Baadhi ya vyakula vimekuwa vikifurahisha pale vinapoliwa, tikiti
maji ni miongoni mwa vyakula hivyo. Kwanza ule mchanganyiko wa rangi
zake hulifanya sio tu kuvutia bali kuwa kama ua lililochanua juu ya meza
ya mlaji husika. Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu. Licha ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado
zile 8% zilizobaki zina faida kubwa sana kiafya jambo linaloonekana
kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo ni baadhi tu ya faida chache kati ya
nyingi za tunda hili la tikiti maji:
Tikiti maji ni chanzo kizuri cha vitamini.
Katika
tunda hilo kuna
- Vitamin A, inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini;
- Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na
- Vitamini B6, inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini
kuwa nishati.Tunda la tikiti maji lina kiwango kikubwa cha lycopene kuliko tunda lolote au mboga za majani. Ikiwa familia yako inaishi kwenye eneo lisilo na vyanzo vya madini ya potasium, unaweza kuwapa tikiti badala yake. Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Sifa ya kipekee iliyopo katika tunda hili, ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Kwa kunywa juisi yake iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo hilo.
Kwa kawaida tunda hili huliwa pejke yake au kwa kuchanganya na matunda mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya afya ya vyakula kila kitu kwenye tikiti maji kina faida kiafya ukianzia kwenye majani tunda na hata nyama yake.
Asante Dr. kwa maelekezo haya
ReplyDeletethanx sana dr kwa somo hili
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteAsanteni sana na Karibuni.
Delete