Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Friday, May 15, 2015

MATATIZO YANAYOMFANYA MWANAMKE ASIPATE UJAUZITO HARAKA-2


Leo naendelea na mada niliyoanza wiki iliyopita, kuhusiana na matatizo yanayowafanya wanawake wasipate ujauzito haraka. Suala la kufahamu mzunguko wa hedhi, siku za kupata mimba linawahusu wote wawili, mume na mke.
Matatizo ya kisaikolojia kwa mwanaume na mwanamke na unene kupita kiasi pia huchangia tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO
Kama tulivyoona, kitendo cha mwanamke na mumewe kukaa zaidi ya mwaka wanatafuta mtoto ni tatizo kwa hiyo linahitaji uchunguzi ambao unafanyika pande zote mbili.

Mwanamke anayesumbuliwa na maumivu chini ya tumbo mara kwa mara naye yupo katika hatari hii kwani upo uwezekano wa kuathiri mirija yake ya uzazi na ikaziba kabisa, mzunguko wa hedhi unavurugika na kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Wanawake wengine hupata maumivu ya kiuno na tumbo kwa muda mrefu, siyo dalili nzuri. Matiti au chuchu kutoa maziwa pia huathiri kwa kiasi kikubwa uzazi kwani ni dalili kwamba homoni inakuwa vigumu kupata ujauzito hasa kwa wasichana.

Maumivu wakati wa hedhi pia ni dalili njema katika mfumo wa uzazi kwani inaweza kuwa una maambukizi sugu ya kizazi, uvimbe katika kizazi au “uterine fibroid”, au tabaka la ndani la kizazi kuwa nje. Hizi ni dalili chache kwa mwanamke.
Kwa upande wa mwanaume dalili pia zipo nyingi kama nilivyoelezea hapo awali, ila kama mwanaume anashindwa kufanya tendo la ndoa hilo ni tatizo kubwa.

Maumivu ya njia ya mkojo, maumivu ya korodani, kutotoa kabisa manii pia ni mojawapo ya tatizo.
Mwanaume anaweza kupata matatizo ya uzazi endapo atavuta sana sigara na matumizi ya vilevi kwa muda mrefu hasa pombe kali na madawa ya kulevya.

Zipo dalili nyingine ambazo hazionekani wazi kwa mwanamke, mfano uwepo wa uvimbe kwenye vifuko vya mayai hali iitwayo kitaalamu “Polycystic Ovurian disease” huambatana na kufunga hedhi kwa muda mrefu hata mwaka, mwanamke huota vinyweleo vingi mwilini hasa miguuni, mapajani, mikononi, ndevu, hali iitwayo kitaalamu “Hirtuism”.

UCHUNGUZI
Hufanyika katika kliniki za magonjwa ya kinamama kwenye hospitali za mikoa na rufaa. Muone daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika hospitali hizo akuchunguze. Epuka matumizi ya dawa bila ya kufanyiwa uchunguzi hospitali. Vipimo mbalimbali hufanyika kama vipimo vya damu kuangalia homoni na maambukizi mengine.

USHAURI NA TIBA
Wahi hospitali ya mkoa au wilaya kwa uchunguzi. Zingatia maelekezo ya daktari wako ili uweze kufanikiwa.

0 comments:

Post a Comment