kwa kitendo cha kumtupa mwanaye.

Mwandishi aliita polisi wa pikipiki ambapo Afande Mwajabu alifika fasta na kumchukua mwanamke huyo na mwanaye na kuwapeleka kituoni kwa mahojiano zaidi.

Awali, akihojiwa na mwandishi wetu kuhusu uamuzi wa kumtupa mtoto wake barabarani, mwanamke huyo alisema:
”Muda huu tunatoka Ustawi wa Jamii kusuluhishwa. Mimi nilipeleka malalamiko, mzazi mwenzangu kagoma kumtunza mwanaye na kuniachia mzigo peke yangu.


Mama huyo akiwa mikononi mwa polisi.

“Nikimuuliza anasema mkewe kamzuia kumtunza mwanangu ndiyo maana na mimi kwa hasira nikaamua kumtupia mwanaye akamlee na mkewe.”

MKURUGENZI WA RUMAFRICA KUSHIRIKI TAMASHA LA FLORA MBASHA


TASWIRA NYUMBANI KWA ALIYEKUWA MBUNGE WA UKONGA DAR


Waziri wa Maendele Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba (katikati) akizungumza na waombolezaji waliofika nyumbani wa Marehemu,Eugen Mwaiposa leo Mchana.


Mume wa Marehemu, ,Ally Mwaiposa (aliyekaa) akifarijiwa na waombolezaji waliofika nyumbani kwake.


Nyumbani kwa Marehemu Eugen Mwaiposa.

HII ndiyo tawsila ya Nyumbani kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar baadhi ya watu pamoja na wabunge wakiendelea kujitokeza kwa ajili ya kuifariji familia ya Mume wa marehemu,Ally Mwaiposa.

Akizungumza na wanahabari mmoja wa wanandugu wa familia hiyo, Fitina Mkandala alisema kuwa mwili wa Marehemu unatarajiwa kuzikwa Juni 6 mwaka huu, lakini akasema kuwa ,ratiba kamili ya mda wa mazishi itatolewa kufuatana na utaratibu wa sheria za Bunge, huku akisema kuwa watoto wa marehemu nao wanatarajia kufika kesho wakitokea masomoni, nchini Canada na mwingine akitokea Uingereza.

Mwili wa Marehemu Eugen unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Kipunguni ‘A’Matembele-Ukonga jijini Dar es Salaam.

SUPER WOMAN JOYCE KIRIA ADHAMINI TAMASHA LA FLORA MBASHA


NEEMA CHANDE AIBUKA NA KITUMBO

Imelda Mtema
Baada ya kupotea kwa muda mrefu, msanii wa filamu ambaye pia ni Miss Ruvuma 2007, Neema Chande ameibuka akiwa na mimba kubwa huku kukiwa na usiri juu ya mhusika wa tumbo hilo.


Msanii wa filamu ambaye pia ni Miss Ruvuma 2007, Neema Chande.

Neema hivi karibuni alikimbilia nchini India kusaka maisha na alipozungumza na mwandishi wetu juzi kwa njia ya simu alisema, watu wajue tu kwamba ana mimba aliyopewa na Muafrika mwenzake na anatarajia kujifungua ‘soon’.

“Nimefurahi sana kwani siku zote nilikuwa nikitamani maisha haya ya kulea tumbo na ‘soon’ nitarudi Tanzania kwa ajili ya kumuweka wazi baba kijacho kwani tuna mipango mizuri ya maisha,” alisema Neema.

Tuesday, June 2, 2015

BABA WA KAMBO WA KIM KADARSHIAN ABADILISHA JINSIA YAKE


Moja ya familia zisizoishiwa vituko na kila mara kuingia kwenye headlines ni pamoja na familia ya Kriss Jenner ambaye ni mama mzazi wa staa maarufu duniani Kim Kardashian.

Baada ya kusambaa kwa muda mrefu habari kuhusu kujibadilisha jinsia kwa baba wa kambo wa Kim Kardashian, aitwaye Bruce Jenner, sasa ni rasmi kuwa baba huyo amejibadilisha jinsia yake na sasa anajulikana kama Caitlyn Jenner.


Uamuzi huo umevuta hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia umeonekana kupokelewa tofauti na familia ya akina Kardashian.. mkewe wa zamani ambaye ni Kriss Jenner na familia yake wameonekana kutopendezwa na uamuzi huo japo yeye mwenyewe hana tatizo kabisa na ishu hiyo kama ambavyo wengine wanamchukulia.


Katika Ukurasa wake mpya wa Twitter alioufungua muda mfupi baada ya kujitangaza na kupata followers wengi, Bruce Jenner ameonesha kufurahishwa na hatua aliyofikia hivi sasa.

WAATHILIKA HAWA WA MADAWA YA KULEVYA MCHUNGAJI ATAJWA


Na Makongoro Oging’
Baadhi ya waathirika wa madawa ya kulevya Wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam ambao kwa sasa wameachana na matumizi ya madawa hayo walimtaja mchungaji wa kanisa moja (jina linahifadhiwa) ambaye alikamatwa na serikali na kwa sasa kesi yake inanguruma Mahakama Kuu jijini hapa.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Said Ismail Ngindo.
Waathirika hao ambao wako katika kikundi chao kijulikanacho kwa jina la Wanamati, walimueleza mwandishi wetu wiki iliyopita kuwa mchungaji huyo lazima abebe lawama zao kwa kuwa alikuwa akiwasambazia madawa hayo yaliyowafanya waathirike.
Waathirika ambao wapo zaidi ya 500 waliyasema hayo mara baada ya kumaliza kikao chao ambacho kilikuwa kikijadili jinsi ya kujikwamua baada ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.Waathirika hao ambao hawakupenda majina yao yatajwe gazetini kwa sababu za kiusalama, walisema mchungaji huyo alikuwa akiwauzia madawa hayo mitaani kwa kuwatumia mawakala wake ndipo polisi waliamua kumfuatilia na kumkamata na kwa sasa ana kesi Mahakama Kuu.

Mmoja wa waathilika wa dawa hizo.
Hata hivyo, waathirika hao wameiomba serikali na taasisi mbalimbali kuwasaidia kimaendeleo kupitia kikundi chao hicho kwa kuwa wameachana na utumiaji wa ‘unga’ na wangependa wajitegemee kwa kufanya shughuli za kuzalishaji mali.
Waathirika hao ambao wengi wao wamesema kwa nyakati tofauti kuwa wamekuwa wakitumia unga kati ya miaka mitano hadi ishirini na kwamba jamii isiwachukie kwa maana na wao walirubuniwa bila kujua madhara ambayo wangeweza kuyapata lakini kwa sasa wako vizuri kwani wamekuwa wakihudhuria kliniki katika Hospitali ya Temeke, Dar.
Wameiomba serikali iendelee kuwapatia dawa za kutibu utumiaji wa madawa kwa kipindi chote cha miaka miwili wanayotakiwa kutumia ili waweze kurejea katika hali yao ya zamani.Mwenyekiti wa kikundi hicho, Said Ismail Ngindo alisema kwamba wameamua kuungana kwa pamoja ili waweze kufanya shughuli za maendeleo baada ya kuachana na madawa na wameiomba serikali iwasaide ili wajikwamue kiuchumi.

Wakiwa kwenye kikundi chao.
“Asilimia kubwa ya wanachama wa kikundi hiki hawana ajira…ni kazi ngumu sana kukaa bila kuwa na kipato, hapa kuna akina mama ambao wamezalishwa kipindi hicho wakiwa watumiaji wa madawa mitaani, sasa wanapata shida kubwa ya kuwalea watoto wao, hivyo kunahitajika msaada mkubwa, “ alisema mwenyekiti huyo.
Taarifa iliyopatikana ndani ya kikundi hicho inasema kwamba imefikia hatua ya viongozi wa kikundi  walioteuliwa na uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Temeke kuwasimamia  wenzao lakini wao wamewachagua viongozi wao ili wawe wakiheshimika zaidi na wana kikundi.