Karibu Fadhaget Sanitarium Clinic

Tunapenda kukukaribisha katika Kitengo cha Sayansi ya Tiba Asilia.

Kitengo Cha Sayansi Ya Tiba Asilia

Kwa Muda mrefu tumekuwa tukisaidia wengi katika matibabu na kutengeneza dawa bora kabisa kiafya.

Je Unapenda Kufahamu Jinsi Ya Kupata Mapacha?

Tunafundisha jinsi ya kupata jinsia unayotaka, jinsi ya kupata mtoto kama umekosa mtoto kwa muda mrefu. Pia hata jinsi ya kupata watoto mapacha tunaweza kukusaidia.

Tunapatikana Katika Mikoa Zaidi ya 10 Tanzania

Tunazidi kuongeza matawi yetu nchini Tanzania na Nje ya Nchi. Kwa sasa tunapatikana katika mikoa zaidi ya 10 na tunazidi kuongeza matawi yetu. Karibu sana.

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wednesday, August 27, 2014

DR. FADHILI EMILY AKUTANA NA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA TIBA (UNIVERSITY OF TEACHING HOSPITAL) NCHINI ZAMBIA, LUSAKA

Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic iliyopo nchini Tanzania aliweza kukutana na wanafunzi wa Chuo cha Tiba kinachotambulika kwa jina la THE UNIVERSITY TEACHING HOSPITAL (U.T.C).


Dr. Fadhili Emily aliweza kumshukuru Mungu kwa kile alichompa katika maisha yake, hasa ule uwezo wa kuweza kutambua na kujua ni dawa gani zinaweza kumsaidia mwanadamu ambaye amekuwa akiteseka sana na magonjwa sugu ambayo yamemsababishia kuonekana kama amekataliwa na dunia.

Pia aliongeza kusema kuwa anapenda sana kuisaidia jamii inayosumbuka na magonjwa sugu yayosababishwa taifa kushuka nyuma kimaendeleo kutokana na nguvu kazi kupungua. Wagonjwa wamekuwa ni watu wa kukaa nyumbani na kuwa tegemezi, hawawezi kufanya kazi kutokana na magonjwa yao kutoruhusu kufanya kazi. Badala ya watu kwenga kufanya kazi wamebaki nyumbani wakiuguzwa na wengine wamesababisha na watu wengine ambao ni wazima kushindwa kwenda  kazini na badala yake wamebaki nyumbani kuwasaidia hawa wagonjwa.
 Akiongea na Rumafrica, Dr. Fadhili Emily alisema anapenda sana kuwasaidia madaktari wenzake ambao bado hawajapata maarifa kama aliyojaliwa na mwenyezi Mungu ya kutambua na kugundua dawa za mimea na matunda ambazonni tiba nzuri kwa binadamu. Kumbuka Mungu huyu ndiye aliyeumba hii mimea na alituachia agizo la kutawala kila kitu kilichopo duniani na sio vilivyomo duniani kututawala.

Hali ya kuonekana watu wanataabika na magonjwa na kuona hakuna wataalamu wa kutosha kutokomeza maradhi yanayowasumbua wagonjwa, Dr. Fadhili Emily aliweza kutuma ujumbe kwa njia ya watsap kwa mkurugenzi wa Rumafrica, Rulea Sanga ukisema, ":Kwa kweli napenda sana kujua na ninatamani sana kusaidia madaktari wenzangu duniani kuhakikisha tunatokomeza maradhi yasiyo ya lazima katika dunia hii, ninawaomba Watanzania wenzangu mnisaidie kwa maombi ili Mungu anyooshe mkono wake niwaletee Chuo Kikuu Afrika cha Tiba zitokanazo na sayansi ya mimea Asili ambacho kitaitwa UNIVERSITY OF MEDICINAL PLANTS IN TANZANIA"

 Kutoka na wazo la kuanzisha Chuo cha tiba za mimea asili, Dr. Fadhili Emily alitoa hoja yake ya msingi na kusema anaona itakuwa vema sana kutoa elimu  ya kutosha juu ya afya ya miili yetu na njisi namna tuwezavyo kutuma lasilimali za kutumia mime na kujitibu wenyewe. Alimaliza kwa kumshukuru Mungu na kumuomba mwenyezi Mungu aibariki nchi ya Tanzania kuwa na amani na utulivu na kuondoa haya mateso ambayo wanapata kutokana na magonjwa

Dr. Fadhili Emily ambaye amekuwa akisafiri nchi tofauti kujifunza na pengine kuwasaidia watu walioko katika nchi hizo ili waweze kuwa na maarifa kama aliyonayo. Safiri zake zimekuwa na matunda makubwa kwani kila anapokuja nchini anakuwa na kitu cha tofauti sana na nguvu za ajabu za kupambana na magonjwa na maradhi yanayowasumbua watu.

Tunakukaribisha sana katika ofisini zetu zilizopo Afrikana, Mbezi Beach.

 MATUKIO KATIKA PICHA













EBOLA BADO TISHIO AFRIKA MAGHARIBI




TAARIFA iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Afya Duniani (WHO), inaonyesha jinsi gonjwa hatari la Ebola linavyozidi kuangamiza wananchi katika eneo hilo.
Agosti 22 mwaka huu, WHO walitoa taarifa kuwa, jumla ya wagonjwa walioripotiwa kuwa na Ebola ni 2,615 kwenye nchi nne za Afrika Magharibi ambapo kati yao 1,427 wamepoteza maisha kwa ugonjwa huo.
Nchini Liberia ambapo ugonjwa huo ulianzia, wagonjwa 1,082 wameripotiwa kuwa nao, huku 624 kati yao wakifariki dunia.
Guinea, 607 wamethibitishwa kuwa na Ebola, huku 406 kati yao wakiwa wamepoteza maisha.
Sierra Leone, watu 392 wameripotiwa kufariki kwa ugonjwa huo na nchini Nigeria, watu watano wamepoteza maisha kwa Ebola kati ya 13 walioripotiwa kuwa na ugonjwa huo.

Sunday, August 24, 2014

KITUNGUU SWAUMU NI KIUNGO NA NI DAWA YA MARADHI ZAIDI YA 30

Kitunguu swaumu hakikosekani katika kila jiko duniani.Ni mmea maarufu sana kwa tiba.Kitunguu swaumu ni jamii ya yungiyungi.Kitunguu swaumu kilicho bora zaidi duniani ni kinachotoka misri kwasababu ya tabia ya ardhi yake na mto nail.Kitunguu swaumu kina harufu ya kipekee isiyowapendeza watu wengi ingawa kimebeba siri nyingi za tiba.Kwa ajili hiyo maana yake kilatini ni HARUFU ICHOMAYO.
Ili kuepukana na harufu ya kitunguu swaumu baada ya kukila,kula tofaa au tafuna majani mabichi ya naanaa,au kunywa maji yaliyotokosewa karafuu.Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba iwapo kitapikwa na kila kinapowekwa muda mrefu ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya majani yake kukauka kabisa).

Kitunguu swaumu kimekusanya protin 49%,sulphur 25%,kiasi fulani cha chumvi,homoni zitoazo nguvu za kiume,viuaji sumu,vikojozavyo,vitoavyo safura,vinavyoteremsha hedhi,vimeng'enyo vyenye kuyeyusha mafuta na viini vyenye kuua minyoo.Kila utafiti unapoendelea ndipo faida na maajabu ya kitunguu swaumu yanapoongezeka.

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SWAUMU;

1.Kiua sumu
2.Kisafisha tumbo
3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)
4.Huzuia mvilio wa damu
5.Kusafisha njia ya mkojo
6.Kutibu amoeba
7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)
8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)
9.Gesi
10.Msokoto wa tumbo
11.Typhoid
12.Kidonda kilichooza
13.Dondakoo
14.Mabaka
15.Baridi yabisi(Rheumatisim)
16.Mishipa
17.Uziwi
18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza)
19.Mafua
20.Saratani(Cancer)
21.Kifaduro
22.Kifua kikuu cha mapafu
23.Kipindupindu
24.Kutoa minyoo
25.Upele
26.Kuvunjavunja mawe katika figo
27.Mba kichwani
28.Kuupa nguvu ubongo
29.Kuupa nguvu fizi
30.Kuzuia meno kung'ooka
31.Nguvu za kiume
32.Maumivu ya kichwa
33.Kizunguzungu/kisunzi
34.Kutuliza maumivu ya meno
35.Kujenga misuli na kutia nguvu
36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis)
37.Shinikizo la damu
38.Kinga ya tauni na ukimwi
39.Magonjwa ya macho

MATUMIZI NA MAANDALIZI KATIKA KUTIBU
Matumizi na maandalizi ya kitunguu swaumu katika tiba yanategemea aina ya maradhi unayotaka kuyatibu,hivyo basi ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa tiba mbadala ili uweze kupata maelekezo sahihi ya namna ya kuandaa kulingana na ugonjwa unaokusumbua.Kumbuka kama tulivyosema awali kuwa kitunguu swaumu kikipikwa kinapoteza nguvu ya tiba kutegemeana na tiba unayokusudia.
Kumbuka pia kwamba kitunguu swaumu huweza kuchanganywa na vitu vingine mfano;maziwa,asali,habatsouda,juisi,shayiri n.k.kutegemea na maradhi unayotaka kuyatibu na kwa ushauri/maelekezo ya daktari.

HATIMAYE DAWA YA EBOLA "ZIMAPP" YAONESHA MWANGA!



Tabasamu la matumaini baada ya kupata ahueni ya Ebola

Hospitali moja nchini Marekani imewaruhusu wamisionary wawili wa kimarekani ambao walikua wakipata tiba kutokana na kuathiriwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, na imethibitishwa hawana athari kwa afya ya
jamii. Dr Kent Brantly na mtabibu mwenziwe Nancy Writebol ambao waliruhusiwa mapema wiki hii walipata maambukizi ya ugonjwa huo wakati wakiwasaidia wagonjwa wa ugonjwa huo nchini Liberia.

Kutokana na maambukizi walopata watabibu hao walipata maambukizi walipewa dawa ya majaribio ambayo haikuwahi kupewa binadamu hapo kabla,na dokta aliyekuwa zamu alishindwa kuthibitisha juu ya nafuu yao kama imetokana na dawa hiyo ya majaribio.

Kufuatia matokeo mazuri ya dawa hiyo ya majaribio dokta huyo wa zamu alijinasibu kuwa kituo chake kimejifunza namna bora ya kumsaidia mgonjwa wa bola na mazingira alimokuwamo, na kuahidi kushirikisha utaalamu huo kwa watabibu kutoka katika nchi za Kiafrica

DR. FADHILI EMILY WA THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC AKISHIRIKIANA NA MADAKTARINI NCHINI ZIMBABWE WAKIFANYA UTAFIKITI WA TIBA NA MADAWA YA MAGONJWA MBALIMBALI.


Kuna watu ambao Mungu amewepa karama fulani ya kusaidia jamii kwa njia fulani ambayo wewe huwezi kuifanya bila msaada wa Mungu. Dr. Fadhili Emily ni muumini wa kanisa la Wasabato. Kwa neema ya Mungu ameweza kutumia matunda na mimea kupata dawa mbali mbalimbali za magonjwa sugu.

Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic kutoka Tanzania ambaye yuko nchini Zimbabwe kwa ziara ya maswala ya utafiti wa tiaba na madawa yake. Akiongea na Rumafrica kwa njia ya simu alisema, yuko nchini Zimbabwe kwa  lengo kubwa la kufanya utafiti juu ya vyanzo vya magonjwa  na matibabu yake.

Siku ya Jumamosi 23/08/2014 aliweza kufanikiwa kukaa na  vijana ambao ni madakatari wa Hospitali ya General ya Victoria Hills  iliyoko nchini Zimbabwe na kujua jinsi namna ya kuweza kuwasaidia wenye maradhi ya Tabia , Afya ya Uzazi pande zote yaani akina mama na akina baba na pia kuwatembelea wagonjwa katika wodi zao ili kuwafariji na kuwapa matumani kutokana na vile wanavyoteseka na magonjwa mbalimbali.

Dr Fadhili Emily aliweza kudokeza kile alichokiona na kujifunza pale tu alipoingia katika wodi ya akina mama ambapo aliweza kuona watu wawili tu kati ya mia moja ndio waliofanyiwa upasuaji, alizidi kusema, walipopewa takwimu ya juu ya wagonjwa wanatakiwa kufanyiwa upasuaji, ilionekana ya kwamba wagonjwa wengi (akina mama) hujifungua bila ya kufanyiwa upasuaji kwa sababu wana Elimu ya kutosha kuhusu afya ya uzazi. Kuna mambo mengi aliweza kuyafanya huko Zimbabwe ambayo si vyema kuyaongelea mitandaoni, ila unaweza kufika katika ofi zake na utajulishwa mengi juu ya tatizo lako la magonjwa.

Hayo ni baadhi ya mambo waliojionea huko Zimbabwe, hata kama tumekupa machache katika mengi ambayo Dr. Fadhili Emily aliweza kujionea na kujifunza, jinsi gani wenzaetu wa nchi za jirani wanapambana na magonjwa yanayowasibu.

Unaweza kufika katika makao makuu ya The Fadhaget Sanitarium Clinic ambayo yako Mbezi Beach Afrikana. Ukifika kituoni ulizazia watu wa bodaboda au bajaji wakuletea The Fadhaget.

Tunamuamini Mungu wetu kwa kila jambo. Mungu akubariki sana

MATUKIO KATIKA PICHA





 









Thursday, August 21, 2014

THE FADHAGET SANITARIUM CLINIC INASIKITIKA KUONA IDADI YA WALIOKUFA KWA EBOLA YAFIKIA 1,350

Tuzidi kumuomba Mungu atuepushe na hili janga la ugonjwa wa Ebola. Ugonjwa huu unazidi kuteketeza watu, vifo vinaongezeka. Unapoomba maombi yako kumbuka kumuomba mweneyzi Mungu atusaidie kuondoa ugonjwa huu usije ukateketeza familia yako.

Mgonjwa wa Ebola akipelekwa eneo maalum kwa matibabu nchini Sierra Leone.

IDADI ya watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi mpaka sasa imefikia 1,350 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Shirika la Afya Duniani (WHO) huku watu 106 wakiripotiwa kufariki kati ya Agosti 17-18 mwaka huu.

Ugonjwa huo ambao husambazwa moja kwa moja kupitia majimaji ya mwilini kutoka kwa mgonjwa mpaka sasa bado hauna tiba.

MAGONJWA YA ZINAA YANAVYOSABABISHA KUZIBA KWA MRIJA WA MKOJO (URETHRAL STRICTURE)



Mrija wa mkojo (urethra) ni njia ya kutolea mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu na unapoziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa tabu na kusababisha maumivu makali sana.
Kitaalamu kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa urethral stricture na  husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa.
Magonjwa ya zinaa yanayoweza kusababisha kovu kwenye njia ya mkojo yapo mengi na tutayajadili katika matoleo yetu yajayo kwani  yapo mengi. Hivyo ni muhimu sana mtu kutibiwa mapema anapokuwa na magonjwa hayo.
Kuziba kwa mrija huo kunaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.Wengi wanaopatwa na tatizo hili ni wale ambao wana historia ya kuugua magonjwa ya zinaa au kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au cystoscope) sehemu hizo au husababishwa na kuvimba tezi dume (BPH) kwa wanaume.
Wengine wanaopatwa na tatizo hili ni wale wanaokuwa na historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya sehemu za siri au  wanaopata maambukizi ya mara kwa mara ya magonjwa kwenye mrija wa mkojo (urethritis).
Tatizo hili mara nyingi huwakumba wanaume na ni mara chache sana kuwakumba wanawake au watoto wachanga  labda wale wanaozaliwa wakiwa na tatizo hili ambapo kitaalamu huitwa congenital urethral stricture.
DALILI
Mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo, kwa mwanaume hutokwa na manii zilizochanganyika na damu,  kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu, kutoa mkojo kidogo sana tena kwa shida, kukojoa mara kwa mara na kushindwa kumaliza mkojo wote.
Wengine huona dalili za mkojo kujitokea wenyewe, hivyo mhusika kujikojolea, kusikia maumivu wakati wa kukojoa au chini ya tumbo au kwenye kinena,  mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa na uume kuvimba.
Mgonjwa aonapo dalili hizo anashauriwa kumuona daktari  ili afanyiwe uchunguzi wa mwili na namna anavyokojoa. Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha kupungua kwa mkondo wa mkojo, uchafu kutoka katika mrija wa mkojo, kibofu kilichojaa/kuvimba kwa mitoki ya maeneo ya kinena, tezi dume iliyovimba au yenye maumivu, kuhisi kitu kigumu chini ya uume.
Daktari akiona moja ya dalili hizo mgonjwa anaweza kuchunguzwa kwa vipimo tofauti kama vile kile cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy),kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya mkojo kutoka, X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram) atapimwa kama ana magonjwa ya zinaa kwa kumfanyia uchunguzi wa mkojo (Urinalysis) pamoja na kuotesha mkojo (Urine culture).
TIBA
Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo mojawapo ya tiba au dawa pekee ya uhakika ni mgonjwa kufanyiwa upasuaji ambao unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo.
Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena hufanyika. Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye bomba lililowekwa chini ya tumbo.
USHAURI
Mgonjwa mwenye tatizo hili atibiwe haraka maana kama tatizo likiachwa linaweza kusababisha kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo kushindwa kufanya kazi.
Watu wajikinge na magonjwa ya zinaa ambayo yanasababisha tatizo hili na wawe  makini na kazi zinazoweza kusababisha kuumia sehemu nyeti na kuzalisha tatizo hili.

Wednesday, August 20, 2014

BINGWA WA MAGONJWA YA AKINA MAMA NA MARADHI YA TABIA, DR. FADHILI EMILY AZUNGUMZIA JUU UGONJWA WA EBOLA.

Dr. Fadhili Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic leo ameeleza katika mitandao ya kijamii kuwa uwezekano wa kutibu ugonjwa wa Ebola kwake ni tatizo, amekili wazi hawezi kutibu ugonjwa huo bali akitambulika mtu ana ugonjwa  huo anamshauri afike Muhimbili hospitalini moja kwa moja  maana ni ugonjwa usio wa kawaida katika mazingira yetu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki madaktari ili tujue wepesi wa kujua siri ya kirusi cha Ebola na kusaidia dunia juu ya matibabu.
http://i1.ytimg.com/vi/8NYzzMmziS4/0.jpgDr. Fadhily Emily wa The Fadhaget Sanitarium Clinic

Tuesday, August 19, 2014

WANAWAKE: MSITUMIE SUKARI SIYO NZURI SANA!

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na jarida moja la masuala ya afya la nchini Uingereza (BMC Public Health), unywaji wa vinywaji vyenye sukari, kiasi cha mara tatu kwa wiki, huweza kunenepesha matiti na unenepaji wa matiti huongeza hatari ya mwanamke kupatwa na saratani ya matiti.

Waliofanyiwa utafiti huo ni wanawake 776 ambao hawajafikia ukomo wa hedhi (Premenopausal) na wanawake 779 waliofikia ukomo wa hedhi (Postmenopausal).

Pamoja na maswali mengine waliyoulizwa, wanawake hao waliulizwa kiasi wanachokula kwa upande wa vyakula na vinywaji vyenye sukari kama vile chokoleti, keki, ice cream, soda, n.k na huwa wanaweka vijiko vingapi vya sukari kwa vinywaji wanavyotayarisha, kama chai au juisi.

Akiongelea matokeo ya utafiti wao, mtafiti na mwandishi kiongozi wa utafiti huo kutoka Chuo Kikuu cha Laval cha Quebec, nchini Canada, Caroline Diorio alisema kuwa matokeo yalionesha kuwepo kwa uhusiano mkubwa kati ya utumiaji wa sukari kwa wingi na kuongezeka kwa ukubwa wa matiti ya wanawake kutoka makundi yote mawili (wasichana na watu wazima).

Katika utafiti wao, wamegundua zaidi kuwa wanawake waliofikisha ukomo wa hedhi matiti yao yaliongezeka ukubwa zaidi kwa kula vyakula vingi vyenye mafuta, wakati wanawake ambao hawajafikisha ukomo wa hedhi, waliongezeka ukubwa wa matiti yao kwa kula vinywaji vyenye sukari visivyopungua vitatu kwa wiki.

Matokeo ya utafiti huo yanatoa picha kwamba kuwa na matiti makubwa kunakosababishwa na ulaji wa sukari pamoja na mafuta kwa wingi huongeza hatari ya kupatwa na saratani ya matiti kwa asilimia 3.

Dk. Dioro anamalizia kwa kusema kuwa utafiti zaidi unahitajika, hususan katika makundi ya watu wenye matumizi makubwa ya sukari. Lakini hata hivyo, amesema kuwa hadi utafiti mwingine utakapofanyika na kuthibitisha vinginevyo, kwa sasa uhusiano wa matumizi makubwa ya sukari na unenepaji wa matiti kwa wanawake uko wazi.

Kwa kuwa unenepaji wa matiti una uhusiano mkubwa na ulaji mkubwa wa mafuta na sukari kwa njia mbalimbali kama zilivyoanishwa hapo juu, na kwa kuwa unenepaji wa matiti unaongeza pia hatari ya mwanamke kupatwa na saratani ya matiti, ni sababu tosha kabisa ya wewe kuamua kuachana na unywaji wa vinywaji baridi vyenye sukari nyingi kwa faida ya afya yako.

Kama ambavyo mara kwa mara tumekuwa tukisisitiza, tuepuke sana matumizi makubwa ya sukari na tunapoitumia basi tuitumie kwa kiasi kidogo sana na badala yake tupendelee kutumia asali na kula kwa wingi matunda na mboga za majani ambazo huwa na sukari asilia ambayo haina madhara mwilini.

KAMA WEWE UMEJIFUNGUA SALAMA, MTOTO WAKO NI MZIMA MSHUKURU MUNGU

DUNIANI kuna mengi kiasi kwamba kama mama umebeba ujauzito kwa miezi tisa na kujifungua mtoto salama na mtoto wako ni mzima unapaswa kumshukuru Mungu kwani kuna watu ambao wanapata usingizi wa mang’amung’amu kutokana na mateso ya watoto wao.


Mtoto Godwin Florence Rweyemamu (3) akilia kwa maumivu anayoyapata.

Mtoto Godwin Florence Rweyemamu (3), mkazi wa Kijiji cha Kamala, Kata ya Bangwe mkoani Kigoma yupo ndani ya mateso makubwa yanayomfanya kulia muda wote kutokana na maumivu makali anayoyapata kwa ugonjwa wa kansa unaotafuna macho yake hivyo kumfanya asione.

HISTORIA YAKE
Akizungumza na Uwazi akiwa katika masikitiko makubwa
nyumbani kwa ndugu yake, Manzese jijini Dar, bibi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Elda Charles Rweyemamu, mjukuu wake huyo alizaliwa akiwa hana tatizo lolote lakini alipofikisha umri wa miaka miwili na nusu akapatwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho upande wa kushoto.

“Tuliamua kumpeleka kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kigoma, Maweni ambapo alitibwa akapata nafuu, tukarudi nyumbani.“Lakini wanasema ukizaliwa na balaa ni balaa tu, mwanzo hadi mwisho.


Mtoto Godwin Florence Rweyemamu (3) akiwa na bibi yake, Elda Charles Rweyemamu.

Kwani baada ya muda ugonjwa ulijirudia tena, sasa si mtoto wa jicho ila jicho likaonekana kuwa na uvimbe kidogo. Mimi na mama yake tulishangaa sana, tukaona lazima tuendelee kuhangaika. Tukampeleka katika Hospitali ya Matiazo.

“Madaktari walijitahidi, wakamtibu akapata nafuu tena na uvimbe katika jicho uliisha, tukajua tumeepukana na hilo.

UGONJWA WARUDI KWA KASI
Akiendeleza kusimulia mateso ya mtoto huyo, bibi huyo alisema:
“Baada ya kukaa kwa muda mfupi, ghafla ugonjwa ulirudi tena, sasa eti hata kichwa kilivimba. Hii hali ilitushangaza sana na tukawa tunaulizana ni nini?

“Nilimwambia mama yake kuwa Mungu ni wa kumtumaini muda wote, hivyo tukampeleka tena Hospitali ya Maweni lakini madaktari wakasema ili mjukuu wangu aendelee kuwa na uhai tuje hapa Muhimbili. Tulifunga safari ya kuja ambapo Julai 21, mwaka huu, tukawa tumefika.”

MATUMAINI YAREJEA, YAYEYUKA
“Tulipofika hapa Muhimbili na kuona hospitali yenyewe ilivyo kubwa na madaktari bingwa wengi niliamini kuwa mjukuu wangu angepona na kurudi naye nyumbani akiwa salama lakini cha kushangaza mambo yakawa tofauti na jinsi nilivyokuwa nikifikiria.

”Madaktari walimfanyia uchunguzi, baada ya siku nne waliniambia ugonjwa alio nao huyu mtoto ni kansa.
“Walinitoa machozi zaidi pale waliponiambia kuwa, hata hivyo hawataweza kumtibu kwa vile tulichelewa kumleta.”

“Lakini hata wao waliniambia wakiwa na masikitiko makubwa kwani nilishangaa kuwaona baadhi ya madaktari wakitoa machozi kwa kumuonea huruma mjukuu wangu kwa jinsi anavyolia muda wote kwa maumivu kama unavyomsikia,” alisema.

Aliongeza kuwa, walichofanya madaktari hao ni kumpa dawa ya kutuliza maumivu na kumwambia bibi mtu warudi nyumbani Kigoma kwa ajili ya kumshukuru Mungu kwa yote.

HANA NAMNA YA KURUDI KIGOMA
“Tangu nimeruhusiwa kutoka Muhimbili, Julai 26, mwaka huu sina jinsi ya kurudi nyumbani Kigoma. Nauli hadi kule ni shilingi 70,000. Kwa sasa nimepata hifadhi hapa Manzese kwa mdogo wangu ambaye anaishi kwa kufanya biashara ndogondogo lakini hana fedha. Kuendelea kukaa kwake ni sawa na kero kwani huyu mtoto amekuwa akilia mara kwa mara hali ambayo ni kero kwa wapangaji wenzake.

“Hata chakula ni tatizo, kila siku inabidi nimpeleke katika zahanati kusafisha macho. Kwa muda wa wiki moja nimetumia shilingi 300,000 kwani aliishiwa damu na inabidi aongezwe halafu kuna dawa za kutuliza maumivu aliongezewa, nina shida kubwa sana.”

KWA NINI BIBI NA MJUKUU?
“Kilichonifanya nije mimi huku Dar ni kwa vile mama yake ni mjamzito. Wakati wowote anaweza akajifungua. Pia ana mawazo mengi sana kwani watoto wake wawili, wa kwanza na wa pili walifariki dunia kutokana na magonjwa ya aina mbalimbali na huyu wa tatu ndiyo madaktari wamesema nimrudishe nyumbani tusuburi kifo,” alisema Elda kwa huzuniu

ANACHOOMBA
Anachoomba bibi huyo ni nauli ya kumuwezesha kurudi nyumbani kwake, Kigoma. Kwa aliyetayari anaweza kumsaidia kupitia namba 0762 175 117,
0784 420 215 au 0719 285 100.

Ndugu msomaji, kama ulivyosikia kilio cha bibi huyo ambaye yupo katika wakati mgumu wa kumuuguza mjukuu wake, hebu msaidie kwa chochote ulichonacho, tunaamini Mwenyezi Mungu atakubariki. Mhariri.

CHANZO NA TAHADHARI ZA UGONJWA HUU HATARI WA EPORA

Ebola ni ugonjwa wa hatari unaosababishwa na virusi vijulikanavyo kwa lugha ya kitaalamu “Ebola Virus”. ugonjwa wa damu kutoganda.



Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za Virusi zinaazosababisha kutokwa na Damu mwilini,(Viral Haemorrhagic Fevers) Chanzo kamili cha virusi vya ugonjwa huu hakijulikani. Katika orodha ya watu 10 waliopata kirusi cha Ebola, basi wastani kati ya watano au tisa hufa.

Hali inayosababisha mlipuko wake pia haijulikani.Ugonjwa huu pia hauna tiba wala chanjo.Hata dawa za jadi hazijathibitika kutibu ugonjwa huu.



Dalili za Ebola

Pale watu wanapopata Ebola, dalili zake za kwanza ni kuonekana kama magonjwa mengine
Dalili za ugonjwa huu ni:-
1. Homa kali, inayoambatana na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili kama pua, njia ya haja kubwa na dogo, mdomoni, masikioni, machoni n.k.
2.  Kutapika damu
3.  Kuharisha damu
4.  Fizi kuvuja damu
5. Kutokwa na damu na kuvujia chini ya ngozi. Kwasababu ya kutokwa na damu sehemu za haja kubwa na ndogo, choo na mkojo pia vitaonekanakuwa na damu.




Kuenea kwa Ebola.
Ugonjwa huu unaenea kwa urahisi sana na haraka kutoka mtu mmoja hadi mtu mwingine kupita njia mbali mbali.
Njia hizi ni:-
· Kuingia mwilini au kugusana na: Mate, Damu, Mkojo, Machozi, Kamasi
majimaji mengine ya mwili, ikiwa ni pamoja na jasho. kugusa mtu aliyekufa kwa ugojnwa wa Ebola kushika/kugusana na wanyama jamii ya nyani. · Kuchomwa na sindano au vifaa ambavyo havikutakaswa Ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana. kugusa taka ngumu au maji taka yaliyotokana na kumhudumia mgonjwa Ebola.

Athari za ebola

· Unasambaa kwa haraka sana Unasababisha vifo vingi kwa muda mfupi · Jamii huingiwa na hofu na wasi wasi na kushindwa kufanya shughuli zao za kawaida ni gharama kuwahudumia/kutibu wagonjwa. · Mipaka inaweza kufungwa na watu wakashindwa kusafiri kutoka eneo/nchi moja hadi nyingine.



Tiba ya Ebola
Hakuna tiba maalumu ya homa ya Ebola. Lakini ikiwa watu wanapata huduma bora kutoka kwa madaktari na wauguzi, wengi wao huishi.

Kinga ya Ebola
Ugonjwa wa Ebola unaweza kuzuilika.Ni muhimu kwa kila mmoja kuwajibika Njia kuu za kujikinga na ugonjwa huu:-

Kuepuka kugusa au kuingiwa na mate, damu, mkojo, jasho, kinyesi, machozi na maji maji mengine yanayotoka mwilini mwa mwenye dalili za ugonjwa wa Ebola. Kwa kuwa ugonjwa huu pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, epuka kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja.


Kutoa taarifa mapema kwa viongozi wa serikali na wa huduma za Afya katika ngazi zote pale anapotokea mtu mwenye dalili za Ebola  uwahi katika vituo vya huduma za Afya pale mtu anapoona dalili za ugonjwa huu. Wananchi wana tahadharishwa kuepuka kushughulikia maiti ya mtu aliyekufa kwa Ebola;badala yake watoe taarifa kwa uongozi wa kituo cha huduma za Afya kwa ushauri.
ufanya ufatiliaji madhubuti wa ugonjwa huu. Wananchi waepuke mila na desturi zinazoweza kuchelewesha kupata huduma muhimu na kuzidi kueneza ugonjwa wa Ebola

Wagonjwa wa Ebola hutengenishwa na wagonjwa wengine ili wasipate kuambukizwa. Zingatia usafi wa mwili na tabia.

KUMBUKA
Ugonjwa wa Ebola ni hatari sana. Unasambaa haraka na unasababisha Madhara na vifo vingi. Epukana nao.