Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Tuesday, July 5, 2016

Quote of The Day, by Dr. Fadhili Emily



"The food you eat can be either the safest and most powerful form of medicine or the slowest form of poison"

-By Dr Fadhili Emily

Saturday, June 18, 2016

Daktari atoboa siri 8 za mimba za wema kuyeyuka - Amani Magazine

Amani News Paper (Source: June 16-22 2016)
Page 2
 





Tuesday, May 24, 2016

Afya Yako - Dr Fadhili Emily


Friday, May 20, 2016

Sikiliza Jinsi ya Kusuluhisha matatizo ya Mimba kutoka



Je Unahitaji watoto mapacha?


Friday, March 25, 2016

Huduma Ya The Fadhaget Sanitarium Clinic Imezidi Kukua kwa Kasi sana. Zifahamu Sababu zake.


The Fadhaget Sanitarium Clinic imezidi kuongeza matawi yake kote nchini. Hii ni kutokana na ubora ambao imekuwa ikitoa kwa wateja wake. Tunajitahidi sana kuhakikisha kuwa tunawasaidia watu mbalimbali wanaofika kwetu na tumehakikisha huduma yetu ikiwafurahisha. Tunazidi kuongeza ubora wetu na tunazidi kuhakikisha kuwa watu wengi wanapona na kufurahia Afya zao tena. Waliokata tamaa katika magonjwa ya uzazi, jinsia, magonjwa sugu na ambayo imeshindikana kutibu, tumejitahidi kuwasaidia wengi.

Tunapenda kuzidi kuwakaribisha na msisite kufika ofisini kwetu na tutakusaidia. Kama hufahamu tunapatikana wapi, tembelea Blog yetu, kwenye Menu (Juu) utaona tunapatikana wapi, fungua link na utaona mpaka Picha za majengo yetu na maelekezo yake. Pia tumeweka na namba za simu kwa watakaotaka kuonana au kuwasiliana nasi watutafute nasi bila shaka tutawaelekeza vyema.

Asanteni sana na endeleeni kujali Afya zenu kwa Mimea na Matunda mbalimbali. Chakula ni Dawa nzuri.

 

Wednesday, January 20, 2016

Je unafahamu Undani Kuhusu Endometriosis?


Je unafahamu Undani Kuhusu Endometriosis? Dr Fadhili Emily ameelezea vyema matatizo hayo na jinsi ya kudhibiti. Tazama video za mafunzo ya kiafya kupitia Channel Hii ya Dr. Fadhili Emily na pia Fuatilia habari zaidi katika account yake ya instagram ya @fadhaget.


Friday, January 1, 2016

Tunapenda kuwatakia Heri ya Mwaka Mpya

Kitengo Cha Sayansi ya Tiba Asilia, The Fadhaget Sanitarium Clinic kinapenda kuwatakia Heri na Baraka za Mwaka Mpya. Tutazidi kuboresha huduma zetu pote nchini kwa kusaidia wenye matatizo mbalimbali ya kiafya kwa kutumia Tiba Asilia Kutibu. 

Tuesday, December 29, 2015

Usikose Kutazama Kipindi cha TUNDA LA LEO.


Monday, December 21, 2015

Usikose kipindi cha Sayansi ya Jamii - Star Tv


Kipindi kitakuwa ni kila siku, katika muda wa Saa 3 na Nusu Usiku, STAR TV.

Sunday, December 6, 2015

Dr. Fadhili Emily Kwenye Mkutano na Resolution Insurance.

Dr. Fadhili Emily akiiwakilisha The Fadhaget Sanitarium Clinic wiki hii alishiriki katika moja ya mkutano ulioweza kutoa elimu kuhusiana na Insurance za Afya. Katika wiki hii aliweza kuonea na kutoa elimu kuhusiana na Madhara ya Matumizi ya simu za mikononi na adhari zake pamoja na njia sahihi za kutumia simu za mikononi kiuslama.


Friday, November 13, 2015

Maumivu ya Tumbo ya Mata kwa Mara kwa Wanawake.



Wanawake wanaosumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu mara kwa mara hupata athari nyingi baadaye endapo kama hawatagundua chanzo cha maumivu hayo.

Katika tumbo la mwanamke kuna mfumo wa kawaida wa tumbo ambao ni tumbo la chakula na mfuko wa haja kubwa, kuna kibofu cha mkojo na mfumo wa mkojo.
Pia kuna mfumo wa uzazi ambao ndiyo tunaozungumzia leo kwa undani.

Mfumo wa chakula una matatizo yake mengi ambayo huambatana na kichefuchefu na kufunga choo, mfumo wa mkojo nao una shida nyingi tu ambazo ni maambukizi au ‘UTI’ au Yutiai ambayo huambatana pia na maumivu katika njia ya mkojo.
Matatizo ya mfumo wa uzazi huambatana na dalili mbili, mojawapo ni ile ya kutokwa na uchafu ukeni.


Chanzo cha tatizo
Maumivu ya mara kwa mara ya tumbo kwa wanawake yanahusiana zaidi na mfumo wa uzazi. Maumivu haya yanaweza kuwa maambukizi katika mfumo wa uzazi ambayo huathiri kuta za ndani za uzazi, maambukizi yanasambaa hadi katika mirija ya uzazi hali iitwayo ‘Salpingitis’ na huweza kusababisha mirija kujaa maji ‘Hydrosalpinx ’ au kujaa usaha ‘Pyosalpinx’.

Maambukizi pia husambaa hadi katika vifuko vya mayai ‘Oophoritis’.
Maambukizi pia huwa ukeni na kitaalamu huitwa ‘Vaginitis’ na hushambulia kuta za uke, yakifika katika mlango wa shingo ya kizazi huitwa ‘Cervicitis’.

Pamoja na kushambulia ndani ya uke na shingo ya kizazi, pia hushambulia nje kabisa ya uke ambapo mwanamke hulalamika muwasho nje ya uke kwenye midomo au mashavu ya uke na hata kutokwa vipele.

Dalili za tatizo
Mwanamke mwenye tatizo ukeni hulalamika muwasho ukeni na kutokwa na uchafu ambao mara nyingi huwa na harufu kama shombo la samaki. Pia hulalamika maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Mwanamke ambaye maambukizi yamefika katika mlango wa shingo ya kizazi hupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine hutokwa na damu wakati wa kujisafisha huona damu kidogo au kama hakuna damu atahisi mdomo wa kizazi umevimba na kushika kitu kama kigololi ndani ya uke.

Mwanamke pia hulalamika kama kuna kitu kinasukumwa wakati wa tendo la ndoa.
Maumivu ndani ya kizazi hasa katika kuta za ndani hupatwa na maumivu baada ya tendo la ndoa, vilevile hupatwa na maumivu chini ya tumbo muda wote yaani kila siku na kumnyima raha. Maumivu wakati wa hedhi na kutokwa na damu nzito nyeusi na wakati mwingine hutoa harufu.

Maumivu yakiwa katika mirija ya uzazi husambaa chini ya tumbo kulia na kushoto, maumivu pia huwa ya muda mrefu na hali hii humfanya mgonjwa apate haja kubwa kwa shida.
Maambukizi katika vifuko vya mayai husababisha siku za hedhi zivurugike na ziwe hazina mpangilio maalum, huathiri upevushaji na uzalishaji wa mayai hivyo kushindwa kupata ujauzito.

Maambukizi nje ya kizazi humfanya mwanamke aumwe tumbo lote na kupata hali iitwayo ‘Perionitis’, hupata homa za mara kwa mara na mwili kuwa mnyonge.
Maumivu ya muda mrefu hudhoofisha afya ya mwanamke, hukosa hamu ya kula na kupoteza raha ya tendo la ndoa na uzazi husumbua.

Maambukizi hushambulia kwa njia ya kupitia ukeni, mfano magonjwa ya ngono, kuharibika au kutoa mimba na hata kwa kufanyiwa upasuaji wa tumbo pia huathiri mfumo wa uzazi.
Vyanzo vingine vinavyoathiri mfumo wa uzazi na kusababisha maumivu ya chini ya tumbo mara kwa mara ni matatizo katika mfumo wa homoni au vichocheo, uvimbe katika kizazi, mirija na vifuko vya mayai.

Athari za tatizo
Maambukizi sugu katika mfumo wa uzazi huathiri mzunguko wa hedhi, uzalishaji mayai ya uzazi, kuziba mirija ya uzazi, kupoteza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa.

Kwa ujumla mwanamke mwenye tatizo hili anaweza kupoteza uwezo wa kuzaa na kuwa mgumba.
Matatizo haya hutokea zaidi kwa mwanamke aliye katika umri wa kuzaa.

Uchunguzi
Matatizo haya hufanyiwa uchunguzi katika kliniki za magonjwa ya kinamama. Vipimo mbalimbali vitafanyika kadiri daktari atakavyoona inafaa.
Matibabu Tiba inaweza kuwa dawa, upasuaji au yoyote ambayo daktari ataona inafaa kutegemea aina na ukubwa wa tatizo.

Friday, October 23, 2015

Dr. Fadhili Emily. (Photos)








Sunday, September 27, 2015

Dr Fadhily Emily On Interview at Times FM.

View Dr Fadhily Emily's Photos on the interview at Times FM Radio, Dar es Salaam Tanzania.





Monday, September 7, 2015

MTI WA MLONGE NA MATATIZO YA MFUMO WA UZAZI KWA WANAWAKE-2




Tuliwahi kuzungumzia kuhusu wanawake wanaokumbwa na tatizo hili la kuvimba kwa mirija ya uzazi na tukawasihi kwamba wanaweza kutumia mti wa mlonge ili kutatua tatizo hili la kuvimba kwa mirija ya uzazi, lakini kwa ufupi tu wangepata kujua ni jinsi gani wanaweza kukumbwa na tatizo kama hili:

VYANZO
Vyanzo vya tatizo la kuvimba kwa mirija ya uzazi ya mwanamke ni kama vile:
Kukumbwa na bakteria mbalimbali sehemu za siri, lakini hili kwa upande mmoja linaweza kuwakuta watu ambao si waaminifu sana kwenye uhusiano wao au kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja.

Pia kuna magonjwa ya zinaa ambayo mara nyingi yanapokaa kwenye mwili kwa muda mrefu pasipo kupata matibabu, pia husababisha tatizo hili la kuvimba kwa mirija ya uzazi.Pia kupata fangasi kwenye shingo ya kizazi cha mwanamke na ikakaa kwa muda bila kupata matibabu basi nayo inaweza kuchangia mtu kupatwa na tatizo hili.

Hivyo basi kama unapatwa na dalili kama hizo za maumivu chini ya kitovu, uchovu wa mwili kupita kiasi, kutopata hamu ya kushiriki tendo la ndoa, maumivu ya kiuno kupita kiasi, hali ya kutokwa na uchafu katika sehemu za siri za mwanamke, endelea kuwa nasi na tutakuelezea nini mlonge unaweza kukufanyia kuondoa tatizo hili japokuwa mimea tiba ipo mingi inayosaidia kuondoa tatizo hili.

Tatizo lingine linaloweza kuondolewa na mmea huu wa mlonge kwa mwanamke ni pamoja na;
ii. Kuna tatizo hili la Pelvic Inflammatory Diseases (PID), hii mara nyingi ni ile hali ya kuvimba kwa kuta za mji wa mimba wa mwanamke lakini pia huambatana na kuvimba kwa mirija ya uzazi ya mwanamke, kama tulivyozungumza katika makala iliyopita kwamba mlonge husaidia sana magonjwa yanayofahamika kama Inflammatory na ile hali ya kuvimbavimba kwenye mwili wa mwanamke sasa tatizo hili la PID ndilo tatizo linalogusia mambo hayo yote.

DALILI ZA PELVIC INFRAMATORY DISEASES (PID)
Mtu ambaye amepima na akakutwa na tatizo hili atakuwa na dalili zifuatazo;
Atakuwa na ile hali ya kupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi, na hii huweza kumpata mwanamke hata kama anakuwa ameshajifungua na maumivu makali wakati wa hedhi tunaita Dysmenorrheal.

Kama tunavyojua ipo Primary Dysmenorrheal ambayo ni maumivu makali sana wakati wa hedhi kwa mwanamke ambaye bado hajapata mtoto, lakini Secondary Dysmenorrheal ni ile hali ya kupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi kwa mwanamke ambaye tayari ameshapata mtoto au watoto.

Tutaendelea wiki ijayo kwa kuwaelezea zaidi dalili za tatizo kama hili la PID na jinsi gani mmea huu wa mlonge unavyoweza kukusaidia kuondoa tatizo hili kwa wanawake.

Kwa ushauri, vipimo na tiba, dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.Nawatakia afya iliyo njema!

Sunday, September 6, 2015

Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuwa Mjamzito

Ujauzito ni safari ndefu inayomchukua mwanamke miezi tisa au majuma arobaini hadi kujifungua. Ni safari yenye mikikimikiki na hatari nyingi kwa mama na mtoto. Tusichukulie suala la ujauzito kama jambo la kawaida ingawa pia ni wajibu kwa mwanamke.

Ujauzito siyo hali ya hatari au kutisha endapo mambo ya msingi yatazingatiwa kabla ya kuwa mjamzito na kipindi cha ujauzito hadi baada kujifungua. Katika kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi ambayo ni mabadiliko humtokea mama na mtoto aliye tumboni.
Katika makala haya tutazungumzia mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kubeba mimba, siyo kila mwanamke anaweza kubeba mimba kwa sababu wengine huwa na matatizo katika mfumo wao wa uzazi, aidha homoni zao hazifanyi kazi vizuri na mayai hayazalishwi au hayapevuki. Huenda pia mirija ya uzazi imeziba au ana matatizo ndani ya kizazi.

NINI CHA KUFANYA?
Ni vyema upange sasa unataka kuwa mjamzito au mwezi fulani unataka kushika mimba, uwe na mpango. Hata hivyo, hakikisha umri wako upo zaidi ya miaka 20 kwa usalama zaidi wa afya yako. Mshirikishe mwenzi wako na mwambie ungependa upate ujauzito, siyo vizuri kushtukiza kwani inaweza kukupa ‘stress’ wewe mwenyewe au mwenzako endapo mmoja wenu hajajiandaa kisaikolojia.

CHEKI AFYA YAKO
Hakikisha una afya njema, huna magonjwa sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa mengine ya moyo, kansa, HIV, kifafa, pumu, siko seli au grupu lako la damu ni RH negative.Endapo una matatizo haya hapo juu, basi haraka wasiliana na daktari wako wa masuala ya uzazi akupe ushauri kwani magonjwa mengine yatakusumbua wakati wa ujauzito, au magonjwa yenyewe yatamwathiri mtoto. Hakikisha huna magonjwa au matatizo katika viungo vya uzazi, mfano kutokwa na uchafu ukeni wenye muwasho na harufu mbaya, vipele au vidonda sehemu za siri, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na damu au usaha ukeni. Vile vile mfumo wako wa uzazi uwe vizuri, matatizo katika mfumo wa uzazi ni kama vile maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi, kutopevusha mayai na kukosa hamu ya tendo la ndoa.

VILEVI ACHA
Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara, hili hata kwa mwanaume anayetaka mtoto. Mwanamke kabla ya kuwa mjamzito hakikisha unakula sana mboga za majani ili upate kiwango kizuri cha vitamin ya Folic Acid, ni vema ule sana mboga za majani au upate virutubisho vya Folic Acid. Endapo hutakuwa na kiwango kizuri cha Folic Acid, kuna hatari ya kuzaa watoto wenye matatizo.

MAZOEZI
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.

YANAYOKWAMISHA UJAUZITO
Matatizo yanayoweza kukusababishia usipate mimba ni kutofahamu siku za kupata mimba, kuziba mirija ya uzazi.Pia uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi na kwenye vifuko vya mayai. Uvimbe wa aina hii unaweza kutibika kwa dawa na ukaisha au kwa njia ya upasuaji, inategemea na daktari wako atakavyoona na kuamua. Kwa upande wa wanaume wanaojiandaa kuwa wazazi, ni vema umjulishe mpenzi wako sasa unataka mtoto au lini unataka mtoto. Tibu magonjwa yanayoathiri mfumo wa uzazi, mfano maumivu ya korodani, maumivu ya njia ya mkojo, upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume. Kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada ya tendo la ndoa manii zote zinatoka ukeni.
Ni vema ukapime mbegu zako za kiume kuona kama zina ubora wa kutosha, usiwe na maumivu yoyote ya mwili kwani yataweza kukusababishia kupunguza nguvu za kiume na kushindwa kufanya tendo la ndoa.

Friday, September 4, 2015

Faida za Tikiti Maji Kiafya.

Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza ya mlaji husika. Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu. Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti maji:


Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini.
 Katika tunda hilo kuna 
 
  • Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini; 
  • Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi;  na 
  • Vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa nishati.


    Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha  lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani. Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.

Halikadhalika tunda hili huweza kukuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu. Tikiti pia lina  Amino Acid na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko wa damu kwenye mishipa yake.

Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.

Kwa kawaida tunda hili huliwa  pejke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.

Wednesday, September 2, 2015

Fahamu Vyakula Vya Kuondoa Gesi Tumboni au Kusaidia Tumbo Kujaa.

Watu wengi wamekuwa wakihangaika sana na matumbo yao kujaa gesi na pengine kuvimba. Leo hii The Fadhaget Sanitarium Clinic imekuletea baadhi ya vyakula vya kula kuondo hili tatizo linakusumbua kwa muda mrefu. Pia kuna dawa maalumu zinapatikana katoika kituo chetu cha tiba kwa njia ya mimea na matunda. Sasa soma hivi vyakula kwa faida yako. 



KWA njia moja au nyingine, unajikuta tumbo limechafuka kwa kujaa gesi, kuuma na hata kuunguruma, unahisi unahitaji kunywa dawa ili litulie. Katika makala ya leo utajifunza njia bora ya kutuliza mchafuko wa tumbo kwa kutumia vyakula badala ya dawa za kisasa ambazo hutuliza dalili na haziondoi tatizo.

CHANZO

Kabla ya kukimbilia kwenye tiba, ni vizuri kwanza kujua chanzo cha tatizo na katika hili unahitaji kujua ni vyakula gani ukila vinasababisha matatizo ya tumbo. Aina ya vyakula inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kuna aina ya vyakula vinajulikana zaidi kusababisha matatizo ya tumbo.
Vyakula na vinywaji vinavyochangia tumbo kujaa na ukosefu wa choo kwa muda mrefu huwa ni soda, ulevi (hasa bia), vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye chumvi nyingi.

Vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakula na uondoaji wa uchafu kwenye utumbo, hivyo huwa kikwazo katika mfumo mzima wa usagaji chakula kwa urahisi.
Ili kujiepusha na matizo ya tumbo ya muda mrefu na hata kuzuia uwezekano wa kuumwa na tumbo mara kwa mara, unashauriwa kula vifuatavyo, karibu kila siku ili kulifanya tumbo lako kuwa safi wakati wote:

PAPAI (PAPAYA)

Baadhi ya utafiti uliyopo, unaonesha kwamba ‘enzyme’ waliyomo kwenye papai husaidia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kulifanya tunda hili kuitwa na mtafiti wa zama za kale Christopher Columbus kama ‘tunda la malaika’.

Watafiti wamebaini kuwa tunda hili, lenye ladha tamu na harufu nzuri, huboresha mfumo wa usagaji chakula, husafisha utumbo, huzuia magonjwa ya uvimbe tumboni na huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.


“Vitamini na virutubisho vya papai vina faida nyingi, lakini faida kubwa ya papai ipo kwenye kirutubisho (Enzyme) aina ya ‘Papain’ ambacho hujulikana kwa uwezo mkubwa ilionao wa usagaji mzuri wa chakula tumboni,” anasema Dk. Cari Case mwandishi wa blog ya masuala ya afya.

Mwandishi huyo anaongeza kwa kusema kuwa papai limekuwa likitumika kama tiba tangu karne ya 18, lakini utafiti wa kisayansi haukugundua faida za papai hadi mwaka 1870 wanasayansi walipogundua kirutubisho cha ‘papain kilichomo kwenye papai na tangu wakati huo tafiti nyingi zimekuwa zikifanywa kuhusu faida za tunda hili na uwezo wa tiba iliyonalo.

MTINDI (YOGURT)

Hata kama wewe si mpenzi wa mtindi, jaribu kunywa na utaupenda, hasa uwezo wake wa kuondoa matatizo ya kujaa gesi tumboni pamoja na matatizo mengine. Mtindi mzuri ni ule ‘plain’ ambao haujachanganywa na ladha au vitu vingine kwa lengo la kuongeza ladha. Bakteria asilia waliyomo kwenye maziwa mtindi ndiyo hufanya usagaji wa chakula kuwa mwepesi.

Mwisho, ili kupata faida ya papai na mtindi kama ilivyoelezwa hapo juu, ni vizuri ukala mara kwa mara kama siyo kila siku, kabla au mara baada ya kula vyakula ambavyo vinaweza kukuletea shida tumboni, au ukaweka mazoea ya kula kila siku ili kuliweka tumbo lako katika hali salama.