Ni jambo
la kawaida kwa mwanamke kuota matiti anapokuwa amefikisha umri wa
kupevuka, lakini jambo hili linapotokea kwa mwanamme inakuwa ni kitu
kisichokuwa cha kawaida. Ukuaji au uotaji wa matiti kwa mwanamme na kuwa
kama ya mwanamke kitaalamu huitwa Gynaecomastia.
Kwa
miaka ya zamani umri wa kupevuka na kuanza kuonekana mabadiliko katika
mwili ilikuwa ni kuanzia miaka 17 au 18, lakini kwa miaka ya hivi
karibuni kumetokea mabadiliko makubwa sana katika staili za maisha
tunazoishi pamoja na mapinduzi makubwa katika sayansi na teknolojia na
hivyo hata miili yetu inapata athari kwa kile ambacho tunaupatia kama
chakula, dawa, vinyaji na vinginevyo. Hivi leo mabadiliko tuliyotegemea
awe nayo mtu mwenye umri wa miaka 18, unayaona kwa mtoto wa miaka 12.
Katika
ukuaji wa mwili wa binadamu, ufanyaji kazi wa viungo mbalimbali katika
mwili pamoja na tabia za kijinsia anazokuwa nazo mtu, vyote hivi
hutawaliwa na kemikali asilia zinazopatikana ndani ya miili yetu ambazo
kwa kisayansi hujulikana kama hormones.
Tukibaki
upande wa mada yetu, Gynaecomastia, kemikali hizi (hormones) ndizo
zinazomfanya mtu awe na tabia za kike au tabia za kiume. Kwa kawaida
mwili wa mwanadamu unazo homoni zote, yaani mwanamke anazo homoni za
kike na pia anazo za kiume, pia mwanamme anazo homoni za kiume na pia
homoni za kike.
Kinachomfanya
mtu awe na tabia za kike ni kwa kuwa homoni za kike ni nyingi kuliko za
kiume, na kinachomfanya mtu awe na tabia za kiume ni kwa kuwa homoni
zake za kiume ni nyingi kuliko zile za kike.
Mabadiliko yanapotokea katika mwili wa mtu juu ya hizi homoni za kike (Estrogens) na zile za kiume (Androgens) ndipo tunapoyaona mabadiliko au tabia ambazo hazijazoeleka kuonekana kwa mtu wa jinsia fulani.
Mwanamme kuota matiti, gynaecomastia husababishwa na mabadiliko katika homoni zake ambapo homoni za kike (Estrogens) zimeongezeka na kuzifanya zile za kiume (Androgens)
kuwa kwa kiwango kidogo mwilini mwake na hivyo kupelekea hata mwili
wake uwe na mabadiliko anayopaswa kuwa nayo mwanamke (kuota matiti).
Miongoni mwa vitu vinavyo sababisha mwanamme awe na matiti kama ya mwanamke ni kama vile:
Matumizi ya dawa
– baadhi ya dawa zinazotumika katika tiba mbalimbali huchangia mwanamme
kuota matiti, mfano baadhi ya dawa zinazotumika katika tiba ya vidonda
vya tumbo, tiba za magonjwa ya moyo na tiba za vijidudu vinavyosababisha
UKIMWI.
Matumizi ya vipodozi
– baadhi ya vipodozi vinavyotumika huwa na mchanganyiko unaofanya
uwiano wa homoni katika mwili ubadilike, mfano vipodozi vilivyo na
mchanganyiko wa , (tea trea oil pamoja na lavender oil), michanganyiko
hii pia huwa katika baadhi ya sabuni, losheni na shampoo.
Vyakula
– mapinduzi katika sayansi pia yamechangia kuwe na aina mbalimbali ya
uandaaji au uzalishaji wa chakula ambapo baadhi ya vyakula vinakuwa na
michanganyiko inayo badili uwiano wa homoni katika mwili wa binadamu,
mfano ni baadhi ya vyakula vilivyozalishwa kwa tekinolojia za baiolojia
(Genetic Modified Organisms ) au kwa kifupi GMOs.
Ili
tuweze kupambana na hali hii, gynaecomastia, ni vyema tukawa waangalifu
katika vyakula, vinywaji na vipodozi tunavyotumia pia tuzingatie ushauri
tunaopewa na wataalamu wa afya juu ya mambo mbalimbali yanayohusu afya
zetu pamoja na matumizi sahihi ya dawa tunazozitumia katika kutibu
matatizo ya kiafya.
0 comments:
Post a Comment